SERIKALI KUWALINDA WAHADZABE – WAZIRI MKUU
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa
nyuki kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles
Ratia katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11,
2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa
nyuki kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles
Ratia katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11,
2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali
iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki
barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
chaArusha ( AICC) Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael na watatu kulia ni
Jacob Edward. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akitazama mazao mbalimbali yanayotokana na nyuki
katika maonyesho yaliyokwenda sambambamba na Kongamano la Ufugaji Nyuki
Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC),
Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu na kushoto kwake ni Mhamasishaji wa ufugaji nyuki na usindikaji
asali wilayani Loliondo, Krystern Erickson.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali
iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki
barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
chaArusha ( AICC) Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael na watatu kulia ni
Jacob Edward. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma kabla ya kufungua kongamno la
ufugaji nyuki Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha
(AICC) Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua Kongamano la Ufugaji
Nyuki Barani Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha
(AICC) Novemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu vifaa vya kukamulia asali
kutoka kwa watalaam wa Kichina, Huang Hejie (kushoto) na Zhinyong Wang
(watatu kushoto) katika kongamano la Ufugaji Nyuki Afrika lililofanyika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Novemba 11,
2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema
Serikali itaendelea kuyalinda makabila madogo nchini yakiwemo ya
Wahdazabe na Wasandawe ambayo yanategemea rasilmali misitu kwa maisha
yao na ustawi wao.
“Tutakuwa tunafanya makosa kama
tutawanyang’anya rasilmali misitu makabila madogo hapa nchini kama vile
Wahadzabe, Wandorobo na Wasandawe kwani ndiyo rasilami pekee
inayowawezesha wapate chakula cha kutosha,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Novemba 11, 2014) wakati akifungua Kongamano la Kwanza la
Ufugaji Nyuki Barani Afrika la Mwaka 2014 lililoanza leo kwenye ukumbi
wa AICC, jijini Arusha. Kongamano hilo linashirikisha wajumbe 590 kutoka
ndani na nje ya nchi. Nchi za nje zinazoshiriki kongamano hilo ni 24,
ambapo kati ya nchi hizo nchi 12 ni za bara la Afrika.
Kongamano hilo la siku tatu
limeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuwakutanisha
wafugaji nyuki, wafanyabiashara, wataalamu na wawakilishi wa taasisi za
ndani na nje ya nchi ili kujadili njia za kuboresha ufugaji nyuki na
kukabiliana na changamoto za ufugaji nyuki hapa nchini na barani Afrika
kwa ujumla.
Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa
Halmashauri na watu wenye maamuzi wasiwasumbue kwa kuwalazimisha
wabadili maisha yao na kutoka kwenye mfumo wa ikolojia (ecosystem) ambao
wameuzoea. “Tusiwabugudhi, tusiwatoe kwenye mfumo wao wa ikolojia.
Tuwasaidie kuwapa teknolojia mpya ili waweze kufuga kisasa na kupata
faida huku wakiishi kwenye mazingira hayohayo waliyoyazoea mpaka hapo
watakapozoea na kuamua kubadilika kwa kubaini kuwa njia zao za zamani
haziwasaidii sana.”
Akizungumzia kuhusu ufugaji nyuki
barani Afrika, Waziri Mkuu alisema ufugaji nyuki umeegemea zaidi katika
rasilimali misitu na kilimo ambapo Afrika kwa asilimia kubwa shughuli
ya ufugaji nyuki hufanyika katika misitu.
“Bara la Afrika lina ukubwa wa
eneo la kilometa za mraba milioni 30.2 na asilimia 20 ya eneo hilo ni
misitu. Asilimia 40 ni misitu ya Savanna ambayo ni muhimu kwa ajili ya
ufugaji nyuki. Mapori haya pamoja na maeneo ya kilimo yana uwezo mkubwa
wa kuzalisha mazao ya nyuki kwa wingi,” alisema Waziri Mkuu.
Akizungumzia kuhusu ufugaji nyuki
nchini Tanzania, Waziri Mkuu alisema takwimu za Shirika la Chakula la
Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani
Afrika inayozalisha asali kwa wingi (tani 34,000 kwa mwaka), ya kwanza
ikiwa ni Ethiopia (tani 45,000 kwa mwaka).
“Inakadiriwa kuwa Tanzania ina
uwezo wa kuzalisha tani 140,000 za asali na tani 10,000 za nta kwa
mwaka. Lakini ni asilimia saba tu ya uwezo huo ndio huzalishwa. Hii ni
kwa sababu zao hilo limepuuzwa tangu siku nyingi na halijapewa msukumo
unaostahili.”
Alisema sekta ya ufugaji nyuki
ina mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu kwa kumpatia chakula,
ajira na kipato. “Wananchi hunufaika kutokana na mauzo ya asali, nta na
mazao mengine ya nyuki, utengenezaji wa vifaa vya ufugaji nyuki,
kusambaza malighafi za viwandani na huduma ya uchavushaji,” aliongeza.
“Wafugaji wa nyuki katika nchi zilizoendelea wanatumia teknolojia ya kuvuna sumu ya nyuki (bee venom), gundi ya nyuki (propolis), maziwa ya nyuki (royal jely)
na chavua (pollen) ambavyo hutumiwa kama virutubisho na dawa. Tafiti
zimethibitisha kuwa gundi ya nyuki hutibu maumivu ya meno, malaria na
homa ya mifupa(arthritis) na kuongeza kinga mwilini. Sumu ya
nyuki imekuwa ikitumiwa kuongeza nguvu za uzazi, kutibu uvimbe na homa
ya mifupa,” alisema huku akishangiliwa.
Waziri Mkuu aliitaka sekta
binafsi na taasisi za utafiti barani Afrika zifanye tafiti zaidi
katika eneo hili na kuwekeza katika teknolojia ambayo inaweza kuvuna na
kuchakata mazao hayo ambayo yana soko kubwa katika viwanda vya
kutengeneza madawa, virutubisho na vipodozi.
Mapema, akielezea kuhusu
kongamano hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu
alisema Juni mwaka jana, Wizara hiyo ilisaini makubaliano na Shirikisho
la Ufugaji Nyuki Duniani (Apimondia) ili waweze kuandaa kongamano la
ufugaji nyuki barani Afrika mwaka 2014.
Alisema kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni: “Kufuga nyuki kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira na kukuza uchumi” yaani “African Bees for a Green and Golden Economy” litahusisha
mada 88 ambazo kati yake, 45 zitawasilishwa na watafiti wa kisayansi,
26 zitakuwa za majadiliano (roundtable) na 17 zitawasilishwa katika
semina.
Alisema kongamano hilo ni kwanza
kwa sababu ni mara ya kwanza kwa kongamano kama kuandaliwa barani Afrika
kwa kushirikiana na Apimondia kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu species za nyuki zilizopo Afrika na mazingira ya ufugaji nyuko barani humu.
Injinia Dkt Binilith Mahenge awataka watanzania kutumia teknolojia ya kisasa kuzalisha mazao
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith
Satano Mahenge akifungua rasmi Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili
mabadiliko ya Tabia Nchi kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal,itakayofanyika kwa muda wa siku mbili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Ndg. Sazi Salula (katikati),
akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (kulia), pamoja na
Mkurugenzi Msaidizi – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt.Richard
Muyungi katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya
Tabia Nchi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu
ya Washiriki kutoka Nje na ndani ya Nchi wakisikiliza kwa makini hotuba
inayotolewa na mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).
Mgeni
Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt
Injinia Binilith Satano Mahenge (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Washiriki kutoka Ndani na Nje ya Nchi waliohudhuria katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia NchWaziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith
Satano Mahenge (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) ,kuhusu umuhimu wa Kongamano hilo lililoandaliwa na
Benki Kuu ya Dunia kwa ushirikianao na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Anayefuatia wa pili kulia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Ardhi,maliasili na Mazingira Mhe.
James Lembeli, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw.
Philippe Dongier (kulia) pamoja na Bw.Vel Gnanendran Mkuu wa Ofisi ya
DFID nchini Tanzania.
………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais –Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania
kutumia teknolojia mpya na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta
nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo
misitu. Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi
unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam.
Alifungua Kongamano hilo kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal.
Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya
zote Tanzania zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo zitaweza
kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira. Aidha alisema kuwa
zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika kuhakikisha utunzaji wa
mazingira unatekelezwa na pia kuzuia uharibifu wa mazingira kwa njia
moja au nyingine.
Akiongea katika Kongamano hilo
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema
Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa ajili ya majadiliano kuhusu program
za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza kustawi licha ya kuwepo kwa
mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania hawana budi kuwa
waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.
Mwisho Waziri Mahenge aliwashukuru
Wadau mbalimbali ambao wamehudhuria kongamano hilo kutoka ndani na nje
ya Nchi. Akiwasihi sana kuendelea kutunza mazingira na pia aliwaomba
watembelee vyanzo mbalimbali vya Utalii vilivyopo Nchini Tanzania ili
kukuza uchumi .
Kongamano hilo ni muendelezo ya
Mkutano wa New York kuhusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mwezi
Septemba mwaka huu na limehudhuriwa na washiriki kutoka Ndani na Nje ya
Nchi ya Tanzania.
PROFESA JOHN NKOMA AWAFUNDA MABLOGGER JINSI YA KUANDIKA KWA USAWA HABARI ZA UCHAGUZI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John
Nkoma akizungumza katika mkutano na Mablogger wakati alipofungua mkutano
huo uliojadili jinsi ya kuripoti kwa usawa habari za uchaguzi wa
serikali za mitaa, Ubunge na Rais kuanzia mwaka huu mpaka mwakani,
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
salaam ambapo pia viongozi wa Muda wa kuratibu uanzishwaji wa Chama cha
Mablogger wamechaguliwa ambao ni Joachim Mushi, Aron Msigwa mwakilishi
kutoka serikalini, Shamimu Mwasha Blog za Biashara, Francis Godwin
mablogger wa mikoani, Othman Maulid mwakilishi kutoka Zanzibar, Khadija
Khalili, William Malecela na Henry Mdimu ambao wataongoza kwa muda
wakati wa mchakato huo mkutano huo umesimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano
TCRA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE)Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene akifunga rasmi mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Kutoka
kushoto ni Josephat Lukaza wa Lukaza Blog, Shamimu Mwasha wa
8020Fashion na Geofrey Wapamoja Blog wakiwa katika mkutano huo
Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma katikati
Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Habbi Gunze ma Aron Msigwa Ofisa
Mwandamizi kutoka Idara ya Habari Maelezo wakiwa katika mkutano huo.
Andrew Kisaka Ofisa Mwanamizi wa Utangazaji TCRA akitoa mada katikamkutano huo.
TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF
TAIFA STARS YAWASILI JOHANNESBURG
Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa
Stars tayari kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa
maandalizi ya mechi dhidi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi hiyo itafanyika Jumapili
(Novemba 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini
Swaziland. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha
Mart Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho
Ngasa ambaye amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Wakati huo huo, kikosi cha
maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa
ya Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo
itachezwa Desemba 9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi cha maboresho cha Taifa
Stars kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa
kinakutana mara moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na
kucheza mechi moja ya kirafiki.
Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
WAAMUZI 23 KUSHIRIKI SEMINA DAR
Waamuzi 23 wa daraja la kwanza
wakiwemo wenye beji la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
wameteuliwa kushiriki semina itakayofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ambayo
pia itakuwa na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test)
wanatakiwa kuripoti Novemba 15 mwaka huu kwenye hosteli ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Wakufunzi wa semina hiyo wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Riziki Majala na Soud Abdi.
Waamuzi watakaoshiriki semina
hiyo ni Ahmed Juma Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles
Peter Simon (Dodoma), Dalila Jafari Mtwana (Zanzibar), Ferdinand Chacha
Baringenge (Mwanza), Florentina Zabron (Dodoma) na Frank John Komba
(Pwani).
Grace Wamara (Kagera), Hellen
Joseph Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni Nkongo (Dar es Salaam), Issa
Bilali Ali (Zanzibar), Issa Haji Vuai (Zanzibar), John Longido Kanyenye
(Mbeya), Jonesia Rukyaa Kabakama (Kagera) na Josephat Deu Bulali
(Tanga).
Kudra Omary (Tanga), Martin
Eliphas Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mfaume Ali Nassoro
(Zanzibar), Mgaza Ali Kinduli (Zanzibar), Samwel Hudson Mpenzu (Arusha),
Soud Iddi Lila (Dar es Salaam) na Waziri Sheha Waziri (Zanzibar).
Subscribe to:
Posts (Atom)