MKUTANO MKUBWA WA KITAIFA WA KUMUOMBEA RAIS NA TAIFA KWA UJUMLA KUFANYIKA AGOSTI 25 CHATO MKOANI GEITA

August 18, 2016



Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Dk.Charles Gadi (wa tatu kushoto), akiongoza maombi baada ya kuzungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano mkubwa wa maombi ya kitaifa wa kumuombea Rais Dk.John Magufuli na Serikali, utakaofanyika Agosti 25 Chato mkoani Geita. Kutoka kushoto ni Wachungaji Denis Kimbilo, Leons Kajuna, Palemo Massawe, Andrew Thomas na Denis Komba.


Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI wa Good News for All Ministry  wameandaa mkutano mkubwa wa kitaifa wa maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli na Taifa kwa ujumba maombi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 25 Chato mkoani Geita.

Katika hatua nyingine viongozi hao wamesema wanaunga mkono azma ya Rais Magufuli ya kuhamishia serikali Dodoma kwani ni jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu, hivyo wameandaa mpango wa kumuombea kwa siku 1001 sawa na miaka mitatu ili afanikiwe.

Wakizungumza Dar es Salaam leo asubuhi  viongozi hao kutoka Good News for All Ministry walisema uamuzi wakuanzisha mchakato wa kuhamisha serikalini jambo la kijasiri na unapaswa kuungwa mkono na watanzania wote kwani ni maono ya Baba wa taifa Julius Nyerere.

Askofu Dk. Charles Gadi alisema tangu Baba wataifa kutangaza azma hiyo serikali zilizotangulia zimefanya jitihada mbalimbali za kuimarisha mji wa Dodoma ili uweze kutumika kama mji mkuu na sasa umefika wakati muhafaka.

“Sisi kama viongozi wa dini tupo nyuma yake na tunaongeza nguvu zetu natunatoa wito kwa watu  wotewaserikali kuhamia Dodoma, kwani jambo hili litaharakisha maendeleo katika mikoa ya pembezoni,” alisema.

AidhaAskofu huyo  alishangazwa na uvumi kuwa endepo baadhi ya watendaji waserikali wakihamia Dodoma kutakwepo na migogoro katika ndoa nyingi kutokana na kutengana kwa baadhi ya familia.

Alisema ni vyema watu wakaheshimu maadili na kuishika misingi, kwani kusafiri hakukufanyi ‘ukachepuka’.

“Hata ukiwa hapa Dar es Salaam unaweza kuchepuka tu,silazimaiwe Dodoma, mambo yaliyowazi ni yetu ila ya liyofichwa ni ya Mungu,” alisema.

Mchungaji Leons Kajuna alisema RaisMagufuli hastishike na kelele za watu zinazobeza azma  yake kwani kawaida ya watu kupinga jambo linaloanzishwa kabla hawajaona mafanikio yake.
“Si wakati tena wakukaa na kunung’unika kuna vitu serikali ikishaamua ni kuvipokea kwa shukurani, 
kwani kufanya hivyo niishara ya nidhamu,” alisema.

Askofu Dk. Charles Gadi alisema mpango waliyo  uanzisha wakumuombea  Rais kwa siku 1001 utaanzia katika mkoa wa Geita  wilayaniChato na   unatarajiwa kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa huo.


“Tutamuombea Rais katika uongozi wake kuwepo na mvua
za kutosha kwani uwepo wa mvua niishara uongozi umekubalika, nauwepowamvuautaondoanjaanamgawowaumeme,” alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WAKADIRIAJI MAJENZI AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

August 18, 2016
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
 Rais wa  Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
 Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
                                                               .......................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi  Tanga, Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.
Amesema serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.
 

SBL yatangaza kudhamini elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

August 18, 2016
Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha ( kulia)   akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) Wakati wa kutangaza mpango kampuni hiyo wa kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha.Pembeni yake ni Meneja wa Miradi ya Jamii wa SBL Hawa Ladha katika mkutano uliofanyika mapema leo katika ofisi za SBL,Temeke  jijini Dar es salaam.

Meneja wa Miradi ya Jamii Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza mpango wa kampuni hiyo kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha,kulia kwake ni Mkurungezi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za SBL zilizopo Temeke Jijini Dar es salaam.

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo mapema leo asubuhi katika ofisi za SBL zilizopo Temeke jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, Agosti 18, 2016 - Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa mara nyingine imetangaza mpango wa kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha.

Huu ni mwaka wa sita mfululizo ambapo SBL  inatoa msaada kwa wanafunzi wa ndani  wanaochukua  kozi za shahada katika vyuo vikuu vya Tanzania  chini ya programu ya kampuni ijulikanayo kama “Skills for Life”. Jumla ya wanafunzi 31wa Tanzania tayari wameshanufaika na  mpango huu ambao ni sehemu ya Mfuko wa Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL Foundation).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha fomu za maombi kwa ajili ya udhamini zinapatikana katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza au kupitia tovuti ya www.eablfoundation.com.

Wanyancha amesema mpango huo uko wazi kwa wanafunzi kutoka nchi nzima ya Tanzania ambao ambao tayari wamepata usajili wa kujiunga na vyuo vikuu nchini katika fani za Biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Uhandisi  na Sayansi ya Chakula katika ngazi ya shahada kutoka vyuo vikuu hapa nchini.

Mfuko wa EABL ulianza  kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi kuanzia wanaojiunga na vyuo vikuu mwaka 2005 ambapo hadi sasa zaidi ya wanafunzi 238 wamenufaika kwa mpango huo wakiwemo 31 kutoka Tanzania. Wengi walionufaika tayari walishamaliza masomo yao  na wanafanyakazi katika makampuni mbalimbali  katika ukanda huo. Mpango huu upo katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mfuko wa EABL umetumia jumla ya zaidi ya Tshs billion 5 kuugharamia tangu mwaka wa 2005.  

Udhamini huu hugharamia ada ya masomo, vitabu, malazi, fedha za kujikimu na programu za ushauri kwa waombaji watakaofanikiwa.
“Lengo letu kuu kupitia mpango huu ni kuwawezesha waombaji  kutimiza ndoto zao maisha,” alisema Wanyancha na kuongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kupokea maombi  ni Septemba 20, 2016.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini kuchangamkia fursa hiyo ili kwa kutuma maombi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ujao.

MAHITAJI MUHIMU:  Fomu za maombi zilizojazwa vizuri  zikiwa zimeambatanishwa na  barua ya usajili kutoka kwa taasisi ya  elimu ya juu, udhibitisho wa hitaji la kifedha na nakala za vyeti vya elimu ya sekondari kidato cha nne na cha sita.
Wanafunzi ambao bado hawajapokea barua za kusajiliwa kujiunga na vyuo vikuu na ambao wanakidhi masharti pia wanaweza kutuma maombi.

photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.t

BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUISAIDIA SEKTA YA MAJI NCHINI

August 18, 2016
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua  kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam.
KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO). 

Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi. 

Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.

Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji alisema Bi. Bird

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.

Changamoto ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo alisema Mhandisi Luhemeja.

Benki ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo, pamoja na Uchumi na Biashara.


RAIS MAGUFULI ATEUA MRISHO GAMBO KUWA MKUU MPYA WA MKOA ARUSHA

RAIS MAGUFULI ATEUA MRISHO GAMBO KUWA MKUU MPYA WA MKOA ARUSHA

August 18, 2016

index 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI.

August 18, 2016
 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia)  na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale.
Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.
Fursa ya ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata Madawati hayo.
Lakini pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.



Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
 
Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi maeneo mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 200.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya kilimo.

“Tunashukuru sana msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia kipato kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda mwingi huwa tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi nyingi sana za kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine watano kuweza kunisaidia kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza madawati kwa gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas Mbua mkazi wa kata ya Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

“Sisi wapiga msasa tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5 hii si haba, kiasi hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao mwaka huu kwa hiyo pesa niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa imebadili kabisa hali halisi nyumbani, nimenunua gunia za mahindi, maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi kusema uongo” anasema Maige Deus mkazi wa Kahama.

“Ninaiomba sana serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee kuchapa kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa nzima tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki kiwanda naunganisha mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili ya wanafunzi.” Anasema Abdul Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha Zacharia and Deus Timber Supply cha Nyang’wale mkoani Geita.

Halikadharika mama nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya wateja katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa tunapika kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi kutokana uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa tenda kabisa ya kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa vizuri na kwa muda, naomba miradi kama hii iendelee tu hadi madawati yatoshe na sisi mitaji itakuwa imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo Nyang’wale kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida mara mbili kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana kwa wadau wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya wilaya kutengeneza madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine imetupa tenda na madawati mia mbili, bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo. Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.

Mashindano ya Tigo Fiesta Super Nyota yafana Jijini Mwanza

August 18, 2016
Msanii pekee wa kike aliyeingia Fainali ya Tigo Fiesta Super Nyota jijini Mwanza,Yasinta akiimba wakati wa shindano hilo lililofanyika ukumbi wa Rock Bottom jijini Mwanza jana. 

Msanii mdogo kuliko wote kwenye  Tigo Fiesta Super Nyota jijini Mwanza, Aga Star akionyesha kipaji chake.






Msanii Nchama akiwania nafasi ya kushiriki fainali za Tigo Fiesta Super Nyota zitakazofanyika uwanja wa ccm Kirumba jijini mwanza jumamosi wakati wa msimu wa fiesta




Majaji wakiongozwa na Gardener G Habash(katikati) wakihesabu kura kwenye mchuano wa  Tigo Fiesta Super Nyota jijini Mwanza.



Washindi walioingia fainali ya Tigo Fiesta Super Nyota jijini Mwanza, wakiwa kwenye picha ya pamoja.



photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com W: www.koncept.co.tz