WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AHADI, ILANI YA CHAMA TAWALA NA MAAGIZO YA VIONGOZI WAKUU

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AHADI, ILANI YA CHAMA TAWALA NA MAAGIZO YA VIONGOZI WAKUU

March 28, 2017
MAHA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza umuhimu wa mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma na kulia kwake waliokaa ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
MAHA 1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.
MAHA 2
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akiratibu shughuli ya uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu uliofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Machi 28, 2017.
MAHA 3
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani) Dodoma.
MAHA 4
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 Dodoma. 
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………..
Na. Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).
Akizindua mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu wa mfumo huo kuwa  umejikita katika kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
“Mfumo huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa maazigo yote na ahadi zilizotolewa ili kuona utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema Mhe.Waziri.
Aidha mfumo utasaidia pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza ufanisi wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali kwakuwa taarifa zote zitapatikana kwa wakati na takwimu za uhakika.
Alibainisha kuwa, kuanzishwa kwa mfumo ni moja ya sehemu ya kuondoa changamoto kadhaa ikiwa ni kuongeza ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa kwa mfumo huo kutatua changamoto za uchelewashwaji wa taarifa, na kutowajibika kwa ujumla na kuleta ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.
Aidha kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua alibainisha kuwa mfumo umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe.Rais Jonh Magufuli na Watendaji  wa Serikali.
Kwa kumalizia Waziri alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na kutoa rai kwa Watendaji wote wa Serikali kuutendea haki kwa kufanya kazi bila uzembe wowote. “rai yangu kwa Watumishi wa Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwani kupitia Mfumo huu, mzembe atajulikana na mchapa kazi atajulikana. Na ikumbukwe tu, wazembe na wavivu hawana nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano”.

UFAFANUZI WA ACACIA DHIDI YA TUHUMA ZA USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA YA DHAHABU/SHABA

March 28, 2017
Zimepita wiki tatu (3), tangu kutangazwa kwa zuio la ghafla la ushafirishaji wa makinikia ya dhahabu/shaba lililotangazwa tarehe 2 Machi. 

Tangu kutangazwa kwa zuio hilo kumekua na upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hadi sasa, Acacia haikutoa tamko lolote hadharani, sababu tumekua tukielekeza jitihada katika kutafuta muafaka na Serikali juu ya nini kifanyike. 

Lakini, kutokana na kiwango kikubwa cha taarifa potofu na zisizo sahihi zenye uvumi mwingi ambao unaweza kutuletea taswira mbaya kwa kampuni, kwa wafanyakazi wetu na pia kwa Tanzania kwa ujumla, tumeamua kuweka wazi hali halisi juu ya hoja mbalimbali. 

 Acacia inapinga vikali kuhusika na madai yaliyotolewa mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya ukaguzi bandarini – Dar es Salaam kwamba sisi tulikua tukifanya njama za kutorosha makontena yenye makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi licha ya katazo lililotangazwa na Serikali. 

Ukweli ni kwamba si Acacia wala wateja wetu walijaribu kusafirisha makinikia haya nje ya nchi. Kabla ya kutangazwa kwa zuio hilo, makontena, 256 ambayo sasa yamehifadhiwa ZamCargo (zamani ikijulikana kama Mofed - ambaye ni wakala wa usafirishaji wa forodha Customs Freight Services, CFS) yalikuwa tayari yamesafirishwa kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, na makontena mengine 21 yaliyokutwa katika bandari ya Dar es Salaam yakiwa tayari yameidhinishwa na idara ya forodha ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na yalikua tayari kusafirishwa. 

Zoezi hili huwa linajumuisha TRA pamoja na Wizara ya Nishati na Madini (MEM) ambao kwa pamoja wanahusika katika mchakato wa kusafirisha mikinikia nje ya nchi kwa utaratibu maalum.

 Acacia imekuwa ikisafirisha makinikia nje ya nchi kutoka mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 2001 na kutoka mgodi wa Buzwagi tangu mwaka 2010 huku ikiweka bayana mapato yote yanayohusiana na makinikia ya dhahabu/Shaba na kuwasilisha Serikalini. Mapato haya pia yamekua yakitolewa kama mrahaba na malipo mengine kama kodi ya mapato kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 

Sheria za Tanzania zinaruhusu migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi kuuza nje ya nchi makinikia ya dhahabu/Shaba, sambamba na kusafirisha makinikia ndani ya makontena. Migodi hii imekua makini kukidhi vigezo vyote vya kisheria na matakwa ya vibali vya usafirishaji (Export Permits).

 Tunapenda umma ufahamu kua kila kitu tunachokifanya kinathibitishwa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA). Kila kontena la makinikia linalosafirishwa linachukuliwa sampuli chini ya uangalizi wa idara zote za usimamizi ambazo ni TMAA na Kampuni ya huduma za maabara (SGS) ili kwamba Acacia na Serikali ziweze kukadiria wingi wa madini ya dhahabu, shaba na fedha yaliyomo.

 Matokeo ya sampuli hizi hupelekwa TMAA, TRA, Acacia na kampuni zenye mitambo maalum ya kuyeyusha na kuchenjua makinikia (Smelters) ili kubaini mrahaba wa awali ambao Serikali italipwa kabla ya kusafirisha makinikia. 

 Ni pale tu ambapo upimwaji wa sampuli umekamilika, na mrahaba umeshalipwa kwa Serikali, ndipo makontenta yanafungwa kwa lakiri maalum za TMAA, MEM na TRA, na makinikia yanaweza kusafirishwa kutoka migodini.

 Kisha makontena husafirishwa wa magari ya kubebea mizigo hadi kituo cha forodha cha Isaka ambako nyaraka za mwisho za kusafirisha nje ya nchi hutolewa na MEM pamoja na TRA, na makontena kuidhinishwa kwa safari ya kwenda bandari ya Dar es Salaam. 

Baada nyaraka zote kukaguliwa na kuhakikishwa na maafisa wa forodha, kila kontena hukaguliwa kwa kutumia mtambo maalumu wa kieletroniki (Scanner) ili kuthibitisha kua ndani yake hakuna kitu kingine chochote isipokua makinikia ya dhahabu/Shaba tu. 

Baada ya hapo makontena huhifadhiwa chini ya ulinzi wa maafisa wa forodha mpaka hatua za mwisho za upakiaji wa makontena kwenye meli tayari kwa kusafirisha nje ya nchi. 

 Acacia iko tayari kushirikiana na Serikali kutafiti uwezekano wa Tanzania kua na kiwanda cha uchenjuaji ambacho kitatoa ajira na kuleta maendeleo kwenye sekta hii. 

Maendeleo ya teknolojia yanaweza kutoa muelekeo stahili juu ya uwezekano huu. Hadi hivi sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi imeendelea na uzalishaji kama kawaida hata baada ya zuio la Serikali na makinikia haya yamehifadhiwa katika maeneo maalumu migodini. 

Lakini hali hii haiwezi kua ya kudumu kutokana na umuhimu wa kukusanya mapato yatokanayo na biashara ya makinikia kwa migodi hii miwili. 

 Acacia inaunga mkono kikamilifu jitihada za bila kuchoka za Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kuwekeza katika maendeleo ya nchi kupitia elimu, ajira na viwanda.

 Acacia ni mwajiri mkubwa nchini Tanzania na sasa tumetoa ajira za moja kwa moja za zaidi ya wafanyakazi 5,000 pamoja na wakandarasi na ajira zingine 55,000 katika uchumi, zinazofaidisha familia na jamii kwa ujumla. 

Kati ya waajiriwa wote wa Acacia, zaidi ya asilimia 96 ni Watanzania. Migodi yetu inasaidia kuendeleza wazawa kupitia idara yetu ya ugavi ili kuwapatia fursa endelevu za kibiashara. 

Tunapenda kuendelea kuwakaribisha maafisa wa serikali kuja kutembelea migodi yetu ili waweze kufahamu mchakato mzima wa kuzalisha madini, kukusanya sampuli na kusafirisha makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi. 

 -- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

WAZIRI MAKAMBA ATOA MAAGIZO KWA MAMLAKA YA NGORONGORO

March 28, 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za kimazingira.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Baraza la wafugaji (hawapo pichani) katika Wilaya ya Ngorongoro. Wafugaji hao walimweleza Waziri kilio cha muda mrefu cha mradi wa Josho Wilayani hapo, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kuleta ufumbuzi mapema.


Na Lulu Mussa
Ngorongoro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira nchini Mhe. January Makamba amesema kuwa ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kudhibiti mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro.

Katika kutatua changamoto hii, Waziri Makamba ameagiza kuundwa kwa jopo la wataalamu kutoka Tume ya Sayansi na Tecknolojia,  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Hifadhi za Taifa za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi sita kufanyika kwa utafiti wa kina wa kisayansi wa kubaini mbinu mpya ya kupambana na mimea hiyo vamizi inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama.

Akizungumza  katika kikao kilichojumisha Wahifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Wajumbe wa Baraza la wafugaji, Waziri Makamba amesikitishwa na kitendo cha Uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro kushindwa kuandaa mpango kabambe wa usimamizi wa hifadhi baada ya ule wa awali kuisha muda wake. Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Ngorongoro kuandaa mpango huo mapema na kuwa shirikishi. " Mpango mtakoandaa hakikisheni kuwa unakuwa shirikishi kwa jamii inayozunguka na wadau na Taasisi muhimu likiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Waziri Makamba pia ameagiza kufanyika kwa ukaguzi wa kimkakati wa Mazingira utakaojumuisha Wilaya nzima ya Ngorongoro na kuitaka Mamlaka ya Ngorongoro kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kutekeleza wajibu huo mapema. Ukaguzi huo wa kimkakati wa kimazingira kwa Wilaya hiyo unatazamiwa kutoa mtazamo wa hali ya mazingira kwa miaka hamsini ijayo.

Aidha, Waziri Makamba ameagiza kufanyika kwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira  ama Ukaguzi wa Mazingira katika Hotel zote zilizopo eneo la hilo na kulitaka Baraza la Taifa la Hofadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupita siku ya Alhamisi tarehe 30/03/2016 kuwaandikia adhabu na kuwatoza faini wahusika wote ambao hawana vyeti hivyo. "Haiwezekani toka mwaka 2004 Sheria ipo na mpaka leo watu wanaendea na mchakato, hii haikubaliki!" Alisisitiza Makamba.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba ametoa miezi sita kwa wamiliki wa Hotel zilizopo katika Mamlaka ya Ngorongoro kuwekeza katika mfumo mpya wa kuvuta maji kutoka Mto Lukusale na kusitisha mfumo wa sasa wa kutoa maji kwenye creator. Pia Makamba ameutaka ungozi wa Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi sita kuandaa ramani itakayoonyesha mito na vijito vyote vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo.

Waziri Makamba ametoa maagizo hayo leo juu ya  namna bora ya kutumia rasilimali ya "creater"  kwa ajili ya utalii na Uhifadhi wa Mazingira, ikiwa  ni pamoja na utekelezaji wa zuio la mifugo ndani ya crater.  Ziara maalumu na mahsusi ya kukagua utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira inayofanywa na Waziri Makamba hii leo imefika Wilayani Ngorongoro.




MAKAMISHNA WAPYA WA UHAMIAJI WAAPISHWA LEO MJINI DODOMA

MAKAMISHNA WAPYA WA UHAMIAJI WAAPISHWA LEO MJINI DODOMA

March 28, 2017
C
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira  aliyeketi katikati akishuhudia Makamishna wapya wa  Uhamiaji wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya kuvishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,  Kulia ni Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi  Hassan Simba Yahaya na  kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala wote wakishuhudia tukio hilo.
C 1
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha,  Edward Peter Chogero  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira  na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi  Hassan Simba Yahaya.
C 2
Kamishna mpya wa Uhamiaji Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
C 3
Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza  Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa  kiapo cha Maadili ya Viongozi wa  Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya kuvalishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
C 4
Makamishna wapya wa Uhamiaji wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
C 5
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira  akitoa maelekezo kwa Makamishna wapya wa Uhamiaji wakati wa hafla ya kuvikwa Vyeo Vipya   iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
C 6
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao  leo katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.  
SERIKALI KUTENGENEZA MWONGOZO WA KUWARUDISHA SHULE WALIOPATA MIMBA

SERIKALI KUTENGENEZA MWONGOZO WA KUWARUDISHA SHULE WALIOPATA MIMBA

March 28, 2017
QQ
Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu kutoka shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI) mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
QQ 1
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen akitoa neno fupi kwa ajili ya kuwakaribisha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu. Ufunguzi wa warsha hiyo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.
QQ 2
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali wanaohusika na elimu kutoka nchi sita za Afrika wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (hayupo pichani), Venance Manori wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha maafisa hao katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu.Warsha hiyo ya siku tatu imefunguliwa jana jijini Dar es Salaam.
…………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Serikali imejipanga kutengeneza mwongozo wa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba wakiwa masomoni ili kuhakikisha wanapata elimu hadi kufikia ngazi za juu.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori alipokuwa akifungua warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia jinsia katika elimu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako.
Manori amesema Serikali ya Tanzania inajitahidi kuzingatia jinsia katika utoaji wa elimu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa elimu ya Msingi na Sekondari uwiano wake ni moja kwa moja japo kuwa idadi ya wasichana hupungua kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba hivyo lengo la warsha hiyo ni kuwasaidia wadau kuweka mipango ya elimu inayozingatia usawa wa kijinsia.
“Serikali yetu imejipanga kuhakikisha wasichana wanapata elimu hadi ngazi za juu lakini mpango huo unakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mimba na ndoa za utotoni hivyo ili kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ngazi za juu za elimu tuko kwenye mchakato wa kuandaa mwongozo kwa ajili ya wanafunzi waliopata mimba wakiwa bado wanasoma kupata nafasi ya kuendelea na masomo,”alisema Manori.
Mkurugenzi Msaidizi amezitaja changamoto zingine zinazowapelekea wanafunzi wa kike kuacha shule zikiwemo za umaskini, mazingira rafiki ya kusomea, mila na desturi zinazomkataza msichana kupata nafasi ya kusoma pamoja na kukosa muda wa kujisomea kwa sababu ya kufanya kazi nyingi wanaporudi majumbani.
Manori ametoa rai kwa Watanzania kuelewa kuwa kila mtoto ana haki na wajibu wa kupata elimu bila kujali jinsia pia ameiasa jamii kuacha kuwaozesha wasichana wenye umri chini ya miaka 18 ili waweze kufikia malengo yao waliyojipangia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen ameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha mipango ya elimu nchini inaangalia usawa wa kijinsia kwa kuwa ni njia moja wapo itakayochochea maendeleo ya elimu kwa watoto wa kike.
“Warsha hii imeandaliwa kwa ajili ya wadau wote kutoa mawazo yao juu ya changamoto za usawa wa kijinsia zinazoikumba sekta ya elimu pamoja na kuwapa fursa wadau hao kushauriana kuhusu mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto hizo ili kuinua sekta ya elimu sio tu kwa Tanzania bali kwa Afrika nzima,”alisema Haldorsen.
Haldorsen ameongeza kuwa mfumo wa elimu umetambua uhusiano uliopo kati ya elimu na usawa wa kijinsia ndio maana wadau wa masuala ya elimu wa Serikali kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika wameamua kuungana kwa pamoja kujadili juu ya tathmini, mpangilio na ufuatiliaji wa elimu unayozingatia jinsia.
Tanzania imekua nchi ya kwanza kuendesha warsha hiyo ya siku tatu iliyoshirikisha maafisa waandamizi wa Serikali wanaoshughulikia mipango ya elimu kutoka nchi za Mozambique, Zambia, Malawi, Uganda, Zanzibar na Tanzania Bara.
Imeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI).

MKUTANO WA WALIMU WAKUU WA SKULI ZA SEKONDARI UNGUJA

March 28, 2017


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi mnazi mmoja mjini unguja katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za sekondari za unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi mnazi mmoja mjini unguja katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za sekondari za unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi mnazi mmoja Mjini Unguja katika mkutano maalum wa Walimu wa Skuli za Sekondari za Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Serikali alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za Sekondari za unguja.
Baadhi ya Walimu wa skuli za Sekondari za Unguja wakiwa katika mkutano wa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya Walimu wa Skuli za Sekondari za Unguja wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakiwa katika mkutano wa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiwa katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za Sekondari za Unguja, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Watendaji mbali mbali wakiwa katika mkutano maalum wa walimu wa Skuli za Sekondari za Unguja, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.] 28/03/2017.
WAZIRI MKUU ATEMBELEA MGODI öWA BUZWAGI NA KUCHUKUA SAMPULI ZA MCHANGA

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MGODI öWA BUZWAGI NA KUCHUKUA SAMPULI ZA MCHANGA

March 28, 2017
AA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  afanya ziara  katika Mgodi wa Buzwagi  27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia  Mchanga  uliowekwa katika  Makontena  kwa ajili yakusafirishwa nnje ya nchi katikati ni Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga  Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja  Mkuu wa  Mgodi wa Buzwagi Bwana  Stewart Hamilton
AA 1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa Nnje ya Nchi na Mgodi wa Buzwagi  uliopo Kahama Mkoani Shinyanga  Waziri Mkuu Alifika katika Mgodi huo 27march2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya Mchanga  ili Serekali Ikaupime katika Maabara za Serekali
AA 2
A0227 Mtaalamu wa Madini akiweka Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya Makontena na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa Madini Wziri Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017 kwalengo ya kujionea aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na Baadhi ya Migodi inayo Chimba Dhahabu hapa Nchini
AA 3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga  Josephine  Matiro katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa  Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Zainabu  Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Picha zote na PMO
…………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,”
Waziri Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama yanastahili.
Aliongeza kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Wakati huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi. Pia  amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache waendelee na majukumu yao.
Kwa upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na vibarua 500.
Alisema kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za madini ya shaba.
Bw. Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia 50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutenganishwa.
“Hapa Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es Salaam,” alisema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
DODOMA.
JUMANNE, MACHI 28, 2017.
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

March 28, 2017
ZA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
ZA 1
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
ZA 2
WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma

BoT YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUMI NA FEDHA

March 28, 2017
Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUMUKO wa bei utokanao na ongezeko la Fedha ni hatari sana katika uchumi wa nchi, Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, ameiambia semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo Machi 28, 2017.

Semina hiyo ya wiki moja inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar, ina lengo la kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu namna bora ya uandishi w ahabari za uchumi na fedha.

Chini ya Sera ya Fedha, (Monetary Policy), Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kama mtengeneza fedha (mchapishaji), inaweza kudhibiti mfumuko wa bei utokanao na ujazi wa fedha kutokana na viashiria vya uwezo wa uzalishaji katika taifa unapopungua au kuonegzeka. Sera ya fedha maana yake ni pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.

“Inapogundulika kuwa kiwango cha fedha ni kikubwa kwenye mzunguko kuliko uzalishaji BoT kazi yake hapa ni kupunguza fedha kwenye mzunguko na hii sio kwa eneo fulani tu la nchi bali ni nchi nzima ambako fedha ya Tanzania inatumika.” Alisema Mchumi huyo.

Akifafanua zaidi kuhusu namna BoT inavyoshughulikia ujazi wa fedha au kupunguza, Lusajo alisema njia pkee inayotumika ni kupitia mabenki ya biashara.

“Kama mjuavyo bei ya Mafuta inadhibitiwa na soko la Dunia, na hata mfumuko wa bei za vyakula unategemea na tabia nchi kama ukame unaopelekea upungufu wa chakula, hapa BoT inachofanya ni kutoa usahuri kwa Serikali ili kupitia vyombo vyake ikiwemo vile vya kodi kufanyia kazi hali hiyo.” Alifafanua Mchumi huyo Mwandamizi wa BoT.

Alisema moja ya hatua za kuongeza ujazi wa fedha kwenye mzunguko ni hatua ya hivi karibuni ya Benki Kuu, (BoT), kupunguza kiwango cha amana zinazowekwa na mabenki ya biashara kwenye Benki Kuu, kutoka asilimia 10 hadi asilimia 8.

“Hii ina maana asilimia 2 ambayo Benki Kuu imeondoa, sasa mabenki ya biashara yanaweza kukopesha wananchi na hivyo ujazo wa fedha kuongezeka kwenye mzunguko.” Alisema Lusajo.

Ieleweke kuwa fedha ili ziongezeke kwenye uchumi lazima zipitie kwenye mabenki ya biashara ambayo yatazitoa kwa wananchi kupitia mikopo. “Na mikopo itolewayo na mabenki iko mingi sana na kwenye taasisi nyingi kama vile SACCOS, VICOBA na hata wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wakubwa na wadogo na watu binafsi pia, alisema

Mchmi huyo pia alisema, Watanzania wengi hawana utamaduni wa kuweka fedha benki ili kuziwezesha benki hizo nazo kuwa na uwezo wa kuwakopesha zaidi wananchi.

Hata hivyo kiwango cha fedha kinachotolewe na mabenki ya biashara hapa nchini ni kidogo kuliko kile ambacho watu wanataka kukopa na hivyo ili mabenki hayo yaweze kukopesha, lazima benki hizo nazo zikope kwa mabenki mengine yawe ya ndani au nje ya nchi.

“Hivyo benki za biashara kwa vile inapaswa kulipa riba huko ilikokopa, na kulipa mishahara wafanyakazi wake, mtu atakayewkenda kukopa lazima alipe riba ya asilimia 20 kwa mfano na ukimuuliza kwanini unamtoza riba hii ya asilimia 20, atakwambia, mimi nimekopa ili niweze kuwakopesha watanzania ambao wengi hawapendi kuweka fedha benki, alifafanua

Akifafanua zaidi, Mchumi huyo alisema, hivi karibuni BoT, imepunguza riba kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12 kwa benki za biashara zinazokwenda kukopa Benki Kuu ili ziweze kutoa mikopo kwa wananchi. Alifafanua Lisajo
Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia Mbeo, akifafanua baadhi ya hoja zilizoulizwa na waandishi wa habari kuhusu mada ya Sera ya Fedha.

Baadhi wa Waandishi wa habari wakifuatilia mada hiyo
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina akizunhuzma mwanzoni mwa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari za Biashara na Uchumi wa Azam TV, Bi. Rahma Salum akizungumza
WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI

WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI

March 28, 2017


Mkurugenzi wa Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (aliyesimama) akisalimiana na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Morogoro.
Wajumbe wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mjini Morogoro.
Viongozi waliokaa meza kuu, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mjini Morogoro.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa makini maelezo ya mafanikio ya Mkutano wa Baraza hilo kwa mwaka 2015/2016 ambayo ni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akizungumza wakati wa Mkutano wa 13 wa Baraza hilo, Mjini Morogoro.
Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, akitoa nen0 la shukrani baada ya hotuba iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akifungua mkutano wa Baraza hilo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Meza Kuu (Walioketi Mbele) wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dorothy Mwanyika, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa idara na vitengo wa Wizara hiyo, mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika akitoka ukumbini alipoongoza Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Mkutano unaofanyika mjini Morogoro.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).


……………..


Na Benny Mwaipaja, WFM-Morogoro


Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuiletea nchi Maendeleo ya haraka kupitia falsafa ya uchumi wa viwanda utakao iwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kusimamia matumizi yake ipasavyo.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, wakati akifungua mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili.

Bi. Mwanyika amesema kuwa Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi, yana malengo ya kuongeza tija, ufanisi na ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi kama agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 likisomwa pamoja na miongozo mingine linavyo elekeza. 

Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo kukumbuka maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuhusu kusimamia ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya matumizi ya Fedha za Umma, ili kujenga uchumi wa Viwanda na kufikia maendeleo stahiki.

“Tuunge mkono juhudi za Serikali kwa kutafsri maelekezo ya viongozi kwa vitendo ili kuthibitisha msemo usemao Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo moyo wa Serikali” alisisitiza Bi. Mwanyika.

Pia Bi. Mwanyika amewashukuru viongozi wa Wizara hiyo kwa kufanikisha mpango wa Serikali wa kuhamia Dodoma ambapo katika awamu ya kwanza wafanyakazi 184 wameripoti mkoani humo licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa makazi. Hata hivyo amewataka watumishi hao kushirikiana katika kutatua changamoto hizo kwa pamoja.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bw. Cyprian Kuyava, amebainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na maazimio mbalimbali ya Mkutano uliopita wa mwaka 2015/2016 kuwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kazi na kuongezeka kwa mshikamano miongoni mwa wafanyakazi licha ya ufinyu wa Bajeti.

Naye Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Susana Mkapa amesema Watumishi wa Wizara hiyo wako tayari kuunga mkono juhudi za Serikali za ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na hatua ya Serikali kuhamia Dodoma.

Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha unafanyika kwa siku mbili kuanzia Machi 27 hadi 28, 2017, huku ajenda kuu ikiwa kufanya mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka 2017/2018.