Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same
Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David wakishiriki katika
ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari ya Njoro
wilayani Same, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
inayotekelezwa na serikali, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-SAME)
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mh. David Mathayo David akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya sekondari ya Njoro wilayani Same.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kama chifu wa wapare mara baada ya kupokelewa na wananchi katika kijiji cha Njoro jimbo la Same magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakati alipowasalimia katika kijiji cha Makanya Same.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mh. David Mathayo David akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Gonjamza Suji wilayani Same.Wana
Wananchi
wakinyanyua mikono yao juu huku wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipowasili katika kijiji cha
Suji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same
Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David wakishiriki katika kazi ya kufukia mabomba ya mradi wa maji katika kijiji cha Gonjaga Suji wilayani Same.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa mradi wa maji katika kijiji cha Suji anaoshirikiana nao kutoka kulia
ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Mbunge wa jimbo la
Same Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same
Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David wakishiriki
wakifungua maji ya bomba mara baada ya Kinana kuzindua mradi huo katika
kijiji cha Suji wilayani Same.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi katika
kijiji cha Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika ziara
ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi jimboni humo
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same
Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David katikati na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakijadiliana jambo huku mvua
ikinyesha kwenye stendi ya mabasi ya Same , Mvua hiyo ilisababisha
kuahirishwa kwa mkutano huo na kupangwa kufanywa baada ya wiki nne.
Wana
CCM wakiimba nyinbo za kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana hayupo pichani pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kabla ya
kuahirishwa kwa mkutano huo mjini Same.