Tuzo za KILI 2014 zimezinduliwa leo, haya ndio mabadiliko yaliyofanywa.
Ni
time ya kufahamu kuhusu tuzo ambazo hutolewa kwa Wanamuziki/Wasanii
mbalimbali wa Tanzania zikiwa zimeanzishwa mwaka 1999 ambapo za mwaka
huu 2014 zimezinduliwa leo February 17.
George Kavishe kutoka TBL ambao ndio Wadhamini wa tuzo hizi amesema
>>> ‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu ni tofauti na
mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga kura
tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category
gani, mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo
Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani’
‘Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia
kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za
kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao kupitia simu ya
mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer gani
aingie kwenye kipengele’ – Kavishe
‘Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura mara mbili ambapo ya
kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena kupiga kura
nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya
Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie
kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama
wimbo uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika
na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’ – Kavishe