MBUNGE WA KIGOMA KUSINI,MHE DAVID KAFULILA NA JESSICA KISHOA WAMEREMETA MJINI UVINZA

November 23, 2014

 Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma,  jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila akiwa kanisani  na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa  kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi 
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba  harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe  Zitto Kabwe na Mhe David  Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma
KATIBU MKUU WA UVCCM APATA MAPOKEZI YA KIHISTORIA MBINGA.

KATIBU MKUU WA UVCCM APATA MAPOKEZI YA KIHISTORIA MBINGA.

November 23, 2014


unnamed
Katibu mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndugu Sixtus Mapunda amepata makubwa wilayani Mbinga yaliyoacha gumzo kubwa wilayani hapo. Mapunda ambaye alitoke wilaya ya Nyasa amepokelewa kwa kishindo kikubwa na viongozi wa CCM pamoja na mamia ya wananchi wa wilaya ya Mbinga ambako ndipo alikozaliwa.
Mapunda ameingia Mbinga jana akitokea wilaya ya Nyasa ambapo ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano (5) Mkoani Ruvuma. Ziara ambayo inalenga kukagua na kuhamasisha ujenzi na uimara wa jumuiya mkoani humo pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi ya mwaka 2010-2015.
Katika hotuba yake Katibu Mkuu amewataka wananchi wa Mbinga kujitokeza kwa wingi na kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotegemewa kufanyika mapema mwezi ujao pamoja na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.
Pia Katibu Mkuu, Mapunda amemtembelea Mzee Constantine O. Millinga mmoja wa waasisi kumi na watano (15) walioanzisha Chama Cha Ukombozi cha TANU wakiongozwa na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mnamo tarehe 7.7 1954. Mzee Millinga ni miongoni mwa wawili kati ya waasisi hao ambao wako hai mpaka hivi sasa.
Mapunda ametoa wito kwaWatanzania, wananchama wa Chama Cha Mapinduzi na hasa Vijana wa Taifa hili, kuwaenzi na kuwatembelea wazee ambao ni waasisi, wazalendo wa kweli na wapigania uhuru wa nchi hii, ambao wametuwekea misingi ya Umoja na Utaifa ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya amani na utulivu.
Katibu Mkuu huyo wa UVCCM anaendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambapo atatembelea wilaya ya Namtumbo na baadae Songea Mjini ambako atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika wilaya hiyo ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.

AFRICAN SPORTS YAIADHIBU VILLA SQUAD MKWAKWANI LEO WAIBAMIZA MABAO 2-1

November 23, 2014
KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS WAKIPEWA NASAHA BAADA YA KUMALIZIKA MECHI HIYO LEO

KATIKATI NI THE BIG BOSI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED AURORA NA KULIA NI KOCHA WA VILLA SQUAD HABIBU KONDO NA KUSHOTO NI MTANGAZAJI WA TK FM SAAMAMY MOHAMED

KATIKATI  NI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,HEMED AURORA NA KUSHOTO NI KOCHA WA TIMU YA MGAMBO SHOOTING,BAKARI SHIME NA KULIA NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI LEO
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
MABAO Mawili yaliyofungwa na Hassani Materema kunako dakika za 18 na 79 yalitosha kuweza kuwapa ushindi timu ya African Sports wa Mabao 2-1 dhidi ya Villa Squad katika mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa leo uwanja wa CCM Mkwakwani.

African Sports ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lake katika dakika ya 18 ambalo lilifungwa na Hassani Materema baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Villa Squad  kabla ya Villa Squad kusawadisha dakika ya 36 kupitia Omary Masha.

TImu zote zilikwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote ziliingia uwanjani hapo zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi wa wachezaji wake.

Wakionekana kujipanga vilivyo,African Sports waliweza kuongeza wimbi la mashambulizi langoni mwa Villa Squad na kufanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 79 ambalo likifungwa na Hassani Materema.

MATUKIO YA MECHI KATI YA AFRICAN SPORTS "WANAKIMANUMANU"DHIDI YA VILLA SQUAD YA MAGOMENI DAR ES SAALAM LEO

November 23, 2014










MPAKA SASA NI KIPINDI CHA PILI MATOKEO NI AFRICAN SPORTS 1,VILLA SQUAD 1,MECHI HIYO INACHEZWA UWANJA WA CCM MKWAKWANI.

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO AKISHIRIKI KUHAMASISHA UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE WILAYA HIYO

November 23, 2014
MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO,ALHAJ MAJID MWANGA AKICHANGANYA MCHANGA KWENYE MASHINE YA KUFYETULIA MATOFALI






MKUU WA WILAYA YA LUISHOTO AKISHIRIKI KUANDAA KIWANJA CHA UJENZI.







YULE MTOTO MZURI ALIYETESWA KIKATILI NA HOUSEGIRL HUKO UGANDA!

November 23, 2014

 
Ni habari ya kusikitisha sana kupata taarifa hizi kwa kila mwenye moyo wa binadamu. Mtoto huyu ambaye alioneshwa akiteswa na house girl katika video iliyorekodiwa kwa siri na camera iliyotegeshwa sebuleni bado yupo katika hali mbaya.
Mtoto alivunjika mbavu kutokana na kukanyagwa sehemu ya mbavu zake. Hivi leo tu tulipost video inaonesha jinsi ambayo mtoto huyu alikuwa akilazimishwa kula wakati akilishwa chakula kwa namna ya kikatili, na kishwa kupigwa na kukanyagwa mara tu alipotapika kutokana na kulishwa chakula kingi na kwa haraka.
Hizi ni habari za kusikitisha sana mtoto mzuri kama huyu malaika asiye na makosa kunusurika kukatizwa maisha yake kwenye mazingira kama haya. Mwandishi wetu anazidi kusisitiza juu ya umakini kwa wazazi na walezi wote kuwa makini katika kuwafahamu vizuri watu wanaowaachia watu wanaowaachia majukumu ya kuwalea watoto wao. 
Ni vyema kujipatia uhakika juu ya tabia za wasaidizi hawa wanaofanya kazi ya kushinda na kulea watoto wetu wakati wote ambao tunakuwa katika majukumu mengine ya kila ili kuweza kuendesha maisha yetu. 
Ni kweli kwamba hatuwezi kufanya haya majukumu wenyewe bila usaidizi wa mabinti wa kazi. Wao ni muhimu na msaada mkubwa katika kuhakikisha kwamba watoto wanabaki salama na shughuli nyinginezo zinaendelea kama kawaida katika kuendesha maisha ya yetu na familia kwa ujumla. Lakini imetupasa kuwa makini kutokana na matukio kadhaa ya ukatili wa jinsi hii kwa watoto. Ni vyema kujua kwa undani tabia na mazingia ambayo msaidizi huyu amelelewa na kukua, na kupafahamu mahali anapotokea na ndugu zake.

KINANA ATAKA VIONGOZI KUWAJIBIKA KABLA YA KUWAJIBISHWA

November 23, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia CCM inasimamia uwajibikaji na kama mtu amekosea awajibike na akishindwa atawajibishwa mapema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pongezi vijana Lindi waliojiunga na UVCCM mkoa wa Lindi kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini mkoa Lindi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma Katiba iliyopendekezwa kwa wananchi wa Lindi mjini kuwapa elimu wananchi juu ya mambo ya msingi hasa maadili katika Katiba iliyopendekezwa .

 Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassoro Ally Hamidi akihutubia wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu mkoani Lindi.
Wafanyabiashara ndogo ndogo wakiuza bidhaa zao za vyakula wakati wa mkutano wa CCM kwenye uwanja wa Ilulu.
  Balozi Abdul Mohamed akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye shina lake namba 2 Rahaleo wilaya ya Lindi mkoani Lindi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa shina namba mbili kwa Balozi Abdul Mohamed wa Raha leo ,wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) akiwa ameketi chini na wanachama wa shina namba 2 Raha leo kwa Balozi Abdul Mohamed  wilaya ya Lindi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM akipandisha bendera ya CCM kwenye Shina la wakereketwa la Wanya Kahawa  Lindi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wanachama wa shina la CCM la Wanywa Kahawa Lindi.
 Hii ndio ilivyokuwa mitaa ya Lindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvuvi kwenye mradi wa ufugaji samaki wa ASM Trading 2005 mradi ambao umetoa ajira kwa vijana 10 wa manispaa ya Lindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi wa dini wa mkoa wa Lindi alipotembelea mradi wa ufugaji samaki wa ASM Trading 2005 mradi ambao umetoa ajira kwa vijana 10 wa Manispaa ya Lindi,
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wa CCM wilaya ya Lindi mjini pamoja na wananchi kubeba zege kwa ajili ya kuweka zege ya nyumba ya Mwalimu wa shule ya msingi Nanyanje.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki palizikatika shamba la kikundi cha kuzalisha mbegu bora ya mihogo Chikonji wilaya ya Lindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtaro wa maji kijiji cha Mnazi Mmoja mkoani Lindi

WACHIMBA KISIMA BAADA YA KUCHOSHWA NA AHADI HEWA YA SERIKALI.

November 23, 2014

Na Salum Mohamed,Pangani,
 WAKAZI wa kijiji cha Mkalamo Wilayani Pangani Mkoani Tanga, wamesema wamechoshwa na ahadi ya Serikali kuwachimbia kisima cha maji safi kijijini hapo na hivyo kuadhimia kuchangishana na kuchimba kwa gharama zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa blog hii, wakazi hao walisema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikitoa ahadi  hewa za kuchimba kisima lakini hadi muda huo hakuna dalili zozote za utekelezaji.

Walisema kufuatia kusuasua huko na wakazi wengi  eneo hilo kuteseka kwa kuyafuata maji umbali mrefu na kuamua kuchangishana kwa kila nyumba kuchangia elfu 20 na kufikisha lengo ambalo wamejiwekea.

“Kipindi kirefu tumekuwa tukiahidiwa kuchimbiwa kisima na hata viongozi wa ngazi za juu nao ni wamoja wapo----hadi sasa hakuna dalili ya ahadi hiyo na kuamua ni vyema tukachangishana wenyewe kwa wenyewe” alisema Rashid Sinani

“Kero tunaijua sisi wenyewe na sio wakuja na ndio maana tunataka kuchangishana wenyewe kwa wenyewe---tuko na imani kuwa tutachimba kisima kwa nguvu zetu” alisema Sinani

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Perani, Juma Kolombo amewashauri viongozi wa Serikali za vijiji na vitongoji kuzifikisha kero za wananchi katika ngazi husika na kuacha kuzikalia katika makabati.

Alisema kuna baadhi ya viongozi wengi wanashindwa kuwajibika na badala yake wamekuwa mzigo kwa wananchi na hivyo kuwataka kubadilika vyengine mkakati wa kuwondosha kwa vikao vya vijiji utafuatwa.

“Kuna viongozi wamekuwa mzoigo wanashindwa hata kupeleka barua za wananchi ngazi za juu---hiyo nadhani ni woga wa kupoteza kibarua chake lakini hatambui kuwa ndio kuwajibika” alisema Kolombo

Aliwataja viongozi hao kuwa ni mzigo kutokana na kutofikisha kero zao hata ngazi za kijiji na hivyo kuona kuwa kibarua ambacho wamepewa na wananchi kupitia masanduku ya kura kimewashinda.

Alisema kipindi cha kufanya hivyo ni chaguzi za Serikali za mitaa ambazo ziko karibu na hivyo kuwataka kuwajibika na kuonyesha moyo kabla ya kipindi hicho kufika vyengine wananchi wanaweza kufanya maamuzi tofauti na wanavyofikiria.
chanzo:kumekuchablog

PICHA NNE ZA MKUU WA WILAYA YA MUHEZA AKIKAGUA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NGOMENI HIVI KARIBUNI.

November 23, 2014
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza Subira Mgalu akikahua ujenzi wa maabara shule ya sekondari ya Ngomeni hivi karibuni.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu akikagua ujenzi wa maabara shule ya sekondati ya Ngomeni hivi karibuni.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza Subira Mgalu akilalamika kusuasua kwa ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari ya Ngomeni hivi karibuni.
    MKUU  wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu wa kwanza kulia akizungumza mara baada ya kukagua moja ya jengo la maabara ya sayansi lilipo wilayani humo hivi karibuni,Stoiri Picha kwa hisani ya KumekuchaBlog