DC Mgaza akisisitiza jambo leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Mkinga

April 25, 2013
MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani leo kulia kwake ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Anna Kiwanuka na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Picha na Mwandishi Wetu 

DC Mgaza akiwa ofisini kwake

April 25, 2013
MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza akiwa ofisini kwake leo wakati alipotembelewa na Mwandishi wa Blogii hii
RUVU SHOOTING, SIMBA SASA KUCHEZA MEI 5

RUVU SHOOTING, SIMBA SASA KUCHEZA MEI 5

April 25, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
 
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

 Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)