MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU CHINI YA UNESCO YAZINDULIWA CHUO KIKUU HURIA, DAR

MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU CHINI YA UNESCO YAZINDULIWA CHUO KIKUU HURIA, DAR

March 22, 2016
img class="wp-image-9423 aligncenter" src="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/03/IMG_7149.jpg" alt="Faith Shayo - Unesco, Tanzania" width="629" height="426" />
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
MAFUNZO kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo yanayohusisha walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro yamelenga kuoanisha ufundishaji na matumizi ya Tehama katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.
Programu hiyo inayotoa ushirikiano mpya kati ya China na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inafanyakazi katika mataifa manane ya kusini mwa jangwa la sahara inatekelezwa kwa lengo la kuwezesha mafanikio kwa malengo ya 2030.
Nchi zinaozhusika na mpango huo ni Tanzania Kongo ya Kinshasa (DRC), Congo, Liberia, Uganda, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Namibia.
Mpango huo ambao kwa ujumla wake , awamu ya kwanza na ya pili unachukua miaka minne umelenga kuwezesha vyuo vya walimu kutoa walimu wa kufunza wenzao kwenye stadi za kufundisha kwa kutumia Tehama.
Mradi huo unaojulikana kama UNESCO-China Funds-in-Trust (CFIT) wenye lengo la kuziba pengo la ubora wa elimu wa kuwawezesha walimu kufundisha kwa kutumia Tehama ulizinduliwa Novemba 22,2012 kwa nchi tatu za kwanza na baadae kuongezwa nchi nyingine tano kufikia nane mwaka 2013.
Mpango huo ni wa dola za Marekani milioni 8 kutoka China mahususi kwa mataifa ya Afrika kuboresha elimu kupitia Unesco.
Prof. Elifas Bisanda
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yanayoendelea katika maabara za Chuo Kikuu Huria (out) jijini Dar es salaam. Walioketi kutoka kushoto ni Basiliana Caroli Mrimi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo pamoja na Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku 10 katika Chuo Kikuu Huria, Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili alisema kwamba program hiyo imelenga kutatua chnagamoto zinazokabili elimu ili elimu iwe ileinayotakiwa kuwezesha maendeleo ya kasi katika sayansi.
Alisema ni lengo la Unesco kupitia ufadhili huo kuhakikisha kwamba kunapatikana walimu bora watakaowezesha matumizi ya Tehama katika kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu ili kutengeneza wataalamu wa baadae katika taifa hili.
Alisema kuna pengo kubwa kuhusiana na ubora wa elimu na kwamba baada ya kumaliza program ya elimu kwa wote mwaka jana nguvu sasa inastahili kuelekezwa katika ubora wa elimu ili kufikia malengo ya 2030.
Alisema changamoto kubwa ni kuleta karibu matumizi ya digitali kwa kuzingatia ukweli wa sasa kwamba matumizi yake ni madogo ukizingatia na haja kubwa inayoambatana na haja ya kuwa na elimu bora.
Alisema ni vyema kuiga mfano wa China kwamba kuna tatizo la kidunia la kielimu lakini linalohitaji suluhu ya eneo la husika kwa kuzingatia rasilimali zilizopo eneo hilo.
Gabriel El Khili - Unesco, Paris
Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili (kulia) akizungumzia madhumuni ya programu hiyo inayoratibiwa na UNESCO wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya wiki mbili kwa walimu yanayoendelea katika maabara ya Tehama Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Alisema mapinduzi ya kitamaduni ya China baada ya kujikomboa yalizingatia elimu na kwa kutumia rasilimali za nyumbani waliweza kusonga mbele na nia yao ya sasa ni kufikiri shida ya elimu na maendeleo kimataifa lakini kupata suluhu ya tatizo hilo kwa nchi husika kwa kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kuboresha elimu.
Anasema mafunzo kwa Tehama maana yake kusambaza elimu bora kwa kutumia nyenzo za Tehama zilizopo kuanzia redio televisheni, CD na kadhalika.
Alisema ni matumzi ya Unesco kwamba mafunzo yanayotolewa yatasaidia kuboresha elimu ya walimu na wanafunzi wao kwa kutumia Tehama, matumizi yake yaliyotukuka ambayo yatasaidia kuimarisha na kutoa ubora wa elimu pamoja na kuwa na walimu wachache.
Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo hayo aliwataka walimu hao kutambua umuhimu wao katika kusukuma mbele lengo la mafunzo hayo na wala si kujipatia cheti cha mahudhurio.
Prof. Ralph Masenge
Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo katika hafla fupi ya ufunguzi.
Alisema ulimwengu wa sasa ni wa walimu kutoa mwongozo wa namna ya kujifunza kwa kumuelekeza mwanafunzi kwa kuwa ulimwengu wa digitali umerahisisha mambo mengi.
Alisema wasishangae wakigundua kwamba wanafunzi wao ni weledi zaidi kuliko wao ila wasaidie kuhakikisha kwamba Tehama inatoa nafasi ya wanafunzi wengi kujifunza na kupata elimu wanayohitaji katika kubadili maisha na uchumi katika jamii.
Alisema kwamba ni matumaini yake kwamba kwa mafunzo hayo elimu ya Tanzania itapaa hasa kutokana na ukweli kuwa China imesema wazi kuwa haitapenda Tanzania kushindwa katika mradi huu wa kuleta maboresho makubwa katika elimu ya Tanzania ili iweze kutumika kutengeneza maarifa.
Profesa Bisanda alisema kwamba kwa sasa Tanzania ina shida kubwa katika masomo ya sayansi (bayolijia,kemia na fizikia ) pamoja na hesabu na kwamba uwapo wa program hiyo kutasaidia kufikisha mafunzo kwa wanafunzi kwa namna bora na yenye uhakika zaidi hata kama walimu wapo wachache.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Pichani juu na chini walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro wakishiriki mafunzo ya matumizi ya Tehama kwa vitendo katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.
Alisema ni vyema walimu wakajifunza namna ya kufanya na kutafuta majawabu ya matatizo kwa kutumia tehama na kuambukiza mwenendo huo kwa wenzao na kwa wanafunzi.
Alisema ni kweli kuwa Tanzania ipo gizani katika ICT kutokana na matumizi yake madogo na hivyo walimu wakielewa na kuwafunza wengine taifa hili litaondoka katika giza hilo na kupata mapinduzi makubwa ya fikira na elimu.
Aidha alisema kwa kutumia ICT wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji hasa katika masomo na mafunzo.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Alitolea mfano kwamba kama wakipata softwea ya mitihani ambayo ipo wanaweza kuokoa zaidi ya shilingi milioni 700 wanazotumia kwa ajili ya mitihani na michakato yake.
“Fikiria unaweka program ambayo mwanafunzi anafanya mitihani moja kwa moja na hii inawezekana, utafanya nini na fedha hizo ambazo unazitumia sasa kwa ajili ya uandazi wa mitihani kuifanya na kuisahihisha” aliuliza na kusema kwamba zingelisaidia vitu vingine.
Alisema kihistoria walikuwa wanakazi kubwa ya kuandaa mitihani na kusambaza lakini mwanzo wa kuwafanya wanafunzi wajieleze kama wanataka kufanya mitihani kwa kutumia Tehama sasa wanatengeneza mitihani kwa kadiri ya maombi na kupunguza gharama.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Picha ya pamoja ya wakufunzi na washiriki.
Faith Shayo - Unesco, Dar es Salaam
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kushoto), Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.

RC DAR ES SALAAM APOKEA MSAADA WA MADAWATI 500 KUTOKA TIGO KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI

March 22, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez mara baada ya kuwasili Shule ya Msingi ya Kawawa iliyopo Manispaa ya Kinondoni kupokea msaada wa madawati 500 kutoka Kampuni ya Simu ya Tigo Dar es Salaam leo asubuhi.
RC Makonda akisalimiana na wafanyakazi wa Tigo.
Ofisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea madawati hayo.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupokea msaada huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza katika hafla hiyo wakati akipokea msaada huo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawawa wakipiga makofi wakati wa kupokea msaada huo.
Wanahabari nao walikuwepo kuchukua taarifa hiyo.
Viongozi na wafanyakazi wa Tigo wakifuatilia kwa karibu hafla hiyo.
Hapa ni furaha tupu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez na Mkurugenzi wa Kanda ya Pwani wa Tigo, Gooluck Charles wakiwa wamekaa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kawawa baada ya kampuni hiyo kuisaidia shule hiyo madawati 50 Dar es Salaamleo asubuhi. Tigo imetoa madawati kwa shule 10 za Manispaa ya Kinondoni ili kuunga mkono jitihada za Makonda za kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kupata elimu.
Mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Joseph Proches akitoa neno la shukurani kwa Tigo kwa kuwapatia msaada huo wa madawati.
Walimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati hayo.
Wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati hayo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya sh.milioni 82.5 kwenye shule 10 za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kusema utawasaidia wanafunzi kupata elimu bora wakiwa katika mazingira mazuri hivyo aliwataka wanafunzi hao kuongeza bidii ya masomo yao. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Tigo yatoa msaada wa madawati 500 kwa shule za msingi Dar

March 22, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia wananchi na wanafunzi katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda(kulia) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (wa pili kulia),wakiwa wameketi kwenye moja ya madawati 500 yalikabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha  ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles (wa tatu kulia)na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Dkt. Aziz Msuya(kushoto). Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
 Mwanafunzi Saidat Proches akishukuru mara baada ya makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akiongea na walimu na wananchi mara baada  makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam

Sherehe ya makabidhiano ilifanyika leo shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga


Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam

Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Wanafunzi wa shule ya msingi kawawa wakishuhudia makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga




Machi 22 2016 Dar es Salaam: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo katika kata ya Mabibo katika manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Gutierrez.

Gutierrez amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye alisema madawati hayo 500 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Dar es Salaam. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 500 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Makonda.



STARTIMES YAKABIDHI MINI PADS 180 KWA WAZIRI NAPE NNAUYE KURAHISISHA UTAFITI WIZARANI

March 22, 2016
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) akipokea moja ya Mini Pads 180 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (wa kwanza kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Wakishuhudia tukio hilo wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel  (kulia).
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akifurahia kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa, Elisante Ole Gabriel na wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na muwakilishi kutoka ubalozini Bw. Mr Gao Wei.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akiteta jambo baada ya kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Pamoja naye kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dr. Lu Youqing.


Na Dotto Mwaibale

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye amepokea Mini Pads za kisasa 180 zenye thamani takribani milioni 90 kutoka kwa kampuni StarTimes Tanzania kwa ajili ya kuwarahisishia kazi wafanyakazi wa wizara yake.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo ndani ya jingo la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mh. Nnauye amebainisha kuwa Mini Pads hizo zitarahisisha kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wa wizara yake kuendana na kasi ya ukuaji wa TEHAMA katika kufanya shughuli zao hususani tafiti.

“Wizara yetu inashughulika na Sekta Nne Kubwa. Nazo ni; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Sekta hizi ndizo zinazokamilisha jina la Wizara yetu. Wizara yangu inashirikiana na Wizara, Taasisi na wadau mbalimbali katika kuletea maendeleo wahusika katika sekta tajwa. Katika Nchi yetu tunazo Halmashauri zaidi ya 170 ambazo kimsingi kila Halmashauri inapaswa kuwa na Ofisa mmoja kwenye kila sekta zetu, hivyo maafisa 4 kwa ajili ya sekta Nne. 

Kimuundo tunakuwa na Afisa mmoja wa kila sekta kwenye kila Mkoa hivyo maafisa 4 kwenye kila Mkoa wa ngazi ya Mkoa.” Alisema Mh. Nnauye

“Baada ya kutafakari kwa kina, tukaona tuanze na kuboresha mawasiliano kwa maafisa wetu ndani ya Wizara, Baadhi ya Mikoa na pia Halmashauri. Tunaamini kwamba mawasiliano madhubuti yakiwepo, itakuwa rahisi kufanya ufuatiliaji wa kina na kuboresha utendaji. Kwa kutambua kwamba kuna haja ya kushirikisha wadau mbali mbali tuliwasiliana pia na kampuni ya Star Times ambayo ni mbia wa TBC kwa ajili ya kutusaidia wanaloweza kwa ajili ya kuanza uboreshaji wa vitendea kazi vya mawasiliano katika sekta zetu.” Aliongezea

“Ni faraja kubwa kuona kwamba wenzetu wa Sar Times wametuelewa haraka na kukubali kutusaidia vifaa hivi vya mawasiliano (Mini Pads) zipatazo 180. Kwa hakika vitatusaidia sana kuboresha utendaji kimawasiliano kwa maafisa wetu wa Wizara na pia Maafisa mawasiliano ambao ni wadau wa kutoa taarifa kwa umma,” alisema na kuhitimisha Mheshimiwa Nnauye, “Ifahamike kwamba kwa jinsi dunia inavyobadilika kwa kasi kubwa sana, masuala ya mawasiliano sio hiari tena bali ni lazima kuwa na mawasiliano ya kimkakati. 

Mpango wetu ni kwamba maafisa wote ambao wanafanya kazi kwneye Halmashauri zote, wapate mawasiliano japo hatua kwa hatua kwenye sekta zote Nne. Tunawashukuru sana kampuni ya Star Times kwa msaada huu mzuri wa kuanzia.”

Kwa  upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao alisema kuwa imekuwa ni fursa kubwa kwa kampuni kuweza kufanikisha watanzania wanatumia vifaa vinavyoendana na kasi ya maendeleo ya tekinolojia duniani kurahisisha kazi.

“Naweza kusema ni fursa ya kipekee kwa Mheshimiwa Waziri kutuona sisi StarTimes kuwa tungeweza kuwatatulia changamoto waliyokuwa nayo kwani zipo kampuni na taasisi nyingi ambazo zingeweza kufanya hivyo. Hili naweza kusema limechangiwa kwa kiasi kikubwa na jitihada tulizonazo katika kuwatumikia watanzania kwa kuwapatia huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali. 

Kwa kiasi kikubwa shughuli zetu tunazozifanya huwezi kuzitenganisha na maendeleo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano. Ninaamini kupitia Mini Pads tulizozikadhi leo wafanyakazi wa wizara watakuwa na fursa ya kupata huduma zetu bila ya wasiwasi wowote.” Alifafanua Bw. Liao


“Idadi ya Mini Pads tulizozikabidhi hii leo ni 180 na tuna matumaini zitakuwa ni msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa wizara kwa idadi iliyotajwa na mheshimiwa waziri. StarTimes tumejizatiti vya kutosha si tu kuwahudumia wateja wetu bali pia kusaidiana nao katika shughuli mbalimbali. Kwa sasa kampuni yetu imelenga zaidi katika kuwekeza na kukuza vipindi na chaneli za nyumbani ili kuwapa watanzania wenye vipaji kuweza kuonekana. Tunashukuru sana ushirikiano tunaoupata kutoka serikali kwani ndio mdau mkubwa katika shughuli za uendeshaji wetu ambao ni zaidi ya miaka mitano sasa tangu tuanze.” Alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania.

UKOSEFU WA WABUNIFU MAVAZI JIJINI MWANZA, WAPATA UFUMBUZI

March 22, 2016
Idda Hassan ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushonaji wa Mavazi Jijini Mwanza ya Mikaela Professional Tailors akionyesha moja ya mavazi yanayoshonwa na Kampuni hiyo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Tofauti na ilivyo katika majiji mengine kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.

Ni kutokana na hali hiyo, Wataalamu na Mabingwa wa Ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali (Kike na Kiume) Jijini Mwanza, Mikalela Professional Tailors, wameahidi kulitambulisha Jiji hilo katika ubunifu wa mavazi ili kuendana na kasi iliyopo katika majiji mengine.

"Awali nilikuwa nateseka sana. Nguo zangu nilikuwa nikishea Jijini Dar au Arusha na nikizivaa watu wengi wakawa wanauliza niliposhonea na kutamani niwapeleke. Nikaona kumbe Mwanza kuna uhitaji mkubwa wa ubunifu na ushonaji wa mavazi hivyo nikaamua kuanzisha kampuni ya ubunifu na ushonaji wa mavazi ya Mikaela Professional Tailor ili kukata kiu hiyo. Alisema Idda Hassan ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.
Zaidi BONYEZA HAPA Kwa Habari Zaidi.

Kipindi cha redio cha Shuga charudi kwa kishindo

March 22, 2016
Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS   Abubakari Magege  akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini




Mwakilishi wa UNICEF   Alice Ijumba  akijibu maswali ya washiriki wa
wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini

 washiriki wa
wa kipindi cha redio cha shuga wakifuatilia mada kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
Alice Ijumba toka UNICEF



Waratibu wa Shuga Radio drama series msimu wa pili - Pendo Laizer na David Sevuri wakichanganua ushiriki wa watangazaji na vikundi vya wasikilizaji

Mshiriki akichangia mada katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini;

Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa - TACAIDS,Fadhila Mturi  akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina elekezi









Vipindi vya redio vya Shuga vitaanza kuunguruma tena kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo vinalenga kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya kondomu na kuepukana na msongo rika.

Mfulilizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio yao,  changamoto wanazopitia ili kutimiza malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha yao ya kila siku.

Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga.

Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na mahudhui ya vipindi, mashirika ya UNICEF pamoja na TACAIDS kwa kushirikiana na kampuni ya True Vision Production wanaendesha mafunzo elekezi kwa vituo vya radio za jamii, mameneja wa radio shiriki, watangazaji na waandishi wa habari pamoja na kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za Halmashauri na Mkoa, ambapo warsha hii inafanyika mkoani Iringa.


Radio zitakazoshiriki katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni Clouds FM, Nuru FM – Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja na Furaha FM, Hope FM, Qibla Ten FM za Iringa

NAIBU SPIKA WA BUNGE AHUDHURIA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KATIKA KUMBI ZA BENKI KUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

March 22, 2016
  Naibu Spika wa Bunge, Tulia Mwansasu (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo alipohudhuria kikao cha kamati hiyo kilichoketi katika Kumbi za Benki Kuu (BoT Dar es Salaam leo.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa  kamati hiyo, William Ngeleja.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, William Ngeleja (kulia), akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge, Tulia Mwansasu (kushoto), katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi Dar es Salaam leo. Naibu Spika jana alihudhuria baadhi ya vikao vya Kamati za Bunge.
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, Joseph Mhagama (kulia), akizungumza na wajumbe wa kamti hiyo (hawapo pichani), wakati akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge kwenye kikao hicho.
 Mjumbe wa kamati hiyo, Omary Badwel akichangia jambo kwenye kikao hicho mbele ya Naibu Spika. Kushoto ni Mjumbe Anna Joram Kidarya.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa kwenye kikao hicho.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Vyama vya ushirika Hufa kutokana na madeni makubwa

March 22, 2016
-- Regards BY: Elimtaa Media, Headquarter Njombe Tanzania web; www.eliab.blogspot.com Email; furahanews1@gmail.com furahanews@gmail.com Facebook; https://www.facebook.com/elimtaamedia Twitter; https://twitter.com/elimtaa Linkedin; https://www.linkedin.com/home?trk=nav_responsive_tab_home Mbl; +255 753 321 191, +255 656 049 045 More News Update your Mind