SAMPULI ZA MAJI YA MTO MSIMABI ZAPIMWA.

July 11, 2017
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumzana wanahabari katikati yam to Msimbazi chini ya Daraja la jangwani baada ya kupima kiwango cha hewa ya Oxygen katika maji ya mto msimbazi na sampuli za maji hayo kupelekwa katika katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali kwa vipimo zaidi, ili kujua kama maji hayo yana madhara kwabinadamu, mazingira na viumbe hai wengine.



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akiangalia kiasi cha hewa ya oxygen kilochopo katika maji yam to msimbazi akisaidiwa na wataalamu kutoka katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali hawapo pichani, katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Evelyn Mkokoi)

ZIMEBAKI SIKU TATU KUFANYIKA KWA MAOMBI YA SHUKRANI KITAIFA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM NI JUMAMOSI

July 11, 2017

Taasisi ya MO Dewji yatunukiwa tuzo ya ubora ya Superbrand

Taasisi ya MO Dewji yatunukiwa tuzo ya ubora ya Superbrand

July 11, 2017
Taasisi ya MO Dewji inayojuhusisha na kusaidia jamii katika elimu, afya na maendeleo ya jamii imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora inayofahamika kama SuperBrand. Taasisi hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji imetunukiwa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ambayo inaifanya. Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema ni heshima kubwa kwa taasisi kupata tuzo hiyo lakini pia itawasaidia kufanikisha miradi mikubwa ambayo wamepanga kuifanya na taasisi kubwa kama ya Bill Gates.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya ubora ya SuperBrand.
“Kwa niaba ya Taasisi ya MO Dewji na kampuni ya MeTL Group tunashukuru sana kwa tuzo hii na huu ni mwanzo mpya wa safari yetu, kama mnavyojua taasisi yetu ilianzishwa mwaka 2014 na katika kipindi cha miaka miwili tumeanzisha miradi mbalimbali kama MO Entrepreneurs na MO Scholars ikiwa na lengo la kuwasaida vijana na tunafuraha Baraza la SuperBrands limetutambua, “Tuzo hii inatusaidia katika miradi mikubwa kwa sasa kama taasisi ya Mohammed Dewji tunataka kufanya ushirikiano na taasisi kubwa kama Taasisi ya Bill Gates, kushirikiana na taasisi za Kenya, Uganda, UK, jina la Mohammed Dewji litakuwa la kwanza na SuperBrand litakuwa ya pili,” amesema Barbara.
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez tuzo ya ubora ya SuperBrand.
Tuzo ya SuperBrand ambayo Taasisi ya MO Dewji imetunukiwa.