RAIS KIKWETE AWAPA POLE WAATHIRIKA WA MVUA YA MAWE KAHAMA

RAIS KIKWETE AWAPA POLE WAATHIRIKA WA MVUA YA MAWE KAHAMA

March 13, 2015

1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Benson Mpesya juu ya madhara makubwa ya mali na maisha ya watu wakati wa ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
56
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya makazi ya dharura kwa  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
8 9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole waalimu wa shule ya msingi ya Mwakata, wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambao pia ni waathirika wa  mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi baada ya kutembelea na kuzifariji  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
11 12 13
……………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12, 2015, amefanya ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane mchana baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi na kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea familia ambazo zimepata madhara makubwa zaidi kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha saa moja tu kuanzia saa nne usiku Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana na upepo mkali na mawe. Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657 zikabomolewa ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa huduma za dharura za chakula, sehemu za kulala, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kwa binadamu. Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali N. Lufunga, Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha Maghuhumwa, nyumbani kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye alipoteza watoto watano katika maafa hayo. Rais Kikwete ametoa pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokuwepo kwenye msiba. Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani pamoja na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais Kikwete jinsi nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao walipokuwa wamelala zilivyoanguka na mama huyo akalazimika kukimbilia nje kwa nia ya kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa na kupoteza maisha. “Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi kile katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha kwa muda mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa. Jameni tusaidie kwa sababu tumekwazika,”Bwana Maburi amemwambia Rais Kikwete. Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana Zacharia Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne katika maafa hayo ya mwanzoni mwa mwezi huu. Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea na kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo yamejengwa kwa msaada wa Serikali. Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembelea eneo la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya Mwakata, ambako walimu hao wamehifadhiwa katika fremu za maduka kutokana na athari za maafa hayo. Rais Kikwete amewapa pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko pamoja. Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea katika maeneo yenu ya makazi ya kawaida.” Rais Kikwete ataondoka kesho, Ijumaa, Machi 13, 2015, kurejea Dar es Salaam baada ya ziara hiyo maalum ya siku mbili katika Mkoa wa Shinyanga.
………………………..
Imetolewa na; Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 12 Machi, 2015

CHRISTIAN BELLA KUTUMBUIZA USIKU WA NANI KAMA MAMA KESHO HARBOURS CLUB

March 13, 2015
MSANII mahiri wa Mziki wa Dansi hapa nchini kutoka kundi la Malaika Band, Christian Bella (kulia)anatarajiwa kutumbiza katika onyesho la Usiku wa Nani Kama Mama litakalofanyika Machi 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Harbours Club jijini Tanga.

Akizungumza LEO,Mratibu wa Onyesho hilo,Mbwana Imamu ambaye ni Mkurugenzi wa Arbab Intertainment alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika kwa asilimia kubwa ambapo msanii huyo atatua mkoani hapa siku moja kabla.

Alisema kuwa onyesho hilo litakuwa ni maalumu kuwapa raha wakazi wa jiji la Tanga ambao walikuwa wameikosa kutoka kwa msaani huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa “Nani Kama Mama” na nyengine nyingi.

  “Unajua wakazi wa jiji la Tanga ni watu wa burudani hivyo uwepo wa Bella kwenye onyesho hili utawapa ladha mashabiki wake kutokana maeneo mbalimbali hivyo hawapaswi kuikosa badala yake wajitokeze kwa wingi “Alisema Mbwana.

Aidha mratibu huyo alisema kuwa baada ya kumalizika onyesho hilo wapenzi na mashabiki ambao watakuwa wamejitokeza watahamishia shangwe kwenye ukumbi wa Club Lacasachika.

  “Hii itakuwa ni baada ya kumalizika kwa party …. Wapenzi wa mziki huo watatumia nafasi hiyo kubadilishana mawazo na kutafakari namna onyesho hilo lilivyokwenda kwa kuendelea kupata burudani kwenye Club hiyo “Alisema Mratibu huyo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI SHARM EL SHEIKH KUHUDHURIA MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU MAENDELE NA UCHUMI WA NCHI YA CAIRO MISRI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI SHARM EL SHEIKH KUHUDHURIA MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU MAENDELE NA UCHUMI WA NCHI YA CAIRO MISRI

March 13, 2015


1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri.
Picha zote na OMR
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, jana kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri
………………………………………………………….
Mhe. Makamu wa Rais aliwasili jana na kupokelewa na mwenyeji wake.  Akifafanua kuhusu mkutano huo Dkt Bila alisema kuwa ‘’Misri ni wadau wetu katika maendeleo,  uhusiano kuwa mkutano huu utafungua fursa zaidi za uwekezaji baina ya nchi zetu. Mkutano huo wa siku tatu utafunguliwa baadaye leo na Rais wa Misri Abdel Fahah  Sisi, na kuhudhuriwa na baadhi ya wageni mashuhuri kutoka Mataifa mbalimbali akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry.

NI MAFANIKIO KUWA NA ASKARI WANAWAKE KATIKA ULINZI WA AMANI UN-MHE SIMBA

March 13, 2015

Katika picha hii ya maktaba anaoneka Mhe. Asha-Rose Migiro ( Mb) wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na baadhi ya askari wanawake kutoka JWTZ wanaoshiriki katika operesheni ya kulinda amani kupitia Umoja wa Mataifa huko Lebanon. Katika mchango wake, Mhe. Simba pamoja na mafanikio mengine ambayo Tanzania imeyapata katika miaka 20 tangu mkutano wa Beijing ni pamoja na askari wanawake kupata fursa za kushiriki katika operesheni za kulinza amani zinazoratibiwa na Umoja wa Mataifa.
Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akizungumza (alhamisi) katika majadiliano ya jumla katika mkutano wa Kamisheni 59 kuhusu Hadhi ya Wanawake. Mhe. Waziri anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwamo wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Tanzania ni kati ya nchi 13 zinazoiwakilisha Afrika katika Kamisheni hii inayoundwa na nchi 45.
Sehemu ya ujumbe wa Mawaziri kutoka nchi za Afrika wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nchi za Afrika.
Pamoja na kuzungumza katika majadiliano ya jumla, Mhe Waziri Sophia Simba pia alipata fursa ya kuhushiriki Mkutano wa Mawaziri kutoka Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afrika karibu na UN. Mkutano huo ulikuwa wa kujadiliana na kupitisha maazimio mbalimbali kuhusu maudhui ya mwongo wa wanawake wa Afrika. Pichani Mhe. Waziri akiwa na Katibu Mkuu wake Bi. Anna Maembe wakifuatilia majadililano hayo.

Na Mwandishi Maalum, New  York

Ushiriki wa askari wanawake   katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za  Umoja wa Mataifa,  ni baadhi ya  mafanikio ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia miaka 20 baada ya Mkutano wa Kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na  Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema hayo  leo ( alhamis) wakati alipokuwa akitoa tathmini na changamoto za utekelezaji wa  maazimio muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo wa  wanawake Beijing. 

Mhe. Waziri Simba, anaongoza ujumbe wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  katika Mkutano wa Hadhi ya Wanawake ( CSW) unaoendelea hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  katika Ujumbe huo  wa Tanzania unajumuisha na washiriki kutoka  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwamo  Mhe. Zainab Omar Mohammed,  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, vijana, wanawake na watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 

“ Katika miaka  miaka  20 iliyopita, yapo  mambo mengi ambayo Tanzania tumepiga hatua za kuridhisha, katika maeneo ya uwezeshwaji  na fursa sawa kwa wanawake. Katiba za pande zote mbili za Muungano  zinaainisha vema kuhusu hadhi ya mwanamke. Na   Katika  katiba mpya inayopendekezwa  hivi sasa  kuna   eneo  ambalo linazungumzia kwa kina Usawa wa Jinsia na Uwezeshwaji wa wanawake.” anasema Waziri Simba.

Vile vile ameeleza  baadhi ya sheria  ambazo ama zimefanyiwa marejeo au kutungwa kwa lengo la kuboresha usawa wa kijinsia. Amezitaja baadhi ya  sheria hizo kuwa ni sheria zinazohusu watoto,  sheria zinazohusu usafirishaji wa binadamu,  sheria ya ardhi, HIV/AIDS na sheria ya makosa ya kujamiana.

 Kuanzishwa kwa dawati la jinsia na watoto katika vituo vya Polisi,  vituo  vya kuhifadhi  watoto,  vituo kwaajili ya  wanawake wanaofanyiwa ukatili na mtandao wa viongozi wa madhehebu ya dini kuhusu ukatili dhidi ya wanawake. Ni baadhi ya mafanikio ambayo yameelezewa na Mhe. Waziri.

Ameeleza  zaidi kwa kusema, Wanawake wengi sasa wanashiriki katika siasa ambapo  kwa mfano  asilimia 36 ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ni wanawake na   kwa upande wa Zanzibar asilimia 33 ya  Wawakilishi ni wanawake. Na  kwamba  kumekuwapo  pia ongezeko  la idadi ya  wanawake Majaji na Mahakimu na wanaoshika nafasi za uongozi.

Mhe. Simba amewaeleza wajumbe wanaoshiriki  mkutano huo  kwamba katika kuhakikisha  panakuwa na fursa sawa  katika  ajira  utumishi wa Umma,   kuna  kifungu   katika sheria za utumishi wa umma vinavyoainisha kwamba  pale  mwanamke na mwanaume wanapokuwa na sifa zinazolingana, basi mwanamke atafikiriwa kwanza.

Kwa upande wa elimu,  pamoja na  kuwa na  uwiano sawa kati ya wavulana na wasichana katika shule za msingi. Anasema elimu ya  msingi inatolewa bure katika shule za serikali   na kwamba utaratibu huo pia utafanyika katika  shule za  sekondari  za umma. Aidha  ameelezea ongezeko la wanafunzi wa kike wanaochukua masomo ya sayansi.

Kwa upande wa Afya,  Mhe. Waziri amesema  Tanzania imepiga hatua za kuridhidha katika upunguzaji wa  vifo vya wanawake wajawazitio na vya watoto wachanga.

Hata hivyo pamoja na  mafanikio  hayo na mengine mengi ambayo  Tanzania inajivunia kuhusu hadhi ya wanawake na watoto wa kike,  anasema kama ilivyo kwa mataifa mengi yanayoendelea, Tanzania pia bado inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo  za uhaba wa fedha kwa miradi inayohusu masuala  ya jinsia,  ndoa na mimba za utotoni,  umaskini wa kaya na ukatili dhidi ya wanawake.


Mhe. Waziri Simba, Tanzania imejifunza kutokana na changamoto hizo na nyinginezo na kwamba imejipanga vema kutekeleza baadhi  ya changamoto hizo  hususani  upunguzaji wa umaskini,  kupitia malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya  2015.

WAZIRI WA AFYA DR.SEIF RASHID MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA UTEPE MWEUPE TANGA.

March 13, 2015

NA MWANDSHI WETU,TANGA

Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya utepe mweupe.


WAZIRI WA AFYA NCHINI,DR.SEIF RASHID
MKUU WA MKOA WA TANGA,SAID MAGALULA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO HAYO

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanafanyika mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano.
 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Magalula Said Magalula wakati akiongea na waandishi wa habari hapo jana.
 

   

WAANDISHI WA HABARI WAKIWAJIBIKA,KUSHOTO NI AMINA OMARI KUTOKA GAZETI LA MTANZANIA,


Alisema kuwa maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na upimaji wa hiari wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti.
 

Aliongeza kuwa pia siku hiyo wananchi wa Tanga watapata fursa ya kuchangia damu kwa ajili ya kutumika kwenye vituo vya afya mkoani hapo.


"Niwaombe wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi katika kilele cha maadhimisho hayo"alisisitiza Magalula
 WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA NA MKEWE WAWASILI JAPAN

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA NA MKEWE WAWASILI JAPAN

March 13, 2015


1
Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kushoto) akizungumza ujumbe kutoka  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Women’s Federation for World Peace  la Umoja wa Mataifa (WFWP) kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo  Mchi 13, 2015 ambako amefuatana Mheshimiwa Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Jakaya Kiwete kwenye mkutano kuhusu namna ya kushughulikia maafa unaotarajiwa kufanyika Sendai Machi 14, 2015.  Kutoka kushoto ni Chieko Sasamoto na  Yoko Shima
2
Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kushoto) akizungumza ujumbe kutoka  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Women’s Federation for WOrld Peace  la Umoja wa Mataifa (WFWP) kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo  Mchi 13, 2015 ambako amefuatana Mheshimiwa Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Jakaya Kiwete kwenye mkutano kuhusu namna ya kushughulikia maafa unaotarajiwa kufanyika Sendai Machi 14, 2015.  Kutoka kushoto ni Chieko Sasamoto, Yoko Shima na Mutsako Setomoto.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana  na Balozi Mteule wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. mashiro Yoshida kwenye Hoteli ya New Otani jijini Tokyo  Machi 13, 2015 ambako Machi 14, 2015 anatarajiwa kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano Kuhusu namna ya kukabiana na maafa  utakaofanyika Sendai.
4
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi Mteule wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. Masahiro Yoshida kwenye Hoteli ya New Otani jijini Tokyo  Machi 13, 2015 ambako Machi 14, 2015 anatarajiwa kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano Kuhusu namna ya kukabiliana na maafa utakaofanyika Sendai.
5
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa katika picha ya pamoja  ujumbe kutoka  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Women’s Federation for World Peace  la Umoja wa Mataifa (WFWP) kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo  Mchi 13, 2015 ambako amefuatana na  Mheshimiwa Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Jakaya Kiwete kwenye mkutano kuhusu namna ya kushughulikia maafa unaotarajiwa kufanyika Sendai Machi 14, 2015.  Kutoka kushoto ni  Mutsako Setomoto,   Chieko Sasamoto, Yoko Shima na Kazunori Arase.
7
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  na Balozi Mteule wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. Masahiro Yoshida (kushoto) kwenye Hoteli ya New Otani jijini Tokyo  Machi 13, 2015 ambako Machi 14, 2015 anatarajiwa kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano Kuhusu namna ya kukabiliana na maafa utakaofanyika Sendai. Watatu kushoto ni mkewe Tunu , Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed na Kulia ni Naibu Waziri wa mambo ya Nje, Dr. Mahadh Maalim.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KINANA AWASILI MONDULI

March 13, 2015


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Monduli tayari kwa ziara ya siku moja jimboni humo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo laMonduli,Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Monduli tayari kwa ziara ya siku moja jimboni humo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea salaam kutoka kwa Chipukizi wa CCM wakati wa mapokezi Makuyuni, Monduli Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi na wananchi wa Monduli.

RAIS KIKWETE AFARIJI WALIOPATWA NA MAAFA YA MVUA YA MAWE,KAHAMA JANA

RAIS KIKWETE AFARIJI WALIOPATWA NA MAAFA YA MVUA YA MAWE,KAHAMA JANA

March 13, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015. jkm2  
Maelefu ya Wakazi wa Kahama wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia mara baada ya kutembelea na kujionea athari ya Mvua ya Mawe kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015.

RC MAGALULA AONGOZA KIKAO CHA PILI CHA BODI YA BARABARA MKOA WA TANGA JANA

March 13, 2015
MKUU WA MKOA WA TANGA,SAID MAGALULA AKIFUNGUA KIKAO CHA PILI CHA BODI YA BARABARA JANA AMBAPO ALISISITIZA UMUHIMU WA UTUNZAJI WA BARABARA ZINAZOJENGWA KWENYE MAENEO MBALIMBALI ILI ZIWEZE KUWA ENDELEVU.

MENEJA WA WAKALA WA BARABARA MKOA WA TANGA(TANROAD),AFRED NDUMBARO AKIFUATILIA MAONI YA WAJUMBE WA KIKAO HICHO
MKUU WA WILAYA YA HANDENI,HUSNA RAJABU AKIWA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO DILIWA WAKIFUATILIA HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA.
MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA AKIFUATILIA MAKABRSHA YA KIKAO HICHO JANA KABLA YA KUANZA KIKAO CHA PILI CHA BODI YA BARABARA
MKUU WA WILAYA YA PANGANI,REGINA REGNALD CHONJO.
MKUU WA WILAYA YA KILINDI,SULEIMANI LIWOWA KATIKATI AKIFUATILIA KIKAO HICHO KULIA NI MKUU WA WILAYA YA MKINGA,MBONI MGAZA
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA, ESTERINA JULIO KILAS KUSHOTO NA MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO,MARIAM JUMAA WAKIFUATILIA MAKABRASHA YA KIKAO HICHO JANA

WAZIRI WA AFYA DR.SEIF RASHID MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA UTEPE MWEUPE TANGA.

March 13, 2015
WAZIRI WA AFYA NCHINI,DR.SEIF RASHID
MKUU WA MKOA WA TANGA,SAID MAGALULA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO HAYO

WAANDISHI WA HABARI WAKIWAJIBIKA,KUSHOTO NI AMINA OMARI KUTOKA GAZETI LA MTANZANIA,