MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA YATEKETEZA VITU MBALIMBALI JIJINI TANGA

February 12, 2016




MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanga imeteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani zaidi ya shilingi milioni 14  zilizopitwa na wakati katika ukaguzi mpaka wa Horohoro na Kenya pamoja na madukani.
Akizungumza mara baada ya kufanyika zoezi la uteketezaji, Meneja kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA), Dammas Matiko, alisema miongoni mwa vyakula na bidhaa hizo ni  nyama za mbuzi na ng’ombe, vipodozi   pamoja na vinywaji vikali  zikiwemo bia.
Alisema ukaguzi huo ulikuwa na changamoto nyingi zikiwemo wafanyabiashara kukataa kukaguliwa na bidhaa zao kuzificha maeneo ambayo ni vigumu kuonekana kwa urahisi.
“Kwa juma zima tumekuwa tukifanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka  hoteli na machinjio, tumefanikiwa kugundua machinjio ya kienyeji mitaani ambayo hayakubaliki ksheria” alisema Matiko na kuongeza
“Ukaguzi huu wa kushtukiza utakuwa endelevu hadi pale tutakapojiridhisha hakuna bidhaa zilizopitwa na wakati na vyama ambazo hazijathibitishwa” alisema
Matiko amewaonya wafanyabiashara kuacha kuagizia bidhaa ambazo zimepitwa na wakati na kusema kuwa sheria haitomvumilia mtu yoyote na badala  yake itawatetea walaji ambao ndio wahanga.
Kwa upande wake Afisa kitengo cha Usalama wa Chakula, dawa na vipodozi halmashauri ya jiji la Tanga, Alice Maungu, amewataka wananchi kuwa na kawaida ya kusoma tarehe za kutengezwa na kuisha muda wa bidhaa anayonunua.
Alisema Watanzania wengi hawana ada ya kujua bidhaa siku iliyotengezezwa jambo ambalo limekuwa likiwaathiri ngozi zao au kuugua magonjwa ambayo chanzo chake ni matumizi ya bidhaa zilizoisha muda wa matumizi.
“Watu wengi hawana kawaida ya kujua bidhaa anayoinunua iko hai au imekufa, hili ni tatizo na ndio maana tunawapa kiburi wafanyabiashara kuagizia bidhaa zilizopitwa na wakati” alisema Maungu
Alisema ni wajibu wa kila mteja anapoenda kununua bidhaa dukani kuangalia tarehe siku iliyotengenezwa na mwisho wa matumizi ikiwa ni kukaribisha  matatizo wakati wa matumizi.
                                                    

 Watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga, wakikusanya mapande ya nyama ya ng’ombe na mbuzi zilizokamatwa sokoni na kuzichoma moto jana dampo la Mwang’ombe  baada ya kubainika nyama hizo ziko na magonjwa katika zoezi lilifanywa kwa siku tatu mfululizo kwa usimamizi wa Meneja  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Kaskazini, Dammas Matiko .
 Meneja kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dammas Matiko, akimwaga bia zilizokamatwa katika baa mbalimbali Tanga ambazo zimeisha muda wake wa matumizi zoezi lililofanyika kwa siku tatu mfululizo na kuzitekelezwa dampo la Mwang’ombe jana

Meneja kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dammas Matiko (kushoto) na Afisa Afya kitengo cha usalama wa chakula na dawa halmashauri ya jiji la Tanga, Alice Maungu (kulia) kwa pamoja wakiteketeza makopo ya rangi zilizoisha muda wake wa matumizi dampo la Mwang’ombe Tanga jana


DK. KINGWANGALLA ATOA SIKU 60 KWA HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA, KUNUNUA MASHINE YA CT-SCAN

DK. KINGWANGALLA ATOA SIKU 60 KWA HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA, KUNUNUA MASHINE YA CT-SCAN

February 12, 2016
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.
Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD), Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa Hospitali.
Dk.Kigwangalla alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.
"Hospitali kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?" alihoji Dk. Kigwangalla.
Dk.Kigwangalla aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya bima ya afya.
Aidha, Dk Kigwangalla amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.
Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya

DSC_3499

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo.

kigwangalambeya2

Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo kitengo cha maabara.

kigwangala mbeya

Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.

kigwazz

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na wafanyakazi katika mkutano wake huo.

kigwangala2

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake...

kigwaz

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo Februari 12.

kigwangala mbeya6

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipata maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe mpya ilikuendana na kasi.

kigwangaz

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.

kigwaz11

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.

kigwanga1

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.

kigwangala

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya).

JUWAIRA DECORATION WAKUANDALIA MAMBO MAZURI VALENTINE DAY KESHO FIKA DUKANI KWAO WAPO BARABARA YA TANGA BEACH RESORT

February 12, 2016


BAADHI YA VINYWAJI AMBAVYO NI MAALUMU KWA WAPENDANAO VIKIWA VIMEANDALIWA KWA AJILI YAKO.


















Waziri Nape mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon

Waziri Nape mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon

February 12, 2016

ki1
: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akikabidhiwa zawadi kutoka TBL kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Lager alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia) na Meneja Masuala ya Nje na Mawasiliano Bibi. Emma Oriyo
ki2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
ki3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akielezea jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa.
ki4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
ki5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia).
ki6
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia).
………………………………………………………………………………………………………
Na: Frank Shija, WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika tarehe 28 Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Hayo yamebainisha na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo ndio waratibu wa mbio hizo Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.
“Mbio za Kili Marathon zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Nape Moses Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”. Alisema Marealle.
Marealle alisema kuwa Mbio hizo  zitakuwa katika makundi manne ambayo ni mbio za Kilomita 42 ambazo ndiyo marathoni yenyewe inayothaminiwa na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za kilomita 21 zinazodhaminiwa na Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha walemavu wanaotumia Baiskeli za matairi matatu na Viti vya matairi zinazodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za kilomita 5 ambazo zinadhaminiwa na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt
Aliongeza katika mbio hizo washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza kwa mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42 watapatiwa zawadi ya shilingi milioni nne kila mmoja.
Aidha alisema kuwa zaidi ya washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo huku kati yao takribani washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.
Kilimanjaro Marathon inatimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa mashindano hayo ni Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na kuratibiwa na Executive Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa mbio hizo ni Kampuni ya Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.
BALOZI WA KOREA AMTEMBELEA WAZIRI WA WIZARA YA AFYA

BALOZI WA KOREA AMTEMBELEA WAZIRI WA WIZARA YA AFYA

February 12, 2016

New Picture (32)
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Barozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Florence Tinguely Mattli wa kwanza kushoto akiwa na Mkuu wa Sekta ya Afya ya Ubalozi wa Switzerland, Thomas Teuscher wa pili kushoto.
New Picture (33)
Balozi wa Korea Nchini Tanzania, Song, Geum-Young akizungumza na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, wa pili kushoto ni Katibu wake Songwon Shin.
New Picture (34)
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati  akizungumza na Barozi wa Korea Nchini Tanzania (Song, Geum-Young) wa kwanza kushoto akiwa na Katibu wake Songwon Shin wa pili kushoto.
Waziri Nchi Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kairuki auagiza Mfuko wa Maendelea ya Jamii (TASAF)

Waziri Nchi Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kairuki auagiza Mfuko wa Maendelea ya Jamii (TASAF)

February 12, 2016

ta1
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw.  Ladislaus Mwamanga akiwatambulisha watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
ta2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa  watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
ta3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa  watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
ta4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo. Wengine ni waandishi wa habari  walioudhuria tukio hilo.
………………………………………………………………………………………….
Waziri Nchi Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.  Angella Kairuki (Mb) ameuagiza  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuendelea kutekeleza  majukumu yake kwa ufanisi ili kusaidia jitihada za serikali za kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.
Mhe.  Kairuki amesema TASAF inayo dhima kubwa ya kuhakikisha kuwa huduma inazozitoa kwa wananchi zinakwenda sambamba na misingi ya uadilifu na utawala bora ili hadhi ya mfuko huo iendelee kuwa kubwa.
Waziri Kairuki ameyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es salaam ambako alizungumza na watumishi  wa mfuko huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara za kikazi  katika taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ambayo amepewa  dhamana ya kuisimamia baada ya kuteuliwa  kushika wadhifa huo  na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli.
“Ninawasisitiza muhakikishe kuwa, walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wananufaika vilivyo na fedha zinazotolewa ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini” alisema Kairuki.
Aidha, Mhe.  Kairuki ameuagiza uongozi wa TASAF kuweka utaratibu utakaowezesha ukaguzi wa mara kwa mara wa walengwa wa Mpango huo nchini kote ili kuhakikisha kuwa watu wasiostahili wanaondolewa kwenye utaratibu wa ruzuku na kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya lazima.
Mhe. Kairuki ameonya vikali dhidi ya uwezekano wa kuweko matumizi mabaya ya fedha kwa kutoa ruzuku kwa watu wenye uwezo jambo ambalo amesema halipaswi kufumbiwa macho na pale itakapobainika wahusika wachukuliwe hatua za kuwaondoa kwenye Mpango na kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki ameuagiza uongozi wa TASAF kutoa mapendekezo ndani ya siku 30 ya namna ya kukabiliana na malalamiko yanayoelekezwa kwa watendaji wa ngazi za vijiji,kata,na hata wilaya ambao wamekiuka taratibu za kuwabaini na kuwaorodhesha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini ili hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo.
Awali akitoa maelezo kwa Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.  Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko umefanikiwa kuandikisha zaidi ya walengwa  Milioni 1.1 ambao wanaendelea kupata ruzuku  na kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2016 zaidi ya shilingi Bilioni 204 zimetolewa kwa walengwa ambapo matokeo chanya yameanza kuonekana  hususani katika Nyanja za elimu, afya na makazi.
Bwana Mwamanga amesema licha ya changamoto zilizopo hususani katika upatikanaye wa fedha za kukidhi idadi kubwa ya walengwa ,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF )umeendelea kufanya juhudi za kutafuta fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo na kuiomba serikali kuona namna inavyoweza kuunga jitihada hizo ili hatimaye vita dhidi ya umaskini iweze kufanikiwa .
Kuhusu Mpango wa  kunusuru kaya maskini, Bw.  Mwamanga amesema walengwa wa Mpango huu wamehamasika kwa kiwango kikubwa huku wengi wao wakionyesha uwezo katika kufuata masharti na taratibu za Mpango hivyo suala la upatikanaji wa fedha kwa uhakika lina umuhimu mkubwa ili kutowavunja moyo walengwa hao.
Naibu waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo atoa pongezi kwa Twiga Stars.

Naibu waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo atoa pongezi kwa Twiga Stars.

February 12, 2016

an1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) akipokelewa na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (kulia) alipofanya ziara katika katika ofisi za TFF na kuzungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
an2
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wapili kulia) moja ya ofisi zinazotumiwa na TFF wakati Mhe. Waziri alipofanya ziara katika katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
an3
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (aliyesimama) akizungumza na ugeni ulioongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutembelea ofisi za TFF pamoja na kuzungumza na wachezaji wa Twiga Stars leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
an4
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisi za TFF na kukutana na wachezaji hao kuwahamasisha wazidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine
an5
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa Twiga Stars leo jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika ofisi za TFF na kuzungumza na wachezaji hao kuwahamasisha wazidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine na wanne kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wanawake Bibi. Amina Karuma
an6
Wafanyakazi wa TFF katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wanne kushoto) alipotembelea ofisi za TFF leo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge na wapili kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
…………………………………………………………………………………………………………..
Na: Shamimu Nyaki – Maelezo
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars) kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali wanayoshiriki ndani na nje ya nchi iliyopelekea kushika nafasi ya nane katika bara la Afrika kwa mwaka 2015.
Pongezi hizo amezitoa leo jijjini Dar es Salaam wakati alipozungumza na wachezaji hao  katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ambapo wameweka kambi kwa ajili ya kujianda na Mchezo wao dhidi ya Zimbabwe utakaochezwa  mwezi  wa tano mwaka huu.
Mhe. Wambura amewataka  wachezaji hao kujituma kwa bidii, kuwa na nidhamu pamoja na kuzingatia maadili ya nchi yetu kwa kuwa wao ni mwanga wa jamii ili waweze kufika mbali kama mchezaji Mbwana Samatta.
“Mnapokuwa kambini zingatieni maadili, kanuni, sheria zilizopo na kuamini michezo ni ajira kwenu na inaweza kubadili maisha yenu kwa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya uwezeshaji” Alisema Mhe. Wambura.
Aidha Katibu Mkuu wa Shrikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine akitoa taarifa fupi ya  utendaji wa Shirikisho hilo amesema kuwa kwa upande wa wanawake TFF inafanya juhudi  za kuanzisha ligi ya Taifa ya mpira wa Wanawake kutoa mafunzo kwa makocha wa mpira wa wanawake pamoja na kufuatilia vipaji vya watoto wa kike waliopo mashuleni.
Bw. Celestine ameeleza changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya shirikisho hilo ikiwemo baadhi ya sheria na kanuni zinazosimamia masuala ya mpira wa miguu Tanzania na FIFA zimekuwa zikitofautiana na sheria za nchi kwa kuwa hazijafanyiwa marekebisho ili ziweze kua na uwiano ambapo Mhe. Naibu Waziri ameahidi kuzishughulikia.
Kwa upande wake kapteni wa Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) Bibi. Sophia Mwasikile amemshukuru Naibu Waziri kwa pongezi alizowapa na kuahidi kuwa wataendelea kufanya vizuri zaidi na kuitangaza nchi vizuri kupitia mchezo huo na kushika nafasi ya juu zaidi ndani na nje ya Afrika.
Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake Twiga Stars imekuwa ni timu pekee Tanzania inayofanya vizuri katika michuano inayoshiriki japokuwa haina wadhamini hivyo ni wakati wa wadhamini kujitokeza kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri zaidi.
WATUHUMIWA 11 WA TRL WAFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM.

WATUHUMIWA 11 WA TRL WAFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM.

February 12, 2016

????????????????????????????????????Watuhumiwa wa mabehewa ya Mizigo TRL wakiwa nje ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam tayari kwenda kusomewa mashtaka yanayoyabili watuhumiwa hao  wanakabiliwa na mashiataka tisa yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kupitisha ununuzi wa mabehewa mabovu 25. (wapili kulia nyuma) aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli Tanzania (TRL), Kipallo Kisamfu.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
???????????????????????????????????? Watuhumiwa wa mabehewa ya Mizigo TRL wakiingia ndani ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
????????????????????????????????????Watuhumiwa wakiwa ndani ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
????????????????????????????????????Watuhumiwa 11 wa mabehewa ya Mizigo TRL wakiwa ndani ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kupitisha ununuzi wa mabehewa mabovu 25.
Watuhumiwa  waliopandishwa kizimbani ni pamoja na Jasper Kisiraga, Mathias Massae, Muungano Kaupunda, Ngoso Ngosomwiles, Paschal Mafikiri, Kedmon Mapunda, Felix Kashaigili, Lowland Simtengu, Joseph Syaizyagi na Charles Ndenge.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG.