WAZIRI JAFFO AWATAKA WANANCHI WA KATA YA KWAGUNDA KUMCHAGUA MGOMBEA WA CCM

January 03, 2018
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mgaza wakati wa mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wa udiwani Kata ya Kwagunda kupitia CCM Saidi Shenkawa ambapo aliwataka wananchi kumpa kura za ndio ili aweze kuwapa maendeleo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo kulia akimnadi  mgombea wa udiwani Kata ya Kwagunda kupitia CCM Saidi Shenkawa ambapo aliwataka wananchi kumpa kura za ndio ili aweze kuwapa maendeleo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuwamchagua mgombea wa CCM ili aweze kushirikiana naye kuwapa maendeleo
Diwani wa Kata ya Majengo (CCM) Mustapha akizungumza katika mkutano huo huku akimuomnbe kura mgombea wa CCM
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini Mzee Malingumu akipiga magoti kumuombea kura mgombea wa CCM katika m kutano wa hadhara ambapo uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 13 mwaka huu kufuatili aliyekuwa diwani wa Kata hiyo kufariki dunia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo akielekea kuzungumza na wananchi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo katikati akionyeshwa kitu kwenye simu na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) na Mjumbe wa baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa,Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo akiwapungua mikono wananchi waliojitiokeza kwenye mkutano huo kushoto aliyevaa shati jeupe ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni na Mbunge wa Jimbo la la Korogwe Vijijini (CCM) na Mjumbe wa baraza Kuu  la Jumuiya ya Wazazi Taifa,Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo akipiga makofi mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la la Korogwe Vijijini (CCM) na Mjumbe wa baraza Kuu  la Jumuiya ya Wazazi Taifa,Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo akiondoka eneo la mkutano kushoto ni
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo kushoto akiteta jambo na Msaanii Dkt Nyau mara baada ya kumalizika mkutano huo katikati ni
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni


RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AAGANA NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROF. BENNO NDULU PAMOJA NA KUKUTANA NA GAVANA MTEULE WA (BOT) PROF. FLORENS LUOGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AAGANA NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROF. BENNO NDULU PAMOJA NA KUKUTANA NA GAVANA MTEULE WA (BOT) PROF. FLORENS LUOGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

January 03, 2018

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga wa kwanza (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu wa kwanza (kulia) mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
6.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga wa kwanza (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu wa kwanza (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya kifedha. Kushoto ni Gavana Mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu kwa furaha Gavana Mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
14
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
15
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Gavana Mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga Ikulu jijini Dar es Salaam.
17
Gavana Mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga akipongezana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

NAIBU MEYA JIJI LA MBEYA (CHADEMA) AAHIDI USHIRIKIANO NA WATEULE WA RAIS MAGUFULI AMSIFU MHE MWANJELWA KUSHIRIKIANA NA VYAMA VYA UPINZANI

January 03, 2018
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Sinde kabla ya kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Baadhi ya wananchi wakimlaki Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018.
Diwani wa Kata ya Manda Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe akitoa salamu za wananchi wa Kata yake kwenye mkutano wa wananchi wa kata jirani ya Sinde kabla ya Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kuzungumza na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo Jana Januari 2, 2018

Na Mathias Canal, Mbeya

IMEBAINIKA kuwa tofauti za kiitikadi baina ya madiwani katika Halmashauri nyingi  nchini, zimekuwa ni kikwazo kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye tija kubwa kwa wananchi.
Tofauti hizo zimekuwa chanzo kikubwa katika utekelezaji wa miradi inayobuniwa na Halmashauri husika, au inayoletwa na Serikali Kuu na wafadhili. Mitazamo ya kisiasa, tofauti ya uwakilishi wa vyama na ubinafsi, ndio sababu kuu.
Katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayoongozwa na Meya na Naibu Meya wanaotokana na vyama vya upinzania hali imekuwa tofauti kwani asilimia kubwa ya madiwani wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli tofauti kabisa na Halmashauri zingine.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana 2 Januari 2018 uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni faida ya watanzania wote hivyo kuna kila sababu ya wananchi kuunga mkono juhudi za serikali yake.
Kyanula alisema kuwa pamoja na kuwa kiongozi anayetokana na chama cha upinzani lakini serikali ni moja hivyo anaungana na wateule wote wa Rais Magufuli katika kutekeleza dhamira ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akimtaja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kama kiongozi wa mfano katika Mkoa wa Mbeya hivyo kuahidi kushirikiana nae kwa karibu.
Naibu Meya huyo amempongeza Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kuchangia jumla ya mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera (Mifuko 20) na Shule ya Sekondari Sinde (Mifuko 20) zilizopo Jijini Mbeya.
Alimtaja Mhe Mwanjelwa kwamba amekuwa mwalimu mzuri wa somo la Uraia Mkoani Mbeya akifundisha kuhusu umoja na mshikamano huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni dhana pana kwa wananchi na hayapaswi kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo amesifu Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kazi kubwa katika utendaji ikiwemo kuanza mchakato wa ujenzi wa vyumba vya madarsa ili kuikabili changamoto ya wingi wa wananfunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2018.

TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU, KINYEREZI

TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU, KINYEREZI

January 03, 2018
Magari na pikipiki zikipita kwa shida Mtaa wa Tanganyika, Kifuru Kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, eneo ambalo nyaya na nguzo za mradi wa umeme unaodaiwa kutelekezwa na TANESCO kituo cha Tabata kwa muda sasa baada ya kuangushwa na mvua za mwishoni mwa mwaka 2017. Magari na pikipiki zikipita kwa shida Mtaa wa Tanganyika, Kifuru Kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, eneo ambalo nyaya na nguzo za mradi wa umeme unaodaiwa kutelekezwa na TANESCO kituo cha Tabata kwa muda sasa baada ya kuangushwa na mvua za mwishoni mwa mwaka 2017.
WAKAZI wa Kata ya Kinyerezi eneo la Kifuru kwa Kinana wameulalamikia uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kituo cha Tabata jijini Dar es Salaam kwa kitendo cha kutelekeza nguzo na nyaya za mradi wa umeme eneo hilo ambapo zime geuka kero. Wakizungumza jana eneo hilo kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wakazi hao, wamesema TANESCO kituo cha Tabata walileta nguzo na nyaya tangu mwaka jana na kuziweka barabara inayoelekea King'azi (Kwa Godoro) Mtaa wa Tanganyika ambapo baada ya mvua za mwishoni mwa mwaka jana 2017 baadhi ya nguzo zilianguka na nyaya kutandaa chini jambo ambalo limekuwa kero baada ya kuziba barabara ya mtaa huo na magari kupita kwa taabu. Mkazi wa Mtaa wa Tanganyika, Rashid Abdallah alisema mradi huo umechukua zaidi ya miaka miwili sasa huku wateja walioomba umeme eneo hilo wamekuwa wakizungushwa kwamba wasubiri mradi huo bila ya mafanikio. "...Tumeomba umeme muda mrefu sana tunaambiwa kusubiri mradi lakini mradi ndio kama hivyo wamekuja wamefunga nyaya baada ya mvua kunyesha zimeanguka na wamezitelekeza hapo hapo chini...tunapita kwa shida na wengine kwa hofu maana nyaya za umeme zipo chini kabisa si wote wapita njia hazijafungwa umeme sasa hii ni hatari," alisema Mkazi huyo wa Mtaa wa Tanganyika. Alisema kwa sasa wamekuwa kama walinzi wa nguzo na nyaya hizo za TANESCO mtaani hapo maana wanahofia zikiibiwa huenda matumaini ya mradi huo wanaoahidiwa kila kukicha kukamilika ukatoweka kabisa. "Sasa hivi tumegeuka walinzi maana tunajitahidi haya manyaya yao (waya za TANESCO) waliotelekeza hapo chini baada ya kuanguka yasiibiwe...," alisema Abdallah.    
Sehemu nyingine katika mtaa huo nyaya zimelala chini pamoja na nguzo kupinda.[ 
Sehemu nyingine katika mtaa huo nyaya zimelala chini pamoja na nguzo kupinda 
Baadhi ya nguzo na nyaya za TANESCO Kituo cha Tabata Dar es Salaam zinazodaiwa kutelekezwa na kituo hicho kwa muda sasa baada ya kung'olewa na mvua. Wakazi wa eneo hilo wameilalamikia TANESCO kwa kushindwa kutatua kero hiyo na kukamilisha mradi.[/caption]   Kwa upande wake mkazi mwingine wa eneo hilo, Senzekwa Magila alisema wanashangaa kuzungushwa maombi yao ya kufungiwa umeme wakielezwa kusubiri mradi ambao haukamiliki ilhali wanaendelea kutaabika. Alisema TANESCO inapaswa kujifunza na kuwa makini kwa uongozi wa sasa kwani unahimiza uchapaji kazi bora unaolenga kuiingizia Serikali na taasisi zake mapato ya kutosha, jambo ambalo wanashangaa wateja wanaomba huduma zaidi ya miaka miwili bila mafanikio. "..Tunashangaa sana wateja tunaomba umeme ili tuweze kuchangia kipato cha shirika na hatimaye Serikali lakini hadi leo tunazungushwa, lakini mapato yetu eneo hili yangeweza kuchangia pato la TANESCO na Serikali. Sasa hivi tunajadiliana kwenda kuwaona viongozi gazi za juu watusaidie labda huenda tutafanikiw," alisema mkazi huyo. Naye mkazi mwingine ambaye alikataa kutaja jina lake alisema kinachowakaza zaidi ni kitendo cha maeneo yote yaliozunguka mtaa huo kuunganishwa umeme lakini wao Mtaa wa Tanganyika hadi leo wamekuwa wakipigwa danadana bila mafanikio. Alisema wengi wao wamejinyima na kuanza kufunga mfumo wa umeme mapema katika nyumba zao lakini hadi leo hawajaunganishwa. "Ukienda kutaka kulipia wanakwambia subiri umeme wa mradi sasa huu umeme wa mradi unatoka nje ya nchi au hapa hapa Tanzania...maana hatuelewi. Mi nadhani kama wameshindwa kutuunganisha waje waondoe kero zao hapa mtaani kwetu maana umeme hatuna lakini kila kukicha tunalinda waya zao na nguzo walizozitelekeza na kuziba njia hapa," alisema mkazi huyo.