Wateja Tigo Pesa kupata 5.6bn/- gawio la tisa la robo mwaka

August 15, 2016
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo, Raun Swanepoel   akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu kampuni hiyo kugawa faida kwa watumiaji wake wa huduma kwa njia ya simu ambapo ni kiasi cha bilioni 5.6 kwa watumiaji wa Tigo pesa,kushoto kwake ni Meneja chapa ,William Mpinga katika mkutano uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita.
Dar es Salaam,   Agosti 09, 2016 -Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo imetangaza tena gawio la robo mwaka la shilingi bilioni 5.6 kwa watumiaji wa Tigo Pesa  ikiwa ni mara ya tisa kwa kampuni hiyo ya simu kugawa faida hiyo kwa watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa njia ya simu.

 Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo, Raun Swanepoel alisema kwa ujumla  kampuni hiyo  imeshalipa watumiaji wake wa huduma za fedha kwa njia ya simu  jumla ya shilingi bilioni 46.2 ikiwa ni malipo ya  robo mwaka tangu  kuzinduliwa kwa huduma hiyo Julai 2014.

 Swanepoel alisema kwamba katika robo ya pili ya mwaka huu kiwango cha faida  kilipanda  na kufikia asilimia 8 kulikosababishwa na  kuongezeka kwa kiwango cha hisa katika mabenki mbalimbali ya biashara.

 “Faida hii ya hisa inalipwa  wateja binafsi, mawakala wa reja reja na washirika wengine wa kibiashara wa Tigo ambao kila mmoja anapokea malipo yake kulingana na thamani ya fedha zilizowekwa kielektroniki ndani ya pochi zao za Tigo Pesa,” alisema Swanepoel.

Swanepoel aliongeza: “Kusema kweli tunafurahi kutangaza ongezeko hili la faida katika gawio la mara ya tisa mfululizo. Hii inaonesha  jinsi tulivyojikita katika  kuwawezesha wateja wetu kufikia  huduma za kifedha  pamoja na nchi zima kwa ujumla  kupitia huduma za Tigo Pesa”.

Alibainisha ongezeko la faida la Tigo, kuboreshwa kwa mazingira ya soko na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa kama moja ya kichocheo kilichosababisha kuongezeka kwa faida hususani kwa upande wa wafanyabiashara. Tigo Pesa hivi sasa ina mtandao mkubwa wa wafanyabiashara  zaidi ya 50,000.

 Swanepoel  alisema kuwa kama ilivyokuwa hapo awali gawio kwa wateja  linakokotolewa kwa kuangalia wastani wa salio la kila siku la mteja la Tigo Pesa katika pochi yake ya simu na kuongeza kuwa mpango huu wa kugawa faida umeainishwa katika kanuni za Benki Kuu iliyotolewa February 2014.


 Mwaka 2014 Tigo Tanzania  ilikuwa kampuni ya kwanza ya simu duniani   kugawa faida iliyozalishwa na fedha za simu zilizopo katika Akaunti ya Udhamini kwa kipindi cha robo mwaka kwa wateja wake.

 Mwisho 
photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com W: www.koncept.co.tz

KAIMU KAMISHNA MSAIDIZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI ATUA TANGA KUANGALIA ENEO LITAKAPOJENGWA GATI KWA AJILI YA KUSHUSHIA MAFUTA GHAFI

August 15, 2016
 Greda likisafisha eneo ambalo linatarajiwa kujengwa gati kwa ajili ya kushushia mafuta ghafi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia akiwa na viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Madini walipotembelea sehemu  ambayo litajengwa gati mpya eneo la Chongoleani jijini Tanga kushushia mafuta ghafi kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini ,Mwanamani Kidaya kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati walipotembelea eneo la Chongoleani ambapo kutajengwa gati ya kushushia mafuta ghafi



Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mwanamani Kidaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kulitembelea eneo hilo leo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumzia namna mkoa huo ulivyojipanga na fursa hiyo mara baada ya kulitembelea eneo hilo
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa tatu kutoka kushoto namna walivyojipanga kutokana na fursa hiyo
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mwanamani Kidaya kushoto akimuonyesha kiti Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella mara baada ya kutembelea eneo hilo






Muonekano wa eneo ambalo kutajengwa gati mpya kwa ajili ya kushushia mafuta ghafi

HOTUBA YA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE KONGAMANO NA MAONESHO YA KITENGO CHA WAHANDISI WANAWAKE CHA TAASISI YA WAHANDISI TANZANIA, TAREHE 12 AGOSTI, 2016 KATIKA UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA, DAR ES SALAAM

August 15, 2016




Rais wa Taasisi ya Wahandisi;
 
Ndugu Mwenyekiti, Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania;
 
Ubalozi wa Norway;
Msajili wa Bodi ya Wahandisi;
Ndugu Wanakamati ya Maandalizi;
Ndugu Wahandisi Wanawake;
Wanahabari;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
 
Asalaam Aleikum! Bwana Asifiwe!
Kwanza kabisa, namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na amani kwa kutujalia uzima wa afya kuweza kujumuika nanyi. Pili natoa shukrani zangu za dhati kwa Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb), Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mwenyekiti wa Kitengo cha Wahandisi Wanawake Tanzania pamoja na kamati nzima ya maandalizi kwa mwaliko huu wa kuja kufungua kongamano hili na maonesho. Ni heshima kubwa kwangu.  Asanteni sana.
 
Naweza kusema nimekuwa mtu mwenye bahati kubwa ya kushirikishwa na kushiriki katika mikutano mbalimbali inayohusu fani mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na wanawake katika kujikwamua kiuchumi. Leo hii nina furaha isiyo kifani kuwa pamoja na wanawake ambao wameweza kumudu kikamilifu kazi ambazo hapo awali tuliaminishwa kuwa ni kazi za mwanaume. Inatia moyo sana kuona kuwa Tanzania tumeweza kupiga hatua katika kumkwamua mwanamke kiuchumi na kuwa mchango wa mwanamke sasa ni mkubwa hata kwenye sekta ambazo hapo awali zilitawaliwa na wanaume.
 
Rais wa Taasisi ya Wahandisi;
Ndugu Mwenyekiti, Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania;
Mabibi na Mabwana;
Kama mlivyosikia katika hotuba ya Mwenyekiti; kitengo cha wanawake wahandisi ni miongoni mwa vitengo chini ya Taasisi ya Wahandisi Tanzania. Nichukue fursa hii kuipongeza Taasisi kwa kuunda kitengo hiki na kukipa majukumu ya kuratibu fursa na changamoto zinazogusa jamii ya Kitanzania; hususani wanawake wahandisi. Ni imani yangu kuwa mnaitumia fursa hii kuainisha vipaumbele; juhudi; na mafanikio ya wanawake wahandisi bila kusahau changamoto mbalimbali zinazowakabili wahandisi  hawa wanawake na jamii kwa ujumla.
 
Leo hii niwaase kwa kusema kuwa wahandisi wanawake wataongezeka na kuimarika ikiwa tu nyinyi ambao mko ndani ya tasnia mtashikamana na kufanya kazi kwa bidii.  Nataka kuwakumbusha ya kwamba iwapo na nyinyi msingepewa ushirikiano na wanawake wenzenu basi idadi hii  ninayoiona hapa leo ingekuwa ndogo zaidi.  Hivyo basi, Naomba mtambue nafasi zenu  na muwe walimu na walezi wa wenzenu katika fani hii. Vilevile muda umefika sasa wa nyinyi kujitolea kwa hali na mali katika kuendesha kampeni za kuwashawishi watoto wa kike ili wajenge ari ya kupenda masomo ya sayansi na hisabati ambayo ndiyo msingi wa mafunzo ya uhandisi.
 
Napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa Ndugu Mwenyekiti ambae pia ni Rais wa Wanawake Wahandisi na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Wizara yake na Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania kuandaa kampeni mbalimbali za kuwahimiza wanafunzi hasa wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati. Nina imani kuwa kwa nafasi yake kama Mhandisi mwanamke; Naibu Waziri na Mzazi ana mchango mkubwa wa kuwaelimisha, kuwaunganisha na kuwaendeleza watoto wa kike  ili kuweza kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia   fani za sayansi na teknolojia.

ZADIA inatoa mkono wa pole kwa Wazanzibari wote Kufuatia kifo cha Mzee Aboud Jumbe

August 15, 2016
zadiaspora@gmail.com
215 459 4449
zadia.org
انا لله وانا اليه راجعون
TAARIFA
Jumuiya ya Wazanzibari Nchini Marekani (ZADIA), imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Mzee Jumbe aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika harakati za kuleta maendeleo na mabadiliko ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Chini ya Uongozi wake, kwa mara ya kwanza Zanzibar ilipata katiba yake na hivyo kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi kama chombo cha uwakilishi wa Umma na kutunga sheria.
Atakumbukwa pia kwa msimamo wake shupavu wa kupigania haki sawa ndani ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar khususan madai yake ya kutaka kuwa na serikali tatu.
Marehemu Jumbe alikuwa rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 kufuatia kifo cha rais wa kwanza wa Zanzinbar Marehemu Abeid Aman Karume. Alilzaimishwa kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisiasa mwaka 1984 baada ya kutuhumiwa kuchafua hali ya hewa ya kisisasa Zanzibar. Uchafuzi ambao si chochote ila ushupavu wake wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mnasaba huu, ZADIA inatoa mkono wa pole kwa Wazanzibari wote kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi wao mzalendo.
Aidha kono wa pole makhasusi uwafikie wanafamilia ya Marehemu, tukimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba, na kumwomba Mola Mlezi amlaze marehemu mahali pema Peponi. Amin.
Omar H Ali, Mwenyekiti, ZADIA
Agosti 14, 2016

AUDIO: KIPINDI CHA KWANZA KURUKA HEWANI NDANI YA 102.5 LAKE FM MWANZA

August 15, 2016
102.5 Lake Fm Mwanza #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo, leo imeanza rasmi kurusha vipindi vyake ambapo kipindi cha kwanza kilichoruka hewani ni #MshikeMshike kinachofanywa na #AishaMussa.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play hapo chini
 Bonyeza HAPA Kufahamu Zaidi

MTATURU: JESHI LA POLISI HALIPASWI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

August 15, 2016
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na askari wa Jeshi la polisi mara baada ya ziara yake katika makao makuu ya Wilaya hiyo eneo la Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kituoni hapo.
 Dc Mtaturu akikagua chumba cha mahabusu kituoni hapo
 Askari watiifu wa Jeshi la Polisi Wilayani Ikungi waliposimama kutoa heshima zao kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi alipotembelea katika ofisi yao (Picha zote na Mathias Canal)

REDIO MPYA YA WANANZENGO 102.5 LAKE FM MWANZA YAANZA RASMI KURUSHA VIPINDI VYAKE HEWANI.

August 15, 2016
Haya sasa ‪#‎MshikeMshike‬ umetua Rock City kupitia 102.5 @lakefmmwanza na Mwananzengo @aysher41 ‪#‎Aisha‬.
Ni kuanzia jumatatu hadi ijumaa, saa tano asubuhi hadi saa saba mchana. ‪#‎LakeFm‬ ‪#‎RahaYaRockCity‬ ‪#‎RedioYaWananzengo‬ ‪#‎Mwanza‬

Mshike Mshike kinakuwa ni kipindi cha kwanza kuruka hewani kuanzia leo Agost 15,2016 kupitia Lake Fm Mwanza na vipindi vingine vinafuatia.
Bonyeza HAPA Kujua zaidi kuhusu Lake Fm

MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND

August 15, 2016

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bwa. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT. 
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti 2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini ya miradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa Halmashauri husika.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bwa. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bwa. Peter Ireton .
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar,Dkt Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

WAZIRI NAPE AFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA WAZI YA TANZANIA JIJINI ARUSHA,WAKENYA WATAMBA

August 15, 2016

Richard Owiti kutoka nchini Kenya akionesha kombe lake la ushindi mara baada kushika nafasi ya kwanza kwa wachezaji wa ridhaa,kwenye mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye (wa pili kulia).Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango wakishuhudia kwa pamoja.


Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi vifaa vya mchezo huo wa Gofu mshindi wa kwanza wa wachezaji wa ridhaa katika Mashindano ya Gofu ya wazi ya Tanzania,Richard Owit kutoka nchini Kenya,yaliofungwa jana jioni katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha,pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango. Mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko mkubwa yalishirikisha washiriki wapatao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya na Unganda.
Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa kulipwa wa mchezo huo wa Gofu kutoka nchini Kenya,Jacob Okelo akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita,kwenye hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania ,yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya USA River na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja Afisa Maendeleo ya jamii na Uhusiano,Justine Kesi ikiwa ni sehemu ya kiasi cha fedha kilichotolewa na Wadhamini waliodhamnini mashindano hayo ya Gofu kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya huduma za jamii mbalimbali kwa vijiji vinavyozunguka viwanja vya Kili Golf,jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jana jioni wakati wa kufunga mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf- USA River  jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa kulipwa na ridhaa wa mchezo huo walishiriki.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

Wazir Nape (wanne kulia) akiwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wa Gofu hapo jana kabla ya kuhitimisha mashindano hayo
Baadhi ya Wadau nao walikuwepo kufuatilia kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya Gofu jana jioni jijini Arusha

Waziri Nape pia alikutana na wadau ambao walidhamini mashindano hayo ya Gofu

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimsikiliza Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA),Mh Godbless Lema,kwenye viwanja vya Kiligolf,USA-River jijini Arusha,ambapo Mh Nape alikuwa mgeni rasmi katika kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania.Pichani kulia ni Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
Waziri Nape (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Gofu kwenye viwanja vya Kiligolf jijini Arusha,kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania,Chris Martin,Mkurugenzi wa viwanja vya Gofu (KiliGolf),Jerome Bruins,Mmoja wa wasimamizi waku wa kampuni ya Group Six International LTD,Janson Huang,na kushoto kwa Waziri ni Mke wa Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nassari,Mh Joshua Nassari,Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango pamoja na Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
Waziri Nape akishiriki kucheza mchezo wa Gofu

Waziri Nape akipata maelezo mafupi kuhusiana na uwanja huo wenye viwango vyote kimataifa cha Kiligolf.
Waziri Nape akifurahia jambo na Mhe Nassri,kulia ni Mke wa Mh Nassari


Waziri Nape pia alipata wasaa wa kutembelea mashimo ya mchezo huo wa Gofu yapatayo 18 ndani ya uwanja wa Kili Gofu,uliopo USA River jijini Arusha.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

TANAPA,NGORONGORO NA IDARA YA WANYAMAPORI SASA KWENDA KIJESHI.

August 15, 2016
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji  mafunzo kwa askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi 
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi  kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji  wa mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
   
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro.

  Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi ,Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
 
Askari na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witness Shoo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo  ya kijeshi kwa askari na Maafisa wa Hifadhi  waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
 
<!--[if gte mso 9]>