KAMA HUJAWAHI KUSHUHUDIA MADAWA YA KULEVYA YANAVYOTEKETEZWA SHUHUDIA SHUGHULI ILIVYOKUWA HAPA TANGA KATIKA KULIFANIKISHA SWALA HILI , “ZAIDI YA KG 2000 ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI ZATEKELEZWA”##

September 28, 2014





 ZAIDI ya kg 2000 za madawa ya kulevya aina ya Bangi yameteketezwa  chini ya Usimamizi wa Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Tanga,Upendo Msuya wakiwemo viongozi mbalimbali wa halmashauri  ya Jiji la Tanga.
Utekelezaji huyo ulifanyika jana kwenye dampo la Duga lililopo Kata ya Duga jijini Tanga ambapo magunia ya dawa za kulevya yapatayo 48 yaliyokamatwa kwenye matukio mbalimbali mkoani hapa yalitekelezwa baada ya kesi za watuhumiwa hao kufanyika.
 
Akizungumza katika utekelezaji huo,Jaji Msuya alisema gunia hizo 48 zilikamatwa kuanzia mwaka 2009 -2013 ndio yaliyotekelezwa kwa awamu ya kwanza ya amri ya mahakama kuu na yaliyotekelezwa kwa awamu ya pili ni amri ya mahakama ambayo ni magunia 14 iliyotolewa na Jaji Msuya.
Alisema kuwa watuhumiwa wa kesi hizo walipatiwa hukumu na walikiwsha kutekeleza vifungo mbalimbali gerezani na wengine walilipa faini ya kati ya milioni 4 hadi 5.
Aidha alisema kuwa watuhumiwa waliokamatwa kutokana mwaka 2011 walikuwa na 10 waliokuwa wametumikia vifungo wakiwemo madereva wa magari na wasafirishaji.
Awali akizungumza mara baada ya tukio hilo,Ofisa Upelekezi Mkoa wa Tanga (RCO),Aziz Kimatta alisema utumiaji wa dawa hayo una madhara makubwa sana kwa binadamu na hivyo kuwataka viongozi wa dini  kuhakikisha wanatoa elimu kwa waumini wao ili kuweza kutokomeza hali hiyo kwenye jamii.
  “Kimsingi ili kuweza kutokomeza hali hii lazima jamii itambue kuwa dawa hizo zina athari kubwa sana kwao pamoja na viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa elimu kupitia mawaidha mbalimbali madhara yake ili kuwabadili kuacha kutumia madawa hayo “Alisema RCO Kimatta.
 
ARJEN ROBBEN KIBOKO...ATAKA KUJENGA NYUMBA BINAFSI YA MAKUMBUSHO

ARJEN ROBBEN KIBOKO...ATAKA KUJENGA NYUMBA BINAFSI YA MAKUMBUSHO

September 28, 2014


Arjen Robben plans to build a museum at home to house the many souvenirs from his illustrious career
Arjen Robben anapanga kujenga nyumba ya makumbusho

WANASOKA wengi wanafanikiwa kutunza vitu vichache kati ya vingi walivyoshinda katika maisha yao ya soka.
Lakini nyota wa Bayern Munich, Arjen Robben amekuwa na wazo la kutunza kila kitu alichofanikiwa kushinda.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Chelsea na PSV Eindhoven  ametangaza kuwa ana mpango wa kujenga nyumba ndogo ya makumbusho na kutunza vitu vyote alivyoshinda kama ishara ya kumkumbuka akimaliza maisha yake.
"Nikiwa nimekaa na mke wangu ndani, niliota kukusanya vitu vyote na kujenga nyumba binafsi ya makumbusho. Itakuwa kwa ajili yangu, familia yangu na marafiki zangu wa karibu," nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliwaambia Bild.
The Dutchman is determined to ensure than 'nothing is lost' from his time at some of Europe's top clubs
Mholanzi huyu anahakikisha kuwa kila alichoshinda hakisahauliki 
Robben won a La Liga title and the Spanish Super Cup during his time at the mighty Real Madrid
Robben alishinda La Liga na kombe la ligi la Hispania wakati huo akicheza Real Madrid

"Nina vitu vingi-zikiwemo jezi za wachezaji wengine. Nimetunza mpira kutoka fainali ya ligi ya mabingwa 2013 (Bayern ikiifunga Borussia Dortmund 2-1 na Robben alifunga goli la ushindi dakika za majeruhi).
"Kuna viatu nilivyoshinda katika michuano ya ubingwa ulaya na kombe la dunia. Wazo ni kuvikusanya pamoja ili kisipotee hata kimoja".
KATIBU MKUU WA CCM A.KINANA AANZA ZIARA WILAYANI LUSHOTO

KATIBU MKUU WA CCM A.KINANA AANZA ZIARA WILAYANI LUSHOTO

September 28, 2014

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kitongoji cha Kwesimu wakati alipokitembelea kikundi cha kuhifadhi  Mazingira katika eneo hilo ambapo ameshiriki kazi za mikono za kuotesha miche katika kikundi hicho, Kinana leo ameanza ziara ya kikazi wilayani Lushoto akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, akiwa ameongoza na na Nape Nnauye  Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi katikati na kulia ni Mh. Henry Shekifu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LUSHOTO-TANGA) 1 
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo.4 
Baadhi ya miche ambayo imeoteshwa na kikundi cha kutunza mazingira cha Kwesimu mjini wilayani Lushoto.5 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.  10 11 
Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Mh. Steven Ngonyani akiwahutubia wananchi wa Mlola wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo 13 
Mkuu wa wilaya ya Lushoto  Mhe. Majid Hemed Mwanga akifafanua jambo kwa wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa wananchi. 18 
Mmoja wa akina mama waliofika kwenye mkutano huo akiuliza swali kuhusu mambo ya afya.

MATUKIO KATIKA PICHA MKWAKWANI KATIKA MECHI KATI YA MGAMBO JKT NA STAND UNITED

September 28, 2014



KIKOSI CHA MGAMBO JKT KILICHOCHAPWA GOLI 1 DHIDI YA STAND UNITED KATIKA UWANJA WA CCM MKWAKWANI TANGA SEPT 27