PANONE FC ILIVYOPOKEA UGENI WA REAL MADRID KILIMANJARO.

August 25, 2014


Waziri wa Vijana,Utamaduni na Michezo Dk Fenera Mkangara akiongoza ugeni toka klabu ya Real Madrid ulipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA.)
Baadhi ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa KIA .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Panone Ltd Patrick Ngiloi akisalimiana na mmoja wa wageni waliokuwa wameambatana na ugeni huo.
Magwiji hao walipokelewa na ngoma ya asili kutoka kikundi cha Msanja cha mjini Moshi.
MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA GRACA MACHEL KWENYE OFISI ZA WAMA .

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA GRACA MACHEL KWENYE OFISI ZA WAMA .

August 25, 2014

IMG_9220
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Mama Graca Machel aliyemtembelea kwenye ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
IMG_9235
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Graca Machel wanaonekana wakifurahia jambo kabla ya kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya WAMA.
IMG_9239
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni wake Mama Graca Machel na wajumbe wawili wa Bodi ya WAMA. Wajumbe hao ni Mheshimiwa Sophia Simba,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (kulia) na Mama Hulda Kibacha (wa kwanza kushoto).
IMG_9252
Mama Garaca Machel akiweka saini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
IMG_9283
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake Mama Graca Machel aliyemtembelea ofisini kwake tarehe 25.8.2014.
IMG_9326
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mama Graca Machel kwenye ofisi za Taasisi hiyo zilizoko karibu na Ikulu.
IMG_9344
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi baadhi ya majarida yanayochapishwa na Taasisi ya WAMA kwa Mgeni wake Mama Graca Machel.
IMG_9354
Picha ya pamoja kati ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wafanyakazi wa Taasissi ya WAMA na Mama Graca Machel na ujumbe wake mara baada ya kufanya mgeni uyo kutembelea ofisi hiyo tarehe 25.8.2014.
IMG_9369
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwaga Mgeni wake Mama Graca Machel wakati akiondoka kwenye ofisi ya WAMA baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo.
IMG_9379
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuagana na Mgeni wake Mama Graca Machel nje ya ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI.
Rais Kikwete atunuku Kamisheni TMA Monduli

Rais Kikwete atunuku Kamisheni TMA Monduli

August 25, 2014

D92A6383
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa majeshi wa kwanza Mzalendo Jenerali Mirisho Sarakikya muda mfupi baada ya kuwasili katika chuo cha jeshi Monduli tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maofisa 179 wapya wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao mwishoni mwa wiki.
D92A6430
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange kushoto na Mkuu wa Chuo cha Jeshi (TMA) Monduli Brigedia Jenerali Paul Peter Massao(kulia) wakimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho kwenda uwanja wa Paredi ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa jeshi katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi(TMA) mkoani Arusha.
D92A6441
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.
D92A6497
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.
D92A6512
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Paredi kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.
D92A6553
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi hkwenye  uwanja wa Paredi la kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.
D92A6628
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
D92A6697
Kikosi cha Bendera kikipita  mbele ya Amiri jeshi mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
D92A6761
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.