YANGA SC NA JKT RUVU KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA

September 20, 2015

Winga wa Yanga SC, Simon Msuva (kulia) akimtoka beki wa JKT Ruvu, Napho Zuberi (kushoto) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga SC ilishinda 4-1
Kiungo wa Yanga SC, Mzimbabwe Thabani Kamusoko akimtoka mshambuliaji wa JKT Ruvu, Samuel Kamuntu
Mshambuliai wa Yanga SC, Mzimbabwe Donald Ngoma akipambana na wachezaji wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhani (chini) na George Minja (kulia)
Simon Msuva wa Yanga SC akipasua katikati ya wachezaji wa JKT Ruvu
Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima akimtoka kiungo wa JKT Ruvu, Ismail Aziz
Beki wa JKT Ruvu, Martin Kazila akimzuia mshambuliaji wa Yanga SC, Mrundi Amissi Tambwe

Maonesho ya ndege za kivita Washington DMV

September 20, 2015


Picha kwa hisani ya Vijimambo na Kwanza Production
Maonyesho hayo yasiyo na kiingilio, yaliambatana na maadhimisho ya miaka 100 ya jeshi la maji nchini hapa.
Maonyesho ya ndege za kivita na vifaa vingine kutoka majeshi ya Marekani, yamefanyika leo na kuhudhuriwa na maelfu ya watazamaji.
 Askari miavuli wakishuka kwa aina yake
 Mmoja wa askari wa mwavuli akishuka katika ufunguzi wa maonyesho hayo
 F-22 Raptor

 F-22 a.k.a Raptor na Mustang zikifanya onyesho la pamoja
 F-22 a.k.a Raptor ikisalimu watazamaji kwa mtindo wake
 Raptor. Ndege inayoaminika kuwa "kali" zaidi katika mashambulizi duniani
 F-22 Raptor inaaminika kuwa ndege ya thamani zaidi duniani, kila moja ikigharimu takriban dola za kiMarekani milioni 150
 F-16 Thunderbirds ambazo ndizo zilikuwa onyesho kuu kwa mwaka huu zikianza maonyesho

MGOMBEA MWENZA CCM AFANYA KAMPENI MIKINDANI NA MAFIA

September 20, 2015
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septemba17, 2015, katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni kwa ajili ya Jimbo la Mtwara mjini, uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara jana, Septemba 17, 2015.
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipokea Wanachama waliohamia CCM, kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakati wa mkutano wa kapnei uliofanyika jana, Septemba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Kada wa CCM, Mtela Mwampamba akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septamba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani, Jimbo la Mtwara Mjini.
 Msanii wa Bongo Movie, Snura akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Vijana wakiungana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kuishangilia CCM, baada ya kuwapokea kutoka vyama vya CUF na Chadema katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septemba 17, 2015.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mafia mkoani Pwani, jana, Septemba 17, 2015.
 Aliyekuwa Mbunge wa Mafia ambaye pia aliingia katika kinyan'ganyiro cha kuomba ridhaa ya CCM kuwania tena ubunge wa jimbo hilo, Abdulkarim Shah, akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo, Mbarak Dau, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika katika Kisiwa hicho cha Mafia.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza Kada wa CUF, Mohamed Albadawi, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. Albadawi awali alikuwa Mgombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CUF baada ya kuongoza katika kura za maoni, lakini baadaye akaenguliwa na chama hicho na kupachikwa, Shomari Kimbau ambaye alihamia CUF baada ya kushindwa katika kura za maoni za CCM.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto), akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

“RC MAGALULA: MSIWAFUMBIE MACHO WANAOCHAFUA TAALUMA YENU”

September 20, 2015
AMINA OMARI TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula ameitaka bodi ya Usajili wabunifu wa Majengo na wakadiriaji wa Majenzi nchini kutowafumbia macho baadhi yao wanaotaka kuchafua sifa ya taaluma hiyo kwa kushindwa kutimiza wajibu wao badala yake wahakikisha wanachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni.

Magalula alitoa wito huo juzi wakati akifungua semina endelevu ya 24 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji  Majenzi inayofanyika mjini hapa iliyowahusisha wataalamu kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.

Alisema kuwa uchukuaji wa hatua hizo kali utawafanya wenye tabia za aina hiyo kuacha mara moja kutokana na kuwa endapo watafanya hivyo wataweza kukumbana na adhabu ikiwemo kulipishwa faini ili iweze kuwa fundisho kwa wengine.

  “Nisema tu hatua mnazozichukua katika kusimamia sheria pamoja na kuwafutia usajili na kuwalipisha faini wale wanaokiuka maadili ya taalumu itasaidia hii ni njia nzuri kwa sababu itaongeza ufanisi kwa baadhi yao kuepuka kufanya vitendo visivyotakiwa “Alisema RC Magalula.

Alisema kuwa katika mkakati wa kuwajengea uwezo wataalamu wazawa,aliwashauri kuungana na kuomba kazi kwa pamoja ikiwemo kuacha ubinafsi kwani hilo limekuwa tatizo kubwa kwa watanzania wengi hali ambayo imepelekea kulalamika kuwa serikali kuwa haiwajali.

Aidha aliwataka wataalamu kuhakikisha wanajitangaza kwa kufuata sheria pamoja na kuonyesha jamii kazi zao zinazotokana na ubora ili kuweza kuwapa utofauti wa kazi iliyofanywa na mtaalam na ile iliyofanywa na mtu asiyekuwa na taaluma.

Mkuu huyo wa mkoa aliipongeza bodi hiyo kwa kuanza kujenga mahusiano na taasisi zingine za nchi za Afrika Masharika na nchi za SADC kwa lengo la kupata uzoefu zaidi katika utekelezaji wa majukumu yenu itakayowezesha kupanua wigo wa kupata kazi.

  “Nipongeza juhudi hizi nikiamini kuwa mahusiano hayo yatakuwa ya manufaa kwenu kama bodi na wataalamu wenu …lakini pia kwa manufaa kwa Taifa kwa ujumla kwa kuzingatia nia dhabiti ya serikali kushirikiana na Mataifa mbalimbali katika kukuza Uchumi…

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwenyekiti wa Bodi ya ya wabunifu wa Majengo na wakadiriaji wa Majenzi,Tonnie Ambwene Mwakyusa alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwakutanisha wataalamu katika sekta ya ujenzi hususani wabunifu wa majengo,wakadiriaji majenzi,wataalamu wa mpango wa miji na wahandisi ili kujifunza na kubadilisha ujuzi.

Alisema kuwa katika utendaji kazi wa wataalamu wao wamekuwa wakikumbana changamoto mbalimbali zikiwemo uelewa mdogo kwa baadhi ya waendelezaji kuhusu umuhimu wa kutumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika kubuni na kutekeleza miradi yao.

Aliongeza kuwa bodi hiyo kwa kuliona hilo inaendelea kuchukua hatua za kutembelea miradi ya ujenzi na kuelimisha waendelezaji wa miradi na wadau wengine ambao wanakiuka sheria kwa ikiwemo kuwachukulia hatua kali kwa kuwasimamisha ujenzi wa mradi na kufunguliwa mashtaka mahakamani.

CHADEMA, NCCR-MAGEUZI WASHIKANA MASHATI VUNJO

September 20, 2015

HALI ya Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (UKAWA), si shwari ndani ya Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kutokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na NCCR-Mageuzi kushindwa kuheshimu makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja kwa kila kata.
Hali hiyo imekuja baada ya wagombea udiwani wa Chadema kukataa kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo hilo NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye amesimama chini ya mwavuli wa Ukawa kwa madai kuwa, amekiuka makubaliano ya umoja huo.
Wagombea hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, katika kipindi hiki cha kampeni, hawatamnadi mgombea ubunge wa Ukawa wakidai hata yeye mgombea ubunge amekuwa akiwapiga vita wagombea udiwani wa Chadema.
Mmoja wa madiwani hao, ambaye ni mgombea wa kata ya Mamba Kusini, Fredy Shayo, alisema hali hiyo imetokea baada ya vyama hivyo kushindwa kuelewana katika makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja, ambapo Chadema na NCCR-Mageuzi vimesimamisha wagombea wao wa udiwani kwenye kata zote 16 za jimbo la Vunjo.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.

September 20, 2015

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
 Mhe. Wilson Masilingi   Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho  Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.  Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi, pamoja na Marystella Masilingi. Mke wa Balozi.
 Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurudi nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kukabidhi hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.