PSSSF YAPITA "BANDA KWA BANDA" KUWAFIKIA WANACHAMA WAKE KWENYE MAOENSHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

April 27, 2023

 

 

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na kutoa elimu kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro, pia unapita “Banda kwa Banda” ili kuwafikia wanachama wake, Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi amesema.

Bw. Njaidi amesema Mfuko unashiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu na kuwahudumia wanachama wake ambao ni wastaafu lakini pia watumishi wa Umma na Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa asilimia 30.

“Lakini tukumbuke kuwa watumishi walio kwenye viwanja hivi nao pia wanawahudumia wananchi kwenye mabanda yao, hivyo tumeona tugawane majukumu, baadhi yetu wako bandani kutoa elimu na huduma kwa watakaofika na sisi tunapita banda kwa banda kuwahudumia." Alifafanua Bw. Njaidi ambaye alifuatana na Afisa Matekelezo Mwadamizi wa Mfuko huo Bw. Charles Mahanga.

Akifafanua alisema kwakuwa huduma nyingi za Mfuko zinapatikana kiganjani (PSSSF Kiganjani) hivyo ni rahisi kuwapatia elimu kwenye mabanda yao ya jinsi ya kutumia huduma hiyo.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.

Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi akiwa na Afisa Matekelezo Mwandamizi PSSSF, Charles Mahanga akimkabidhi kipeperushi cha PSSSF Msimamizi Mkuu wa banda la Jeshi la Polisi, Mkaguzi Msaidizi Zuwena Mwita.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Masahariki, Bi. Zaida Mahava (kulia) akimuhudumia mwanachama

Bw. Njaidi (kushoto), akitoa elimu kwa maafisa wa polisi.

Banda la NMB
Banda la NSSF
Banda la CRDB
Banda la CRDB
Banda la WCF

Banda la OSHA

RAIS SAMIA SULUHU PAMOJA NA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI,IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

April 27, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2023. Rais wa Rwanda Mhe. Kagame amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya Siku 2.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo Rasmi na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2023

 

JIJI LA TANGA LAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KWA KUONYESHA UONGOZI ULIOTUKUKA

April 27, 2023



Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Robo tatu kilichoketi leo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza wakati wa kikao hicho


Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa kikao hicho
Sehemu ya madiwani wakiwa kwenye kikao hicho
Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwa kwenye baraza hilo
Sehemu wa madiwani wakifuatilia hoja mbalimbali



Na Oscar Assenga, Tanga. 

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga limepongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutimiza miaka miwili madarakani kwa kuonyesha uongozi uliotukuka katika mambo mbalimbali ikiwemo kuendeleza miradi mikubwa iliyoacha na mtangulizi wake hayati Dkt John Magufuli. 

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mshtahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya tatu ambapo alisema licha ya kuendeleza miradi lakini pia ameanzisha mingine mikubwa ikiendana na kupelekea fedha nyingi kwenye ngazi ya Halmashauri ikiwemo Tanga Jiji ambao pia wamenufaina nazo. 

Shillow alisema pamoja na hayo lakini Rais Dkt Samia Suluhu amefungua upya milango ya ajira kwa watumishi wa umma baada ya kuingia madarakani kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma na kuwapatia unaafuu katika kodi mbalimbali ili waweze kukidhi mahitaji yao na kudumu masiaha yao.

“Lakini jambo jingine ni Rais Dkt Samia Suluhu kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kuondosha riba kwa wanafunzi kwenye mikopo hiyo sambamba na kufungua milango ya demokrasia kwa kuenzi utanzania umoja, mshikamano na undugu kwa watanzania bila kujali tofauti za kiitikadi “Alisema Mshtahiki Meya huyo.

Hata hivyo alisema kwamba wanampongeza pia kwakutoa matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanywa kidigitali kwa mara ya kwanza tokeo nchi ipate uhuru ikiwemo kugawa vishikwambi vilivyotumika katika sensa kwenye idara ya elimu sekondari na msingi za Halmashauri nchini ili kuimarisha elimu na uwekaji wa takwimu za elimu pamoja na kuifungua nchi kwenye mambo ya utalii na mahusiano ya kikanda na kimataifa.

Mwisho.