MTAMA WAIFAGILIA KAMPENI YA TGGA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA

May 20, 2017
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akitoa elimu kwa wanafunzi kuhusu Hedhi salama kwa wasichana  (Manustretion Hygiene) wakati wa kampeni iliyoendeshwa na chama hicho  katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Richard Mwaikenda, Mtama
WALIMU na Wanafunzi Mkoa wa Lindi, wamefurahishwa na Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyofanyika kwa uwazi katika Shule ya Sekondari Mtama.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa juzi na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Lindi, yalishirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na walimu katika Jimbo la Mtama.

Akielezea kuhusu kampeni hiyo, Mwanafunzi Fasda Mahamudu wa Shule ya Sekondari Mtama, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemfanya aelewe vizuri kuhesabu siku zake za hevi na jinsi ya kuwa msafi ikiwemo kuoga mara tatu kwa siku na kila baada ya kupata haja.

Naye Amana Amah mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Likongopele, alisema amefurahishwa na kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya uwazi na kwamba imemfumbua mambo mengi ikiwemo kuzijua aina mbalimbali za pad za kisasa na jinsi ya kuzivaa wakati wa hedhi. Aliomba TGGA kuieneza kwa uwazi elimu hiyo katika shule mbalimbali vijijini.

Naye Mratibu Elimu Kata ya Mtama, Marcelinus Lukanga, aliwataka wasichana kujiunga kwa wingi TGGA ili waondokane na woga, hofu na kutokuwa na aibu jambo ambalo pia litawasaidia kuwa huru, safi, salama na kutopata kirahisi maambukizi hasa wakati wa hedhi.

Pia aliwashauri akina baba na kaka kutokuwa mbali na wasichana kwani nao ni wajibu wao kuwasaidia na ikiwezekana kuwapatia msaada wa hali na mali ikiwemo kuwanunulia vifaa vinavyowafaa wakiwa hedhi.

Mwalimu Mariamu Hashima wa Shule ya Msingi Lihimba, aliiisifia kampeni hiyo kwa kuendeshwa kwa uwazi na ukweli, lakini alishauri kuwa mafunzo hayo yatenganishwe kwa watoto wa shule za msingi kuwafundisha zaidi jinsi ya kujiandaa kupata hedhi na vifaa anavyopaswa kuwa navyo.

Timu ya kampeni hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, Mkufunzi Msaidizi Rehema Kijazi, Kiongozi wa Girl Guides Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango.





 Wanafunzi wakishangilia baada ya kufurahishwa na elimu ya hedhi salama
 Mmoja wa viongozi wa Girl Guides Happiness akihamasisha wakati wa kampeni hiyo
 Walimu kutoka shule mbalimbali Jimbo la Mtama, wakisikiliza kwa makini wakati wa kampeni hiyo
 Rachel ambaye ni Girl Guides kutoka Uganda, akiwalekeza wasichana jinsi ya kutengeneza pad
 Girl Guides kutoka Madagascar akionesha namna ya kutengeneza pad
 Michelle Girl Guides kutoka Rwanda ambaye yupo nchi katika exchange program akionesha jinsi ya kutengeneza pad ya kawaida
 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akihutubia na kuwahamasisha wanafunzi wasichana kujiunga na TGGA
 Mratibu Elimu  Kata ya Majengo, Marsenus Lukanga (kulia) akimkabidhi kasha la vihifadhi (Pad),  Mwanafunzi wakati wa Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama (Manustretion Hygiene) kwa Wasichana iliyoendeshwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi.




 Viongozi wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi waliokabidhiwa makasha ya vihifadhi ya pad zitakazogawiwa kwa watakaopata hedhi shuleni kwao.

 Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.
Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.

CHIN BEES AACHIA WIMBO NA VIDEO MPYA ‘NYONGA NYONGA’

CHIN BEES AACHIA WIMBO NA VIDEO MPYA ‘NYONGA NYONGA’

May 20, 2017



Dar es Salaam, May 20, 2017,

Baada ya kujitengenezea heshima adimu kama ‘Prince wa Trap’ Tanzania kupitia ngoma yake, Pepeta, Chin Bees ameachia wimbo mpya ‘Nyonga Nyonga’ pamoja na video yake.

Wimbo huo wenye mahadhi ya dancehall iliyochanganyikana na ladha za aina yake za Kibongo, unadhihirisha uwezo wa Chin katika kubadilika kwenye mahadhi mbalimbali kama atakavyo. Nyonga Nyonga ambao ni wimbo wa pili wa rapper huyo akiwa chini ya usimamizi wa label ya Wanene Entertainment.

 “Ni dancehall lakini za watu fulani ambao wamezimiss. Ni muziki fulani tofauti ambao hata mtu akisikiliza lazima atabounce,” anasema. Ameongeza, “It’s a typical African hit na ikishakuwa hivyo inaweza kusikilizwa kokote Afrika kwasababu nilichokifanya ni vitu ambavyo viko musical, kote duniani wanaweza wakafeel. It’s a new tone,” anasema.

“Nimewaletea watu kitu ambacho ni tofauti ambacho kitawafanya wacheze na mind zao ziwe fresh kwa kusikiliza.”
Wimbo huo umetayarishwa na Dr.Reggy, mpishi ambaye amewahi kufanya miradi mingi na Chin Bees siku za nyuma. “Dr.Reggy ni producer wangu wa kwanza kabisa, nimeanza kufanya naye kazi kitambo kabla hata sijawa na jina kubwa,” anafafanua.

Video ya wimbo huo imefanyika katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam huku rangi za nguo walizovaa wote wanaoonekana, zikitengeneza picha ya kuvutia machoni na yenye Uafrika mwingi.
Kuhusiana na video hiyo Chin amesema, “Imefanyika hapa hapa Wanene na tuliamua kuifanyia nje zaidi tofauti na video yangu iliyopita ya Pepeta ambayo yote ilifanyika ndani. Tumefanya kwenye yale mazingira ya mtaani kabisa.”

“Theme ya video ilikuwa ni kuonesha rangi za mtaani na mavazi pamoja na mazingira halisi ya Kitanzania na yenye muonekano wa kizamani,” anasema Director H aliyeiongoza video hiyo.
Nguo hizo zimebuniwa na mbunifu wa mavazi, Samuel Sebedayo (SAMZ) huku Rehema Samo akihusika kwenye styling.

Nyonga Nyonga ni wimbo unaotarajiwa kuwa katika albamu ya kwanza ya Chin Bees iliyopangwa kuachiwa baadaye mwaka huu.

Kuangalia video ya Nyonga Nyonga, bofya hapa: https://www.youtube.com/watch?v=-z0HGHpMEwo&feature=youtu.be
Kupakua wimbo bofya hapa: http://bit.ly/NyongaNyonga

KUHUSU CHIN BEES

Chin Bees ni rapper mwenye asili ya Arusha aliyejizolea umaarufu kwa kipaji chake si tu katika kurap, bali pia kuimba nyimbo za aina mbalimbali. Pamoja na nyimbo zake zikiwemo Pepeta, Zuzu, Pakaza, Ruba na zingine kufanya vizuri redioni na kwenye runinga, ameshirikishwa kwenye ngoma za  wasanii wakubwa wakiwemo Nick wa Pili na kushiriki kuandika nyimbo za wasanii kama Navy Kenzo na Vanessa Mdee. Yuko chini ya usimamizi wa label ya Wanene Entertainment

KUHUSU WANENE ENTERTAINMENT

Wanene Entertainment kampuni ya utayarishaji wa maudhui yenye studio za kisasa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na yenye makazi yake jijini Dar es Salaam. Imejikita katika utengenezaji wa maudhui ya sauti, video na picha kwa kutumia wataalam waliobobea katika sekta hiyo. Wanene imedhamiria kuleta mapinduzi katika burudani kwa kutayarisha bidhaa zenye kiwango cha kimataifa.

NI KARATA MUHIMU KWA SERENGETI BOYS

May 20, 2017
Serengeti Boys - Timu ya Taifa ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17, kesho Jumapili Mei 21, mwaka 2017 inarusha karata muhimu katika mchezo hitajika dhidi ya Niger kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika - AFCON u-17.
Serengeti Boys itaingia Uwanja wa Port Gentil hapa mjini Port Gentil huku mkononi ikiwa na pointi 4 ilizovuna katika michezo yake miwili ya awali kwani ilianza kupata sare tasa dhidi ya Mali Mei 15, mwaka huu kabla ya kuifunga Angola Mabao 2-1 katika mechi zilizofanyika Uwanja wa l’Amitee jijini Libreville.

Vijana wa Serengeti Boys ambao wamefikia Hoteli ya Strange Complex, wana ari ya ushindi dhidi ya vijana wenzao wa Niger ambao wana alama moja waliyoipata kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Angola walipocheza mwanzoni mwa wiki hii. Niger walipoteza mchezo wa pili dhidi ya Mali. Walifungwa mabao 2-1.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime amesema: “Huu ni mchezo muhimu wa kupata matokeo muhimu kwa vijana wetu. Tumejiandaa vema kuwania nafasi ya angalau kuingia nusu fainali.”
Shime ambaye wakati wote amekuwa akishukuru uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa namna unavyojitoa kuiandaa timu hiyo kwa kuipa kambi tulivu nchi mbalimbali, amesema: “Hili ni deni.”
Akifafanua zaidi, Shime ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi, anasema: “…Nina deni. Nadaiwa na uongozi wa TFF chini ya Jemedari Jamal Malinzi, pia nina deni kwa Watanzania ambao wamekuwa wakihaha kutuombea dua na kuichangia timu hii. 
RAIS YOWERI MUSEVENI AWASILI NCHINI TAYARI KWA KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS YOWERI MUSEVENI AWASILI NCHINI TAYARI KWA KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) JIJINI DAR ES SALAAM

May 20, 2017
muse1
Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni akilakiwa na Waziri wa NIshati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu J. K. Nyerere tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)unaofanyika leo tarehe 20/ 5/ 2017 Ikulu jijini Dar es salaam
muse2
Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni akisalimiana  na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu J. K. Nyerere tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)unaofanyika leo tarehe 20/ 5/ 2017 Ikulu jijini Dar es salaam

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA RODRICK MPOGOLO AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA JIMBO LA UBUNGO NA KIBAMBA

May 20, 2017
 Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia) akicheza muziki na Katibu Mwenezi wa Kinondoni, Mwinyimku Sangaraza, wakifurahia hotuba ya Naibu Katibu MKuu Bara baada ya kuwahutubia katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, katika Ukumbi wa CCM Manzese, wakati wa ziara yake ya kuimarisha Chama kwa kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo hilo la Ubungo jijini Dar esSalaam , jana. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, akizungumza kutoa tathmini ya usalama wa kisiasa katika Wilaya yake mbele ya mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick  Mpogolo, aliyekuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, jana. 
 Msanii ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Makurumla, Shukuru Mbundi, akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara wakati wa mkutano wa kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo jana. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Naibu  Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa, Mabalozi na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiwatambulisha Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Mabalozi wa Kata ya Manzese na kuwapa majukumu baada ya kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam.
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi (kushoto) akisebeneka na baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Manzese wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara , Rodrick Mpogolo, jana. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Kibamba, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Hoja Kata ya Salanga, jijini Dar es Salaam, jana.
 Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Salanga Jimbo la Kibamba, wakiwa bize kutunza kumbukumbu ya elimu iliyokuwa ikitolewa kwao na Naibu Katibu Mkuu jana.
 Baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Salanga wakisimama na kuimba kumpongeza Naibu Katibu Mkuu wakati wa ziara hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Salanga, Euzedius Chilipwei, wakati akiwa katika ziarayake ya kuimarisha Chama Jimbo la KIbamba jana.

BENKI YA CRDB YAWAPA SEMINA WANAHISA WAKE, JIJINI ARUSHA LEO

May 20, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha. Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo
kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano
Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
Mwenyekiti wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mwasajuni akiongoza semina hiyo
Meja kuu ikifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwa wanahisa.
Muwasilisha Mada ya iliyohusu Mambo yananoathiri Thamani na Bei za Hisa katika Soko, Laurian Malauri kutoka Orbit Securities akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada yake hiyo.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akipitia moja ya vitabu vya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo
kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo
kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Naibu Wakurugenzi  Watendaji wa Benki ya CRDB PLC,  Saugata Bandyopadhyay (kulia) na Esther Kitoka wakiteta jambo, wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Jukwaa la Dunia la Uchumi nchini Jordan

May 20, 2017



Na Othman Khamis Ame, 
OMPR, Jordan

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejenga uwezo zaidi wa kukabiliana na vitendo vya rushwa katika azma yake ya kujenga uchumi imara utakaostawisha Taifa kwa kuongeza Mapato kupitia Sekta ya Utalii sambamba na Ujenzi wa Viwanda vipya vya kudumu. 
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa la Dunia la Uchumi { world Economy Forum } wakati akiwasilisha Muelekeo wa Tanzania katika uimarishaji wa Sekta ya Utalii hapo katika Ukumbi wa Mfamle Hassan Bin Talal pembezoni mwa Bahari Nyeusi Mjini Amma Nchini Jordan. 
Balozi Seif alisema zipo jitihada za ziada zilizochukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ndani ya Sekta ya Utalii kutokana na Rasilmali nyingi zilizopo ikiwemo Mbuga za Wanyama, Ardhi yenye Rutba, Fukwe za kuvutia pamoja na Mlima wa Pili kwa urefu Duniani Kilimanjaro zilizoifanya Tanzania kujikita zaidi katika uimarishaji wa Seklta hiyo. 
Alisema Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikichukuwa juhudi mbali mbali kwa kushirikiana na Sekta na Taasisi Binafsi kuendeleza Viwanda na soko la Biashara ya Utalii lenye muelekeo mkubwa wa kutoa ajira hasa kwa Vijana wanaomaliza masomo yao ya Sekondari na Vyuo Vikuu. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza washiriki wa Warsha hiyo ya mambo ya Utalii ndani ya Jukwaa la Dunia la Uchumi Mjini Amman Jordan kwamba Tanzania tayari imeimarika katika kukabiliana na matukio ya Kigaidi ili kutoa nafasi kwa Wawekezaji wa Kimataifa kutumia fursa zilizopo Tanzania katika kuwekeza miradi yao hasa ile ya Utalii.
 Alieleza kwamba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa inaendelea kuwa kisiwa cha Amani ndani ya Mwambao wa Afrika Mashariki na Ukanda wa Kusini ya Afrika ya Jangwa la Sahara kutokana na ushiriki wake uliojaa nidhamu katika ulinzi wa maeneo hayo. 
 Alisema kutoka na hali hiyo ya amani na utulivu iliyopo Nchini Tanzania Makusanyo ya mapato kupitia sekta ya Utalii yanakadiriwa kufikia Shilingi Bilioni 1.6 licha ya kukumbwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia Nchi pamoja na kutumia Teknolojia ya Habari katika kuutangaza Utalii nje ya Nchi. Akifafanua Sekta ya Utalii kwa upande wa Visiwa vya Zanzibar Balozi Seif alisema Sekta hiyo ambayo kwa sasa imechukuwa nafasi ya Tatu katika Uchumi wa Dunia imekuwa tegemeo kubwa la Uchumi wa Zanzibar. 
Balozi Seif alifahamisha kwamba tokea kuimarishwa kwa fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Utalii Zanzibar mwanzoni mwa Miaka ya 80 zipo fursa nyingi za ajira zinazokadiriwa kufikia Laki 376,000 rasmi na zile zisizo rasmi na kuleta faraja kwa Wananchi walio wengi. 
Alisema Lengo la Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo ni kufikia fursa za ajira zipatazo Laki 500,000 hadi ifikapo mwaka 2020. Balozi Seif alieleza bila ya shaka kwamba Utalii kwa sasa imekuwa Sekta muhimu katika ukuaji wa Uchumi Kidunia uliopanda na kufikia kiwango cha asilimia 9% kinachokisiwa kugharimu Dola za Kimarekani Trilioni 1.3 katika bidhaa zinazosafirishwa kutokana na Sekta hiyo. 
Alisema rikodi ya Bara la Afrika ya Watalii Milioni 14.8 ndani ya Mwaka 2000 imeongezeka hadi kufikia Milioni 68 kwa Mwaka 2015 ikifikia asilimia 62% ya idadi ya wageni wa nje wanaoingia Bara hilo walioibua ajira zipatazo 25,000,000 sawa na asilimia 7.1% ya ajira zilizoibuka ndani ya Bara hilo. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliipongeza Jordan chini ya Kiongozi wake Mfalme Abulla wa Pili kwa uamuzi wake wa kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi . 
Jordan imekuwa mwenyeji wa Jukwaa la Dunia la Uchumi { World Economy Forum } kwa takriban mara Tisa sasa na 16 kwa Kanda na Mashariki ya Kati ya Kaskazini mwa Afrika Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum - WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland likilenga kusaidia kuepuka vita sambamba na kupunguza wimbi la Wakimbizi katika eneo la Mashariki na Kati na Kaskazini ya Bara la Afrika.