MME WA FLORA MBASHA AMWAGA MACHOZI MAHAKAMNI..SAKATA LA KUMBAKA SHEMEJI

March 07, 2015
Mwimbaji wa muziki wa injili, Emmanuel Mbasha, anayekabiliwa na kesi ya kumbaka mtoto wa miaka 17, juzi alitoka kwenye chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala akibubujikwa machozi.
Hali hiyo ilimtokea mara baada ya shahidi wa pili wa kesi hiyo, aliyejulikana kwa jina la Suzan, kutoa ushahidi wake.

Kwa kuwa kesi hiyo inasikilizwa kwenye chemba (chumba maalumu ambacho waandishi na watu wasiohusika hawaruhusiwi kuingia) haikuweza kujulikana mara moja ni kitu gani kilichofanya mwimbaji huyo ambaye kwa sasa ameachana na mkewe, Flora Mbasha alie.
Mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa na Mbasha kuondoka kwenye viwanja vya mahakama hiyo akiwa na wakili wake, Ngassa Ganja, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alisema shahidi huyo aliieleza mahakama jinsi binti anayedaiwa kubakwa alivyomsimulia namna alivyotendewa kitendo hicho.

Alisema shahidi huyo alitoa ushahidi wake mbele ya hakimu Flora Mjaya.
“Mnakumbuka ile siku ambayo shahidi namba moja (binti aliyebakwa) alivyoieleza mahakama kwamba walikwenda kwa dada yake kumtafuta Flora ndipo akabakwa na Mbasha? Basi huyu shahidi namba mbili (Suzy) ndiye yule dada yake,” alifafanua.

Katuga alisema shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa alipata taarifa zote hizo baada ya binti anayedaiwa kubakwa kukimbilia nyumbani kwake na kumpa taarifa zote.
“Lakini kwa mujibu wa sheria (CPA) namba 186 kifungu kidogo cha tatu, inanizuia kueleza kwa kina yale ambayo shahidi huyo ameieleza mahakama,” alidai Katuga.

Kwa upande wake, wakili wa Mbasha, Ganja, alisema kuwa licha ya shahidi huyo kueleza kwamba binti anayedaiwa kubakwa alipigwa na Mbasha, yeye shahidi hakumkagua ili kujiridhisha kama ni kweli alipigwa ama la.
“Ni kweli ameieleza mahakama ushahidi ambao Katuga amewaeleza, ila shahidi huyo hakumkagua (binti aliyebakwa) ili kujua kama ni kweli,” aliongeza.
Mbasha alifika mahakamani hapo mapema saa tatu asubuhi.
Hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa kwa muda kutokana na wakili wake, Ganja kuchelewa kufika mahakamani hapo.
Ilipofika saa tano, kesi hiyo iliitwa tena na ushahidi huo kusikilizwa kwa takriban saa mbili, mbele ya hakimu Mjaya.

Katika kesi hiyo Mbasha ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa muziki wa injili, Flora Mbasha, anadaiwa kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17, kati ya Mei 23 na 25 mwaka jana eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.
Septemba 5 mwaka jana, binti huyo aliieleza mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake huyo kwa awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.
Kesi hiyo inasikilizwa mahakamani kwa siri kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu ili kulinda haki ya binti huyo

KIKWETE AZINDUA RASMI AZAM TV JIJINI DAR ES SALAAM JANA

March 07, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam jana Machi 6, 2015. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV  Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa
 RAis Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara  pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV   wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara  pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV   wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad  juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakitmbezwa sehemu mbali mbali za Azam TV na mwenyeji wao Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na  Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
FANI ZA SANAA KUTUMIKA KUELIMISHA UMMA MAUDHUI YA KATIBA PENDEKEZWA

FANI ZA SANAA KUTUMIKA KUELIMISHA UMMA MAUDHUI YA KATIBA PENDEKEZWA

March 07, 2015

gab1 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi Leah Kihimbi akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha kumi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na katikati ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
gab2
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasalimia wadau wa Utamaduni huku akiwa ameshika moja ya dhana za utamaduni alipokua akifungua kikao cha kumi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo. gab3 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na wadau wa Utamaduni alipokua akifungua kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
gab4 
Afisa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya Bw. Godfrey Msokwa akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
gab5 
Mmoja wa washairi (kushoto) akiburudisha wadau wa Utamaduni wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha ngoma kijulikanacho kama Jivunie Sanaa Tanzania kikitumbuiza wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. gab8 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa mwenye suti) katika picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya Utamaduni baada ya kufungua kikao kazi cha kumi cha Sekta hiyo jana jijini Dar es Salaam. (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)………………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Maafisa Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kutumia sanaa kupitia fani mbalimbali kuhamasisha juhudi za kuifahamu na kuipokea katiba inayopendekezwa ili jamii ya watanzania kuweza kujipatia katiba inayokidhi mahitaji yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni, Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.

Profesa Gabriel amesema kuwa lengo la kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni ni kutanabaisha maudhui ya Katiba inayopendekezwa hivyo kuwataka wadau wa utamaduni kutumia tasnia ya sanaa inayoumbwa na herufi K tatu zinazolenga Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha jamii katika masuala mbalimbali.

“Utamaduni ni kama inta inayoshikamanisha watu, ni vyema wadau wa utamaduni mkatumia talanta mliyonayo kufikia fikra za watu kwani suala la katiba pendekezwa ni letu sote kama watanzania hivyo tujivunie kwa kuweka mambo kwenye vitendo na kuishi yale tunayoyasema” amesema Profesa Gabriel.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa sanaa imekua ikitumika kusaidia makundi mbalimbali katika jamii kutoa sauti zao kwenye mambo mbalimbali na kuamini kuwa sanaa ina nafasi kubwa ya kuhamasisha na kuelimisha jamii maudhui ya katiba inayopendekezwa.

Bibi. Kihindu amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kimewashirikisha maafisa utamaduni kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara kikiwa na madhumuni ya kueleza mchango wa fani za sanaa katika kuelimisha umma maudhui ya katiba inayopendekezwa na kutoa ufafanuzi wa masuala ya Sekta ya Utamaduni yaliyozingatiwa katika Katiba inayopendekezwa.
  Akizungumza kwa niaba ya maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara, Afisa Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kitawawezesha wadau wa utamaduni kutumia sanaa kuifikia jamii na kutekeleza maazimio yatakayokusudiwa na kikao hicho.

Kikao kazi cha 10 cha Sekta ya Utamaduni chenye kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa zielimishe Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa kimelenga kutumia sanaa kama kichocheo na mbinu mojawapo ya kuelimisha, kuonya na kuelekeza mambo mbalimbali yanayoihusu jamii.
WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA WAZIRI MWENZAKE WA KENYA ITB BERLIN

WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA WAZIRI MWENZAKE WA KENYA ITB BERLIN

March 07, 2015

laz1 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.
laz2 
Mh. Waziri Nyalandu akihojiwa katika banda la Tanzania na mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Check inn cha Qatar Bw. Tajamul Hussain kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
laz3MKurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Zara tours kutoka Moshi Tanzania bibi Zainabu akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalndu alipotembelea banda la Tanzania kujionea namna waoneshaji wa Tanzania wanavyoitangaza Tanzania katika maonesho ya ITB berlin.
laz4 

Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Mh. Phylis Kandie akisakata rhumba na Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Nyalandu katika banda la Tanzania.
…………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana na waziri mwenzake wa Biashara na Utaliiwa Kenya Bibi Phylis Kandie katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya Utalii. Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania katika maonesho hayo.
Spika Makinda, Wenyeviti wa Bunge Watembelea Miradi ya NSSF Dar

Spika Makinda, Wenyeviti wa Bunge Watembelea Miradi ya NSSF Dar

March 07, 2015

Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa shukrani kwa uongozi wa NSSF mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Kigamboni.
Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Kigamboni.
Baadhi ya viongozi wa NSSF wakimuongoza Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge katika ziara yao ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Joseph Nyamuanga (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Mwenye kanzu ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau.

Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (aliyenyoosha mkono) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (aliyenyoosha mkono) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (wa pili kushoto mbele) akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa miradi mikubwa mbalimbali linayoendelea kuwekeza nchini ambayo imekuwa chachu ya maendeleo na kukuza hadhi ya nchini.
Spika Makinda ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akitembelea baadhi ya miradi mikubwa ya NSSF iliyopo jijini Dar es Salaam, ukiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la kubwa la kisasa linalojengwa kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na Mji wa Kigamboni pamoja na mradi mkubwa wa ujenzi wa Mji wa Kisasa unaojulikana kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa kwa ubia pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa zenye hadhi mbalimbali kulingana na mahitaji ya watu.
Akizungumza wakati akitembelea miradi hiyo, Makinda alisema miradi hiyo mbali na kuleta maendeleo nchini inakuza hadhi ya nchi pamoja na kuirahisishia serikali katika utoaji huduma kwa wananchi wake.
Aliiomba Serikali kupitia Wizara mbalimbali na jamii nzima kuendelea kutoa ushirikiano dhidi ya miradi hiyo kwani inachangia maendeleo kuanzia ngazi ya jamii pamoja na taifa kwa ujumla. Aliwataka wananchi kutumia fursa iliyopo ya kununua na kukopa nyumba zinazojengwa na shirika hilo kwani mbali na kujengwa kwa hadhi anuai na kisasa zimepangiliwa jambo ambalo linarahisisha utoaji wa huduma za jamii dhidi yao.
Alisema kwa maendeleo ya sasa ni nchi ya Tanzania pekee ambapo raia wake hujenga nyumba wenyewe, kwani mataifa mengi yaliyoendelea nyumba hujengwa na mashirika na kuuzwa kwa raia jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa miji iliyopangiliwa tofauti na ilivyo Tanzania.
“…Duniani kote watu wanaojenga nyumba wenyewe hadi sasa ni Tanzania tu, na hii ndio chanzo kikubwa cha nchi yetu kuendelea na kuwa na miji ambayo haijapangiliwa (ujenzi holela). Lazima tubadilike unajua ukiwa na mji uliopangiliwa ni rahisi hata kuwahudumia wananchi wako…,” alisema Makinda.
Aidha alishauri uwepo wa utaratibu mzuri wa kukopesha nyumba za kisasa zinazojengwa na NSSF ili wahitaji wapewe na kulipa kwa awamu huku wakimilikishwa nyumba hizo jambo ambalo litaondoa adha ya upatikanaji wa makazi bora kwa wananchi.
Katika ziara hiyo Spika Makinda aliambatana na Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama , Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka pamoja na Kamati ya Uongozi ya Bunge la Tanzania ambao kwa pamoja walilipongeza Shirika la NSSF na kushauri kuendelea kuwekeza pia katika mikoa mingine inayochipukia kimaendeleo kwa sasa ili kusambaza huduma maendeleo mengine.
Awali akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa alisema licha ya changamoto zilizojitokeza mradi huo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 75 ya ujenzi wake.
Kwa upande wake, Mhandisi Juhus Nyamuhokya wa kampuni ya Ujenzi ya Hifadhi wabia wa NSSF katika ujenzi wa Kijiji cha kisasa cha ‘Dege ECO Village’ kinachojumuisha ujenzi wa nyumba 7,460 za kisasa zenye hadhi tofauti kulingana na mahitaji alisema ujenzi wake utajumuisha miaka minne ukijengwa kwa awamu tatu.
Mhandisi Nyamuhokya alisema awamu ya kwanza ya mradi huo inakamilika Desemba 2015, awamu ya pili itakamilika Desemba 2016 huku awamu nyingine ikitarajiwa kukamilika Desemba 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau alimshukuru Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa kutembelea miradi hiyo ambayo ina lengo lakuchochea maendeleo ya taifa na wananchi kiujumla.

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE KUWA MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

March 07, 2015

Na Happy Shirima - Habari Maelezo. 

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo [WAMA] anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam .

Akizungumzia maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam , Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar se salaam Mhe. Raymond Mushi amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake Tekeleza, Wakati ni Sasa “.

Amesema ujumbe huo unaikumbusha jamii kujenga mazingira  wezeshi kwa kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .

Ameeleza  kuwa wadau kote nchini wanatakiwa kuelimishwa ili kuangali upya wajibu wao kwa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu , uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu ya maendeleo yao binafsi, familia na taifa zima.

“Lengo la maadhimisho haya ni kukumbuka wajibu wa kila mmoja  kushiriki katika mikakati  ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa” Amesema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa yanaambatana na maonyesho ya kazi na bidhaa mbalimbali za vikundi vya ujasiriamali na kuzishirikisha Asasi za Kiraia  zinazojishughulisha na masuala ya utoaji wa Elimu ya Uraia na sheria ya utunzaji fedha.

Ameongeza kuwa siku ya kilele  kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Barabara ya Lumumba na kuishiaviwanja vya mnazi mmoja ambayo yatapokewa na mgeni rasmi  na wananchi  wa mkoa wa Dare s salaam.