Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya RAILA ODINGA amtembelea Rais Dkt. JOHN MAGUFULI wilayani CHATO

April 02, 2016
. Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasili
kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kwenda
kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 
………………………
Waziri Mkuu
Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni
katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
 
Mheshimiwa Odinga
ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga,
wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02
April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais
Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe
Mama Janeth Magufuli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake
Chato mkoani Geita mara baada ya Kuwasili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana na
Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga mara baada ya kuwasili nyumbani
kwake Chato Mkoani Geita.
 
Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
 
“Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato” Alisema Mheshimiwa Odinga.
 
 
Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.
Waziri
Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli mara baada ya kuwasili Chato.
. Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwa na Rais
John Magufuli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Odinga
Bi. Ida Odinga wakisali kwenye makaburi ya familia ya Mhe. Rais Chato Mkoani
Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na
mama mzazi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara
baada ya kuwasili Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyepo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
“Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato” Alisema Mheshimiwa Odinga.
Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama Mzazi wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
02 April, 2016
Waziri Prof. Mbarawa aongea na wafanyakazi wa Mkoa wa Kigoma na Katavi.

Waziri Prof. Mbarawa aongea na wafanyakazi wa Mkoa wa Kigoma na Katavi.

April 02, 2016

RW1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiongea na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo wakati akifanya majumuisho ya ziara yake, mkoani Kigoma.
RW2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akiangalia namna mkonogo wa Taifa ulivyopitishwa katika moja ya madaraja ya Mto Malagarasi. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Kamugisha Kazaura akiangalia kwa makini.
RW3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma….. wakati alipomtembelea ofisini kwake.
RW4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tano kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoani Kigoma.
RW5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst) Raphael Muhuga wakati alipomtembelea ofisini kwake.
RW6
Wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakimsikiliza Waziri wa Wizara Prof. Makame Mbarawa, (hayupo pichani), wakati alipoongea nao mkoani Katavi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

LA KWETU CONCERT, TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI 2016 KUFANYIKA NCHINI TANZANIA.

April 02, 2016
Linatarajiwa Kufanyika Tamasha Kubwa la Muziki wa Injili hapa nchini. Tamasha hilo limepewa jina la "LA KWETU CONCERT" na litafanyika katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga, Mbeya, Arusha, Dar es salaam na mingineyo.

Tamasha hilo linaandaliwa kwa Ushirikiano na Waimbaji wa Muziki wa Injili, Watangazaji na Waandishi wa Habari chini ya Kampuni ya FAMARA INTERTAINMENT ya Jijini Mwanza, ambapo wadau mbalimbali wanakaribishwa ili kufanikisha tamasha hilo ambalo litakuwa la aina yake.

NOAH YAACHA NJIA BANDARINI JIJINI DAR ES SALAAM NA KUTUMBUKIA KWENYE MTAR

April 02, 2016
 Mwananchi wakiangalia ajali ya Noah yenye namba za usajili T 367 DAK iliyoacha njia na kutumbukia kwenye mtaro jirani na Kanisa la Mtakatifu Joseph, Bandarini Dar es Salaam jana asubuhi.
 "Ni kama anaongea maskini mmiliki wa Noa hii hivi watu waliokuwa wamepanda wamesalimika ?"

 Noa ikiwa mtaroni. Chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kufahamika.

ZAIDI YA WAFANYAKAZI 250 WA DAWASCO WAFANYA USAFI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

April 02, 2016
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco ) Mhandisi Cyprian Luhemeja akishiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watumishi wa Dawasco.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiweka maji katika moja ya mashine inayotumika kuzibulia miundombinu ya maji taka ijulikanayo kama Jet Machine.
Wafanyakazi wa Dawasco wakijaribu kuweka sawa mpira wa kunyunyiza maji ili kuondoa vumbi wakati wakifanya usafi katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Wafanyakazi wa Dawasco  wakiendelea na usafi katika maeneo mbalimbali ya Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Afisa Mtendaji Mkuu Dawasco Mhandisi Cyprin Luhemeja akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi baada ya kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Wengine ni wafanyakazi wa Dawasco.
Wafanyakazi wa Dawasco wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi ,Cyprian Luhemeja akitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala ,Raymond Mushi ambaye pia alikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na Dawasco mara baada ya wafanyakazi wake kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi akizungumza na wafanyakazi wa Dawasco mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitali hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco akizungumza na wanahabri mara baada ya kufanya zoezi la usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meneja wa Dawasco eneo la Magomeni Mhandisi Paschal Fumbuka akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitai ya Taifa ya Muhimbili.
Baadhi ya vitendea kazi vya Dawasco vikiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .
 (0755659929)

KATIBU MKUU UVCCM TAIFA KUUNGURUMA KATIKA MKUTANO WA HADHARA HII LEO JIJINI MWANZA.

April 02, 2016
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Katibu Mkuu Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM Taifa), Shaka Hamdu Shaka, hii leo anatarajiwa kuunguruma Jijini Mwanza, katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kirumba, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Zidi Bonyeza HAPA

JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA ITAKUWA NI MIEZI MITATU KWA NCHI NZIMA

April 02, 2016
 Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo.
 Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha  Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.

Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.


Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na  kuzisajili na kufanya malipo  katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri. 

Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa

"Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi" alisema Mssanzya.

Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.

Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.

"Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)