RAIS Dk.SHEIN AWAAPISHA MAWAZIRI LEO.

RAIS Dk.SHEIN AWAAPISHA MAWAZIRI LEO.

April 10, 2016

K1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Amina Salum Ali kuwa Waziri wa  Biashara, Viwanda na Masoko katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Haroun Ali Suleiman kuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais katiba ,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora,katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Mohammed Aboud Mohammed kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Issa Haji Ussi  Gavu  kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Ali Abeid Karume kuwa Wazi wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Hamad Rashid Mohamed kuwa Waziri wa Kilimo,Mifugo,Maliasili na Uvuvi   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Haji Omar Kheir kuwa Wazir wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K8 K9 K10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Mohammed Ahmed Salum kuwa Naibu Wazi wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji    katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K11
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Said Soud Said kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum  katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K12
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Lulu Msham Abdulla kuwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo,Maliasili na Uvuvi    katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K13
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Mmanga Mjengo Mjawiri kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K14
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Juma Ali Khatib  kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum  katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.]
K15
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu, [Picha na Ikulu.]
K16
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu, [Picha na Ikulu.]
KIWANDA CHA KARATASI MUFINDI KUTOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI ISHIRINI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

KIWANDA CHA KARATASI MUFINDI KUTOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI ISHIRINI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

April 10, 2016

8
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bw. Jowika Kasunga akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina (kushoto) wa namna ambavyo wilaya imeelekeza Kiwanda cha Mbao cha Sao Hill na Green Resources Limited cha Mufindi kutunza Mazingira, (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bi Roselyne Mariki.
9
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia kipande cha gogo ambacho ni moja ya waste product  (taka) inayotoka katika kiwanda cha Sao Hill and Green Resources Limited  baada ya uzalishaji wa mbao na nguzo ambayo taka hiyo ya gogo pia hutumika kutengenezea gundi.
10
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akitoa maelekezo kwa uongozi wa kiwanda cha Sao Hill and Green Resources Limited, wa namna ya kuondosha taka za nguzo (hazipo pichani) zilizozagaaa katika eneo la kiwanda hicho..alipofanya ziara ya viwanda, ukaguzi wa usafi wa mazingira na kupanda miti Mkoani Iringa leo.(Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………………..
Kiwanda cha kuzalisha karatasi cha Mufindi Paper Mills kilichopo wilayani Mufindi Mkoani Iringa, kimetozwa faini ya shilingi milioni ishirini kwa kukiuka sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa katika kipindi kisichozidi wala kupungua wiki mbili imetokana na ukiukwaji wa sheria ya mazingira kwa utiririshaji wa kemikali hatarishi kwa viumbe hai na mazingira katika mto kigogo, na maeneo ya jirani na vijiji vinavyo uzunguka mto huo.
Akimfafanulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina alipofanya ziara kiwandani hapo, Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kanda ya Nyanda za Juu kusini. Bw. Godlove Mwaisojo, ameeleza kuwa moshi, vumbi na majitaka yanayotoka katika mitambo ya kiwanda hicho baada ya uzalishaji wa karatasi, yamezidi viwango vya sheria kwa kuwa na kemikali hatarishi kwa baiyonuwahi na mazingira na hivyo Baraza limekuwa likielekza mara kadhaa uongozi wa kiwnda hicho kurebisha mfumo wa utoaji taka bila utekelezaji wa aina yoyote.
Bw. Mwamsojo alimueleza Mh Naibu Waziri Mpina Kuwa, kiwanda hicho kimeshauriwa na baraza kuhakiki ubora wa hali wa hewa, na mitambo yao ya uzalishaji lakini kilikaidi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bw. Jowika Kasunga, amemueleza Mh. Naibu Waziri Mpina kuwa, pamoja na ukiukwaji wa utekelezaji wa sheria ya mazingira unaofanywa na kiwanda hicho, pia menejimenti ya kiwanda hicho imekuwa na mgogoro mkubwa  wa ardhi na mahusiano mabaya  na wanakijiji wanaozunguka kiwanda hicho, na kuwa karibia hekta elfu kumi na nne za misitu  zilizopo katika eneo hilo, zipo katika mgogoro wa muda mrefu baina ya wanakijiji na muwekezaji huyo, ambapo mgogoro huo umepelekea eneo hilo kutotumika  na wanakijiji wala muwekezaji huyo.
Mh. Naibu Waziri Mpina, ameutaka uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wizara husika kutatua mgogoro huo wa ardhi, ili uzalishaji wa rasilimali ya misitu uendelee kwa manufaa ya taifa.
Kwa upande wake Mkuregenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Bw. CHOUDARY kutoka barani Asia, alikubaliana na adhabu hiyo na kuhaidi kurekebisha mitambo ya uzalishaji katika kiwanda hicho kwa kipindi kisichozidi wiki mbili.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina, pia ilihusisha ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha uzalishaji mbao,nguzo na nishati cha Sao Hill and Green Resources Limited, cha Mjini Mufindi na kujionea namna ambavyo kiwanda hicho kinavyokabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kumiliki mashamba makubwa ya misitu katika vijiji vya Mapanda na Achimbile, na kufanya biashara ya hewa ukaa.
WANANCHI WA USHIRIKA TUKUYU WAZUILIWA KUJENGA ZAHANATI

WANANCHI WA USHIRIKA TUKUYU WAZUILIWA KUJENGA ZAHANATI

April 10, 2016

1 
Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi hao ambao waliomzunguka kutoa kero yao ya kuzuiwa kuendelea na ujenzi wa zahanati.
4 
Wananchi wa kata ya Ushirika-Tukuyu wakiwa wamebeba bango kuonesha kilio chao kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto.
2 3 
Mmoja wa mwanakamati akimueleza mgogoro wao wa eneo la ujenzi wa zahanati kati yao na mkurugenzi wa halmashauri yao.
………………………………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura
Wananchi wa kata ya ushirika wilayani tukuyu wameusimamisha msafara wa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto uliokua ukitoka wilayani kyela kuelekea mbarali kwa madai hawana kituo cha afya wala zahanati kwa miaka hamsini sasa.
Wananchi hao ambao walikua wameshika bango kubwa lililoandika hawamtaki mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa madai ya kuwasimamisha ujenzi mara mbili
Akieleza kilio chao katibu.wa kamati ya ujenzi  bi.fatma mwandegele alisema eneo hilo limeingia kwenye mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu kati ya kijiji cha mpunguso na aliyekua katibu tarafa wa kata ya pakati bw.mwakapala
Hatahivyo alisema kesi kuhusu eneo hilo ilishamalizika na wananchi walikusanya nguvu zao kwa kuchangia simenti na mawe hata hivyo simenti hiyo iliharibika
Waziri Ummy Mwalimu ilimrazimu kwenda kuliona eneo hilo ambalo  limechimbwa tayari kwa kuanza msingi huku mawe yakiwa yamerundikwa pasipo kuendelea na ujenzi alimuagiza mganga mkuu wa mkoa ambaye alikua nae kwenye msafara wake,siku ya jumatatu wafike eneo hilo pamoja na mkurugenzi na mganga mkuu wa wilaya ili waeleze kwanini wasiendelee na ujenzi wa zahanati hiyo.
“Nawaomba wananchi muwe watulivu ili tujihakikishie kama kesi hiyo imekwisha na kwanini tusiendelee na ujenzi huu na jumatatu kabla ya.saa tisa mchana niwe nimepata ripoti ya eneo hili
Aidha,Waziri huyo aliwathibitishia wananchi hao kwamba lazima zahanati ijengwe kwenye kijiji hicho ili kiweze kuwahudumia wananchi na kuwaahidi.serikali itawaletea wahudumu pamoja na dawa,vifaa na vifaa tiba.
WAZIRI UMMY MWALIMU AMEAHIDI KUWAPELEKEA DAWA ZA KUTIBU MAJI(WATER GUARD) WANANCHI WA KYELA.

WAZIRI UMMY MWALIMU AMEAHIDI KUWAPELEKEA DAWA ZA KUTIBU MAJI(WATER GUARD) WANANCHI WA KYELA.

April 10, 2016

1 
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto akisalimiana na watoa huduma wa hospitali ya wilaya ya kyela.
2 
Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya wilaya wakimsubiri kumpokea waziri wa afya.Mh.Ummy Mwalimu amewakumbusha watoa huduma hao kuwahudumia wananchi kwa kufuata weledi wa taaluma zao.
5 
Waziri Ummy Mwalimu akipata maelezo kwenye dirisha la wanaotumia kadi ya mfuko wa wa jamii(CHF) toka kwa mhudumu(hayupo pichani)wa hospitali ya wilaya ya kyela.
3 
Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na watendaji wa wilaya ya Kyela,kushoto ni makamu mwenyekiti wa wilaya Stephen Mwangalaba,na kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo dkt. Thea Ntara.
4 
Mkuu wa Wilaya ya Kyela dkt.Thea Ntara akitoa taarifa ya wilaya kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,alipotembelea hospitali ya wilaya ya kyela.
Picha na mpiga picha wetu.

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA ATOA MAFUNZO KWA WATOTO WA KITUO CHA MICHEZO CHA JAKAYA KIKWETE YOUTH PARK

April 10, 2016
 Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (kulia), akiwaelekeza jinsi ya kucheza mpira wachezaji wa Timu ya vijana waliochini ya miaka 20 ya Sunderland alipotembelea Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Kanu yupo nchini kwa ziara ya siku tano kwa mwaliko wa Kampuni ya StarTimes Tanzania ambapo jana alitoa msaada wa vyakula, magodoro, sabuni na vyombo vya matumizi ya jikoni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi ya Majimatitu ya Mbagala wilayani Temeke.
 Hapa akiwa katika picha ya pamoja na timu  hiyo ya watoto.
 Akielekeza namna ya kucheza mpira.
 Maelekezo yakiendelea.
 Watoto hao wakichezwa kwa kufuata maelekezo ya Kanu 
(hayupo pichani)
 Kanu akiwagawia fulana wachezaji hao.
 Hapa akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa watoto hao.
 Akiendelea kutoa maelekezo ya jinsi ya kucheza mpira.
 Watoto wa kituo hicho wakimshangilia Kanu (hayupo pichani)
 Kanu akiwa katika picha ya pamoja ya Buguruni Youth Centre.
 Kanu akizungumza na watoto wanaopata mafunzo ya soka katika kituo hicho.
Kanu akikagua timu ya watoto hao.

Na Dotto Mwaibale

MCHEZAJI nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Naijeria, Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ametembelea na kushiriki kwenye mafunzo na watoto kwenye kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park cha jijini Dar es Salaam jana.

Kanu ambaye amekuja kwa shughuli za kampuni hiyo atakuwepo nchini Tanzania kwa muda wa siku tano alifurahi sana kuona watoto wameandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya michezo mbalimbali kwani sio wote waliopata fursa hiyo.

“Wakati mimi ninaanza kucheza mpira hakukuwa na kituo kizuri kama hiki wala jezi, viatu na walimu wazuri mlio nao sasa. Hii ni fursa ya kipekee kwenu nyinyi kuweza kuonyesha 
juhudi za kujifunza ili mje kuwa kama mimi siku za mbeleni. 

Leo mimi nimekuwa maarufu ni kwa sababu nilikuwa na nidhamu, bidii, dhamira na kuwasikiliza walimu wangu walipokuwa wananifundisha. Hatimaye leo hii nina mafanikio makubwa, ninaishi maisha mazuri, wazazi wangu pia wanaishi mahali pazuri, wanasafiri na kupata wanachokitaka kwa sababu tu ya mimi kufanikiwa.” Kanu aliwaambia watoto wa kituo cha Jakaya Kikwete Kampuni ya StarTimes ambayo imo zaidi ya nchi kumi barani Afrika imemtua mchezaji huyo kama balozi katika 
kuwawakilisha katika shughuli mbalimbali. 

Kanu anatarajia kuwa chachu kwa katika kampuni hiyo hususani katika kuboresha na kuongeza vipindi na chaneli za michezo kwani waafrika wengi wanapenda soka.

“Ninaamini mchezo wa soka ndio unaopendwa na watu wengi zaidi duniani na waafrika ni miongoni mwao. StarTimes mpaka sasa wamepiga hatua kubwa katika kulisimamia hili, mpaka sasa tayari wana haki miliki za kuonyesha ligi za Budensiliga na Serie A za Ujerumani na Italia. 

Hiyo ni hatua kubwa kwani wateja wanafurahia michezo hiyo inyoonekana moja kwa moja kwa vifurusushi vya bei nafuu. Kama balozi ninaahidi kushirikiana na kampuni katika kuboresha zaidi vipindi vyake na pia kuishauri kujikita zaidi na michezo ya nyumbani. 

Kama mnavyoona kwa mara ya kwanza tumedhamini ligi daraja la kwanza.” Aliongezea mchezaji Kanu alihitimisha kwa kuwataka watoto wa kituoni hapo kuonyesha bidii, utii na dhamira ya dhati kwa kila wanachokifanya, “Ningependa kuwashauri wadogo zangu kuwa popote utakapokwenda duniani kwenye mchezo wa soka, viwanja na mipira inayotumika ni hii hii wala hakuna tofauti yoyote. 

Hivyo basi sioni kama kuna kitu cha kuwazuia na nyinyi msifanikiwe. Kama nilivyowaambia awali, bidii, nidhamu, dhamira na utii kwa walimu wenu ndio msingi wa mafanikio ya mwanasoka yeyote Yule duniani. Nawatakia kila la kheri na siku nyingine nikija Tanzania naahidi kuwatembelea tena.”

Kwa  upande wake Kocha Mkuu wa Kituo cha Vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete,  Eduard Tamayo alielezea furaha yake kwa kampuni ya StarTimes kuandaa kitu kama hiko na kukiteua kituo hiko kuwa mwenyeji wa ugeni wa Kanu nchini Tanzania.

“Nimefurahi sana kwa ujio aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Naijeria na vilabu vikubwa barani Ulaya kama vile Ajax, Inter Milan na Arsena, Nwankwo Kanu kutembelea hapa na kushiriki mafunzo na watoto. Hii ni bahati kubwa sana kwa watoto hawa kwani ni nadra sana kutokea, kupata mafunzo, kuzungumza, kupata ushauri na kuuliza maswali moja kwa moja kwa Kanu. Ninatumaini itakuwa imewapa motisha kubwa sana.” Alisema  Tamayo

Kocha Mkuu huyo kituoni hapo alihitimisha kwa kuwataka wazazi kuwapeleka na kuwasajili watoto kituoni hapo kwa mafunzo kwani wanapokelewa na kuwapatia mafunzo mazuri kwa kuviendeleza vipaji vyao. Na kwamba kituo hiko ni fursa kwa watanzania hivyo ni vema kukitumia vizuri.