March 10, 2014

MGIMWA AENDELEA NA KAMPENI TOSAMAGANGA NA KALENGA LEO


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa kitongoji cha Tosamaganga wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Kalenga kupitia tiketi ya CCM Ndugu Godfrey Mgimwa ambapo aliwaambia wananchi hao tutafute viongozi wa mfano wa Kitanzania ambao hawatatuchonganisha na watoto wao.
March 10, 2014

MSD YAZINDUA KITUO CHA USAMBAZAJI DAWA MULEBA MKOANI KAGERA

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe akihutubia kwa niaba ya 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Garib Bilal aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa kituo hicho.
Ofisa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Shangwe Stephen akiwa kwenye hafla hiyo.

MEYA AFUNGA MAFUNZO YA WALIMU WA MCHEZO WA KIKAPU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI TANGA.

March 10, 2014
MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI AKUZINGUMZA NA WASHIRIKI WA SEMINA YA WALIMU WA MPIRA WA KIKAPU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ILIYOSHIRIKISHA WASHIRIKI KUTOKA WILAYA ZA KILINDI,MUHEZA,PANGANI,MKINGA,KUSHOTO NI AFISA MICHEZO MKOA WA TANGA,DIGNA TESHA NA KULIA NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,HAMISI JAFFARI

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,HAMISI JAFFARI ALIYESIMAMA AKIZUNGUMZA JAMBO KWA WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO ANAYEFUATIA NI MEYA WA JIJI LA TANGA OMARI GULEDI,AFISA MICHEZO MKOA WA TANGA,DIGNA TESHA NA MKUFUNZI  ALIYEKUWA AKIENDESHA  MAFUNZO MR MNAJURA LEO KWENYE UKUMBI WA HARBOURS CLUB


MMOJA KATA YA WALIMU WASHIRIKI KWENYE MAFUNZO HAYO AKIPEWA CHETI CHA KUHITIMU MAFUNZO NA MEYA WA JIJI LA TANGA OMARI GULEDI LEO WANAOSHUHUDIA KUSHOTO NI AFISA MICHEZO MKOA WA TANGA,DIGNA TESHA NA KULIA NI MWENYEKITI WA CHAMNA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,HAMISI JAFFARI


KATIBU WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,CALISTIUS AKISOMA RISALA FUPI KWA WAHITIMU HAO LEO

KIBADENI:TUTAPIGANA KUSISHUKE DARAJA LA LIGI KUU TANZANIA BARA.

March 10, 2014
KOCHA MKUU wa timu ya Ashanti United,Abdallah King Kibadeni amesema malengo yake makubwa kwenye timu hiyo ni kuhakikisha anapigana kufa na kupona ili kuweza kuibakiza timu hiyo kwenye daraja la Ligi kuu Tanzania bara.
Kibadeni alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mechi yao na Coastal Union ambapo timu hizo zilitoka sare ya kutokufungana mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani.

TWFA KUSAKA WAFADHILI KWA AJILI YA LIGI YA WANAWAKE.

March 10, 2014
CHAMA cha Mpira wa Miguu wa wanawake nchini Tanzania (TWFA)kimesema kuwa  kipo kwenye mikakati kabambe ya kutafuta wafadhili ambao wataweza kusaidia kufadhili ligi  za wanawake kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuweza kuinua kiwango cha soka hilo.

Katibu wa Chama hicho Taifa,Amina Karuma aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkoani hapa ambapo alisema mikakati hiyo ni pamoja na kushirikisha na shirikisho la soka nchini TFF ili kuweza kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake kupitia programu ya grass root inayoshirikisha wanawake na wanaume.

March 10, 2014
KADO:Amnyima raha Chippo:

MLINDA Mlango namba moja wa Klabu ya Coastal Union Shabani Kado mwishoni mwa wiki alimpa mawazo mazito Kocha Mkuu wa timu hiyo,Yusuph Chippo mara baada ya kuumia kwenye mechi yao na Ashanti United na kulazimika kutoka nje ya uwanja wakati mchezo huo ukiendelea.
Kado aliumia mara baada ya kukumbana na mshambuliaji wa Ashanti United Hussein Said na hivyo nafasi yake ilichukuliwa na mlinda mlango wa akiba Said Lubawa ambaye aliweza kulinda lango hilo mpaka mchezo huo unamalizika.