UJUMBE WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA - NDC - WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA JIJINI DAR

February 23, 2017
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(meza kuu) akiongea na ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa. Ujumbe huo wa Washiriki wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini leo Februari 23, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisisitiza jambo kwa Maafisa kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa utambulisho mfupi kwa Wakufunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania alioambatananao katika ziara ya mafunzo.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana katika picha
 Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakipata maelezo mafupi toka kwa Wataalam wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo katika Kiwanda 
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akijalibisha kiti Maalum cha kunesa kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa katika Kiwanda cha Seremala Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam kama inavyoonekana katika picha.
 Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani).
 Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akikabidhi zawadi kwa Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya(kushoto) mara baada ya uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(wa sita toka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzo waliyoifanya katika Jeshi la Magereza(wa nne toka kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Friedkin Conservation Fund yachangia Saruji mifuko 3000 na Mabati 1000 Simiyu

Friedkin Conservation Fund yachangia Saruji mifuko 3000 na Mabati 1000 Simiyu

February 23, 2017
Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 ikiwa ni msaada. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika tukio hilo. Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Pratik Patel akizungumza katika tukio la kampuni hiyo kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo yaani Mwiba Holdings pamoja na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 kama msaada. Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (kulia) akimtamkia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) kuwa mbali na kampuni hiyo kutoa mifuko 3000 ya saruji kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Wataongeza msaada wa mabati 1000. Wengine ni Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa FCF, Pratik Patel (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.[/caption] Na Mwandishi Wetu, Simiyu KAMPUNI kitalii zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechangia mifuko 3000 ya saruji na mabati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani humo. Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mkono mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli kuendeleza elimu ya hasa katika maeneo ya wafugaji ambako kampuni hizo zinafanya shughuli za uwindaji wa kitalii. Kampuni zilizokabidhi misaada hiyo juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa ni pamoja na Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja zimetoa saruji hiyo yenye thamani ya sh milioni 48 na mabati yakiwa na thamani ya sh milioni 25. Vifaa hivyo vya ujenzi vitatumika kujenga vyumba vya madarasa na mabweni kwa ajili ya shule zitakazotumiwa na watoto wa jamii za wafugaji zinazoishi jirani na maeneo ya shughuli za uwindaji wa kitalii wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu.   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia tamko la Mkurugenzi, Abdulkadir Mohamed (hayupo pichani) kuahidi kuongeza msaada wa mabati 1000 huku Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akikabidhiwa kipaza sauti kurudia kauli ya neema za mabati 1000 toka FCF.] Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni ya FCF kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka pamoja na Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi mchango huo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, wakati wa hafla iliyofanyikia katika viwanja vya stendi Mjini Mwanhnuzi, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Abdulkadir Mohamed alisema kuwa mchango huo unatokana na kuanzishwa kwa mfuko uwekezaji katika pori hilo. "Tunatoa msaada huo ikiwa ni kuunga mkono Serikali yetu ya awamu ya tano katika jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini,na tumeanza kuwasaidia wananchi tunaoshirikiana nao katika shughuli za uhifadhi na huu ndio mwanzo wa kuendeleza ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii,” alisisitiza Mkurugenzi huyo Alisema kuwa pamoja na kuchangia misaada hiyo,kampuni yake imekuwa ikitoa misaada katika vijiji tisa vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama Pori Makao (WMA) na ranchi ya Mwiba hasa katika kusaidia uboreshaji wa huduma za jamii na hasa elimu. “ Mpaka sasa Kampuni kupitia makampuni yake matatu tayari wamechangia kiasi cha sh Milioni 3000 kwa vijiji tisa pamoja na vingine 15 vinavyopakana pori hilo, ambapo shule, zahanati, pamoja na vituo vya maendeleo vimejsengwa katika vijiji hivyo kwa kushirikiana na halmashauri” Alisema Mohamed. Aidha, aliongeza kuwa mchango huo umechangiwa na mafanikio mazuri ya shughuli za utalii zinazoendelea katika maeneo hayo na uwekezaji wa kampuni hiyo wilayani humo, huku akibainisha kuwa shughuli hizo zinazidi kupanda kila mwaka wilayani humo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiongozana na wageni wake katika hafla hiyo. Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akijitambulisha katika hafla ya FCF kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu

 Mkurugenzi huyo aliahidi kuwa kutokana na kuimarika kwa shughuli hizo na kuwepo kwa mazingira mazuri ya uwekezaji,hasa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wananchi, hasa wavijiji vinavyopakana na pori hilo, wamepanga kuongeza uwekezaji wao kwa dola za kimarekani milioni 100. 

 Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum Mkoa (CCM) Leah Komanya alipongeza mchango wa mwekezaji huyo, huku akiunga mkono kwa kuchangia mabati 50 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Makao. 

 “ niwaombe hawa wawekezaji wetu wasichangie kwenye vijiji hivyo tisa peke yake, bali wachangie hata kwenye kata nyingine za wilaya yetu ambayo ipo chini sana kielimu ili kila mwananchi atambue mchango wao, na niwapongeze kwa kuunga mkono ujenzi wa shule hasa mabweni kwa watoto wa kike” Alisema Komanya 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, akizungumza kabla ya kupokea msaada huo, alimtaka Mkurugenzi huyo ambao alidai kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro ya kila mara kati ya wananchi na kampuni hiyo ili kurejesha imani ya kuendelea kushirikiana na wawekezaji hao. Mbali na hilo Mtaka alipongeza Kampuni hiyo kwa mchango wake, huku akielelekeza saruji hiyo pamoja na mabati vitumike kwa ajili ya kujenga mabweni katika shule za sekondari zinazopakana na pori hilo. 

 Mtaka aliwataka wawekezaji hao kuwa karibu na wananchi kwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri na alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuwapatia kiwanja cha kujenga ofisi ili iweze kuratibu kwa karibu ushirikiano huo na wananchi. 

Kwa sasa mgogoro uliodaiwa kuwapo kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wa Makao, umemalizika baada ya msuluhishi aliyeteuliwa na pande zote mbili, Jaji Thomas Mihayo, kutoa uamuzi hivi karibuni baada ya walalamikaji kushindwa kuwasilisha utetezi wao kwa wakati. 

Hata hivyo, taarifa zimeeleza kwamba hali hiyo imetokana na kurejea kwa mahusiano kati ya pande hizo mbili na kuonekana njia bora zaidi ya kusuluhisha migogoro ni mazungumzo yasiyo na gharama zinazoweza kuigharimu serikali ya kijiji na wilaya. --

TPDC WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

February 23, 2017
Wanahabari mkoa  wa  Iringa  walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa.
 Wanahabari mkoa  wa  Njombe   walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa 

Wanahabari mkoa  wa  Ruvuma   walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa 
 Meneja mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu (TPDC)  akitoa  neno wakati wa utangulizi wa warsha hiyo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma.

Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe  ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.

“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.

Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya nchi yetu.

‘’Waandishi Wahabari mnapaswa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa uchumi wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili kuisaidia kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi kiuzalendo.”

Aliongeza kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa Taifa, mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha wananchi wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba hilo litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza kujenga nchi yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.

Kasesela alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za kikabila, kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye kujenga nchi yetu na si vinginevyo.

Alisisitiza vile vile juu ya utoaji taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au uharibifu wa aina yoyote katika miundombinu hii, akiongea katika warsha hiyo alisema “miundombinu hii ya gesi na mafuta ni mali ya watanzania hivyo kuilinda ni jukumu letu sote kama wazalendo wa nchii hii”.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Afisa mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu alisema warsha hii inalenga kuendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wetu wa habari kuweza kuripoti kwa umahiri na ustadi habari za mafuta na gesi.

Mselemu aliwashukuru waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuupasha habari umma na kuwaasa kwamba kalamu yao ina nguvu hivyo ni vyema ikaendelea kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa kutoa taarifa sahihi kila wakati.

Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa juu (TPDC) alisisitiza juu ya matarajio yasiyo halisia yaliyopo miongoni mwa wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari kusaidia kuwaeleza wananchi juu ya uhalisia wa sekta.

Kayombo alisema kwamba uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                            
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.
Hata hivyo Kayombo alisisitiza juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza bidhaa.

Naye mwanasheria wa TPDC  Barnabas Mwashambwa alisema sheria mpya ya petroli ya mwaka 2015 inawataka wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kama ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni iingie ubia na kampuni ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.
Sheria imeeleza kwamba ubia huo lazima umpe mzawa ushiriki usiopunguza asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na ni vyema ikachangamkiwa.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad ameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda wa kutosha zaidi katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema sekta, ombi ambalo liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.

Katika mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na Faida Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye Vituo vya Kujaza Magari. 
TPDC imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hii mpya na changa ya mafuta na gesi hapa nchini.

Benki ya Standard Chartered yakabidhi vifaa vya michezo kwa Coca Cola, Mwananchi

February 23, 2017
 Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited, Bakari Machumu (wa kwanza kushoto) vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100  tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) na Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited ambaye ni bingwa mtetezi Majuto Omary (wa pili kulia).
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) akimkabidhi Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited, Bakari Machumu (wa kwanza kushoto) vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100  tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa kwanza kulia) pamoja na kwa Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited, Majuto Omar (wa pili kulia) wakati wa halfa fupi ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited, Majuto Omar ( kulia) seti ya jezi  kwenye hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (katikati).
 Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa pili kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya Coca cola, Samuel Mwakatumbula wa pili kutoka (wa pili kushoto) kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100  tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa kwanza kushoto), Simon Masanja mchezaji wa timu ya Coca cola (wa kwanza kulia) na Salehe Omar mchezaji wa timu ya Coca cola (katikati).
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wachezaji wa timu ya Coca cola, Simon Masanja (kulia) vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100  tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa pili kulia), Mwenyekiti wa timu ya Coca cola, Samuel Mwakatumbula wa pili kutoka (wa pili kushoto) na Salehe Omar mchezaji wa timu ya Coca cola (katikati).

Na Mwandishi wetu,
Benki kongwe nchini Standard Chartered imekabidhi vifaa kwa timu za Mwananchi Communication Limited na Coca cola kwa ajili ya mashindano ya ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anified) yaliyopangwa kufanyika Jumamosi, kwenye viwanja vya JMK Park Kidongo Chekundu.
Mbali ya kutafuta washindi wa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Afrika Mashariki, mashindano hayo pia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100  tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba amesema jumla ya timu 32 kutoka mashirika mbalimbali yanatashiriki katika  mashindano hayo.
“Tunatarajia timu 32 kushiriki hapa nchini na mshindi ataweza kuingia kwenye fainali ya Kanda ya Afrika Mashariki itakayoshirikisha timu moja moja kutoka Keny na Uganda, ambapo mshindi, atakwenda Liverpool kuangalia moja ya mechi za ligi kuu ya Uingereza ya Liverpool na vile vile kushindana katika mashindano mengine yatakayoshirikisha timu kutoka mabara ,”  alisema Mramba.
Mbali ya mashindano, mshindi pia atapata mafunzo ya siku tatu kujifunza mambo ya soka na kutoka kwa magwiji wa mashindano hayo.
Mramba amesema kwamba benki hiyo ya Standard Chartered ilianzishwa mwaka 1917 na mwaka huu inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na imetenga zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 100 kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kutimiza umri huo kwenye sekta ya kifedha.
Wakati huo huo mmoja  wa wachezaji waliowika miaka ya themanini na tisini wa timu ya Liverpool, John Barnes atawasili nchini mwanzoni mwa mwezi Machi tayari kwa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 yatakayohusisha timu za makampuni katika eneo hili la Afrika Mashariki.
Uzinduzi wa  awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, yenye kauli mbiu “barabara ya kuelekea Anfield” inatarajiwa kutimua vumbi kwenye viwanja  vya Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo timu mbili za wachezaji watano watano zitacheza kwa dakika kumi na mshindi atapewa zawadi.
Mashindano hayo ya Standard Chartered yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii kwenye viwanja vya JK Youth Park.
Yakiwa katika mwaka wake wa sita, mashindano ya Kombe la Sndard Chartered yamekuwa yakiimarika mwaka hata mwaka na kutoa washindi kutoka pande zote za dunia. Mataifa ambayo yamenyakua kombe hilo ni pamoja na Kenya (2016), Korea Kusini (2015) Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012).
-- Zainul A. Mzige, Managing Director, Mzige Media Limited, www.thebeauty.co.tz +255714940992.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan, Ivory Coast

February 23, 2017
 Rais Mstaafu na  Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa za ELimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina alipomtembelea katika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast.
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Kikwete amewasilisha kwa Rais Adesina ripoti ya Kamisheni ya Elimu na kuwasilisha rai ya Kamisheni hiyo ya kuiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia nchi za Afrika kugharamia miradi na mageuzi ya sekta ya elimu katika nchi zao. Rai hiyo ya Kamisheni inatokana na ripoti kubaini kuwa misaada na mikopo inayotolewa kwa sekta ya elimu imekuwa ikishuka ikilinganisha na zile zinazotolewa kwa miradi ya afya na miundombinu. Kamisheni inaamini kuwa bila kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, watoto wapatao milioni 223 duniani (takribani milioni 160 wakiwa Afrika) watakosa fursa ya kupata elimu ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Rais Adesina ameupokea ujumbe huo na kusema kuwa takwimu zilizoibuliwa na Ripoti ya Kamisheni 'zinakatisha tamaa na pia zinatoa changamoto'. Rais Adesina ameahidi kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika itaitizama Ripoti hiyo na mapendekezo yake na iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Kamisheni katika kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo katika elimu barani Afrika. Amesema kuwa Benki yake inatambua kuwa kuwekeza katika vijana na nguvu kazi ya Afrika ndio jawabu la maendeleo ya uhakika huko mbeleni.
Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Makhtar Diop pembezoni mwa mkutano wake na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Ziara ya Rais Mstaafu nchini Ivory Coast itahitimishwa kwa kukutana na Rais wa Ivory Coast Mhe. Alassane Ouattara.
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya ELimu, Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa kwa furaha na mwenyeji wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina ofisini kwake jijini  Abidjan, Ivory Coast
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha ripoti ya Kizazi cha Elimu kwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Adesina
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt, Makthar Diop pembezoni mwa mkutano huo.

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALLY HASSAN MWINYI KATIKA SHEREHE YA UHURU WA KUWAIT USIKU HUU JIJINI DAR ES SALAAM

February 23, 2017
 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
  Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
Keki ya hafla hiyo  ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. 
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiwa katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kulia kwake  ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga.

Rais Magufuli awapongeza madaktari Muhimbili na amsaidia Neema Mwita Wambura aliyeunguzwa moto kifuani

February 23, 2017


 Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano.  Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.
 Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.
  Dada Neema Mwita Wambura (32) wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni  kitendo kilichofanywa na mume wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema Mwita Wambura (32) mara baada ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada Neema Mwita alifanyiwa upasuaji mara nne katika siku za nyuma hospitalini hapo Muhimbili ili kutibu majeraha yake hayo ya moto.