KAMISHNA GENERALI WA DAWA ZA KULEVYA AIPONGEZA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

January 29, 2024



Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai David Elias kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai David Elias kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.








Na Sylvester Omary, Dodoma

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa utoaji wa haraka wa ripoti za uchunguzi na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi.

Kamishna Jenerali ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square.

“Nawapongeza kwa kuwahisha ripoti za uchunguzi na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita kwa kununua mitambo imara na yenye ubora katika uchunguzi wa kimaabara na kupata ithibati za mifumo ya kimataifa” alisema Kamishna Jenerali.

Aidha, Kamishna Aretas Lyimo, alipongeza Mamlaka kwa kuwa na mifumo ya taarifa za uchunguzi wa kimaabara na wa taarifa za mashahidi wataalam ambayo inasaidia kubadilisha taarifa na wadau wengine wa haki jinai.

“Nawapongeza pia kwa kuwa na mifumo ya kufanyia kazi ya kisasa, hii yote inasaidia kuongeza utendaji kazi na kusaidia vyombo vingine na Mahakama kwenye utendaji haki ili kuleta ustawi kwa Taifa” alisema.

OFISA MKUU WA FEDHA - AngloGold Ashanti ATEMBELEA GGML

January 29, 2024

 Na Mwandishi Wetu


OFISA Mkuu wa masuala ya fedha (CFO) kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Gillian Doran wiki iliyopita alikaribishwa na kuutembelea mgodi huo uliopo mkoani Geita.

Mbali na Doran pia Meneja Mwandamizi wa Ushuru – Afrika, Jacques Labuschagne na Makamu wa Rais wa masuala ya Fedha – Afrika, Himesh Persotam pia waliitembelea GGML.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Doran amesema ziara yao haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita.

"Ziara hii haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita."

Yusuph Mhando, Meneja Mazingira (aliyeupa mgongo kamera), akimfafanulia CFO wa AngloGold Ashanti Gillian Doran (wa pili kutoka kulia) namna kanuni za mazingira zinazotambuliwa na kufuatwa na GGML katika shughuli zake.
Zulu Nkanyiso ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Mtambo wa uchenjuaji akijibu maswali kutoka kwa Gillian Doran, Ofisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, kuhusu muongozo wa GGML wa usimamizi na uhifadhi wa takasumu (TSF).

Mhandisi wa GGML anayedhibiti ubora na viwango vya miradi, Maftah Seif akitoa maelezo zaidi kuhusu teknolojia ya hali ya juu itakayotekelezwa katika kituo kipya cha GGML chenye uhusiano na TANESCO. Mradi huo ni ushahidi wa juhudi za GGML zinazoendelea za kuboresha kuongeza ufanisi wa kiutendaji.
Gilbert Chamlonde, Meneja – uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi akitoa muhtasari wa historia ya uzalishaji wa mgodi wa Nyamulilima kwa Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, Gillian Doran.

Gillian Doran ambaye ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti (katikati), pamoja na Himesh Persotam (mwisho kushoto), Makamu wa Rais: Masuala ya Fedha - Afrika, na Jacques Labuschagne, Meneja Mwandamizi wa masuala ya Ushuru Afrika, (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja kando ya mgodi wa Nyamulilima na baadhi ya menejiment ya GGML.

NAIBU KATIBU MKUU PROF. MDOE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMAHIRI CHA TEHAMA DIT

January 29, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Sayansi) Prof.James Mdoe ametembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha kufundishia Umahiri wa Tehama katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambacho kitatengeneza wataalamu katika masuala ya ujenzi wa Teknolojia.

Ujenzi wa Kituo hicho kikubwa nchini unadhaminiwa na Benki kuu ya dunia (WB).

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo leo Januari 29,2024 Jijini Dar es Salaam, Prof. Mdoe amewataka mkandarasi kuongeza watendaji kazi kwa lengo la kusaidia kazi kukamilika kwa wakati ili kuruhusu majengo hayo yaanze kutumika katika mtaala mpya wa kujenga umahiri katika fani hizo.

Aidha ameeleza kuwa majengo ambayo yanajengwa yananafasi kubwa ya kubeba watafiti ambao watahitaji kufanya tafiti katika chuo hicho ambapo amesema kuwa taasisi hiyo Ina mashirikiano na watu wengi.

Pamoja na hayo amesema kuwa katika kituo hicho kitakuwa na maabara ambazo zinahusiana na kutengeneza roboti, kujifunza masuala ya akili bandia (artificial intelligence) na mambo ya mtandao.

"Tunatengenza maabara Kuna watu watakuja kutengeneza maroboti,watajifunza masuala ya akili bandia,masula ya mtandao,,ujenzi huu ulitakiwa ukamilike februari Sasa wameongezewa miezi miwili kwenye jengo hili na la bweni". Amesema Prof. Mdoe.

Ujenzi huo unakadiriwa hadi kukamilika kwake utatumia Bilioni 21.9 katika mradi huo ambao umelenga kuleta mapinduzi makubwa ya kidigiti nchini kwa kuzalisha wahitimu wenye Umahiri wa Tehama.










MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 30,2024

January 29, 2024

 

VETA SINGIDA YAISHUKURU EWURA KWA MAFUNZO

VETA SINGIDA YAISHUKURU EWURA KWA MAFUNZO

January 29, 2024

 

Mhandisi Mwandamizi wa Umeme EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo (kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa VETA Singida namna ya kufanya maombi ya leseni kwa mfumo wa LOIS wakati wa mafunzo yaliyotolewa na EWURA chuoni hapo, leo 29 Jan 2024.

   

Wanafunzi wakifuatilia kwa umakini mafunzo kutoka kwa Wataalam wa EWURA juu ya udhibiti wa sekta ya umeme hususani masuala ya leseni leo, 29 .01. 24 katika chuo cha VETA Singida.

 Na.Mwandishi Wetu-SINGIDA

 

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Singida kimeishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wake 100 wa fani ya Mifumo ya umeme.

Msajili wa Chuo hicho, Bw. Gelshom Maloda ameiomba EWURA kuendesha mafunzo ya mara kwa ili kuwajengea uwezo wanafunzi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya sekta ya umeme.

Mhandisi mwandamizi Wa Umeme EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo, amewasilisha mada kuhusu masuala ya msingi ya Mifumo ya Umeme na Madaraja ya leseni za EWURA na namna ya kuomba leseni hizo kwa mtandao kupitia mfumo wa LOIS . Mfumo huo unapatikana katika tovuti ya Mamlaka www.ewura.go.tz.

Wanafunzi wamesisitiziwa umuhimu wa kumiliki leseni zinazotolewa na EWURA, ikiwa ni pamoja na utambulisho wa utalaamu wao, ubora wa huduma na usalama wa mali, watu na mazingira.

Mafunzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 29/1/2024, yameratibiwa na EWURA Kanda ya Kati, inayohudumia mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa na Morogoro.

WAJUMBE TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA DODOMA

January 29, 2024

 

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati Januari 30,2024.


Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati Januari 30,2024.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati Januari 30,2024.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati Januari 30,2024.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika picha ya pamoja. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe.Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni Mhe. Jaji Asina Omari, Mhe Balozi Omar Ramadhani Mapuri. Waliosimama kutoka kushoto ni Mhe. Jaji wa Rufaa Mwanaisha Kwariko, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar na Mhe. Magdalena Rwebangira.


Wajumbe wa Tume, Mhe.Jaji (R) Mwanaisha Kwariko (Kulia) na Mhe. Jaji Asina Omari wakiwa katika Banda la Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).

Wajumbe wa Tume, Mhe.Jaji (R) Mwanaisha Kwariko (Kulia) na Mhe. Jaji Asina Omari wakiwa katika Banda la Mahama Kuu upande wa Mirathi.

Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira akiwa katika Banda la wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).

Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omari akiwa katika Banda la Chuo cha Mahama Kushoto (IJA).
Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akiwa katika Banda la Wadau wa Hakika Jinai.

Wajumbe wa Tume, Mhe.Jaji (R) Mwanaisha Kwariko (wapili kushoto) na Mhe. Jaji Asina Omari (kushoto) wakiwa katika Banda la Mahama Kuu upande wa Mirathi.