March 16, 2014

BREAKING NEWZ,UWANJA WA NDEGE YAATANGAZWA HALI YA KUTOKUWA SALAMA

Ndege ya shirika la ndege la Malawi
Mamia ya wasafiri wamekwama katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Blantyre, Malawi baada ya uwanja huo kusemekana kutokuwa salama.

PENZI LA MR BLUE LAENDELEA KUMTESA NAJ

March 16, 2014

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ambaye huwa anaishi na kufanya Kazi nchini Uingereza Naj amefunguka kuwa Tangu aachane Mr Blue zaidi ya Mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita hajawahi kukutana na Mwanaume na wala hajawahi kumpenda mwanaume yeyote, Naj amefunguka hivi karibuni kabla hajaelekea U.K akaendelea kunitiririkia kuwa alikua na Mr Blue kwa miaka mitano na ikaishia kwa yeye kukimbiwa na Blue akamkana hadharani na kuanzisha mahusiano na mwanadada mwingine hali iliyomhuzunisha na kujutia muda wake, Naj akamalizia kwa kuniuliza Je angeutumia muda huo kwa kupiga kazi si angekua mbali sana? kwa hiyo sasa hivi anacho angalia ni kazi tu kwa kwenda mbele, yuko singoooooooooooooo,
March 16, 2014

VODACOM Tanzania yatoa msaada ya Miavuli 20 kwa Jeshi la usalama Barabarani

001.POLICE
Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa  akipokea msaada wa miamvuli(20)kutoka kwa Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi,wanaoshuhudia wa pili kutoka kulia ni Tumaini  Kimaro, Simoni Lugangila na Emmanuel David. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
002.POLICE
Menaja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akifungua mmoja ya miamvuli(20)kabla ya kuikabidhi rasmi kwa Mkaguzi Msaidi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni ,Byego Marwa(kulia) msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
March 16, 2014
 Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili akiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo mbunge huyo alimwelezea  Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe(hayupo Pichani)namna alivyotekwa, kuteswa na watu aliodai kuwa ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha Chama Ch Mapinduzi (CCM), Green Guard.
 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akimjulia hali na kumsikiliza Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili akiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo mbunge huyo alimwelezea kiongozi huyo namna alivyotekwa, kuteswa na watu aliodai kuwa ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha Chama Ch Mapinduzi (CCM), Green Guard.

 Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee, namna ambavyo Mbunge Rose Kamili alikuwa akiendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.
 Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili lililotokea jana usiku katika Kijiji cha Kitawaya, Kaa ya Luhota, jimboni Kalenga, wakati alipokuwa akizungumza na mawakala wa CHADEMA, ambapo imedaiwa kitendo hicho kilifanywa na vijana wa ulinzi wa CCM.
March 16, 2014

Picha Kutoka Kampeni Za CCM Chalinze:Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete Kweli Amedhamiria Kuwakomboa Wanachalinze

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
March 16, 2014

MOTO WATEKETEZA NYUMBA ZA POLISI TANGA

moto_24117.jpg
Nyumba za Askari wa jeshi la polisi zilizopo eneo la chumbageni nyuma ya kituo cha polisi kikuu cha chumbani jijini Tanga zaungua moto.
March 16, 2014

NDOTO ZA BANDARI MPYA YA MBEGANI YAKAMILIKA

????????  
Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wawakilishi wa wanavijiji vya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani na Timu ya Uthamini wa Ardhi wa eneo la mradi. Waliokaa viti vya mbele ni viongozi wa Timu ya ukaguzi, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kulia) na Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia). Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.????????  
Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) akizungumza katika mkutano huo.
March 16, 2014

WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA SIKU YA UTEPE MWEUPE TANZANIA MKOANI RUKWA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa katika zoezi la ukaguzi wa mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu na huduma za mama wajawazito na watoto wachanga katika maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe Tanzania yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa katika Tarafa ya Mtowisa. Dkt. Seif Rashid alimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambae awali alikubali kushiriki maadhimisho hayo ambapo amekabiliwa na majukumu mengine ya kitaifa. Kushoto kwa Dkt. Seif Rashid ni Mratibu wa Taifa wa Utepe mweupe Mama Rose Mlay. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni “WAJIBIKA MAMA AISHI”
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akihutubia katika maadhimisho hayo ambapo aliwapongeza wadau wote wanaopigania na kusaidia afya ya mama na watoto na kuahidi kutoa kipaombele katika bajeti kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto nchini. Aidha amezitaka Halmashauri nchini kutoa kipaombele kwa kuongeza bajeti zao katika kuhudumia afya ya mama wajawazito na watoto wachanga.
March 16, 2014

MAJI YAVUNJA NDOA PEMBEZONI MWA ZIWA TANGANYIKA,SOMA ZAIDI HAPA

Imefahamika kuwa,Ukosefu wa Maji kwa wakazi wa Mwambao wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma limekuwa sugu ,hali inayosababishia wanawake  wanaoishi katika vijiji  husika  kuvunjika kwa ndoa  zao .

Changamoto hiyo inayowakabili wakazi hao inatokana na viongozi husika kutokuwajibika ingawa vijiji hivyo vipo pembezoni mwa ziwa Tanganyika hali inayochangia jamii iwe sehemu ya uchafuzi wa mazingira ya ziwa hilo lenye rasilimali ya madini ya gesi,samaki ,dagaa wa aina mbalimbali.

Mkazi wa Kalalangabo,  Kabwe  Mzee alisema  kumekuwa na mgogoro wa mahusiano  hasi kati ya mke na mume kwa kuwekeana dhana potofu kuwa huenda mkewe hakuwa kisimani kusubiri maji na hivyo kupelekea ndoa zao kuvunjika.
 MAN UNITED WAKALISHWA 3-0 NA LIVERPOOL OLT TRAFFORD, GERRARD ALMANUSRA APIGE HAT-TRICK!!

MAN UNITED WAKALISHWA 3-0 NA LIVERPOOL OLT TRAFFORD, GERRARD ALMANUSRA APIGE HAT-TRICK!!

March 16, 2014
LIVERPOOL kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano iliyopita wamepata ushindi katika dimba la  Old Trafford baada ya kuwafumua wenyeji Manchester United mabao 3-0.
Nahodha mashuhuri wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uingereza, `Mr. Liverpool`,  Steven Gerrard alifunga mabao mawaili, huku bao la tatu likitiwa kambani na Luis Saurez.
Gerrard alifunga kwa penati dakika ya 34 baada ya Rafael kuushika mpira kwa mkono, na alifunga penati nyinginie dakika ya 46 kufuatia Phil Jones kumfanyia madhambi Joe Allen eneo la hatari.
Nyota huyo wa England angefunga mabao matatu `Hat-Trick` katika dimba la Old Trafford tangu mwaka 1936 endapo angefanikiwa kutia kambani penati ya tatu waliyopewa dakika ya 79 baada ya Nemanja Vidic kumfanyia madhambi Daniel Sturridge, lakini alikosa penati hiyo.
Vidic alitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini  penati ya tatu inaonekana haikuwa halali kwani Sturridge alionekana katika video akimdanganya mwamuzi na kushinda janja yake.
Kikosi cha Man Utd leo: De Gea 6, Rafael 5,Jones 5, Vidic 5, Evra 5.5, Fellaini  5 (Cleverley 76, 6), Carrick 5, Mata 4.5 (Ferdinand 87), Rooney 4.5, Januzaj 5 (Welbeck 76, 6), Van Persie 4.5.
Kikosi cha Liverpool: Mignolet 7, Johnson 7, Skrtel 8, Agger 7.5, Flanagan 7.5, Henderson 7.5, Gerrard 8.5 (Lucas 87), Allen 8, Sterling 6 (Coutinho 72, 6), Sturridge 8, (Aspas 90+1), Suarez 8.
Unbelievable: Luis Suarez celebrates after scoring the third in the 3-0 win at Old Trafford
 Hawaamini: Luis Suarez akishangilia bao la tatu alilofunga katika ushindi wa  3-0 uwanjani  Old Trafford
March 16, 2014

ADEN RAGE: SIGOMBEI TENA UONGOZI SIMBA - UCHAGUZI MKUU MEI 4 MWAKA HUU

20140316-133233.jpg
By Israel Saria on March 16, 2014

JK ACHANGIA UWANJA WA SIMBA

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, jana ametangaza rasmi kwamba hatagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Mei 4 mwaka huu.

Hata hivyo Rage kabla ya kutangaza maamuzi yake ya kutotetea cheo hicho katika uchaguzi mkuu ujao, wanachama wa klabu hiyo walianzisha vurugu katika mkutano mkuu huo uliotishwa maalumu kwa ajili ya kufanya marekebisho wa katiba kutokana na kiongozi wao huyo kuwaita ‘mbumbumbu’.
March 16, 2014

WAZIRI MAJI MH JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA RASIMI WIKI YA MAJI KITAIFA MKOANI DODOMA

 Waziri wa maji Jumanne Maghembe akipata maelezo kutoka kwa mtalamu kutoka nnchini Australia Eng Johann Fabach kuhusu bomba lililo tengenezwa kwa teknolojia ya kisasa nchini Australia ambalo haliharibiki kwa urahisi wala kupata kutu kulia ni mkurugenzi msaidizi wa kutoka Prima Business ya nchini Australia Bibi Annastella Baradyana maonyeshohayo yanafanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mjini Dodoma. 
Ofisa Habari wa Dawasa Neli Msuya akitoa maelezo kwa waziri wa Maji Jumanne Maghembe kuhusu shughuli zinazo fanywa na Dawasa mjini  . Picha na chris Mfinanga
March 16, 2014

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS ZUMA WA AFRIKA KUSINI LEO IKULU, DAR ES SALAAM

 UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.


Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam. 
Mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete. 
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Machi,2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
March 16, 2014

GODFREY MGIMWA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA KALENGA NI USHINDI WA KISHINDO MATOKEO YA AWALI

Godfrey Mgimwa akibebwa juu juu na wanachama na wapenzi wa CCM baada ya matokeo kuonyesha ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga leo.
March 16, 2014

Azam FC Vs Coastal Union jana.

 Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal akifuatilia mechi kwa umakini uwanja wa Chamazi leo, ambapo Wagosi wa kaya walilala 4-0.
March 16, 2014

ONA CHAMA CHA MAPINDUZI WALIVYOFUNIKA KALENGA KABLA YA KUANZA KUPIGWA KURA ZA UBUNGE LEO LIVE!!

Katibu Mkuu CCM,Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga wakiingia kwenye Uwanja wa Mkutano Kata ya Nzihi Jimbo la Kalenga,Pia walichukua muda kusalimiana na Wananchi wa Kata ya Nzihi waliokuwa na Shauku ya Kusikia maneno ya Viongozi hawa wa Chama Cha Mapinduzi.
March 16, 2014
Watanzania wanne (mwanaume mmoja na wanawake watatu) wamekamatwa na kilo 2.2 za heroin kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
March 16, 2014

YANGA SC CHUPUCHUPU KUPATA AJALI MBAYA, BASI LAO LANUSURIKA KUPINDUKA ILIKUWA NI MBILINGE YA KUTOKEA MADIRISHANI ASUBUHI YA LEO MIKESE

Hatari; Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akiruka dirishani kutoka kwenye basi la timu hiyo baada ya kunusurika kupinduka asubuhi ya leo eneo la Mikese, Morogoro wakati wakijaribu kukwepa basi la abiria. Yanga SC ilikuwa inatokea Morogoro ambako jana ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar na kutoka sare ya bila kufungana.
Basi la Yanga likiwa limeinama upande mmoja baada ya kukwepa basi la abiria. Hakuna aliyeumia na timu imeendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam baada ya mkasa huo
March 16, 2014

MTATIRO: KUMPA JAJI WARIOBA DAKIKA 60 ILI AWASILISHE RASIMU YA KATIBA NI JAMBO LISILO HAKI, NI KINYUME KABISA NA KANUNI ZA BUNGE TULIZOPITISHA NA NI KULIBURUZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Kanuni ya 47(a) ya bunge maalum la katiba inaeleza kuwa "Mwenyekiti(wa bunge maalum la katiba) baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Tume(ya mabadiliko ya katiba) watapanga muda unaofaa kwa ajili ya Mwenyekiti wa Tume(ya mabadiliko ya katiba) kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum"
Jambo la ajabu ni kuwa, jana jumamosi, mhe. Samweli Sitta(namheshimu sana) ametangaza kuwa, siku ya kesho jumatatu jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ATAWASILISHA RASIMU KWA MUDA USIOZIDI DAKIKA 60.
March 16, 2014

BREAKING NEWSSS!!! SOMA HAPA AJIRA MPYA YA WAALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14


OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA 
MITAA (OWM - TAMISEMI)

AJIRA MPYA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA 
MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14. 
WANANCHI WAILALAMIKA KUWA SERIKALI HAIJAWALIPA FIDIA KUWEZA KUPISHA UJENZI WA UWANJA WA KIMATAIFA TANGA.

WANANCHI WAILALAMIKA KUWA SERIKALI HAIJAWALIPA FIDIA KUWEZA KUPISHA UJENZI WA UWANJA WA KIMATAIFA TANGA.

March 16, 2014

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
BAADHI ya Wakazi waliokuwa wamejenga katika eneo ambalo shirikisho la soka nchini kwa kushirikiana na shirikisho la soka duniani (FIFA) wanatarajiwa kujenga uwanja wa Kimataifa wamelalamika kuwa serikali bado haijawalipa fidia ili kuweza kupisha ujenzi wa uwanja huo.

Hatua ya wakazi hao inatokana na kuona Rais wa Shirisho la soka nchini (TFF)Jamali Malinzi akitembelea uwanja huo na kuanza mikakati ya ujenzi wa uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu mabilioni ya fedha za kitanzania.

Wakizungumza katika nyumba zao wanazoishi ndani ya eneo la shirikisho hilo lililopo Mnyanjani jijini Tanga baadhi ya waathirika hao ambao wengi wao ni akina mama Christina Lucas alisema wamekuwa wakihangaikia fidia kila kukicha kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ili waweze kupisha ujenzi wa uwanja wa kimataifa bila mafanikio yoyote.