YANGA SC YAPATA BONGE LA BEKI TAIFA STARS, MWENYEWE ASEMA YUKO NJIA MOJA JANGWANI

May 14, 2015

Mwinyi Hajji Mngwali tayari kutua Yanga
Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
BEKI wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mwinyi Hajji Mngwali amesema yuko tayari kutua Yanga SC.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Mngwali anayechezea KMKM ya Zanzibar amesema amefanya mazungumzo ya awali na Yanga SC na kimsingi yuko tayari kutua Jangwani.
“Ndiyo, Yanga wamezungumza na mimi, ila hatujamalizana. Lakini niseme wazi niko tayari kutua Yanga SC,”amesema.
Mngwali yupo katika kikosi cha Taifa Stars ambacho kipo Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Kombe la COSAFA.
Stars iliwasili Johannesburg, Afrika Kusini usiku wa juzi na ikalazimika kulala huko kabla ya jana asubuhi kuunganisha safari kwa basi kuja Rustenburg ambako imefikia hoteli ya Hunters, nje kidogo ya mji.
Wachezaji waliowasili na Stars hapa ni makipa: Deogratius Munish ‘Dida’ (Yanga) na Mwadini Ali (Azam), mabeki ni Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM).
Wengine ni viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar).
Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba), Mrisho Ngassa (Free State Stars), Simon Msuva (Yanga), John Bocco (Azam FC) na Juma Luizio (ZESCO United).
Taifa Stars imepangwa pamoja na Namibia, Lesotho na Zimbabwe katika Kundi A, wakati Kundi B lina timu za Shelisheli, Madagascar, Mauritius na Swaziland.
Kila timu itakayoongoza kundi, itaungana na wenyeji Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia kwa ajili ya hatua ya Robo Fainali.
Mpinzani wa Tanzania katika hilo, anatarajiwa kuwa Zimbabwe, ambaye hata hivyo alitolewa na Taifa Stars katika mechi za kufuzu AFCON mwaka jana.
Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia zimeingia moja kwa moja katika Robo Fainali kwa sababu zipo juu viwango vya ubora wa soka vya FIFA.
Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoro, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mayotte, Msumbuji, Namibia, Reunion, Shelisheli, Swaziland, Zambia na Zimbabwe, lakini katika kuiongezea ladha ya ushindani, sasa hivi zinaalikwa na timu kutoka nje ya ukanda huo.

SIMBA SC YATUPA NDOANA ZAKE KWA BEKI TEGEMEO RWANDA, TENA KINDA TU

May 14, 2015

Na Princess Asia, DAR ES SAALAM
SIMBA SC imetupa ndoana zake kwa Emery Bayisenge wa APR ya Rwanda, lakini kumpata kazi ipo.
Bayisenge, beki hodari wa kati mwenye umri wa miaka 21 tu, ni tegemeo la Rwanda kuelekea michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika CHAN mwakani, inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kwa sababu hiyo, Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) halitapenda kukipoteza kisiki hicho kabla ya CHAN ya mwakani, ambayo wao watakuwa wenyeji. 
Simba SC inamtaka Emery Bayisenge, lakini kikwazo ni FERWAFA inayotaka kumtumia katika CHAN mwakani

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ni shabiki mkubwa wa beki huyo na BIN ZUBEIRY inafahamu yuko katika jitihada kubwa za kuhakikisha anamhamishia Msimbazi.
Bayisenge mwenyewe kwa mvuto wa maslahi na hamu yake kubwa ya kucheza Tanzania, yuko tayati kutua Simba SC- lakini FERWAFA ndiyo kikwazo. 
Bayisenge ambaye kabla ya APR alichezea Amagaju na Isonga, amekuwa akiichezea Amavubi tangu mwaka 2011.
CHAN ijayo inatarajiwa kufanyika Rwanda kuanzia Januari 16 hadi Februari 7 ikishirikisha jumla ya timu 16.
Serikali yawashauri Vijana Mkoani Ruvuma kujishughulisha na ujasiriamali

Serikali yawashauri Vijana Mkoani Ruvuma kujishughulisha na ujasiriamali

May 14, 2015

1
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw. Nachoa Zacharia kulia akiongea na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa Maafisa hao walipokuwa katika ziara ya mafunzo stadi za maisha,ujasiriamali na elimu ya uongozi kwa vijana wa Mkoa wa Ruvuma, kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Vijana cha Sasanda kilichopo mkoani Mbeya Bw. Laurian Masele.(Picha na Benjamin Sawe)
2
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mh. Charles Mhagama akisisitiza jambo kwa maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa ziara ya mafunzo ya stadi za maisha,ujasiriamali, mfuko wa Vijana na elimu ya uongozi kwa vijana wa Mkoa wa Ruvum, kulia Afisa Vijana kutoka Wizarani Bi. Amina Sanga na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa.(Picha na Benjamin Sawe)
3
: Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada ya jinsi ya Vikundi vya vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea vilivyokidhi vigezo vinavyoweza kunufaika na mfuko huo,mafunzo hayo yamefanyika mkoani Ruvuma.(Picha na Benjamin Sawe)
4 (2)
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa akitoa mada juu ya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007, Stadi za Maisha na ujasiriamali kwa Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.(Picha na Benjamin Sawe).
MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA

MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA

May 14, 2015

01
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Mary Mwanjelwa, Bungeni mjini Dodoma Mei 14, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
02
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akichangia bungeni mjini Dodoma Mei 14, 2015.
03
Mbunge wa Viti Maalum, Mary Chatanda akichangia bungeni mjini Dodoma Mei 14, 2015.
05
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akizungumza na Mkuu wa mkoa wa  Njombe, Dr. Rehema  Nchimbi (kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bnge mjini Dodoma Mei 14, 2015.
KATIBU MKUU TAMISEMI, SAGINI ASISITIZA UIMARISHAJI WA ELIMU

KATIBU MKUU TAMISEMI, SAGINI ASISITIZA UIMARISHAJI WA ELIMU

May 14, 2015
DSC_0069
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi katika kumwezesha mtu kujitegemea.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog kuhusu maendeleo na changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki ya maadhimisho ya elimu inayofikia tamati leo mjini Dodoma.
Alisema katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa unawaondoa watu kwenye ajira ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji wa elimu ndio kitu cha msingi kabisa.
Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini.
Alisema kuna mambo mengi ambayo yanastahili kuangaliwa kwa sasa kutokana na vigezo vya ufanisi wa elimu kuonesha changamoto zinazokabili sekta hiyo pamoja na kuimarika kwake.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupungua kwa uandikishaji wa watoto na mdondoko.
Alisema viongozi, wazazi pamoja na walezi wamesahau wajibu wao na kumwachia mwalimu pekee katika kumlea mwanafunzi kimasomo na hii ndio chanzo kikubwa cha mdondoko na ufaulu mbaya.
Alisema ni vyema watu wakajiuliza hawa wanaondoka wanakwenda wapi na wanafanya nini.
“kuna sheria ambapo viongozi wa kata wanaruhusiwa kuwachukulia hatua na kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokwamisha elimu, lakini watu hawachukia sheria hiyo” alisema.
Aidha alisema ubora wa elimu una vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kujituma kwa walimu katika ufundishaji na kuwa na dhamira ya kuwapa watoto vitu vyenye maana.
Alisema kuna mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuinua elimu na usimamizi unapokuwa mkali na wahusika kuadhibiwa ndio ufanisi unafanyika na mdondoko kuangaliwa.
Alisema ipo haja kubwa ya kuwekeza kwenye elimu kwa viongozi na wadau kutimiza wajibu wao.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Makuru Petro akitoa tathmini ya sekta ya elimu kwa wadau wa sekta ya elimu alisema pamoja na ongezeko la ufaulu ndani ya miaka miwili ipo haja ya kutathimini uimara wa mfumo katika kutoa huduma ya elimu.
Alisema pamoja na ufanisi kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wanaokacha shule kunaonesha mfumo kuwa na kasoro na lazima uangaliwe.
Aidha alisema sekta ya elimu wamepokea asilimia 97 ya bajeti yake na kwamba asilimia 70 imeenda kwenye halmashauri ambako ni watekelezaji wa miradi ya elimu.
Tathmini hiyo inayowakilisha wizara zote zinazoshughulikia elimu kama TAMISEMI, Elimu na Maendeleo ya jamii na wadau wengine wa elimu ni sehemu ya shughuli inafanywa kila mwaka kwa lengo la kutambua kilichofanyika, changamoto na namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo walisema kwamba ndani ya miaka miwili kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu hasa ufaulu na ubora wa elimu.
DSC_0078
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) mjini Dodoma.
DSC_0252
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimweleza yaliyomo kwenye taarifa ya ripoti ya hali ya Elimu ilivyo dunia (EFA Global Monitoring Report 2015) “Education For All 2000-2015” ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto kidunia iliyoandaliwa na Shirika la UNESCO alipomtembelea ofisini kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja mjini Dodoma ambapo pia alikutana na wadau wa sekta ya elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Elimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
DSC_0254
DSC_0258
DSC_02611
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akimwonyesha takwimu za Tanzania zilizomo kwenye ripoti hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini.
DSC_0276
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.
DSC_0273
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO, Zulmira Rodrigues (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma.

MANJI AAMBIWA; “UMEMALIZA MUDA WAKO YANGA SC”, KAMATI YAITISHA UCHAGZUI JULAI 12 DAR

May 14, 2015


UCHAGUZI Mkuu wa Yanga SC utafanyika Julai 12, mwaka huu katika ukumbi ambao utatajwa baadaye.
Taarifa ya Katibu Kamati ya Uchaguzi ya Yanga SC, Francis Kaswahili iliyotumwa TANGA RAHA leo imesema kwamba, fomu za wagombea zitaanza kutolewa Mei 17, mwaka huu kwa kuzingatia ratiba.
“Jambo hili ni la kikatiba na wala halina mjadala, tunataka Yanga iwe na viongozi ambao watatokana na utashi wa Wanayanga ni matumaini ya kamati ya uchaguzi kwamba hapatatoka mtu mwingine wa kutaka kuvunja misingi ya katiba.
Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji ameambiwa amemaliza muda wake madarakani

“Huu ni utamaduni wa mwanadamu anayeishi katika mfumo wa demokrasia na hasa ikizingatiwa kwamba mwaka 2015 ni mwaka pia wa uchaguzi, wa Rais , Wabunge na Madiwani,”amesema Kaswahili. 
Ameongeza kwamba, lengo ni mwendelezo wa kupokezana vijiti na kwamba kiongozi bora atapatikana kwa misingi bora ya kikatiba na si vinginevyo.
Itakumbukwa kwamba kwa mara ya mwisho Yanga SC ilifanya uchaguzi wake Julai 18, mwaka 2010 na Wakili Lloyd Biharangu Nchunga alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu wake, Devis Mosha na Wajumbe; Charles Mgondo, Ally Mayayi Tembele, Mzee Yussuf, Theonest Rutashobolwa (marehemu), Titus Ossoro, Sara Ramadhani, Mohamed Bhinda na Salum rupia. 
Hata hivyo, kwa vipindi tofauti baadhi ya viongozi walijiuzulu nyadhifa zao na hivyo ikalazimika kufanyika uchaguzi mdogo ufanyike Julai 15, mwaka 2012 na Yussuf Manji alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu wake Clement Sanga na Wajumbe; Aaron Nyanda, George Manyama, Abdallah Bin Kleb na Mussa Kutabaro. 
“Na itakumbukwa kamba wale wote ambao waliingia kwa kuziba nafasi wzi walikuwa wanatumikia mhula ulioanza tarehe 18/07/2010 na ulikoma tarehe 17/07/2014 na hivyo viongozi wote nafasi zao kwa sasa zipo wazi,”amesema Kaswahili.
CHNZ:BINZUBEIRYBLOG

TASWIRA YA SOKO LA SAMAKI SAHARE JIJINI TANA LEO JIONI

May 14, 2015


 Wachuuzi wa samaki bandari ya Sahare Tanga wakisubiri wateja. Kipindi hiki cha mbalamwezi samaki wamekuwa wakipatikana kwa wingi. Ndoo moja ya samaki aina ya dagaa ilikuwa ikiuzwa shilingi 8,000 wakati fungu moja na sakami aina ya kibua ni shilingi 1,500.






Changamoto maboresho usimamizi wa fedha za umma zatajwa

Changamoto maboresho usimamizi wa fedha za umma zatajwa

May 14, 2015
Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani. Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP. Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP.

 PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake. Mratibu wa Mradi huo ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo. Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi. Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu. Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma. Mradi pia umefanikiwa kuimarisha ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini, kutumika kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya kuingiza mahitaji ya Mpango wa miaka mitano na kugawa rasilimali na pia kuchapishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali hivyo kuongeza kiwango cha uwazi. Mengine ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 badala ya sheria iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo mengine imeiweka PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi, na kubaki na shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma. Vile vile sheria imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya ununuzi wa umma. "...Kujenga uwezo wa watumishi katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Kwa mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu, wakaguzi, wachumi; maafisa wa ununuzi...kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kulitumikia taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya mfumo wa IFMS ili kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa mfumo wa kusimamia mali za serikali (Asset tracking software) katiak ofisi zote za kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali." Alisema Mratibu huyo. Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua ya 3 ya AFROSAE, uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5 ulibadilishwa na kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi kuliko ule wa mwanzo, Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda serikali za mitaa na kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa fedha toka serikali kuu kwenda kwenye LGAs. Mratibu alibainisha kwa sasa Ofisi ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo wa IFMS, na hivyo kuongeza ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya kimataifa ya International Public Sector Accounting Standards Cash Basis (IPSAS). Mradi wa PFMRP ulianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika serikali na taasisi zake, huku ikitekelezwa sambamba na programu nyingine za kitaifa katika sekta ya umma. *Imeandaliwa na www.thehabari.com ____________________________________________________ Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

KINAPA YATANGAZA OFA YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA WATALII WA NDANI WA AFRIKA MASHARIKI

May 14, 2015

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani ya kipindi cha miaka 10 huku asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni wazawa.

Asilimia hiyo inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda Mlima huo kwa muda wa siku moja hali inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi zetu ili kujionea urithi tuliopewa na Mungu.

Mhifadhi utalii wa KINAPA,Eva Mallya alisema katika kuhamasiosha utalii wa ndani ,KINAPA imeandaa zoezi maalumu ambalo litadumu kwa muda wa siku nne kwa watanzania walio walio karibu na mlima kuweza kuupanda kwa muda wa siku moja na kurudi.

Mhifadhi utalii katka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akizungumza juu ya ofa iliyotangazwa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima huo kwa siku moja na kurudi hadi kilele cha Shira.

“Tumeandaa zoezi rahisi kwa kila mmoja mwenye nafasi aweze kupanda,sehemu kubwa itakuwa ni kwa kutumia gari ambapo walio tayari watachukuliwa na gari hadi eneo fulani kabla ya kutembea umbali mdogo na kutizama uwanda wa Shira katika mlima Kilimanjaro.”alisema Mallya.

Alisema zoezi la uandikishaji kwa ajili ya watakao penda kupanda katika mlima huo tayari limeanza katika vituo vilivyoko jirani na Duka la Maua mkabala na Rafiki Supermarket ,Hosptali ya rufaa ya KCMC na njia Panda ya Himo.

Mallya alisema mpandaji atapaswa kujitegemea kwa Sweta na Jacket kwa ajili ya baridi ,suruali raba pamoja na chakula huku mhusika akitakiwa kulipia kiasi cha sh 15,000 kama kiingilio cha hifadhini.
Afisa masoko wa KINAPA ,Antypas Mgungusi akisistiza jambo wakati akizungumzia juu ya ofa ya safafri ya kupanda Mlima Kilimanjaro huku akishauri wenye sherehe zao kutumia nafasi hiyo kupanda Mlima huo kwa ajili ya kufanya sherehe zao,alitaja sherehe ambazo zinaweza fanyika katika hifadhi hiyo ni pamoja na wale wenye kukumbuka siku zao za kuzaliwa wanaweza fanya hivyo wakiwa kileleni,lakini pia kwa wale wanaoenda Honey Moon baada ya ndoa pia wameshauriwa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha ofa.

Kwa upande wake afisa masoko wa KINAPA,Antypas Mgungusi alisema safari ya kupanda mlima Kilimanjaro imekuwa ikitumiwa na baadi ya watalii kufanya matukio ya kihistoria ikiwemo kufunga ndoa na wengine
kuadhimisha siku zao za kuzaliwa wakiwa kileleni.

“Imezoeleka kuwa watu wanapokuwa na matukio yao yakiwemo ya mikutano,au Honey moon baada ya ndoa na siku za kuzaliwa wamekuwa wakifanya sherehe zao mijini,lakini kuna maeneo mengine kama haya ya
hifadhi kufanyia mambo hayo”alisema Mgungusi.

Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kwa kuhifadhi barafu kwa kipindi cha mwaka mzima licha ya kupitiwa na mstari wa Ikweta huku ukiwa ndio mlima pekee uliosimama peke yake ukilinganisha na milima mingine duniani.
Ukiwa katika hifadhi hiyo utafurahia mandhari mbalimbali za mlima huo.

Baadhi ya watalii wa ndani wakielekea katika kilele cha Shira safari ambayo inatajwa asilimia 70 wanaenda kwa usafiri wa gari.


Wengine wanaweza pia kupanda na watoto wao.
Hivi ndivyo safari ya mwisho huwa.
Njiani utakutana na uoto mbalimbali wa asili .
Zipo tenti kwa ajili ya watalii wanaoendelea na safari.
Waliofanikiwa kufika kilele cha Shira hawakusita kuonesha furaha zao kwa kucheza .

BALOZI WA FINLAND NCHINI TANZANIA AZINDUA KITUO CHA MSAADA KWA WAHANGA WA UKATILI

May 14, 2015

Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akiwa katika picha ya pamoja na watoa ushauri.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara baada ya kufungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo hicho.
Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza kwa niaba ya wadau wa Kwieco wakati wa sherehe hizo.


Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akikata utepe kuashiria kuazna kutumika kwa majengo hayo.


Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa KWIECO,Jaji Aishiel Sumari akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi ,Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia,mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje chini ya shirika la UKUMBI.
Katibu tawala wa mkoa a Kilimanjaro ,Martha Ufunguo akitoa salama za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) Elizabeth Minde akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Katika kituo hicho wahanga watapatiwa malazi ya muda na huduma zingine za kijamii km matibabu, chakula, msaada wa kisheria, mafunzo ya ujasiriamali n.k.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya KWIECO ,Clement Kwayu akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Loe Rose Mbise wakai wa sherehe ya uzinduzi wa kituo hicho.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara wakati akitembelea majengo ya kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ambayo yamejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo chini ya shirika la UKUMBI.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka alikabidhi kitabu cha "Politics of Gender "kwa mkurugenzi wa Kwieco ,Elizabeth Minde.


Watoa ushauri wa shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO)wakiimba wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) akimpokea Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka aliyefika kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Maeneo mbalimbali ya kituo hicho.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.