Habari kutoka shirikisho la soka nchini (TFF)leo

Habari kutoka shirikisho la soka nchini (TFF)leo

March 17, 2013
Habari zote na Boniface Wambura,Dar es Salaam.

WAANGOLA KUCHEZESHA MECHI YA STARS
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Angola kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas).

Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ivory Coast ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne na kufuatiwa na Taifa Stars yenye pointi tatu.

Mwamuzi wa mechi hiyo ni Helder Martins de Carvalho wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Inacio Manuel Candido huku Ricardo Daniel Cachicumi akiwa mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Antonio Muachihuissa Caxala.

Waamuzi hao watawasili nchini saa 1.20 usiku Machi 22 mwaka huu kwa ndege ya Kenya Airways wakitokea Luanda, Angola kupitia Nairobi, Kenya.

Kamishna wa mechi hiyo atakuwa David Fani kutoka Botswana anatarajiwa kuwasili Machi 22 mwaka huu saa 1.45 usiku kwa ndege ya South African Airways.

Naye mtathmini wa waamuzi (referee assessor) Neermal Boodhoo kutoka Afrika Kusini atawasili nchini Machi 22 mwaka huu 1.45 usiku kwa ndege ya South African Airways.

Mwisho.
 
MECHI YA RUVU SHOOTING, YANGA YAINGIZA MIL 62/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Yanga iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 62,228,000 kutokana na watazamaji 10,929.

Viingilio katika mechi hiyo namba 146 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,336,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,492,406.78.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,289,880.48, tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 4,373,928.29, Kamati ya Ligi sh. 4,373,928.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,186,964.14, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 850,486.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 850,486.06.

Mwisho.

TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI KUIWINDA MOROCCO

Taifa Stars imeanza kambi jana jioni (Machi 16 mwaka huu) ambapo wachezaji 14 kati ya 23 walioitwa wameripoti na kufanya mazoezi leo asubuhi chini ya Kocha Kim Poulsen.

Wachezaji walioripoti ni nahodha Juma Kaseja kutoka Simba na msaidizi wake Aggrey Morris wa Azam, Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Shomari Kapombe (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Wengine ni Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngasa (Simba) na Simon Msuva (Yanga).

Wachezaji Hussein Shariff, Issa Rashid na Shabani Nditi ambao timu yao ya Mtibwa Sugar jana ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) mjini Turiani wataripoti kambini leo jioni.

Kikosi hicho kitakamilika Jumanne asubuhi baada ya wachezaji walio katika kikosi cha Azam nchini Liberia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho kurejea nchini. Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo (DRC) wanatarajiwa kutua nchini kesho usiku.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

DC Mboni Mgaza akishiriki katika upandaji wa miti .

March 17, 2013
MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza akijiandaa kupanda miti wakati ufunguzi wa jengo jipya la Ofisi ya Kata ya Muhinduro wilayani humo wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Essau Ngatunga.Picha na Mwandishi Wetu.

DC Mboni Mgaza akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Muhinduro.

March 17, 2013

DC Gambo akitoa neno kwenye ufunguzi wa ligi yake

March 17, 2013
MKUU wa wialaya ya Korogwe,Mrisho Gambo akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Ligi ya Gambo Cup mwishoni mwa wiki wilayani humo,anayemfuatia ni Mjumbe wa NEC CCM wilayani ya Bagamoyo na mwenye miwani ni Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kaskazini,Vicky Bishumbo ambao ndio wadhamini wa ligi hiyo.

Vijana mcheze kwa kujituma na umakini mkubwa.

March 17, 2013
MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Ligi ya Gambo Cup mwishoni mwa wiki wilayani Korogwe.

DC Mboni Mgaza awakabidhi wananchi Trekta

March 17, 2013
Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza aliwasha trekta kabla ya kuwakabidhi wananchi wa Kijiji cha  Mhinduro  Majengo wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Kata hiyo juzi ambapo trekta hilo liligharimu sh.milioni 40,000,000.