MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MAKATIBU MAHUSUSI MJINI DODOMA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MAKATIBU MAHUSUSI MJINI DODOMA

May 19, 2017


A
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa 5  wa Chama cha Makatibu Mahususi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete ,mjini Dodoma. unnamed
 Sehemu ya wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
…………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Makatibu Mahsusi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na waache tabia ya kutoa siri za ofisi zao kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua mkutano wa Tano wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Mji Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uadilifu na uaminifu ni njia pekee ya kuaminiwa na viongozi wao hivyo ni muhimu kwa makatibu mahsusi nchini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa katika maeneo yao ya kazi.
Makamu wa Rais pia amewahimiza makatibu mahsusi kufanya tathmini ya utendaji wao wa kazi na wawe tayari katika kujifunza mbinu mpya za utendaji zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia.
“Sote tunafahamu kuwa dunia imekuwa ni kijiji kutokana na utandawazi unaoletwa na mifumo ya teknolojia hivyo kutokana na mabadiliko haya hamna budi nanyi kubadilika na kwenda na wakati ili msiangaliwe kwa mtazamo hasi wa kuwa wapiga cha tu
Kuhusu uanzishwaji wa Shahada ya Uhazili, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia makatibu mahsusi kuwa Serikali imekubali kuanzisha shahada hiyo ambapo masomo yake yataanza mwezi wa Tisa mwaka huu kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika mikoa ya Dar es Salaam na Tabora.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza makatibu mahsusi kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu kwa kuzingatia kuwa elimu haina mwisho.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amesema Serikali inafanyia kazi baadhi ya kero zinazowakabili makatibu mahsusi ikiwemo kuboresha maslahi ya kada ya uhazili nchini.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kada hiyo pamoja na watumishi wengine wanapata maslahi bora ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi kazi.

TAR TIMES YAINGIA UBIA NA TPB KUUZA LUNINGA ZA KIDIJITALI KWA MKOPO

May 19, 2017


Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akikata utepe kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya Luninga za kisasa kwa kushirikiana na Star Times.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal wakifungua kitambaa kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya kuashiria uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akipeana Mikono na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya mara baada ya uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakionyesha moja ya Luninga zitakazokuwa zinakopeshwa kupitia benki ya Posta.
Baadhi ya watumishi wa kampuni ya StarTimes Tanzania ambao wamehudhuria sherehe hiyo

TEA YAANZA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI PUGU.

May 19, 2017


Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa TEA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela akizungumzia faida zinazotokana na mradi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akimkabidhi mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Miliki NHC Bw. Hassan Mohamed, ukarabati huo unafanywa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akiwaongoza wadau walioshiriki hafla ya makabidhiano ya mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukagua baadhi ya majengo na miundo mbinu ya shule hiyo itakayofanyiwa ukarabati.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu Bw. Jovinus Mutabuzi akishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kuamua kukarabati miundo mbinu ya Shule hiyo ili kukuza kiwango cha elimu. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela
Baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari Pugu yatakayofanyiwa ukarabati na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na yatagharimu zaidi ya milioni mia tisa. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).
Na Fatma Salum- MAELEZO
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa kukarabati Shule ya Sekondari Pugu iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mkataba wa ujenzi kwa Mkandarasi wa mradi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 984 zitatumika katika awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule hiyo.

“Awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule hii itaanza tarehe 1 Juni, 2017 na itafanyika kwa muda wa miezi minne. Ukarabati katika awamu hii utahusisha madarasa, vyoo kwa ajili ya wanafunzi walemavu, mabweni, jengo la utawala, mifumo ya TEHAMA, mifumo ya maji safi na maji taka pamoja na mifumo ya umeme”alifafanua Bibi. Shirima.

Alieleza kuwa zoezi hilo la ukarabati lilitanguliwa na upembuzi yakinifu wa kubaini hali halisi ya mahitaji ya ukarabati na kazi hiyo ilifanywa na Mtaalamu Elekezi (Consultant).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela alipongeza jitihada za TEA za kukarabati miundombinu ya elimu hasa kwa shule kongwe za Sekondari nchini kote mradi ambao utasaidia kuboresha elimu na kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

“Manispaa ya Ilala inaahidi kushirikiana na TEA na uongozi wa Sekondari ya Pugu kutekeleza zoezi hili na kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu.” alisema Palela.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu Bw. Jovinus Mutabuzi alieleza kuwa shule hiyo ina historia kubwa katika nchi yetu na kuishukuru Serikali kupitia TEA kwa ukarabati huo utakaosaidia kurudisha shule hiyo katika hali yake ya awali. 

Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeazimia kukarabati jumla ya shule kongwe za Sekondari 17 ikiwemo shule ya Sekondari Pugu na zoezi hilo limeshaanza kwa shule za Sekondari Nganza, Same na Ilboru.

WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR KUCHANGAMKIA FURSA ZA TADB

May 19, 2017
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari (katikati) akiongoza kikao cha pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
 Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (wapili kulia) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari.
 Wajumbe wa kutokana TADB wakifuatilia kwa makini mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kulia) akieleza dhima ya Benki ya Kilimo katika kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (katikati) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati walipotembelea na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar (hawapo pichani). Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kushoto).

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari akihiimiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.

Na Mwandishi wetu,           
Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar imesema itakuwa ya mwanzo kuanza kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ili kuchagiza uwekezaji katika sekta ya uchakataji wa mazao na masoko ili kuongeza tija kwa maendeleo visiwani Zanzibar.

Mkakati huo umewekwa bayana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Bakari H. Bakari wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake.

Bw. Bakari amesema kuwa ujio wa Benki hiyo unatoa fursa kubwa sana kwa sekta zilizo chini ya wizara yake ikiwamo biashara, viwanda na masoko.

“Tuna imani kubwa ujio wa TADB utatusaidia kutatua changamoto zinazozikabili sekta hizi ambazo zinakabili na changamoto ikiwemo ukosefu wa masoko ya mazao; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo,” alisema.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

Bw. Assenga alisema visiwa vya Zanzibar vitaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo visiwani humo kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.
TIMU YA AZANIA YAKWEA PIPA KUELEKEA UINGEREZA

TIMU YA AZANIA YAKWEA PIPA KUELEKEA UINGEREZA

May 19, 2017
Timu ya Azania imeondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield yatakayofanyika kwenye uwanja wa klabu ya Liverpool wa Anfield. Timu hiyo imeondoka na msafara wa watu 10 ambapo kati yao wachezaji ni saba ambao ni Shabaka Hamisi, Rajabu Ally, Akhamedy Afifu, Abdala Khalidi, Thomas Bishanga, Alidi Said na Brayan Dobadi. Wachezaji wa Timu ya Azania wakibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kukwea pipa kuelekea nchini Uingereza.[/caption] Azania itashiriki mashindano hayo ikiwa ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered Safari kwenda Anfield kwa Afrika Mashariki na Kati na ikiwa kwenye mashindano hayo itakutana na timu zingine kutoka Botswana, Nigeria, Hong Kong, Korea, Singapore, India pamoja na Uingereza. Timu hiyo itafika Uingereza Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu zingine, Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia mchezo wa Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani kwa ajili ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22. Mariam Sezinga (kushoto) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania akiongoza msarafa huo wa timu ya Azania kuelekea nchini Uingereza. Kikosi cha Timu ya Azania katika picha ya pamoja na kiongozi wa msafara huo Mariam Sezinga (wa kwanza kushoto) wa Benki ya Standard Chartered nchini kabla ya kuingia lango kuu la kusafiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Timu ya Azania wakiingia ku-'check in' tayari kukwea pipa kuelekea nchini Uingereza. Mariam Sezinga (kulia) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania akihakikisha hati zote zimekamilika tayari kwa ku-'check in' katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Timu ya Azania wakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Dubai usiku wa kuamkia leo safarini kuelekea nchini Uingereza.
MUHAS WATAKIWA KUWEKA MAKAZI YA KUDUMU OLOLOSOKWAN

MUHAS WATAKIWA KUWEKA MAKAZI YA KUDUMU OLOLOSOKWAN

May 19, 2017
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetakiwa kuhakikisha kwamba wanatumia vyema kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na uwezo mkubwa katika tiba mtandao. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Warsha hiyo ilikuwa inakokotoa tiba mtandao ili kuwezesha mradi wa majaribio wa Tiba mtandao unaohusisha wadau mbalimbali kutekelezwa. Kitovu cha mradi huo ni kijiji cha Ololosokwan kilichopo Waso wilayani Ngorongoro. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Thebeauty.co.tz) 
 Katibu huyo alisema kutumia kikamilifu kwa kijiji hicho hakumaanishi kuwa na majengo bali kutumia kufunza wataalamu mbalimbali kutokana na ukweli kuwa kijiji hicho sasa kitakuwa mfano wa utendaji katika kusaidia wananchi wa Tanzania. “Uwapo wa kijiji hiki ni tukio kubwa kwetu kwani ni kijiji cha kujifunzia, namna ya kutibu, namna ya kukusanya takwimu namna ya kubaini mahitaji na … ni mfano wa namna gani teknolojia inaweza kufanya mambo makubwa” alisema Ulisubisya . Alisema yeye anaamini kwamba si lazima wataalamu watiba wafundishwe eneo moja, kama ilivyo sasa, lakini wanaweza kufundishwa katika eneo kama Ololosokwan na hivyo kuwajenga pia kisaikolojia kwamba wanaweza kufanyakazi pembezoni bila ya tatizo. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) akichangia jambo wakati wa kuhitimisha warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Wa pili kushoto ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya (wa pili kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia). 
Alisema mafanikio ya dhana ya tiba mtandao yatasaidia sana kuboresha hali ya watanzania kwa kuwa mahitaji yao yatajulikana mapema na kutokana na ukweli kuwa mradi wenyewe unahusisha pia ukusanyaji wa data wa uhakika kwa kuzingatia mahudhurio ya watu na magonjwa yao. Pia alisema kwa utekelezaji thabiti utaonesha namna ambavyo Watanzania tuko mbele na kusema kwamba mradi huo wa tiba mtandao anauelewa na ameupigania sana nje ya nchi ambako amekwenda kuzungumza. “Mwaka jana mwezi Desemba nilienda kwenye mkutano Washington unaohusu Tiba mtandao na tumeuza sana hili wazo la tiba mtandao kwa wenzetu, kwa hiyo watakuja kujifunza tunafanyaje” alisema Dk. Ulisubisya na kuongeza kwamba Wizara yake itatoa ushirikiano wa kutosha kuona dhana hiyo inatekelezeka tena kwa ufanisi. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) akitoa maoni wakati wa kufunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. 
Kwa mujibu wa mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu na kutanuka kwa jinsi inavyowezekana kwa kuangalia ufanisi wa kijiji. “Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira Tiba mtandao katika kijiji hicho itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na watendaji waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa. Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Tehama wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Felix Sukums akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao kwa mgeni rasmi (hayupo pichani), Kushoto ni Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen.[/caption] Aidha akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo Zulmira alitaka kuwapo kwa matumizi ya maabara ya kisasa iliyopo hapo ili iweze kusaidia taifa. Hata hivyo mwakilishi huyo wa UNESCO alisema kwamba Daktari wa wilaya ambako kijiji cha Ololosokwan kipo anahitaji kiasi cha dola elfu 70 kukamilisha baadhi ya mambo ili kuwa na uhakika pamoja na kuleta madaktari wa Afrika mabingwa kuja kufanya kazi kwa muda. Akizungumzia suala hilo, Dk Ulisubisya alisema kwamba anajua shida iliyopo, lakini akamwagiza DMO kukaa na DAS (Katibu Tawala Ngorongoro) kuona namna ya kufanikisha haja ya sasa ya nyumba za makazi kwa gharama nafuu na kusema anaamini wanaofaidika wako tayari kusaidia kidogo. Alisema bajeti hiyo naamini inaweza kupungua kwa kutumia mali ghafi rahisi yenye kudumu zaidi. [caption id="attachment_2081" align="aligncenter" width="1404"] Majadiliano yakiendelea katika kuboresha mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao wa kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika MUHAS.[/caption] Pia aliwashukuru UNESCO kwa kuwezesha Ololosokwan kuwa sehemu ya kujifunza na kutanua mradi wa tiba mtandao ambao amesema kwa kuzingatia teknolojia iliyopo sasa Watanzania na dunia kwa ujumla wanapata nafasi ya tiba bila kuwa karibu na bingwa. Katika utekelezaji wa mradi huo hatua ya pili mifumo yote (maunganisho ya kisetelaiti) inatarajiwa kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuanza matibabu ifikapo Oktoba mwaka huu au mapema zaidi. Mradi huo unoanza kwa majaribio unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwani na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao. Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akifafanua jambo kwa mgeni rasmi wakati wa kuhitimisha warsha hiyo. 
Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mwezi Novemba mwaka 2016. Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo. Warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha , Manyara , Kilimanjaro na Dar es salaam ilichambua dhana ya tiba mtandao na kuidadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na na namna ya kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini. Mmoja wa washiriki akiwalisha maoni kwenye warsha ya siku 1 ya kujadili mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyomalizika MUHAS jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini wataalamu kutoka KCMC, MUHAS, UNESCO, wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akimshukuru mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya mara baada ya kufunga warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) baada ya kuhitimisha warsha ya siku 2 ya mradi wa tiba mtandao iliyofanyika jijini Dar es Salaa., MUHAS. Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akimpongeza Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen mara baada ya kufunga warsha ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam.
SHUJAAZ RADIO SHOW NA CHANGAMOTO ZA WASICHANA

SHUJAAZ RADIO SHOW NA CHANGAMOTO ZA WASICHANA

May 19, 2017

Ile show ya redio ya vijana maarufu kama Shujaaz Radio Show ikiongozwa na DJ Tee, wiki hii tarehe 20 itakuwa inaangalia matatizo yanayowakumbwa wasichana kutokana na shule kuwa mbali na makazi yao hivyo kusababisha mafanikio duni katika elimu ya wasichana nchini Tanzania.

"Kwa sababu pia ni story inayozungumziwa sana hapa Bongo kwa sasa hasa suala la sheria ya kumrudisha msichana shuleni baada ya kujifungua, tumeamua kuungana kwa pamoja na vijana wengine kulizungumzia hili kwa kina." alisema DJ Tee.

Shujaaz Radio Show husikika kila Jumamosi kupitia vituo vitano vya redio nchini Tanzania, vikiwemo East Africa Radio (saa tisa alasiri) na TBC FM (saa kumi na moja jioni). Vituo vingine ni Abood FM ya Morogoro (saa nne asubuhi), Chuchu FM ya Zanzibar (saa tisa alasiri) na Kings FM ya Njombe (saa kumi jioni).