Ujumbe kutoka USAID Marekani waipongeza Tanzania

October 18, 2017
Binagi Media Group
Mapambano dhidi ya ugongwa hatari wa Malaria yameendelea kuonyesha mafanikio mkoani Mwanza, baada ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo kupungua kutoka asilimia 19.01 mwaka 2011/12 hadi asilimia 15.1 mwaka 2015/16.


Hiyo ni kutokana na juhudi za serikali kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo shirika la misaada la watu wa Marekani USAID ambalo limeendelea kusaidia vyandarua vyenye kinga kwa ajili ya mapambano dhidi ya malaria.

Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi aliyasema hayo jana wakati wa zoezi la kugawa vyandarua bure katika shule ya Msingi Senge iliyopo Kata ya Bujashi wilayani Magu ambalo lilishuhudiwa pia na ujumbe kutoka USAID Marekani.

Alisema mbali na kuua vimelea vya Malaria kwa kutumia viuatilifu, pia serikali inagawa vyandarua bure katika shule za msingi, vituo vya afya, zahanati pamoja na hospitali ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Monica Ngalula pamoja na Marco Yusuph ni baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Sese, walishukuru kwa kugawiwa vyandarua hivyo na kwamba vitawasaidia wasing’atwe na mbu wa Malaria wakiwa wamelala nyumbani kama ilivyokuwa hapo awali.

Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka USAID, Chriss Thomas alifurahishwa na juhudi za Tanzania kupambana na ugonjwa wa Malaria na kuahidi ushirikiano zaidi wa kusaidia mapambano hayo ili kuokoa maisha ya watu hususani akina mama wajawazito pamoja na watoto ambao wamekuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka USAID, Chriss Thomas akizungumza na wanahabari
Ujumbe kutoka USAID Marekani ukiwa shule ya msingi Sese wilayani Magu kushuhudia zoezi la ugawaji vyandarua
Mwanafunzi wa shule ya msingi Sese akipokea chandarua kutoka USAID
Mwanafunzi wa shule ya msingi Sese akipokea chandarua kutoka USAID
Ugeni kutoka USAID Marekani
Shule ya msingi Sese wilayani Magu ni miongoni mwa shule za msingi 941 ambazo wanafunzi wake wananufaika na zoezi la ugawaji vyandarua bure mkoani Mwanza.
HAKUNA MATATA’ YA TUMAINI MSOWOYA KUACHIWA ALBAMU YAKE OCTOBER 29

HAKUNA MATATA’ YA TUMAINI MSOWOYA KUACHIWA ALBAMU YAKE OCTOBER 29

October 18, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera anatarajia kuwa mgeni rasmi katikauzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tumaini Msowoya, katika ukumbi wa Highland Hall mjini Iringa.
Wageni wengine wa heshima kwenye uzinduzi huo ni  Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha Baby Baraka Chuma, wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.
Akizungumza na Mwanaspoti, Msowoya alisema tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.
“Naenda Iringa kurudisha shukrani zangu kwao, nataka wajue nipo huku sio tu kwa sababu ya kazi bali huduma ya kuimba niliyoanza ”
Alizitaja nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni Hakuna Matata, Mwamba, Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu, Wanawake Jeshi Kubwa, Samehe na Mungu wa Rehema.
“Kazi hii nimeifanya chini ya usimamizi wa JB Production ikisimamiwa na Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye meneja anayesimamia kazi zangu kwa sasa,’ alisema Msowoya.
Wasanii watakaomsindikiza
Meneja wa Msowoya, Smart Bilionea Producer Baraka alisema tayari waimbaji na kwaya  mbalimbali kutoka Iringa na Dar es Salaam watamsindikiza kwenye uzinduzihuo.
Alizitaja kwaya zizothibitisha kumsindikiza kuwa ni Wakorinto wa Pili kutoka Mufindi, Muhimidini na kwaya ya Vijana kutoka Iringa mjini.
Baadhi ya waimbaji ni  Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu ni Mungu tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine maarufu kwa jina la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses Simkoko, Ritha Komba na Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.
Wengine ni Rebecca Baraka, Jesca Msigwa, Ester Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis Lukosi,  Wadi Mbelwa, Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu Mgogo, Emma Sanga na Victoria Mwenda kutoka Iringa.
“Waimbaji watakaomsindikiza ni wengi nab ado tunaendelea kuwasajili wengine. Bado tupo kwenye mazungumzo na Bahati Bukiku ambaye anaangalia ratiba yake, ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.
Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya kutokana na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.
Historia
Hakuna Matata ni albamu ya pili ya Msowoya baada ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.
“Bahati mbaya niliitengeneza kutokana na kiwango kidogo hivyo iliishia kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii ni nzuri na wakazi wa Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.

RC APIGA MARUFUKU UTOAJI WA LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI AMANI MUHEZA

October 18, 2017

MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya Tatu za Zigi Juu,Zigi Chini na Kuhuhwi zilizopo kwenye Bonde la Mto Pangani katika eneo Amani wilayani Muheza na mradi wa maji mserereko kwa ajili ya vijiji vya Mashewa,Kimbo na Shembekeza

 MKUU wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
 MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza katika uzinduzi huo

Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa  UNDP ambao wamefadhili mradi huo akizuungumza katika uzinduzi huo
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza akizungumza katika uzinduzi huo Jumanne Omari
 Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
 Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
 Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na uchimbaji haramu wa madini katika eneo la Hifadhi ya Amani wilayani Muheza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akitembelea maeneo hayo kujionea athari ambazo zimetokana na uchimbaji haramu wa madini kwenye eneo la vyanzo vya Maji Amani na Hifadhi ya Msitu
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jumuiya ya watumiaji wa Maji na Mradi wa Maji Mserereko kwa vijiji vya Masheww,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akizundua mradi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo anayeshuhudia mwenye kilembe cheusi kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Mhandisi Zena Saidi
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akimtwisha ndoo mkazi wa eneo hilo kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa kwanza kulia ni Kaimu  Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza kushoto  ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said

Sehemu za wananchi wakishuhudia uzinduzi huo
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ameitaka wizara ya Madini kuacha kuendelea kutoa leseni za uchimbaji wa madini eneo hifadhi ya Amani wilayani Muheza huku wakitaka zilizotolewa kufutwa kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kwenye eneo hilo.

WANAHABARI WA TANZANIA WATEMBELEA KAMPUNI YA HUWAWEI NCHINI CHINA

October 18, 2017

 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa ndani ya Kiwanda cha Kampuni ya  Huwawei walipotembelea Kiwanda hicho kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.

 Wanahabari wakiwa katika kiwanda hicho.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja  Shenzhen nchini China, walipokwenda kutembelea kampuni ya Huwawei na kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikwemo utekelezaji wa mradi wa elimu wa Smart Education na e-Education unaotekelezwa katika shule ya msingi Baogang iliyopo nchini humona hivyo kukabiliana na tatizo la uhaba walimu.mpango huo pia wanatarajia kuuleta hapa nchini ili kuweza kuboresha sekta ya elimu.(Na mpiga picha Wetu)

TRUMARK WAPATA MAFUNZO YA KUBORESHA UFANISI TOKA SHIRIKA LA PUM KUTOKA NCHI YA NETHERLANDS

October 18, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akimshukuru Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka  nchi ya Netherlands,  Paulus Joseph Maria Jaspers wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

SERIKALI YALIPA MADENI YA NDANI BILIONI 190 KATIKA KIPINDI KIFUPI

October 18, 2017
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na  watumishi wa Mamlaka hiyo.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika  Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
 Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Bw. Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.
 Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji wa elimu kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi hiyo.
 Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu katika kazi zao.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati -walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Mkoa huo.
 Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Bw. Seif Mkude (kulia) akielezea kuhusu utayari wa wafanyabiashara wa Mkoa huo kulipa kodi wakati wa Mkutano kati ya wafanyabiashara wa Mkoa huo na Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati).
WAZIRI KAMWELWE AFURAHISHWA NA UTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI MOSHI

WAZIRI KAMWELWE AFURAHISHWA NA UTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI MOSHI

October 18, 2017
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tenki la Maji la Njari.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira wakifungua bomba kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Mang’ana.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amkimtua ndoo kichwani mama kutoka Kijiji cha Mang’ana, akiashiria kutimiza lengo la Serikali ‘‘kumtua mama ndoo kichwani’’ baada ya uzinduzi wa Mradi wa Mang’ana.
Msafara wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ukielekea kwenye Chanzo cha Maji cha Mang’ana katika uzinduzi wa Mradi wa Mang’ana.



Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ametoa pongezi nyingi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) kwa kufanikiwa kutoa huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 100 kwa Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Hayo aliyasema alipokuwa akizindua Mradi mkubwa wa Maji wa Manga’na, uliopo Kata ya Uru Kaskazini, utakaohudumia zaidi ya vijiji 11 katika Manispaa ya Moshi na Wilaya ya Moshi Vijijini baada ya kupokea taarifa ya hali ya huduma ya maji katika Mji wa Moshi.

“Nawapongeza MUWSA kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya, kwa kuwa ndio lengo la Serikali, kuwa ifikapo mwaka 2020 maeneo ya vijijini huduma ya majisafi na salama ifikie asilimia 85 na mijini asilimia 95. Nyinyi leo hii mmeshavuka lengo hilo kwa Manispaa ya Moshi, kwa kweli nimefurahishwa sana na jambo hili na mnastahili pongezi nyingi’’, alisema Mhandisi Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe aliendelea kusema kuwa kwa kufanikiwa lengo hilo, mamlaka hiyo sasa itaongezewa maeneo mengine zaidi, ili kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wengine wa Moshi Vijijini ambao hawajafikiwa na huduma ya maji, na kuahidi kama Waziri mwenye dhamana ya maji atawatafutia fedha kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kamwelwe ameagiza halmashauri zote nchini, kuwa usifanyike ujenzi wowote wa miradi kabla ya kupata chanzo cha maji cha uhakika, ili kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji nchini.

Waziri Kamwelwe alisema ni ufisadi kutengeneza miundombinu ya maji, bila kuwa na chanzo cha uhakika cha maji. Sitakubali miradi ikamilike halafu isitoe maji, wakati umefanyika uwekezaji mkubwa wa fedha za Serikali. Hivyo, ni marufuku mradi wowote kukamilika bila kutoa maji.

Naye Mkurugenzi wa MUWSA, Joyce Msiru alisema katika taarifa yake kuwa mradi huo ni moja ya miradi mikubwa iliyotekelezwa na mamlaka yake, ukiwa umegharimu zaidi ya Sh. bilioni 2 na utahudumia zaidi ya wananchi 34,000.

Mkurugenzi Msiru alitaja baadhi ya vijiji vitakavyohudumiwa na mradi huo kuwa ni Kariwa, Longuo, Njari, Rau, Okaseni na Msuni.