MAJAMBAZI WAPORA MILIONI 126 ADA ZA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MTAKATIFU CHRISTINA TANGA.

February 01, 2015


WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia juzi walivunja ofisi ya mhasibu katika shule ya sekondari Mtakatifu Christina iliyopo kata ya Maweni Tarafa ya Pongwe na kufanikiwa kuiba fedha taslimu milioni 126 ambao ziliokuwa ni ada za wanafunzi katika shule hiyo.

Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (ACP),Juma Ndaki alisema tukio hilo lilitokea Januari 26 mwaka huu saa kumi usiku katika shule hiyo iliyopo wilaya ya Tanga.

Akielezea namna tukio hilo lilivyogundulika, Kaimu Kamanda Ndaki alisema kuwa Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Marry Singano (66) kabila Mhehe na Mkazi wa Sahare jijini Tanga aligundua kuvunjwa kwa ofisi ya uhasibu na kuibiwa fedha hizo.

Alisema kuwa baada ya watu hao kuiba fedha hizo walichoma moto ofisi hiyo ya mhasibu na kisha kutokomea kusikojulikana.

Aidha alisema kuwa katika tukio hilo wapo watu watano wanaotiliwa mashaka ambao ni Jefta Mtiba Kabula na wenzake na hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na upelelezi unaendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika.

Wakati huo huo,mkazi mmoja wa jijini Tanga alifariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki eneo la Nyinda Mtendelee wakati akitembea kwa miguu.

Kaimu kamanda Ndaki alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 26 mwaka huu saa nane na nusu mchana huku maeneo ya ofisi ya ardhi kata ya Majengo Tarafa ya Ngamiani Kati wilaya ya Tanga.

Alitaja pikipiki yenye namba T.116 CQQ aina ya Huoniao ikiendeshwa na mtu asiyefahamika ilimgonga mtembea kwa miguu Tiki Wendo(24) Dereva na mkazi wa Nguvumali na kufariki dunia .

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wakati mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo na msako mkali unaendelea kumtafuta.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »