UHURU:AWAPA RAHA MASHABIKI WA COASTAL UNION

September 20, 2013

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Coastal Union,Uhuru Seleman juzi aliweza kuwakonga nyoyo mashabiki wa soka mkoani hapa kutokana na aina ya uchezaji ambayo alikuwa akiutumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya timu yao na Rhino Rangers ya Tabora.

Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya kufungana bao 1-1,uliocheza kwenye dimba la Mkwakwani na kuhudhuriwa na mashabiki mbalimbali wa soka mkoani hapa.

Uhuru alionekana mwiba hasa baada ya kumiliki mpira kwa dakika kadhaa huku akitoa pasi nzuri kwa wachezaji wenzake kitendo ambacho kiliwaacha roho mashabiki wa soka na kuanza kupiga kelele za shangwe.

Akizungumza na Tanga Raha,Uhuru alisema siku zote amekuwa na ndoto ya kucheza vizuri na kujituma ili kuweza kufanikiwa kurudisha nafasi yake katika kikosi cha timu ya Taifa na kusema ataendelea kupambana na kumuomba mungu afanikiwe katika hilo.

WANACHAMA AFRICAN SPORTS JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI-SHEWALLY

September 20, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.
WAPENZI wa Klabu ya African Sports na wanachama wa zamani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ya kuomba uanachama ili waweze kupata fuksa ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wao utakaofanyika hivi karibuni.

Akizungumza jioni hii na Tanga Raha,Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports “Wanakimanumanu”Asseli Shewally alisema mchakato wa kujaza fomu za uanachama wa klabu hiyo tayari umeshaanza na fomu hizo zinapatikana makao makuu ya klabu hiyo barabara kumi na mbili jijini Tanga.

Shewally alisema lengo la kusajili wanachama upya ni katika kupitisha katiba mpya ili hatimaye kuweza kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya watakaoingoza timu hiyo.

Aidha aliwataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati ili kuweza kupata viongozi watakaoiletea maendeleo timu hiyo.

DC GAMBO KUBARIKI MASHINDANO YA AWESO CUP.

September 20, 2013

NA OSCAR ASSENGA,KOROGWE.
MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ligi ya vijana ya Aweso Cup itayaoanza kutimua  kesho katika uwanja wa soka Mswaha.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na Diwani wa Kata ya Mswaha ,Aweso Omari ikiwa na lengo la kuinua vipaji vya wachezaji wachanga na kukuza kiwango cha soka katika kata hiyo ili iweze kuwa na timu tishio siku zijazo.

Akizungumza na blog hii,Mratibu wa Mashindano hayo,Zaina Kassama alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kueleza tayari timu 10 zimethibitisha ushiriki wao.

Kassama ambaye pi ni Katibu wa Chama cha Soka wilayani Korogwe(KDFA) alizitaja timu shiriki katika mashindano hayo kuwa ni Majengo FC,Cosovo FC,Star FC,Ringstone FC na Mafuleta SC.

Alizitaja timu nyengine kuwa ni Tabora FC,Mswaha Kambini,Mwenga FC,Kwaluma FC na Mandera Lutuba ambazo zitachukua ili kuweza kupatikana kwa bingwa wa mashindano hayo msimu huu wa mwaka 2013.

WADAU WA SOKA WAWAPA SOMO MASHABIKI WA COASTAL UNION.

September 20, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.
WADAU wa soka mkoa wa Tanga wamewashauri wapenzi na mshabiki wa klabu ya Coastal Union kuwa wavumilivu hasa pale timu yao inaposhindwa kufanya vizuri katika mechi zao za nyumbani na ugenini badala yake waungane pamoja ili kuitakia mema timu hiyo katika michezo yake ijayo kwenye Ligi kuu Tanzania bara.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya mashabiki wa soka mkoani hapa kutaka kupaniki katika mechi ya Coastal Union na Rhino Rangers ya Tabora ambapo mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana baoa 1-1,mchezo uliopigwa uwanja wa mkwakwani.

 Akizungumza na blog hii moja kati ya wadau hao,Msusah Junior alisema suala la matokeo mabaya kwa timu halisababishwi na mwalimu ila inatokana na aina ya uchezaji wa wachezaji siku husika kutokana na kuwa kazi kubwa ya mwalimu na kuipa maelekezo timu kabla ya kuanza mechi.

Naye.Zambi Bakari alisema wachezaji wanapaswa kujituma hasa pale wanapokuwa mchezo na sio kupaniki kwani kufanya hivyo kunaipelekea timu husika kushindwa kufanya vizuri na kuwanyima raha wapenzi na mashabiki wao.

Kwa upande wake,Mzee Deo alisema lazima mashabiki wa soka wafahamu kuwa kuna matokea ya aina mbili kufungwa,kutoka sare na kushinda hivyo wanapaswa kuridhika na matokeo ya aina yoyote na kuwataka wapenzi na wanachama kuendeleza mshikamao ili timu hiyo iweza kufanya vema mechi zao zilizosalia hasa katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.
Mwisho.

VINARA SIMBA KUWAKABILI MBEYA CITY VPL

September 20, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.

Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).

Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.

Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

KIKAO CHA BARAZA LA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TANZANIA KILIVYOFANYIKA MJINI ZANZIBAR HIVI KARIBUNI.

September 20, 2013
MAKATIBU WA JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA CHAMA CHA MAPINDUZI MIKOA YA SITA,KUSHOTO NI LINDI,MWANZA,KATAVI,TANGA,DODOMA NA SINGIDA WAKIELEKEA KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM TANZANIA KILICHOFANYIKA MJINI ZANZIBAR HIVI KARIBUNI.

KATIBU WA UVCCM MKOA WA TANGA ACHENI MAULID KUSHOTO AKIJADILIANA NA KATIBU UHAMASISHAJI  WA KUSINI UNGUJA SHEHA.

MAKATIBU WA UVCCM MIKOA YA SINGIDA,DODOMA,TANGA NA LINDI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KABLA YA KUANZA KIKAO CHA BARAZA KUU LA VIJANA MJINI ZANZIBAR HIVI KARIBUNI.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA AKIWAELEZA WAJUMBE WA BARAZA LA UVCCM NAMNA YA MATUMIZI YA SIMU KWENYE KIKAO CHA BARAZA HILO KILICHOFANYIKA MJINI ZANZIBAR HIVI KARIBUNI. 

KATIBU WA UVCCM MKOA WA TANGA,ACHENI MAULID AKIWA KATIKA KABURI LA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR,AMANI ABEID KARUME.

PENGO LA UDULLA LAONEKANA COASTAL UNION

September 20, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga
PENGO la beki wa kati wa Klabu ya Coastal Union Crispian Udula limeanza kuithiri timu hiyo mara baada ya jana kuonekana dhahiri kwenye mechi yao ya Ligi kuu na Rhino  Rangers ya Tabora kwenye mchezo uliocheza kwenye uwanja wa Mkwakwani, uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Udulla alikuwa ni msaada mkubwa katika timu hiyo hasa kwenye nafasi ambayo alikuwa akiicheza ambapo jana ilionekana kupwaya na kushindwa kutumika vema kama siku zote.

Mchezaji huyo alishindwa kucheza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyeipata kwenye mechi ya Coastal Union na Yanga iliyopigwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Taifa ambapo tayari atakuwa amemaliza adhabu hiyo na huenda akacheza mechi yao na Ruvu shooting Jumamosi hii.

Udulla ni miongoni wachezaji hatari waliosajiliwa na Klabu ya Coastal union ya Tanga msimu huu ambapo amekuwa tishio sana kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu akitokea kwenye timu ya Bandari nchini Kenya.

Timu ya Coastal Union tayari imekwisha kucheza nne imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi tatu huku wadau na wapenzi wa timu hiyo wakiendelea kuiombea mafanikio mema kwenye michezo yao iliyosalia kwenye ligi hiyo.