RAIS DKT. MWINYI AFUNGUA SKULI YA SEKONDARY YA MWEMBELADU ZANZIBAR.

January 09, 2024

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi kulia akikunjuwa Kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni katika Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Muonekano wa Jengo la Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Husein Ali Mwinyi Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali MwinyI akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni katika Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi  akiwa na Mkewe Mama Mariamu Mwinyi wakimsikiliza Mwanafunzi Bibiye Abdul-rahman Amour wakati akitembelea Darasa la Compyuter Room na kusalimiana na Wanafunzi katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni  Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni  Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi pamojana Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Darasa la Nne kutoka Skuli ya Jendele Abdukarim mohamed Nahadha na Khamisuu Juma Mohamed baada ya kusoma Utenzi Mzuri katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni  Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi akitoa hotuba katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni  Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi katikati akiwa pamojana Viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa waliofanya sanaa ya ngoma na utenzi katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini .Ikiwa ni  Shamra shamra za Miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.

PICHANA YUSSUF SIMAI /MAELEZO ZANZIBAR.09/01/2024.J

MUME AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE KISHA KUMKATA VIPANDE NA KWENDA KUMTUPA MTONI

January 09, 2024


Njombe

Tumaini Luvanda (35) mkazi wa Dombwela wilaya ya Makete mkoani Njombe ameuawa kwa kukatwa na panga vipande na kisha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, na baadhi ya viungo kutupwa katika mto ulio jirani na nyumbani katika eneo la Kabinda wilayani humo ambapo tayari Polisi inamshikilia Juma Kyando (36) ambaye ni mume wa Tumaini (Marehemu) kwa kuhusika na mauaji hayo.

Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Iwawa ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Dombwela Joseph Mbilinyi amesema tukio limetokea usiku wa kuamkia January 8,2024 ambapo alifika nyumbani kwa mtuhumiwa mara baada ya kupigiwa simu na majirani na kumkuta Kyando akiwa na Panga jambo lililomfanya apige simu Polisi ili kuomba msaada.

"Baada ya Polisi kuja yeye alikuwa ameshamuua mkewe tayari na kumuweka kwenye mfuko wa kisarufeti na kwenda kutupa kwenye mto,cha kwanza kwenye uwanja wake tuliuona Moyo wa mwanadamu ndio tukaanza kufuata kwenye mto kwasababu alikuwa anavuta sarufeti lakini kufika kwenye mto tukaona kisarufeti kinaelea kwenye maji tukakiopoa na kuendelea kufuata tena mto tukakiona kiungo kingine ambacho ni ubavu upande wa titi na shingo nacho tukakipoa tukaanza kutafuta kichwa ambacho kimetusumbua kwa muda mrefu"amesema Mwenyekiti

Mkuu wa Polisi wilaya ya Makete mrakibu mwandamizi wa Polisi Assel Mwampamba amesema tukio hilo si la kawaida na kutoa ushauri kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na namba za jeshi la Polisi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza "Hili lingezuilika sasa ametoka na Panga mkakimbia wote na wanaume acheni uwoga yaani mtu yuko mmoja anacharanga mtu ninyi mmekimbia mngekuwa mnamrushia mawe asingeendelea kukata mtu pale"

Kwa upande Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe Mrakibu wa Polisi Joseph Mwalongo akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe mara baada ya kufika eneo la tukio amesema kuwa ni lazima mtuhumiwa aweze kuchukuliwa sheria "Niwape pole kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe,mwenzetu bwana Juma amejichukulia sheria mkononi jeshi la Polisi lazima tumchukulie hatua stahiki na tumpeleke Mahakamani haraka iwezekanavyo"

Medrick Kyando ni ndugu wa Mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe pamoja na baadhi ya majirani wamesema Kyando ni fundi wa kujenga alikuwa hana makundi pia hana historia ya kuwa na matatizo ya akili na alikuwa anaishi vizuri na mke wake lakini wanashangaa kuona ametekeleza tukio hilo la kikatili lililowashtua ambapo kwa sasa anaacha watoto wadogo watatu akienda Polisi na mkewe akiwa amefariki.


Chanzo:michuziblog

RAIS DKT SAMIA AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA SHIRIKA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR (ZSTC)PEMBA

January 09, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Soud Said Ally kuhusu Kituo cha kupimia Karafuu kilichopo katika jengo hilo la Kitega Uchumi la ZSTC Pemba tarehe 09 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Chakechake Pemba mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) tarehe 09 Januari, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Chakechake Pemba mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) tarehe 09 Januari, 2024

Wananchi wa Chakechake wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.

 


JESHI LA PALESTINA NA HAMAS LINATUMIA SILAHA ZA KOREA KASKAZINI-SHIRIKA LA KIJASUSI

JESHI LA PALESTINA NA HAMAS LINATUMIA SILAHA ZA KOREA KASKAZINI-SHIRIKA LA KIJASUSI

January 09, 2024

 

BOMBO LA MAFUTA EACOP LATOA MIFUKO 1,000 YA SARUJI KWA WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO HANANG

January 09, 2024

 Na Mwandishi Wetu


Kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoikumba Wilaya ya Hanang, Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) imetao saruji mifuko 1,000 ya saruji ikiwa ni kama msaada kwa jamii zilizoathirika.

Saruji hiyo itatumika kasaidia ujenzi wa nyumba zaidi ya 101 ambazo Serikali imepanga kuwajengea waathirika wa maafa hayo ya aina yake

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bi Queen Sendiga alisema "Maafa ya hivi karibuni yaliyotokea katika Wilaya ya Hanang yameziacha jamii zetu katika uhitaji mkubwa, msaada wa ukarimu wa kibinadamu kutoka kampuni ya EACOP umekuja kama mwanga wa matumaini katika nyakati hizi za changamoto.

Tunashukuru kwa mwitikio na msaada wao katika kusaidia juhudi zetu za kujenga upya na kurejesha maisha ya kawaida ya jamii kutokana na janga hili”

Maporomoko makubwa ya ardhi hususani miteremko mikali ya Mlima Hanang yameathiri maeneo ya miji ya Katesh na Gendabi. EACOP inatambua wajibu wa kushikamana na jamii zilizoathiriwa na janga hili, hasa kwa kuzingatia kuwa Wilaya ya Hanang ni mojawapo ya maeneo ambayo bomba letu linapita.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa EACOP Tawi la Tanzania, Bi. Catherine Mbatia alisema kuwa "Mchango wetu wa msaada wa kibinadamu ni ushuhuda tosha wa dhamira yetu katika kusaidia wenye uhitaji na unasisitiza dhamira yetu ya uwajibikaji wa kampuni katika jamii"

Maafa hayo yamegharimu maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa katika mashamba, na kupelekea maelfu ya watu kupoteza na kuhama makazi yao. Katika kukabiliana na maafa haya, EACOP imechangia mifuko 1,000 ya saruji ili kutoa msaada muhimu kwa wahanga wa mafuriko katika Wilaya ya Hanang.

Mmoja wa wanufaika wa msaada wa kibinadamu alisema kuwa "Napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa msaada wa EACOP. Msaada uliopokelewa utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zinazotukabili, na kutoa faraja na ahueni kwa familia zilizoathirika. Ushirikiano huu kati ya EACOP na jamii ni mfano bora unao onesha umoja katika nyakati za shida ”

EACOP inaamini katika nguvu na kuchukua hatua kwa pamoja, na hivyo imedhamiria kutumia rasilimali zake ili kuchangia ipasavyo katika kurejesha maisha ya kawaida na kujenga upya jitihada za wilaya.

Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya EACOP ya uwajibikaji wa shirika katika majukumu na msaada wa kijamii, kwa kutilia mkazo dhamira yetu katika ustawi wa maeneo tunapofanyia kazi. Kampuni inathamini umuhimu wa kuwa shirika la kiraia linalowajibika na linalothibitisha muunganiko wa shughuli zetu na jamii tunazozihudumia.EACOP itafanya kazi kwa karibu na serikali za mitaa na viongozi wa kijamii katika kutoa msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga (kushoto) akipokea sehemu ya mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bomba la mafuta Ghafi la Africa Mashariki (EACOP) Catherine Mbatia (kulia) ikiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya  ardhi. Makabidhiano hayo yalifanyika Wilayani Katesh jana
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga (Wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bomba la mafuta Ghafi la Africa Mashariki (EACOP) Catherine Mbatia (kulia) ikiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya  ardhi. Makabidhiano hayo yallifanyika Wilayani Katesh jana. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Hanang na EACOP.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Bomba la mafuta Ghafi la Africa Mashariki (EACOP) baada ya kupokea msaada wa mifuko 1,000 ya saruji iliyotolewa na bomba hili ikiwa ni msaada wa ajili ya waathirika wa maporomoko ya  ardhi. Makabidhiano hayo yaliyofanyika Wilayani Katesh jana

MKUU WA MKOA WA TANGA AWAONYA MAFATAKI

January 09, 2024











Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kinamba akiwa amekaa kwenye dawati na wanafunzi wa shule ya msingi Bombo mara baada ya kutembelea shuleni hapo leo january 8,2024.




Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akiwa amekaa na wanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Bombo iliyopo jijini hapa mara baada ya kutembelea shuleni hapo kukagua kuwasili kwa wanafunzi hao kwa mwaka mpya wa masomo 2024.








Na Mwandishi Wetu,TANGA

SERIKALI mkoani Tanga imetoa onyo kali kwa wanaume ambao wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kuacha tabia hiyo huku ikiwaagiza wakuu wa wilaya  za mkoa huo kusimamia na kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote ambaye atabainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa Januari 8 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati wa ziara yake ya kuzitembelea shule za Msingi Bombo na Sekondari Old Tanga kukagua hali ya kuripoti kwa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2024 ambapo pia amatoa onyo kwa wazazi na walezi ambao wamekuwa wakimaliza kesi kifamiliya na wahusika mara baada ya watoto wao kupata ujawazito.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba vipi vitendo  kwa baadhi ya wananchi wasiokuwa na tabia nzuri wanaoitwa "Mafataki"ambao wamekuwa wakitembea na  wanafunzi hii sio sawa na haikubaliki.

"Niwaambie kwamba wakati wangu mimi kama mkuu wa mkoa wa Tanga sitavumilia , sitastahamili walasitakuwa na simile na mtu yeyote anayeharibu maisha ya mwanafunzi , ukitaka kufanya hivyo chukua umri wako jumlisha na miaka 30 ya gerezani uone utatoka ukiwa na umri gani" Alisisitiza RC Kindamba

Katika kusisitiza jambo hilo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka  wakuu wa wilaya za mkoa huo kusimamia watoto hao na watakaobainika kujihusisha na vitendo vya mapenzi na watoto wa shule wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

"Nimeanza  kupata kesi kutoka kwa baadhi ya wazazi kesi zikishaenda mahakamani baadaye wanawaficha watoto au wanakaa kikao kifamilia mtu yeyote atakayecheza na watoto wa shule ajue anacheza na watoto wa serikali" Alisema 

Hata hivyo aliwataka  wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule baadala ya kubaki nao nyumbani huku akisisitiza michango yote itakayokuwa wakichangishwa wazazi na walezi kwaajili ya wanafunzi lazima iwe imepata kibali kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa.


"Mhe Rais Dkt Samia Suluhu ameshatoa fedha kwaajili ya watoto wote wawe wanasoma bila ya ada kwahiyo kusiwe na kisingizio cha wazazi kutoleta wanafunzi kwenye mashule sitaki kusikia michango ambayo haina kichwa wala miguu michango yote inayochangwa kwenye mashule ni lazima iwe na kibali kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa"Alisema 

Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa alizipongeza shule za Msingi Bombo na sekondari Old Tanga kwa kuvuka lengo la kusajili wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2024 ambapo shule ya msingi Bombo ilitarajia kusajili wanafunzi 70 na imefika 71 huku Old Tanga ambayo ilitarajia kusajili wanafunzi 114 ambapo amesema wataendelea kutembelea na kukagua kuona wanafunzi ambao wamesharipoti .


Akitoa taarifa kuhusu wanafunzi ambao wamesharipoti mkuu wa shule ya Old Tanga Juma Mgunya amesema kuwa shule hiyo awali ilipangiwa kupokea wanafunzi 114 lakini ikaongezewa wengine 86 wa uhamisho hivyo kufikisha jumala ya wanafunzi 200 ambao wote watapata viti pamoja na madawati pindi wawapo darasani.


"Shule ya Old Tanga ilipangiwa kupokea wanafunzi 114 lakini nmeongezewa wanafunzi wengine wa uhamisho na sasa jumla tuna wanafunzi 200 na mpaka sasa ambao wameshafika ni wanafunzi 109 kati ya wanafunzi 200 ambao nimepangiwa , wanafunzi wote walipangiwa shule ya Old Tanga watakuwa na viti pamoja na meza ambazo zitatosha kutokana na wanafunzi wa kidato cha nne ambao walimaliza mwaka jana" alisema Mwalimu Mgunya.


Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Bombo Denis Mushi amesema kuwa shule hiyo ilitarajia kusajili wanafuzi 70 ambao wamefanikiwa na kufika 71 kwa upande wa darasa la awali huku darasa la kwanza wakitarajia wanafunzi 120 mpaka sasa wamesajili wanafuzi 121 na hivyo kufikisha wanafuzi 1002 kwa shule nzima kwa mwaka huu wa masomo.


"Shule ya Msingi Bombo iliweka maoteo ya kusajili wanafunzi 70 kwa darasa la awali na mpaka hivi sasa tumesajili wanafunzi 71 na kwa darasa la kwanza tuliweka malengo ya kusajili wanafunzi 120 na mpaka leo tumeshasajoli wanafunzi 121 na hivyo kufikia asilimia 100 ya malengo kwa darasa laawali na la kwanza hivyo baafa ya usajili huu shule itakuwa na jumla ya wanafunzi 1002 wavulana 492 na wasichana 510" alisema Mwalimu Denis


Alisema shule ya msingi Bombo ilipokea kiasi cha shilingi Milion 81, 300, 000 kwaajili ya kutekeleza mradi wa BOOST kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo ambapo ujenzi huo umekamilika na tayari madarasa yanatumika na hivyo kuondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi katik vyumba vya madarasa.


"Tulipata mradi wa BOOST ambao ulitekelezwa hapa shuleni kwa mwaka 2023 ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na matundu ya matatu ya vyoo ujenzi huu ulighalimu kiasi cha fedha Milion 81, 300, 000 kutoka serikali kuu na ujenzi huu umekamilika kwa aailimia 100 tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali ya mkoa wa Tanga kwani mradi wa BOOST uliotekelezwa umepunguza msongamano mkubwa wa wanagunzi katika vyumba vya madarasa" aliongeza


Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akifundisha baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Bombo alipotembelea shuleni hapo kukagua wanafunzi walisajiliwa tayari kwa kuanza masomo kwa mwaka 2024.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI YATEMBELEA KAZI YA UBORESHAJI MFUMO WA SEKTA YA ARDHI

January 09, 2024


Na Munir Shemweta, WNMM ARUSHA

Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii imetembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.

Mfumo huo unatarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga na utarahisisha na kuharakisha upatikanaji huduma za sekta ya ardhi kwa kuwa wananchi watakuwa wakipata huduma kwa njia ya mtandao.

Akizungumza wakati wa kuikaribisha Kamati hiyo jijini Arusha tarehe 8 Januari 2023 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema, mfumo unaoboreshwa na timu ya wataalamu mkoani Arusha asilimia mia moja utakuwa ni wa kidigitali.

‘’Baada ya kazi ya maboresho ya mfumo kukamilika, hatua zozote za ardhi zitakuwa zikifanyika kwenye mfumo na suala la mwananchi kwenda ofisi za ardhi kupata huduma ni uamuzi wake mwenyewe’’. Alisema Mhe. Silaa

Mkurugenzi wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Flateny Hassan ameeleza kuwa, boreshaji wa Mfumo unafuatia Wizara ya Ardhi kuwa na changamnoto kadhaa kwenye mifumo yake jambo alilolieleza kwamba limesababisha kuwepo uhitaji wa kuunganisha mifumo yote ili kuwa na mfumo mmoja utakaohusika na sekta ya ardhi.

‘’Kazi inayofanywa na timu ya wataalmu jijini Arusha kwa sasa imefikia asilimia 85 na matarajio ni kwamba ikifika Juni 2024 mikoa ya awali iliyopangwa itakuwa imefikiwa’’. Alisema Flateny

Maboresho yanayofanyika ni pamoja na mfumo unaoruhusu watumishi wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi zao, mfumo unaoruhusu wananchi kuomba huduma kwa njia ya mtanadao na huduma ya Mobile App ambao mwananchi anaweza kupata huduma kupitia njia ya mkononi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa katika jitihada kubwa za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinapatikna kwa haraka na urahisi kupitia mifumo ya kidigitali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda alipowasili na timu yake kukagua kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha. Katikati ni Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.


Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda jijini Arusha kukagua kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi tarehe 8 Januari 2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava akizungumza wakati Kamati yake ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.

Baadhi ya wataalamu wanaofanya kazi ya kufanya Maboresho Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa na Naibu wake Mhe. Geophrey Pinda wakifuatilia uwasilishwaji taarifa ya kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

MHE . KAPINGA: TGDC ONESHENI MATOKEO CHANYA KWA KUZALISHA UMEME

MHE . KAPINGA: TGDC ONESHENI MATOKEO CHANYA KWA KUZALISHA UMEME

January 09, 2024




Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kampuni hiyo, Tarehe 08 Januari, 2024 Jijini Dar es salaam

Dar Es Salaam

Kampuni ya Uendelezaji wa Joto Ardhi Tanzania (TGDC) imetakiwa kuonesha Matokeo Chanya kwa kuzalisha Umeme kwa kutumia Rasilimali ya Jotoardhi ili kuunga Mkono Mpango wa Serikali wa kuwa na Nishati Safi na Endelevu.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo pamoja na Menejimenti ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukutana na baadhi ya Taasisi na Kampuni zilizo chini ya Wizara ya Nishati kwa lengo la kuona Utendaji kazi wa Taasisi hizo Tarehe 8 Januari 2024, Jijini Dar Es Salaam.
- Advertisement -


Mhe. Kapinga ameieleza TGDC kuwa wabunifu na kutumia uwezo wao wote kuhakikisha kuwa Kampuni hiyo inaanza kuzalisha umeme kwa kutumia Rasilimali ya Jotordhi kwa kuwa tayari baadhi ya maandalizi yameshafanyika katika maeneo ya vipaumbele.

Amesema kama ambavyo Serikali imejipambanua kuwa inatekeleza Mpango wa Nishati Safi na Endelevu, ni wakati wa TGDC sasa kuonesha uwezo wao katika kufanikisha hilo ili kutoa mchango mkubwa kwa Taifa.

Vilevile amewasisitiza kuwa ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya na ya haraka zaidi ni vyema wakaongeza ubunifu, uthubutu, kushirikiana na kutoridhika na kila wanachofanya ili kupiga hatua mbele zaidi. Hali hiyo itaondoa changamoto ya umeme unayoikumba nchi kwa kuzingatia kuwa nishati ya Jotoardhi ni endelevu.

“Nchi na Watanzania wanataka kuona umeme unaozalishwa kutokana na Jotoardhi,TGDC ni wakati wenu sasa kuonyesha uwezo wenu wa kuleta matokeo Chanya kwa Taifa, tumieni Ubunifu na Uwezo wenu wote kuhakikisha kile mlichokikusudia kinafanikiwa na kuonekana kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyoelekeza kuwa uzalishaji wa umeme utaongezeka kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo Jotoardhi, vilevile kuunga mkono Mpango wa serikali wa kuwa Nishati Safi na Endelevu”, alisema Mhe. Kapinga.

Aidha amewapongeza TGDC kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha umeme unapatikana na pia amewataka kutumia vyema Weledi na Taaluma walio nayo kulinda Kampuni hiyo ili kupata matokeo ya haraka.

“TGDC lazima muonyeshe mchango wenu Nishati Safi na Endelevu ili Nchi na Dunia ione uwepo wenu na Serikali inataka matokeo hivyo mjikite katika hilo na watanzania wanaamini katika matokeo” alisisitiza Mhe. Kapinga.

Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbuttuka, amewaeleza TGDC kuwa ofisi yake iko wazi wakati wote ili kupokea changamoto zozote zinazowakabili ili kuwasaidia na kuzitatua pale watakapoona wanakwama katika kutekeleza majukumu yako.

Sambamba na hilo amewataka kushirikiana, kuwa wabunifu na wenye uthubutu kuhakikisha kile walichokikusudia kinafanikiwa na watanzania wanapata umeme.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGDC Prof. Shubi Kaijage na Meneja Mkuu wa TGDC, Mha. Mathew Mwangomba wamemuakikishia Naibu Waziri Kapinga kuwa watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanazalisha umeme wa Jotoardhi haraka iwezekanavyo na wanaendelea kutoa elimu ya Rasilimli ya Jotoardhi kwa wadau mbalimbali ili wawe na uelewa mpana zaidi kuhusu mradi huo wa kimkakati.

Wamesema kuwa kampuni hiyo ina miradi mitano ya kipaumbele ambayo ni ule wa Ziwa Ngozi unaotajiwa kuzalisha Megawati 70 lakini kwa kuanzia wataanza na Megawati 30. Mradi Mingine ni wa Kiejo- Mbaka mkoani Mbeya Megawati 60, Songwe mkoani Songwe Megawati 5 hadi 38, Luhoi mkoani Pwani Megawati 5 na Natroni mkoani Arusha Megawati 60.

Miradi yote hiyo iko katika hatua mbalimbali ambapo nguvu kubwa imeelekezwa katika Mradi wa Ngozi ambapo tayari mtambo wa kuchoronga visima vya Jotoardhi umepelekwa huko na hivi karibuni wataanza kazi ya uchorongaji.



Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kampuni hiyo, Tarehe 08 Januari, 2024 Jijini Dar es salaam.



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athuman Mbuttuka akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) Wakati ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (Hayupo pichani) alipotembelea Kampuni hiyo, Tarehe 08 Januari, 2024 Jijini Dar es salaam.



Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mha. Mathew Mwangomba akieleza maendeleo ya kazi zinazofanywa na Kampuni hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (Hayupo Pichani) iliyofanyika Tarehe 08 Januari, 2024 Jijini Dar es salaam.




Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Prof. Shubi Kaijage akizungumza na wajumbe wa Bodi na menejimenti ya Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania(TGDC) wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Judith Kapinga Iliyofanyika Tarehe 08 Januari, 2024 katika Ofisi za kampuni hiyo Jijini Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC)wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika Tarehe 08 Januari, 2024 , Jijini Dar es salaam