April 04, 2014
MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI KUSHOTO AKIKABIDHI KOMBE LA UBINGWA WA LIGI YA MKOA KWA NAHODHA WA TIMU YA AFRICAN SPORTS JAMES MENDRY LEO ANAYESHUHUDIA KATIKATI NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI TFF ,KHALID ABDALLAH.      



KATIBU WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TANGA,BEATRICE MGAYA WA KWANZA KUSHOTO WALIOKAA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI TFF,KHALID ALIYEVAA KANZU NA KOFIA NA KOCHA MKUU WA TIMU YA MGAMBO SHOOTING,BAKARI SHIME WAKIZUNGUMZA NA SHABIKI WA SOKA MKOA WA TANGA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO

SHANGWE BAADA YA KUKABIDHIWA KOMBE HILO LEO.

MWENYEKTI WA KLABU YA COASTAL UNION,HEMED AURORA ALIYEVAA KANZU AKIFUATILIA KWA UMAKINI MCHEZO MAALUMU KATI YA COASTAL UNION U-20 DHIDI YA AFRICAN SPORTS AMBAPO AFRICAN SPORTS ILIIBUKA NA USHINDI WA MABAO 2-1.

WA KWANZA KUSHOTO NI KOCHA MKUU WA COASTAL UNION YUSUPH CHIPPO ,BENNY MWALALA MCHEZAJI WA ZAMANI WA COASTAL UNION NA YANGA WAKIFUATILIA KWA UMAKINI MCHEZO HUO WA LEO

TIMU YA AFRICAN SPORTS WAKIWA NA KIKOMBE CHA UBINGWA WA MKOA WA TANGA WALICHOKABIDHIWA LEO.

April 04, 2014

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YATETA NA WANAHABARI DAR

 Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa kuanza utafiti katika mapitio ya mfumo wa sheria unaosimamia haki za walaji ikiwa ni hatua mojawapo katika mchakato wa kuundaa  sheria inayowalinda watumiaji wa huduma mbalimbali hapa nchini. Kulia ni Afisa Sheria wa Tume hiyo ni Fred Kandonga.
Afisa Sheria wa wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Fred Kandonga akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu sababu zilizopelekea Serikali kuamua kufanya utafiti utakaopelekea kutungwa kwa sheria itakayosaidia kuwepo kwa mfumo nwa biashara wenye uwiano katika ushindani. Katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi, anayemfuatia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi na Mwisho kushoto ni Afisa habari wa Tume hiyo Munir Shemweta.
************************************
April 04, 2014

RIDHIWANI KIKWETE AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI,KUZUNGUMZIA MWENENDO WA KAMPENI ZAKE

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao wakati akizungumzia mwenendo mzima wa Kampeni zake,leo April 4,2014,Nyumbani kwake Msoga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
April 04, 2014

JAJI AUGUSTINEO RAMADHANI AWATAKA WAJUMBE KUJADILI RASIMU KWA MAKINI

Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani akiongea jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina, pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba.
Kamishana wa zamani wa Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar – ZEC, Dkt. Nassor Seif Amour akitoa ufafanuzi  jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).  Pembeni ni Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya, wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
April 04, 2014
Release No. 054
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 4, 2014

SIMBA KUIVAA KAGERA SUGAR VPL
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 24 kesho (Aprili 5 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo Kagera Sugar itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa kati ya Mbeya City ambayo itakuwa mgeni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam. Ashanti United inayofundishwa na Abdallah Kibaden ipo katika mkakati wa kukwepa kushuka daraja.

Keshokutwa (Aprili 6 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Coastal na Mgambo Shooting Stars (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT na Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers na Mtibwa Sugar (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Yanga dhidi ya JKT Ruvu (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam).

Raundi hiyo itakamilika Aprili 9 mwaka huu kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
April 04, 2014

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema waliokuwa wajumbe wa tume hiyo hawajawahi kudai malipo ya pensheni ya Sh200 milioni kama inavyodaiwa. 
 
April 04, 2014
Mjane wa Abasi Mwila, Judith Mwila akipanga bidhaa katika genge lake lililopo Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam jana. Judith ni miongoni mwa watu tisa watakaonufaika na fidia ya Sh672 bilioni baada ya kumpoteza mume wake, Abasi katika shambulio la kigaidi la mwaka 1998 kwenye ubalozi wa Marekani nchini. Picha na Michael Jamson 
April 04, 2014

VPL: ASHANTI VS MBEYA CITY, YANGA VS JKT RUVU NI MITANANGE MIZITO ZAIDI WIKIENDI HII, MECHI YA SIMBA, KAGERA HAINA `PRESHA`!!

 Na Baraka Mpenja .
LIGI kuu soka Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho na keshokutwa, huku mechi kubwa yenye uzito wa hali ya juu ni kati ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu na ile ya Ashanti United na Mbeya City.
Kesho jumamosi zitapigwa mechi mbili ambapo wauza mitumba wa Ilala watawakaribisha Mbeya City katika dimba la Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mechi hii itakuwa na mvuto wake kutokana na mazingira ya timu zote mbili katika msimamo wa ligi hiyo.
Mbeya City wapo nafasi ya tatu wakiwa wameshuka dimbani mara 23 na kujikusanyia pointi 45, pointi moja nyuma ya mabingwa watetezi Yanga waliopo nafasi ya pili kwa pointi 46 baada ya kucheza mechi 22.