TASNIA HALISI WHATSAAP GROUP YAZINDULIWA KWA KISHINDO JIJINI DAR ES SALAAM
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAANDISHI
wa habari ambao ni wanachama wa kundi la Whatsaap lijulikanalo kama TASNIA
HALISI wamezindua kundi hilo leo Oktoba 28, 2017 kwa sherehe kabambe ya
kukata na shoka iliyohanikizwa na nyama choma, vinywaji vya kila aina na muziki.
Mratibu
wa shughuli hiyo, Bi. Angela Msangi amesema, kundi hilo ni mukusanyiko wa
wanataaluma na wadau wa habari na linalenga kuwaleta pamoja wana tasnia kwa nia
ya kubadilishana taarifa na kusaidiana kitaaluma na kijamii.
Katika
uzinduzi huo uliosindikizwa na burudani ya muziki umeshuhudia waandishi kutoka
sehemu mbalimbali nchini wakishiriki.
Katika
sherehe hiyo, shampeni mbili zilifunguliwa ikiwa ni pamoja na kukata keki.
Tigo yachangia katika ukuaji wa teknolojia na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao nchini
washiriki wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini wakifurahia jambo , ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii jijini Dar es Salaam. |
Mafunzo kwa wafanyakazi wa nyumbani, waajiri pamoja na watendaji Jijini Mwanza
Binagi Media Group
Utafiti
uliofanywa na Shirika la hutetea haki za watoto wafanyakazi wanyumbani WOTESAWA
Jijini Mwanza, unaonyesha kwamba watoto hao bado wanakumbana na aina mbalimbali
za ukatili ikiwemo utumikishwaji.
Utafiti huo
uliofanyika mwaka jana ulibaini kwamba asilimia 91.9 ya watoto wafanyakazi wa
nyumbani katika Kata nne za Jiji hilo hawana mikataba ama makubaliano baina ya
wazazi na waajiri wao, asilimia 5.4 wana mikataba huku asilimia 80 ikionyesha
wapo wanaofanya kazi bila malipo huku wanaolipwa mshahara chini ya shilingi
20,000 wakiwa ni asilimia 20.
Utafiti huo
ulifanyika katika Kata za Igogo ambapo watoto wafanyakazi wa nyumbani 43
walifikiwa, Mkuyuni 42, Nyamagana 32 pamoja na Butimba 37 na hivyo kufanya
idadi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani waliofikiwa kuwa 154, wavula wakiwa ni
16 na wasichana 138.
Hali hii
inaongeza chachu kwa shirika la WOTESAWA kuwajengea uwezo watoto wafanyakazi wa
nyumbani, waajiri wao pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani,
Watendaji, Wenyeviti wa Mitaa, Maafisa Ustawi wa Jamii, pamoja na maofisa wa
dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi kama anavyoeleza Mkurugenzi wa shirika
hilo, Angel Benedicto.
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto
Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto akizungumza kwenye semina hiyo
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza Mratibu wa Shirika la WOTESAWA
Mratibu wa Shirika la WOTESAWA, Elisha Daud akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mratibu wa Shirika la WOTESAWA, Elisha Daud akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
MAFUNDI WA TANESCO WAWEKA KAMBI MBEZI KWA MALECELA KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOSOMBWA NA MAFURIKO YA MVUA ZA VULI
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
JUHUDI
kubwa zimekuwa zikifanywa na wahandisi na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania,
(TANESCO), kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua za vuli zilizonyesha kwa
siku mbili mfululizo jijini Dar es Salaam na hivyo kusababisha maeneo kadhaa ya
jiji kukosa umeme.
Eneo
la Mbezi chini ni moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya ambapo kwa uchache nguzo
nne zimesombwa na maji na kupelekea nyaya za kuafirisha umeme kukatika.
Leo
Oktoba 28, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO bi Leila Muhaji, alifanya ziara
kutembelea maeneo hayo yaliyoathirika ili kujionea mwenyewe na hivyo kuwa na
majibu sahihi kwa wateja abao wamekuwa wakiulizia juu ya tatizo hilo lakukosa
umeme.
Akiwa
katika eneo la Mbezi chini eneo la daraja la “Kwa Malecela” ambako nguzo hizo
zinakatisha kwenye daraja hilo na kukuta mafundi wakienendelea na kazi ya
kusimika nguzo na kufunga nyaya.
Kwa
mujibu wa Muhandisi Mkuu wa TANESCO Kinondoni Kaskazini Mhandisi Godlove
Mathayo, amesema mafundi wanafanya jitihada kusimika nguzo na kushughulikia tranforma
mbili moja iliyoko eneo la Victor5ia na nyingine hapo kwa Malecela, na kazi
hiyo ikikamilika basi umeme utarejea usiku huu.
:Kuna
baadhi ya transoma zimezingirwa na madimbwi ya maji na tunashindwa kuzifikia
kwa sasa na pindi maji yatakapopungua kazi ya kuzirekebisha tranforma hizo
tutafanya marejkebisho ili umeme uweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
“Amesema
baada ya matengenezo hayo yanayoendelea sasa, wakazi ambao wanategemea kupata
umeme ni wote wa maeneo ya Kwa Malecela, Victoria na Kawe kwa maana ya eneo la Mbezi
Chini.” Alisema.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja Uhusioano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba
radhi wateja waloathirika kutokana na hitilafu hiyo na kuwasihi kuwa wavumilivu
kwani mafundi wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha umeme unarejea katika
hali yake ya kawaida.
“Lakini
niwaombe tu wananchi watoe taarifa pale wanapoona maeneo yao hayana umeme,
watufahamishe ili mafundi wafike kwa haraka na kufanya marekebisho, wanaweza
kufanya hivyo kupitia anuani zetu na mitandao ya kijamii ya Shirika.” Alisema.
Miundombinu
imeathirika kutokana na mvua hizi za vuli lakini nitoe tahadhari umeme na maji
haviendani, wananchi wasisogelee miundombinu ya umeme wanapoona nguzo imelala
au waya umelala wasiguse watoe taarifa na mafundi wetu ambao wana vifaa maalum
watafika mara moja na kuondoa hatari hiyo. Alifafanua Bi. Leila.
Winchi ikinyanyua nguzo wakati wa urejeshaji miundombinu ya TANESCO eneo la Kwa Malecela Mbezi chini jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2017.
Fundi wa TANESCO akiwa amebeba vipuri wakati wa zoezi la kurejesha miundombinu ya umeme iliyoathirika na mafuriko ya mvua za vuli enel la Mbezi chini jijini Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kinondoni Kaskazini, Mhandisi Godlove Mathayo, (kulia), akimuoneyesha Kaimu Meneja Uhusiano, TANESCO, Bi Leila Muhaji, jinsi kazi inavyoendelea eneo la Mbezi Kwa Maalecela jijini Dar es Salaam Jumamosi Oktoba 28, 29017.
MBEGU BORA ZA MIGOMBA, VIAZI LISHE NA MIHOGO KUWAKOMBOA WAKULIMA MKOANI KAGERA
Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Muleba, Kokushubila Pesha akipanda mbegu ya muhogo katika shamba darasa la kikundi cha Ujamaa lililopo Kata ya Magata Karutanga wilayani humo. |
Ofisa Mtendaji wa kata ya Magata Karutanga Joyce Rassia akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa shamba darasa la kikundi hicho. |
Dkt. Kigwangalla atembelea pori tengefu la Loliondo ashuhudia uhalisia wa mgogoro
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla mapema jana Oktoba 27,2017
ameweza kutembelea eneo la pori tengefu la Loliondo lililopo Wilayani
Ngorongoro Mkoani Arusha na kujionea mambo mbalimbali juu ya mgogoro wa
muda mrefu maarufu Loliondo.
Waziri
Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea katika eneo hilo katika kushuhudia
kiini hicho cha mgogoro uliozidi zaidi ya miaka 20, ambapo anatarajia
kurejesha majibu kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais mara tu baada ya
kumaliza ziara yake hiyo pamoja na kukutana na watalaam wake wa Wizara.
Waziri
Dkt. Kigwangalla ameweza kuoneshwa eneo lenye mgogoro baina ya
mwekezaji pamoja na wananchi wa jamii ya wafugaji kwenye eneo hilo
sambamba na kufuatilia mipaka baina ya maeneo mbalimbali yanayozunguka
mipaka ya pori hilo tengefu pamoja na hifadhi ya Serengeti.
Awali
Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika mkutano wa wazi kwenye Mji wa Wasso
aliweza kusitisha operesheni zilizokuwa zinaendelea katika pori hilo
tengefu la Loliondo na huku akiagiza mifugo yote iliyoshikiriwa na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo haijafikishwa mahakamani kuachiwa
huru huku ile mingine iliyofunguliwa kesi kuendelea kushikiriwa mpaka
shahuri la msingi litakapotatuliwa.
Aidha,
Waziri Dkt. Kigwangalla amewataka wananchi hao jamii ya wafugaji katika
mgogoro huo kuacha mara moja kuingiza mifugo ndani ya hifadhi licha ya
kusitisha Operesheni iliyokuwa ikifanyika na kuwataka wakae meza moja ya
majadiriano kupata ufumbuzi.
Akiwa
ndani ya pori hilo pia alishuhudia kundi kubwa la wanyama mbalimbali
kwenye maeneo hayo ambapo imeelezwa awali hawakuwapo kutokana na
kukimbia mifugo iliyokuwa imeingizwa na wafugaji hao.
Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla akiwasili eneo la Loliondo kushuhudia kiini cha mgogoro huo
Dkt.Kigwangalla
akiwa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Elimu Mh.Ole Nasha wakati alipofika kukagua kiini cha mgogoro
huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akitazama wanyama eneo
lenye mgogoro ambalo ni pori tengefu la Loliondo ambalo awali lilikuwa
limevamiwa pamoja na mifugo ya wananchi.
Dkt. Kigwangalla akifuatilia ramani yenye kuonesha eneo la pori tengefu la Loliondo
Baadhi
ya wanyama walioonekana wakati Waziri Dkt.Kigwangalla alipotembelea
pori hilo ambapo awali wanyama hao walitoweka kutokana na kuingizwa
kwamifugo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akijadiliana jambo na Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka (kulia) pamoja na Mhifadhi Mkuu
wa Serengeti William Mwakilema wakati wakikagua maeneo hayo yenye
mgogoro huo wa Loliondo.
Dkt.Kigwangalla wakikatisha katika maeneo hayo ya Loliondo wakati akikagua maeneo yenye migogoro.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa
wananchi waliokuwa wakitoa kilio chao kuhusiana na mgogoro huo wa
Loliondo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akizungumza na wananchi
jamii ya wafugaji (Hawapo pichaani) wakati alipotembelea eneo la
Loliondo ili kubaini kiini cha mgogoro huo.
NAIBU WAZIRI AWESO AWATAKA WAKAZI WA PANGANI KUWA NA MSHIKAMANO ILI KUPATA MAENDELEO.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Pangani kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika uwanja wa sokoni ambapo alisisitiza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani akizungumza katika mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Pangani.Zainabu Issa akizungumza katika mkutano huo ambapo alimuomba Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo kuiwekea msukumo barabara ya Tanga-Pangani ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wilaya hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya PanganiSeif Saidi akizungumza katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Sabas Chamnbasi akizungumza katika mkutano huo |
Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi (CCM) John Semkande akizungumza katika mkutano huo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akilakiwa na wananchi wa Jimbo la Pangani wakati alipokwenda kuhutubia wananchi wa wilaya ya Pangani
kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika uwanja wa sokoni ambapo
alisisitiza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kusukuma mbele
gurudumu la maendeleo
NAIBU Waziri wa
Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akilakiwa na wananchi wa Jimbo la
Pangani wakati alipokwenda kuhutubia wananchi wa wilaya ya Pangani
kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika uwanja wa sokoni ambapo
alisisitiza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kusukuma mbele
gurudumu la maendeleo
NAIBU Waziri wa
Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akiingia eneo la mkutano kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Pangani
NAIBU Waziri wa
Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akiwapungia mkono wananchi wa Jimbo hilo
NAIBU Waziri wa
Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo
NAIBU Waziri wa
Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso katikati akifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani.
Kikundi cha Burudani kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa hadhara.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga akifuatilia mkutano huo
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mji wa Pangani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso
Subscribe to:
Posts (Atom)