AFRICAN SPORTS YASHINDWA KUIGARAGAZA LIPULI,YALAZIMISHWA SARE YA BAO 1-1,MKWAKWANI JIONI HII,KURUGENZI FC YASHINDWA KUIFUNGA POLISI DAR

October 15, 2014
KIKOSI CHA LIPULI FC YA IRINGA KILICHOCHEZA NA AFRICAN SPORTS LEO LIGI DARAJA LA KWANZA

KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS KILICHOLAZIMISHWA SARE NA LIPULI FC YA IRINGA LEO MKWAWANI.
HAPA WACHEZAJI WAKISALIMIANA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO





NA MWANDISHI WETU,TANGA.

TIMU za soka African Sports na Lipuli FC ya Iringa leo zimeshindwa kutambiana baada ya kulazimishana sare ya kufungana bao 1-1 ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi daraja la kwanza ngazi ya Taifa mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.

katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ya ushindani mkubwa kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu ,African Sports ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lake dakika ya 44 Ally Ramadhani kwa njia ya Penati iliyotokana na shambuliaji wao Hassani Materema kuangushwa eneno la Hatari.

Baada ya tukio hilo mwamuzi wa mechi hiyo Klina Kabala kutoka Dar es Salaam kuamuru ipigwe peneti iliyopigwa kuifundi na mshambuliaji huyo na kuzama wavuni.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu.

Wakionekana kujipanga na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye kipindi cha kwanza,Lipuli FC waliweza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa African Sports na kufanikiwa kuandika bao la kusawadhisha kwenye dakika ya 54 kupitia Abdallh Mussa.

Katika mechi nyengine iliyochezwe kwenye dimba la soka Mafinga timu za Kurugenzi FC  na Polisi Dar zimegawana pointi moja moja baada ya kulazimishana sare ya kutokufungana.

UCHAGUZI MDOGO TPLB NOVEMBA 15 # SDL WAONGEZEWA MUDA WA USAJILI # MAREKEBISHO YA RATIBA FDL KUNDI A

October 15, 2014

Mkutano Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo moja ya ajenda ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi moja ya uongozi kwenye bodi hiyo.

Nafasi hiyo ya ujumbe kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB iliyokuwa ikishikiliwa na Kazimoto Muzo imebaki wazi baada ya klabu yake ya Pamba ya Mwanza kushuka daraja kutoka la Kwanza hadi la Pili.

Hivyo, wagombea wa nafasi hiyo ni kutoka kwenye klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Klabu hizo zina nafasi mbili kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB ambapo nyingine inashikiliwa na Omari Mwindadi wa klabu ya Mwadui ya Shinyanga. 
SDL WAONGEZEWA MUDA WA USAJILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili wa wachezaji kwa timu za Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa siku saba ambapo sasa utamalizika Oktoba 21 mwaka huu.

Awali usajili huo unaofanyika kwa njia ya mtandao (online) ulikuwa umalizike jana (Oktoba 14 mwaka huu), lakini ni klabu chache ndizo zilizoweza kusajili ndani ya muda uliopangwa.

Klabu ambazo hazijakamilisha shughuli hiyo ya usajili, zinatakuwa kukamilisha ndani ya siku hizo saba kwani TFF haitaongeza tena muda wa usajili. Vilevile klabu za SDL zinakumbushwa kuwasilisha majina ya viwanja vya nyumbani ambavyo timu zao zitatumia kwenye ligi hiyo.

TFF ilifanya mafunzo ya usajili kwa maofisa usajili wa klabu hizo Oktoba 6 na 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Timu za SDL zimegawanywa katika makundi manne ya timu sita zitakazocheza ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Kundi A lina timu za Mpanda United ya Katavi, Ujenzi (Rukwa), Mvuvumwa FC (Kigoma), Mji Mkuu FC (Dodoma), Milambo (Tabora) na Singida United (Singida).

Kundi B ni Mbao FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Eleven Stars (Kagera), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba (Mwanza) na AFC (Arusha). Kundi C ni Navy, Mshikamano, Transit Camp na Abajalo za Dar es Salaam, Kiluvya United (Pwani) na Kariakoo (Lindi(.

Timu zinazounda kundi D ni Magereza (Iringa), Town Small Boys (Ruvuma), Njombe Mji (Njombe), Volcano FC (Morogoro), Wenda FC (Mbeya) na Mkamba Rangers (Morogoro).

MAREKEBISHO YA RATIBA FDL KUNDI A
Mechi nne za Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho ili kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Timu za African Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Nayo mechi ya Polisi Dar es Salaam na Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, sasa itachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Mechi ya Friends Rangers na Ashanti United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani Pwani, Oktoba 26 mwaka huu, sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28 mwaka huu.

Pia mechi ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MAKUBURI-DAR

October 15, 2014

 
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Stella Kivugo (kulia), akijaribu kufungua bomba la maji, baada ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Makaburi, Bw. James Ngoitanie (wa nne kushoto), kukata utepe kuzindua kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni watendaji wa Mtaa wa mwongozo. (Na Mpigapicha Wetu)
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Dar es Salaam, Bw. James Ngoitanile (wa nne kushoto), akifurahia kwa kuonesha mkasi juu baada ya kukata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji safi, kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni. Kulia ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Stella Kivugo na Meneja Mauzo wa TBL Kinondoni, Bw. Joseph Nicholaus (wa pili kulia).
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Dar es Salaam, Bw. James Ngoitanile (wa nne kushoto), akifurahia kwa kuonesha mkasi juu baada ya kukata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji safi, kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Stella Kivugo na Meneja Mauzo wa TBL Kinondoni, Bw. Joseph Nicholaus (wa pili kulia).
 
Mwenyekiti wa Mtaa wa Makaburi, Bw. James Ngoitanie (wa nne kushoto), akifungua koki ya maji baada ya kukata utepe kuzindua kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Stella Kivugo, Meneja Mauzo wa TBL Kinondoni, Bw. Joseph Nicholaus (wa tatu kulia)  na watendaji wa Mtaa wa mwongozo. (Na Mpigapicha Wetu)
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Bw. James Ngoitanile, akimtwisha ndoo ya maji Mjumbe wa Shina, Bi. Zubeda Samata, baada ya kuzindua bomba la maji safi lilijengwa kwa Hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Saaam.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Bw. James Ngoitanile, akimtwisha ndoo ya maji Mjumbe wa Shina, Bi. Zubeda Samata, baada ya kuzindua bomba la maji safi lilijengwa kwa Hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Saaam.