RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA WIZARA YA KAZI,UWEZESHAJI,WAZEE,VIJANA,WANAWAKE NA WATOTO

RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA WIZARA YA KAZI,UWEZESHAJI,WAZEE,VIJANA,WANAWAKE NA WATOTO

October 20, 2016
z1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto katika  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
z2
Viongozi katika Wizara ya  Viongozi katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
z3
Waziri wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  Mhe,Moudline Cyrus Castico akisoma   utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
z4
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Bi.Fatma Gharibu Bilali (kulia) akifafanua vifungu vya utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 katika kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kushoto) Mshauri wa Rais ushikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Ikulu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,
z5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (katikati) wakati akichangia katika kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja (kushoto) Waziri wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  Mhe,Moudline Cyrus Castico,
z6
Mkurugenzi wa Ajira Ameir Ali Ameir katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto akielezea mifumo na utaratibu wa Ajira wakati katika kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 katika   robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016, kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 20/10 /2016.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA NSSF JIJINI ARUSHA, SERIKALI YAPUNGUZA DENI LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

October 20, 2016


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali tayari imeshalipa sh. bilioni 722.7 kati ya sh. bilioni 964.2 za madeni ya michango ya jumla ambayo Serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini. 
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 20, 2016) wakati akifungua Mkutano wa Sita wa wadau wa NSSF ulioanza leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Arusha na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 600. 
Amesema sekta hiyo imekua kwa asilimia 15 kutoka sh. trilioni 8.9 mwaka 2015 hadi kufikia sh. trilioni 10.2 mwaka 2016. “Hadi kufikia Juni 2016, takwimu zinaonesha idadi ya wanachama imeongezeka na kufikia milioni 2.1. Rasilmali za mifuko zimefikia shilingi trilioni 10.28 na mafao yaliyolipwa kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Juni 2016 ni shillingi trilioni 2.93. Michango ya wanachama kwa mwaka ni shilingi trilioni 2.15 uwekezaji katika nyanja mbalimbali umefikia kiasi cha shilingi trilioni 9.29,” ameongeza. 
Waziri Mkuu pia amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara awaandikie barua waajiri wote wanaodaiwa na shirika hilo na kuwataka wawasilishe fedha wanayodaiwa mara moja na wale ambao hawatalipa ndani muda utakaowekwa wafikishwe mahakamani na yeye apewe taarifa.

“Kumekuwepo na changamoto ya muda mrefu ya baadhi ya waajiri kutolipa michango kwa wakati hali inayoleta usumbufu mkubwa kwa wanachama hasa wanapofikia muda wa kustaafu. Suala hili halikubaliki, hivyo natoa maelekezo kwa waajiri wote nchini waheshimu sheria na wawasilishe michango yao kwa wakati,” amesisitiza. 
Mbali ya kuwabana waajiri, Waziri Mkuu pia amewataka wanunuzi wa nyumba za shirika hilo na wapangaji wote wanaodaiwa wakamilishe malipo yao na wasipofanya hivyo ndani ya muda uliopangwa wafikishwe mahakamani. 
“Nimeambiwa pia lipo tatizo la wadaiwa wa nyumba yaani wanunuzi na wapangaji. Suala hili lilitolewa maelekezo na Waziri wa Nchi, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu. Nataka nisisitize kuwa watu wote walionunua nyumba za NSSF na bado hawajakamilisha malipo na wale waliopanga lakini hawalipi kodi wanatakiwa kulipa haraka au wakabidhi nyumba hizo kwa NSSF ziuzwe kwa watu wengine, vinginevyo nao wafikishwe mahakamani.”

Akizungumzia utendaji wa shirika hilo, Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa shirika hilo na Bodi ya Wadhamini kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa sukari nchini. Amesema kiwanda kitakachojengwa, kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza wanachama katika mfuko wa NSSF. 

Nimefurahishwa na uamuzi wa NSSF na PPF kuungana ili kukabiliana na tatizo la sukari nchini. Tumeelezwa hapa kuwa mashirika haya yatashirikiana kujenga Kiwanda cha Sukari kitakachozalisha tani 200,000 kwa mwaka. Kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la Mkulazi lililopo mkoani Morogoro,” amesema. 
Mapemaakielezea utendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara alisema limeboresha mafao ya wanachama wake kutoka sh. 80,000 hadi sh. 100,000 kwa mwezi. 
Alisema limeanza kufanya upembuzi yakinifu wa kujenga nyumba za watumishi Dodoma ili kuendana na uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma. “Upembuzi bado unaendelea lakini tumeshabaini kuna uwezekano wa kujenga nyumba 200 hadi 300 mkoani Dodoma,” alisema.

Kuhusu uwekezaji kwenye ujenzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni, Dar es Salaam, Prof. Kahyarara alisema uwekezaji huo unalipa kwa sababu makusanyo ya tozo kwa watumiaji yamefikia asilimia 109. “Tuna uhakika kwamba fedha tulizowekeza zitarudi,” amesisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 45 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 900 yenye thamani ya sh. milioni 15 kwa ajili ya waathirika wa tetememo la ardhi mkoani Kagera. Amepokea msaada huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Prof. Samuel Wangwe. 
Akiwasilisha msaada huo, Prof. Wangwe alisema wameguswa na tatizo lilitokea mkoani Kagera na wameamua kutoa mchango ili kusaidia juhudi za Serikali kukabiliana na maafa hayo. Pia alisema wamekamilisha ahadi yao ya madawati 6,000 yenye thamani ya sh. milioni 400 ambayo waliitoa awali. Waziri Mkuu aliwashukuru kwa misaada hiyo na kuwahakikishia kwamba itafikishwa kwa walengwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. 
 Wabunge Aesh Hilaly  wa Sumbawanga Mjini na  Mohamed Mchengerwa wa Rufiji  wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majliwa wakati alipofungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSFmjini Arusha Oktoba 20, 2016. 

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza   kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba  20, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kupokea tani 45 za saruji  zenye thamani ya shilinigi milioni 15 zilizotolewa na NSSF  kabla ya kufungua  Mkutano wa  Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi, Meneja Mkuu wa Malipo wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Francis Mcharage cheti cha kuthamini michango   ya wafanyakazi wa shirika hilo kwa NSSF kila mwenzi  wakati alipofungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha  (AICC) Oktoba 20, 2016.  Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na wapili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Profesa Samuel Wangwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti  na Usimamizi wa Sekta  ya Hifadhi ya Jamii, Irene Isaka baada ya kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Kongamano la Nne Gesi na Mafuta lafanyika Dar

Kongamano la Nne Gesi na Mafuta lafanyika Dar

October 20, 2016


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akifugua kongamano la nne linalohusu gesi na mafuta lililoambatana na maonesho , lililokutanisha wadau mbalimbali kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto), akibadilishana mawazo na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile (kulia) katika kongamano hilo
Kutoka kulia; mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kongamano hilo.
Washiriki kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa shirika hilo katika kufanikisha kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka Benki ya Standard Chartered, Thomas Bisonga (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka kampuni inayojihusisha na ujenzi wa mabomba ya gesi kutoka China (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Meneja Mawasiliano kutoka kampuni ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini ya Statoil, Genevieve Kasanga (kushoto), akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba akieleza jambo katika kongamano hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (katikati waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa kongamano hilo. 



Na Greyson Mwase, Dar es Salaam 

Kongamano la Nne linalohusu sekta ndogo ya mafuta na gesi lililoambatana na maonesho kuhusu sekta hiyo na kukutanisha Wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni zinazojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, Vyuo Vikuu, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali limeanza kufanyika jijini Dar es Saalaam. 

Kongamano hilo lilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo ambapo aliwaeleza wadau hao kuwa, usimamizi madhubuti wa sekta ndogo ya gesi na mafuta utaleta mapinduzi makubwa kwenye ukuaji wa viwanda na kuiwezesha Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 

Katika kongamano hilo linalofanyika kuanzia tarehe 20 – 21 Oktoba, 2016, Dk. Pallangyo alisema kuwa kutokana na kiasi kikubwa cha gesi kilichogunduliwa ambacho ni futi za ujazo trilioni 57.2, kampuni mbalimbali za kigeni zimeanza kujitokeza na kuwekeza katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo gesi imegunduliwa 

Alisema kutokana na uwekezaji katika shughuli za gesi na mafuta, kumekuwepo na mabadiliko ya kiuchumi katika mikoa hiyo kama vile kuongezeka kwa fursa za ajira, malazi na utoaji wa huduma kwa wawekezaji. 

Aliongeza kuwa ni vyema wananchi hususan wa maeneo hayo kujiandaa na uwekezaji mkubwa katika mikoa hiyo ambapo kwa sasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kunatarajiwa kujengwa viwanda vikubwa vya mbolea, vitakavyoleta neema katika mikoa hiyo. 

Alisema katika kujiandaa na kasi ya ukuaji wa sekta za gesi na mafuta nchini serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na sera na sheria zitakazowezesha wazawa kuwa sehemu ya umiliki wa uchumi wa gesi na mafuta. 

Alitaja mikakati mingine ni pamoja na uanzishwaji wa kozi zinazohusu masuala ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 

Aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikipeleka nje ya nchi kusomea masuala ya gesi na mafuta katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree), wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika ngazi ya shahada. 

“Lengo letu kama Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalam wa kutosha watakaoshiriki katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta,” alisema Dk. Pallangyo. 

Wakati huo huo akizungumza katika kongamano hilo, mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu alisema kuwa lengo la kongamano hilo lilikuwa ni kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu sekta za gesi na mafuta nchini. 

Alisema mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na uelewa kuhusu sekta za gesi na mafuta, sera na sheria za mafuta na gesi, ushirikishwaji wa wazawa kwenye sekta za gesi na mafuta, changamoto na matumizi endelevu ya mafuta na gesi na rushwa. 

Kongamano hilo liliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
WATANZANIA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI NA UZALISHAJI KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI.

WATANZANIA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI NA UZALISHAJI KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI.

October 20, 2016



Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi akielezea mikakati ya KAIZEN kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi wakipokea tuzo zao wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu toka kushoto waliokaa) pamoja na Balozi wa Japan nchini na Mwakilishi wa JICA Tanzania wakiwa katia picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi walioshinda tuzo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

Na. Eliphace Marwa – Maelezo

Watanzania watakiwa kuongeza thamani na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watanzania kuongeza thamani ya bidhaa na uzalishaji ili kuongeza fursa za ajira.

Mwijage ameyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN zinazoratibiwa na Shirika la uhusiano wa kimataifa laJapan (JICA).

“Tuko hapa hii leo kushuhudia sherehe za utoaji wa tuzo katika sekta ya viwanda ambayo ni matunda ya dhana za KAIZEN kwani tuzo hizi zinatolewa kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kutekeleza mbinu za KAIZEN ili kuweza kutoa changamoto kwa makampuni mengine” alisema Mh. Mwijage

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA ofisi ya Tanzania Bw. Toshio Nagase aliipongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na kitengo cha KAIZEN Tanzania kwa kuandaa sherehe yenye mafanikio kwa mara nyingine kufuatia ili iliyofanyika mwaka jana.

“Baada ya uzinduzi wa mpango wa miaka mitano, sisi sote tumetambua umuhimu wa kukuza viwanda ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa Tanzania”, alisema Bw. Toshio

Aidha Bw. Toshio alibainisha baadhi ya maeneo ambayo KAIZEN imefanikiwa kuwa ni pamoja na kuhakikisha ubora wa bidhaa na kubadilisha tabia pamoja na kutoa motisha kwa wafanyakazi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi amesema kuwa anaamini kuitangaza KAIZEN nchini Tanzania ni jambo la muhimu ili kutengeneza viwanda vyenye ushindani na kufanikisha lengo la kukuza viwanda kuelekea mwaka 2025.

SIMBA CEMENT YAZIPIGA TAFU SHULE TATU TANGA KUPUNGUZA KERO YA MADAWATI

October 20, 2016
KUFUATIA Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara  Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa, amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement)  na kuyataka mashirika na taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya wanafunzi kusomea chini.

MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT MITO YA BARAKA JIJINI DAR ES SALAAM AHUDUMU KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

October 20, 2016
Mchungaji  Bruno Mwakibolwa kutoka Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Temeke Jijini Dar es salaam, jumapili iliyopita Oktoba 16, 2016 alihudumu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika kanisa hilo akitokea nchini Kenya.

Ilikuwa Ibada iliyojaa neema ambapo Mchungaji Mwakibolwa aliwahimiza waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kumtumia Mungu kwa moyo wa kweli na watabarikiwa maishani mwao.

Alisema ziko njia mbalimbali za kumtumikia Mungu ikiwemo kuhakikisha waumini wanajikita katika kumjengea Mungu Makanisa bora ili kuwezesha neno la Mungu kusonga mbele.
Na BMG
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Mama Mchungaji, Mercy Daniel Kulola, akiwa katika ibada hiyo
Kiongozi wa timu ya kusifu na kuabudu, EAGT Lumala Mpya akihudumu katika ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo
Hii pia ni miongoni mwa njia bora kumtumikia Mungu
Kutoka kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Jijini Dar es salaam, Bruno Mwakibolwa, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola pamoja na Mama Mchungaji, Mercy Daniel Kulola.
Mmoja wa waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza akiwa kwenye ibada hiyo
Waumini wa EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza wakiwa kwenye ibada hiyo.

WASHINDI WA SHINDANO KUHUSU MASOKO YA MITAJI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

October 20, 2016
Mgeni rasmi, naibu waziri wa fedha na mipango Mhe, dkt Ashatu kijaju akiwa na majaji katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu
washindi nafasi ya tatu wakikabidhiwa zawadi mfano wa hundi yenye thamani ya sh laki tano
 
Mgeni rasmi akitoa vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko Ya mitaji

Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya    hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu; na kutoa vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa julius nyerere.
 

Wajumbe wa bodi ya mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana wakiwa katika picha ya pamoja mara ya   hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu; na kutoa vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa julius nyerere.

SHULE YA SEKONDARI YA MALANGALI YAPATA NEEMA KUTOKA KWA MALANGALI ALUMNI ASSOCIATION (MAAS)

October 20, 2016
Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania
mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo ilivyowapa mafanikio hadi sasa walipofikia.



 na fredy mgunda,Iringa

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamewataka vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali walinufaika na elimu kutoka shule ya malangali kurudisha fadhila katika shule hiyo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka na shule ya mangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo. 

“Wafanyakazi na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania.” Alisema Kevela

Kevela amesema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule walizosoma.

Naye Padre wa kanisa la kikatoriki mkoani mbeya Telesipholi Tweve aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

“Leo nimerudi katika shule hii ya malangali kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi kama MAAS tumeanza kwa kukarabati ukumbi ambao utakuwa na faida kwao kwa kutumia kwenye sherehe na kukodishwa pia”.alisema Tweve

Kwa upande wake mwenyekiti wa Malangali Alumni association (MAAS) Paul Mng’ong’o alisema kuwa wameanza kuisaidia shule ya Malangali muda mrefu kwa kuwa tayari wameshakarabati ukumbi wa shule,wamewanunulia tv na king’amuzi kwa ajili ya habari na wanaendelea kutatua matatizo ya shule hiyo.

“Hebu angalia sisi tuliosoma hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka shule hii,tunaviongozi wengi,matajili wengi ,wakulima wakubwa sana hapa nchini wote wamesoma katika shule hii”.Alisema Mng’ong’o

Lakini pia Mng’ong’o alisema kuwa lengo la kundi la Malangali Alumni Association kuunganisha wanafunzi wote waliowahi kusoma shule ya secondary ya Malangali na kuweza kupeana malengo na kusaidiana pale wanapokwama kimalengo.

Shule ya Malangali ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa maisha.

kaika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.