MKUBWA NA WANAWE YAMZAWADIA ASLAY GARI KATIKA BIRTHDAY YAKE.

May 07, 2015

 
Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye moyo wa kibinaadamu. Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu @mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari Na ninaushukuru uwongozi mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu @babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii wenzangu wa @yamoto_band mungu ndie atakaewalipa ... Nawatakia usiku mwema woote na Watu wa Dodoma Tukutane kesho pale Matei
AIRTEL YATOA PUNGUZO KABAMBE LA GHARAMA ZA MAWASILIANO

AIRTEL YATOA PUNGUZO KABAMBE LA GHARAMA ZA MAWASILIANO

May 07, 2015
????????
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora na zenye ubunifu nchini jana  imeendelea kudhihirisha hilo kwa kuzindua huduma mpya inayotoa  punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu (Dynamic Tariffing) Itakayojulikamana kama “Airtel Zone”. Sasa wateja wa Airtel wa malipo ya awali sasa watafaidi kupiga simu kwa gharama ndogo yenye punguzo la hadi asilimia 99 kwa simu za nchini.

Huduma hii ya Airtel Zone imezinduliwa kwa mara ya kwanza na Airtel ili kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano ya simu za mkononi na kutoa fursa kwa wateja wake kuongea zaidi kwa gharama nafuu mara tu watakapo jiunga kwa kupiga namba 107 na kufuata maelekezo au kupiga *149*39# kisha kuchagua) ‘
Akiongea wakati wa uzinduzi Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” uzinduzi wa punguzo la gharama za kupiga simu  ni uthibitisho wa dhamira ya kampuni ya Airtel kuwapatia watanzania dili lenye thamani halisia ya fedha zao na kuwawezesha watu wengi zaidi nchini kuwasiliana kirahisi. Lengo letu ni kuendelea kutoa huduma za kibunifu na zenye gharama nafuu ili kukithi mahitaji ya watanzania wote. Wateja wetu watakaojiunga na huduma ya “Airtel Zone” kuanzia leo, sasa hivi wataweza kupiga simu na kupata punguzo la hadi asilimia 99 na punguzo hili litategemea mahali alipo mteja”
????????
“Hii ni punguzo litakalosaidia sana wateja wa Airtel kupata unafuu wa kuwasiliana kibiashara, masomo au kwa kuwasiliana na ndugu jamaa au wapendwa wao bila kuwa na wasiwasi juu ya gharama zao za simu” alieleza bw, Nyakundi
Tunaamini huduma hii ya “Airtel Zone” imekuja kwa wakati muafaka wakati mawasiliano ya simu za mkononi ni nyenzo muhimu katika ukuzaji wa shughuli za kiuchumi na za kijamii aliongeza Nyakundi
Akifafanua zaidi kuhusu huduma hii Mkurugenzi wa Mawasilaiano Bi Beatrice Singano Mallya, alisema” punguzo la gharama litategemea mahali mteja alipo na muda anaopiga simu, mteja atapata ujumbe utakaomuonyesha kiwango cha punguzo anachopata kwa mahali alipo, alikadhalika mteja anaweza  kupiga *149*39*0# ili kuangalia kiwango cha gharama ya kupiga simu. Huduma hii ya “Airtel Zone” ni kwa wateja wa malipo ya awali  na punguzo hili litatumika kupiga simu za ndani tu .
????????
Sambamba na hilo mteja atakayekuwa na kifurushi cha muda wa maongezi kama vile Airtel yatosha na vifurushi vingine punguzo litaanza pale tu kifurushi chake cha muda wa maongezi kitakapoisha. 
Kuujiunga ni rahisi, bure na mara moja tu, piga 107 ufate maelekezo au piga *149*39#” aliongeza, Singano Mallya.

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA ISHIRINI WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

May 07, 2015


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya CRDB  unaotarajia kufanyika May 8  jijini Arusha.
SAM_2456Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Mtambuka Benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay
SAM_2443Baadhi ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha wakiwa katika mkutano huo.
SAM_2437Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo akiwa katika mkutano huo.
SAM_2432Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB
SAM_2450Kulia ni Katibu wa Bodi ya CRDB, John Baptist Rugambo, katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Frederick Nshekanabo, Kushoto Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja.
SAM_2454Mwandishi kutoka TV1, Arusha Jane Edward akijaribu kuchukua taswira katika mkutano huo.
SAM_2447 Meneja Kitengo cha Huduma kwa Wateja kwa njia ya simu, Ena Mwangama (kulia) na Edwin Nchimbi Ofisa Masoko wakifutilia mkutano huo.
SAM_2458Kulia ni Meneja Usajili wa Hisa kutoka Benki ya CRDB Emmanuel Ng’ui na Dorice Ngikari kutoka ofisi ya Katibu wakifatilia jambo
SAM_2460Mwandishi wa habari kutoka Mwananchi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Crdb Dk. Charles Kimei.
Na Pamela Mollel, Arusha

YANGA MABINGWA WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2014 - 2015

May 07, 2015



Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014- 2015, Yanga wakishangilia ubingwa wao huo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhidi ya Azam FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.Mtanange huo ulimalizika kwa Azam kushinda Bao 2-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MMG.

Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub cheti cha pongezi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Sepp Blatter kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara 2014 - 2015.Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi wa nne.
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Mwali kabla ya kukabidhiwa kwa wenyewe.
Watu wa huduma ya kwanza wakifatilia mchezo huku wakiangalia yule atakaeumia na kwenda kumsaidia, hii ni kutokana na Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hapa jijini Dar leo.
Nyanda wa Timu ya Azam, Mwadini Ali akiwa makini kulinda wakati mashambulizi yakiandama upande huo.
Msambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akimkimbiza Kiungo wa Kati wa Azam, Mudathir Yahya wakati wa mtanange wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Azam imeshinda bao 2-1.