MAMA SAMIA AITEKA ROMBO NA VUNJO

MAMA SAMIA AITEKA ROMBO NA VUNJO

August 25, 2015

1
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya leo, Agosti 25, 2015, katika mji mdogo wa Tarakea,  jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro.
(Picha na Bashir Nkoromo).
6
Samia akimsikiliza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Vunjo,Innocent Meleck, katik mkutano wa ahadhara wa Vunjo.
2 4 5
Samia akiwajula hali kina mama waliojifungua katika hospitali ya Huruma, Rombo mkoani Kilimanjaro.

MTANGAZAJI WA DIRA YA DUNIA SALIM KIKEKE ATEMBELEA OFISI ZA MICHUZI BLOG JIJINI DAR ES SALAAM

August 25, 2015


Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke alipotembelea katika ofisi za MICHUZI MEDIA GROUP (MMG), leo jijini Dar es Salaam.

Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akifanya mahojiano na Michuzi tv online,Chalila Kibuda  jijini Dar es Salaam leo.

 Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi, akisalimiana na Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke jijini Dar es Salaam leo. 

Kutoka kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi,Mpiga picha za Video, Bakari Issa Madjeshi,Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke,Mwandishi wa habari ,Chalila Kibuda, Mwandishi wa habari na Mpiga picha Avila Kakingo na Mpondela  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mahojiano na Mtangazaji wa BBC leo jijini Dar es Salaam.

Ziara ya Rais Dk.Ali Mohamed Shein Pemba

Ziara ya Rais Dk.Ali Mohamed Shein Pemba

August 25, 2015

x1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuzindua Tawi la Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika Chuo cha Benjamin Willium Mkapa Mchanga mdogo kaskazini Pemba leo,(kulia)Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein na (kushoto) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna,
[Picha na Ikulu.]
x2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Said Mohamed Seif wakati alipotembelea katika madarasa ya Tawi la Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika Chuo cha Benjamin Willium Mkapa Mchanga mdogo kaskazini Pemba leo baada ya kufanya uzinduzi rasmi.
x3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akitoa  maelezo wakati alipotembelea maktaba ya  Tawi la Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika Chuo cha Ualimu cha Benjamin Willium Mkapa Mchanga mdogo kaskazini Pemba leo baada ya kufanya uzinduzi rasmi.
x4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Said Mohamed Seif (katikati) wakati alipotembelea katika madarasa ya Tawi la Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika Chuo cha Ualimu cha Benjamin Willium Mkapa Mchanga mdogo kaskazini Pemba leo baada ya kufanya uzinduzi rasmi.
x5
Wanafunzi katika Chuo cha Ualimu cha Benjamin Williuam Mkapa  na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya mchanga mdogo wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza baada ya uzinduzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika Chuo hicho leo katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo Mkoa wa kaskazini Pemba.
x6
Baadhi ya Wazee na Wananchi wa Kijiji cha Mchanga mdogo Kaskazini Pemba wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika Chuo hicho leo katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo Mkoa wa kaskazini Pemba.

MASABURI ASEMA CHAGUA DOUBLE M

August 25, 2015


Gari maalum la kampeni za mgombe Ubunge wa Jimbo la
Ubungo jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Didas
Masaburi likipita eneo la Manzese kuhamasisha wananchi kushiriki mkutano wa
uzinduzi wa kampeni za CCM, Jangwani juzi.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha
Mapinduzi, Dk Didas Masaburi akiwapungia mikono wapiga kura wa jimbo lake
wakati alipoongoza msafara wa wanaCCM wa jimbo hilo kuelekea viwanja vya
Jangwani, Dar es Salaam kumsikiliza mgombea urais wa chama hicho, Dk John
Magufuli juzi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha
Mapinduzi, Dk Didas Masaburi akiwapungia mikono wapiga kura wa jimbo lake
wakati alipoongoza msafara wa wanaCCM wa jimbo hilo kuelekea viwanja vya
Jangwani, Dar es Salaam kumsikiliza mgombea urais wa chama hicho, Dk John
Magufuli juzi.
Source: Father Kidevu Blog
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubunge kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi, Dk Didas Masaburi (katikati) akisalimiana na mgombea ubunge wa
chama hicho katika Jimbo la Sengerema, William Ngeleja. Kulia ni Mbunge wa
Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji, wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za
CCM Jangwani, Dar es Salaam juzi.
TAASISI YA BILL NA MELINDA GATE YAANGALIA UWEZEKANO WA KUSAIDIA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA KILIMO NCHINI TANZANIA.

TAASISI YA BILL NA MELINDA GATE YAANGALIA UWEZEKANO WA KUSAIDIA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA KILIMO NCHINI TANZANIA.

August 25, 2015

x1
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates Bw. Stanley Wood akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) nchini Tanzania kuangalia uwezekano wa taasisi hiyo kusaidia miradi ya ukusanyaji wa Takwimu za kilimo nchini Tanzania.Kushoto kwake ni Mratibu wa miradi wa Taasisi hiyo Bi.Bhramar Dey.
x2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu umuhimu wa takwimu za Kilimo nchini Tanzania na mikakati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha upatikanaji wa Takwimu za kilimo nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw.Morrice Oyuke.
x4
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof.Innocent Ngalinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya chuo anachokiongoza katika kutoa elimu kwa watakwimu wa kilimo nchini Tanzania na mpango wa chuo hicho kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za  kilimo kwa kutumia wataalam wanaozalishwa.
x5
Mtakwimu mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi.Elizabeth Talbert( kulia) na Meneja wa Idara ya Viwanda na Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Joy Sawe wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wawakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates jijini Dar es salaam.
Picha na Veronica Kazimoto.
…………………………………………………………………………………….
Na  Aron Msigwa
Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gate imekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)kuangalia namna ya inavyoweza kusaidia  upatikanaji wa Takwimu Bora za Kilimo nchini Tanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanyika kwa  mazungumzo hayo jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi wa Taasisi hiyo anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo Bw. Stanley Wood amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali Barani Afrika na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika  zilizopewa kipaumbele na kunufaika na taasisi hiyo.
Amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na matokeo chanya, taasisi hiyo inaangalia uwezekano wa kusaidia upatikanaji wa takwimu bora za kilimo.
” Juhudi kubwa imefanywa na Tanzania katika kufanikisha mambo mbalimbali, kwa upande wetu tumeona vipaumbele vilivyopo ili tuweze kuona namna  tunavyoweza kutoa mchango wetu kusaidia ukusanyaji wa takwimu Bora za kilimo , kikubwa ni kuendelea  kujenga ushirikiano wa kuwezesha ufanisi wa tafiti mbalimbali” Amesema.
Wood ameeleza kuwa taasisi ya Bill na Melinda Gates imekuwa ikichangia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Barani Afrika kupitia mashirika ya kimataifa yanayohusika na utoaji wa huduma kwa umma na kuitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika  zinazonufaika na miradi  hiyo.
Amesema taasisi ya Bill na Melinda Gate kwa kipindi kirefu imekuwa ikitoa kipaumbele kusaidia miradi ya afya hasa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi, kusaidia huduma za Afya ya mama na mtoto  pamoja na kuweka mkazo  katika kuimarisha huduma za maji safi na maji Taka Barani Afrika.
Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein azindua miradi ya maendeleo katika Mkoa kaskazini Pemba

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein azindua miradi ya maendeleo katika Mkoa kaskazini Pemba

August 25, 2015

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume akiwa katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wq kaskazini Pemba,
[Picha na Ikulu.]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume   katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wq kaskazini Pemba.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa majisafi na salama katika kijiji cha Taif wete kaskazini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuifungua  miradi mbalimbali ya Serikali kisiwani humo, mradi uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ADB,
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua mfereji kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa majisafi na salama katika kijiji cha Taif wete kaskazini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuifungua  miradi mbalimbali ya Serikali kisiwani humo,mradi uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ADB,
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtwisha Ndoo ya Maji Mwajuma Ahmed Abdalla baada ya kufungua Mradi wa Maji safi na Salama katika kijiji cha  Taif Wete Pemba Mkoa wa Kaskazini leo akiwa katika ziara ya kuifungua  miradi mbalimbali ya Maendeleo, mradi ambao uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ADB,

NYUMBU KUENDELEA KUWAWEZESHA WANANCHI KUJIINUA KIUCHUMI

August 25, 2015

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu miradi mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo inayodhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo utengenezaji wa matrekta madogo( power Tiller) ambayo yanalenga kumkomboa mkulima hapa nchini kwa kuondokana na matumizi ya jembe la makono.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) umuhimu wa kutoa habari za kuelimisha kwa jamii hasa zitakazowawezesha kuwajengea uwezo wa kimaarifa na kuwainua kichumi kupitia elimu hiyo.
Mhandisi Mkuu Msanifu Albert Wikedzi akiwaonesha waandishi wa Habari (Hawapo pichani) aina mbalimbali za sanifu zinazofanyika katika shirika hilo, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika kiwanda hicho Mjini  kibaha.
 .Mhandisi Mkuu wa Karakana kutoka Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Ayoub Mnzava akiwaonesha waandishi wa habari trekta ndogo (Power Tiller) iliyotengenezwa kwa lengo la kuongeza uwezo wa wazalishaji wa mazao ya kilimo kote nchini.
 Mkuu wa Kitengo cha Usubiaji Mhandisi Anderson Ole Zakaria akiwaeleza waandishi wa habari namna kitengo hicho kinavyofanya kazi ili kukidhi mahitaji ya kiwanda ambapo alisema kitengo hicho kinayeyusha hadi tani 2.5 za chuma zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotoka katika shirika hilo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim akiwaonesha waandishi wa habari moja aina ya gari la kivita lililotengezezwa na shirika hilo.
.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara hiyo,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe na kushoto ni mwandishi mwandamizi wa Channel Ten.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

VODACOM NA MONEYGRAM WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

August 25, 2015

 Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi  wa makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram (Moneygram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kutuma fedha na kuingia moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini.Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam.
003.Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(katikati) na Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kulia)wakimshuhudia Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt(kushoto)akisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram(Monegram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(katikati) akiwashuhudia Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt(kushoto) na Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kulia)wakipongezana mara baada ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa  kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram(Moneygram M-Pesa)ambayo yatawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kushoto) na Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt,wakiteta jambo wakati  wa hafla ya Uzinduzi  wa makubaliano yaushirikiano wa  kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram (Moneygram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kutuma fedha na kuingia moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini.Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(kulia) akijibu maswali kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma ya za kutuma na kupokea fedha kupitia njia ya M-pesa na Moneygram(Monegram M-Pesa)kati ya Vodacom Tanzania na  Moneygram huduma hizo zitawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam. ,Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel na  Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt.

Makubaliano mapya yanawawezesha wateja kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti za M-Pesa nchini Tanzania.

DAR ES SALAAM (Agosti 25, 2015) —Kampuni ya MoneyGram inayotoa huduma za kutuma pesa duniani na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania zimetangaza kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M-Pesa. Kwa sasa, kuna watumiaji wa huduma ya M-Pesa zaidi ya milioni saba nchini Tanzania ambao hufanya miamala ya zaidi ya trilioni mbili kila mwezi.

Ushirikiano huo mpya utawawezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kutuma fedha moja kwa moja kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini ambao ni wateja wa M-Pesa kwa njia rahisi, inayofaa, salama na haraka zaidi. Hatua hiyo itafungua uwezekano wa kukuza utumaji pesa kwenda Tanzania, ambao kwa sasa ni umefikia dola za Marekani bilioni 1.2.

Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo pia ulihudhuriwa na Herve Chomel, Makamu wa Rais wa MoneyGram Upande wa Mauzo Kanda ya Afrika na Jacques Voogt, Ofisa Mkuu wa wa Idara ya biashara ya huduma za M-Pesa wa Vodacom Tanzania.

“Kampuni ya MoneyGram inafurahi sana kufanyakazi na Vodacom kutoa huduma ya haraka, uhakika na salama  kwa mamilioni ya wateja watakaotuma na kupokea pesa,” alisema Chomel. “Vodacom M-Pesa tayari imesaidia kuongeza huduma za utumaji pesa kwa gharama nafuu kwa mamilioni ya watu wa makundi mbalimbali nchini Tanzania na ushirikiano huu mpya utawawezesha zaidi watu walio vijijini na mijini kupokea pesa kutoka kwa marafiki na jamaa zao wanaoishi nje ya nchi.”
Aliongeza kusema, “MoneyGram inaendelea kukua Afrika yote kutokana na uhusiano mzuri ilionao na kampuni za mtandao wa simu, mabenki, ofisi za posta, watoahuduma za rejareja ili kuwapa kipaumbele zaidi wateja wetu. Kwa sasa, MoneyGram inatoa huduma zake kwa zaidi ya nchi 200 huku ikiwa na mtandao wa za mawakala zaidi ya 350,000 kote duniani ambapo 25,000 wanatoka Afrika.”

“Uhusiano huu mpya na MoneyGram unatuwezesha kuingiza nchini dola za Marekani bilioni 1.2 kwa wateja wetu kila mwaka, anasema Voogt. “Utawarahisishia zaidi na kuwezesha familia na marafiki kupokea pesa kupitia M-Pesa. Hii ni njia mojawapo tunakwenda mbali zaidi kwa ajili ya wateja wetu.”



Wateja wa M-Pesa nchini Tanzania wanaweza kupokea pesa kutoka MoneyGram moja kwa moja kwenye akaunti za simu zao kutoka kwa wateja katika nchi zaidi ya 120 kwa saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki na siku 365 kwa mwaka kulingana na mfumo uliopo. Wateja wanaoishi nchini Marekani wanaweza kutuma pesa kwenda kwenye akaunti za M-Pesa kwa haraka na usalama zaidi  kutoka kwa wakala wa MoneyGram au MoneyGram kwa njia ya mtandao.

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID KUHUSU HALI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

August 25, 2015

 Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari hawaponi pichani juu ya Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono Kunywa maji yaliyo safi na salama – yaliyochemshwa au kutiwa dawa Hakikisha usafi wa mazingira yako wakati wote ikiwa ni pamoja na chooni Kutokula matunda au kitu chochote bila kukisafisha kwa maji safi na salama Kuhakikisha unatumia choo kwa ufasaha na wakati wote Kuwahi mapema na toa taarifa kituo cha huduma  ya afya kilicho karibu na wewe endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au kutapika
 Katibu Mkuu wa Wizari wa Afya na Usitawi wa Jamii.Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya Usafirishaji holela wa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Ni vyema kutoa taarifa iwapo kuna abiria mwenye dalili  za ugonjwa huu ili ushauri uweze kutolewa wa namna ya kumsafirisha.
 Mwakilishi wa Shilika la Afya Duniani( WHO) Dk Rufaro Chatora akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya  Kufungua kambi za wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa zote tatu za Dar es Salaam ambapo kwa Kinondoni kambi ipo Mburahati, Ilala, kambi ipo kituo cha Afya Buguruni  na Temeke katika Hospitali ya Temeke. Kwa Mkoa wa Morogoro kambi zimefunguliwa Sabasaba na St Thomas.
Waandishi wakimsiliza kwa makini Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid.
Picha na Emmanuel Massaka.

IDADI YA WAGONJWA WALIYORIPOTIWA KUAMBUKIZWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU AMBAO UMELIKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM PAMOJA NA MKOA WA MOROGORO IMEFIKIA WAGONJWA 262  NA VIFO 8.
                                                                                 
Idadi ya wagonjwa waliyoripotiwa kuambukizwa na Ugonjwa wa Kipindipindu ambao umelikumba jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Morogoro imefikia wagonjwa 262,huku vifo  hadi sasa toka ugonjwa huo ugundulike Agost 15 mwaka huu vikifikia nane.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Daktari Seif Rashidi wakati akizungumza nawaandishib wa habari ikiwa lengo ni kutoa taarifa juu ya Ugonjwa huo hatarI ambao umeibuka kwa kasi jijini Dar es salaam pamoja na Mkoani Morogoro.

Aidha alisema kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa katika jiji la Dar es salaam walioambukizwa ni 230 na vifo saba,ambapo Manispaa ya Kinondoni ina wagonjwa 186,Manispaa ya Ilala wagonjwa 22 na Temeke 22 nakwamba wagonjwa waliyolazwa kwenye  kambi  za matibabu ni 71 ambazo ni Mburahati wagonjwa 47,kambi ya Buguruni 15 huku kambi ya Temeke ni wagonjwa 9.

Aliendelea kufafanua kuwa wagonjwa  wengi wamekuwa wakitoka katika maeneo mabalimabali ambapo katika Manispaa ya Kinondoni ni maeneo ya   makumbusho,kimara,Tandale,Manzese,Saranga,Magomeni,Mwananyamala,kibamba,kigogo,Goba,Burahati,Kinondoni na Kijitonyama.

Manispaa ya Ilala ni Buguruni,Majohe,Chanika,Ilala sharif shambana Tabata huku Katika Manispaa ya Temeke wagonjwa wengi ni kutoaka katika maeneo ya kwa Azizi Ally,Keko na Yombo Vituka.
Alisema Mkoani Morogoro wagonjwa waliyoripotiwa Agost 24 mwaka huu ni 32 na kifo kimoja ambapo pia wagonjwa wapatao 15 wamehifadhiwa kwenye kambi ya Matibabu ya Sabasaba Mkoani humo.
Waziri huyo wa Afya na Ustawi wa Jamii ametoa tahadhari kwa jamii kuchukua tahdhari pamoja na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo,kuzingatia usafi wa mazingira,kuchemsha maji ya kunywa,kunawa  mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula chakula,kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikoni,kuzingatia usafi wa vyoo pamoja na kula vyakula ambavyo vimeandaliwa kwenye mazingira safi na salama.

Naye mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora amesema kuwa lazima kuwepo na hatua za haraka za kusafisha visima kwa kemikali maalumu na kuhamasisha jamii kutumia vidonge vya kusafisha maji au kuchemsha maji.

Aidha aliongeza kuwa mamlaka husika zichukue hatua za haraka na madhubuti kushugulikia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazigira katika maeneo husika nakwamba suala hilo siyo la Wizara ya Afya pekee bali ni ushirikiano na Wadau wengine ikiwemo sekta ya Uchukuzi,Mawasiliano,Maji na Elimu.

Katika hatua nyingine Wizara ya Afya imetoa namba za simu ya mkononi kwa wananchi  ambazo ni 0767300234 ambapo zitatumika kuwasiliana moja kwa moja na mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili kupata maelekezo ya kitabibu mara baada ya kuhisi dalili za maambuki ya ugonjwa huo.    

FAIDA BENKI YA EXIM YAKUA KWA ASILIMIA 69

August 25, 2015

 Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati)akisisitiza jambo  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kushoto) na Meneja Mwanadamizi wa utafiti na uchambuzi wa biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Mrawa (wa kwanza  kulia)
Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (wa kwanza kulia)akisisitiza jambo  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (katikati) na  Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde
Benki ya Exim Tanzania imefanikiwa kujipatia faida ya sh. bilioni 12.79 (kabla ya kodi) katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu, takwimu zinazoonyesha ongezeko la faida kwa asilimia 69 katika benki hiyo.
“Ongezeko hilo ni kubwa ikilinganishwa na faida yash.bilioni 7.56 tuliyoiopata katika robo mwaka iliyotangulia na hivyo basi tunajisikia fahari kutangaza faida hii mbele yenu,’’ alibainisha Afisa Fedha Mkuu wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Kwa mujibu wa Bw Ponda faida hiyo pia ni sawa ongezeko la asilimia 28 ikilinganishwa na faida ya kiasi cha sh. bilioni 13.96 katika kipindi cha miezi sita kwa mwaka uliopita.
 “Katika robo mwaka hii iliyoisha mwezi Juni, jumla ya mapato kwenye faida  itokanayo na riba ilikuwa kwa asilimia 26 hadi kufikia sh. bilioni 17.9  ongezeko lilichangiwa na gharama nafuu ya amana zetu sambamba na usimamizi bora wa fedha,’’ alibainisha.
Zaidi Bw. Ponda alisema katika kipindi hicho  faida isiyotokana na riba ilikuwa kwa asilimia 43 hadi kufikia kiasi cha sh. bilioni 12.3 kutoka sh. bilioni 8.6 iliyorekodiwa katika mwaka uliopita.
Benki hiyo pia ilikuwa na mapato mgao kutokana na uwekezaji wenye ukubwa kiasi cha sh. bilioni 2.3 ikilinganishwa na kiasi cha sh. bilioni 2 kilichorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.
"Nguvu ya ukuaji wa mapato inaoyesha mafanikio ya Benki.. Tunaendelea kuboresha  ufanisi katika uendeshaji na utoaji wa huduma zetu ili kuwaridhisha zaidi wateja wetu. Kwa ripoti hii  matokeo yanaonyesha kwamba Exim tumeonyesha utendaji bora hasa kwa kuhusisha rasilimali watu na technolojia iliyo bora zaidi "aliongeza.