December 31, 2013

MAJANGILI WAIBUKA UPYA , MMOJA AKAMATWA NA NYAMA YA SWALA KARIBU NA HIFADHI YA RUAHA IRINGA

Swala   wakiwa katika hifadhi 
WAKATI  taarifa ya wizara ya maliasili  na utalii iliyotolewa na naibu  waziri mwenye dhamana na  wizara  hiyo  Lazaro Nyalandu  kudai kuwa   kumekuwepo na ongezeko kubwa la ujangili wa wanyama katika hifadhi  za Taifa baada ya oparesheni ya  tokemeza ujangili kusimama ,jeshi   la  polisi mkoani Iringa  linamshikilia  mkazi mmoja  wa   kijiji  cha Idodi wilaya ya Iringa  vijijini Bw Kegete Makoga (56)  kwa  tuhuma  za  kukutwa na nyara  za  serikali ambazo ni nyama ya  swala  kilo 8 .

Kamanda  wa  polisi  wa mkoa wa Iringa  Ramadhan Mungi ameueleza  mtandao huu   leo  kuwa tukio  hilo lilitokea  Desemba 29 majira ya saa 3 usiku  katika tarafa ya Idodi  karibu na maeneo ya hifadhi ya Taifa ya  Ruaha .

 Alisema  kuwa  mtuhumiwa huyo  alikamatwa na askari  wa  hifadhi ya   Taifa ya  Ruaha Iringa ambao  walikuwa katika  doria katika  hifadhi  hiyo.

Kamanda  Mungi  aliasema   kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa na  nyama  hiyo ya Swala  baada ya doria ya askari  hao  na kwa  sasa anashikiliwa na jeshi la  polisi  kwa  uchunguzi zaidi kabla ya  kufikishwa mahakamani  kwa kosa la  kukutwa na nyara  za  serikali kinyume na utaratibu.

CHANZO:FRANCIS GODWINBLOG

December 31, 2013


HAFLA YA KUKABIDHI RASIMU YA PILI YA KATIBA
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba mara baaada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Hall kupokea Rasimu ya Pili ya Katiba. Kulia ni Mhe. Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu huku Jaji Mkuu wa Tanzania Bara Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Muungano Mhe Anne Makinda na Spika wa Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho wakisubiri zamu zao
 Rais Kikwete akimuamkia  na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
 Rais Kikwete akimuamkia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya
December 31, 2013

MBUNGE MSINGWA AMCHARUKIA ZITTO KABWE KUWA SI MAARUFU KULIKO CHADEMA ,AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA RASMI YA KATIBA MPYA

Wananchi wa jimbo la Iringa mjini  wakiwa katika mkutano wa mbunge Peter Msigwa leo 

Mbunge wa  jimbo al Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwahotubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini  leo katika uwanja  wa Mwembetogwa .


...................................................................................................
MBUNGE  wa  jimbo la  Iringa  mjini mchungaji peter Msigwa amemshukia  mbunge wa  jimbo  la Kigoma  kaskazin Bw  Zitto kabwe  kuwa  si  maarufu kuliko Chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema)  huku  akiwapongeza  mawaziri  watatu  wa  JK akiwemo naibu waziri wa maji Dr  Binilith Mahenge na waziri  wake  Jumanne Maghembe  kuwa  si mawaziri mizigo ndani ya baraza la   mawaziri wa serikali ya  Kikwete.

 Mbali ya  kuwapongeza  mawaziri hao  pia   mbunge Msingwa amempongeza waziri wa ujenzi Dr John Magufuli  kuwa amekuwa akifanya kazi vema na  kumpongeza Rais Dr Jakaya  Kikwete  kwa kukamilisha mchakato    na msimamo wake juu ya rasmi mpya  ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa  Tanzania.

December 31, 2013

WATAKA KAMATI IWATAJE WABUNGE WANAOHUSIKA NA UJANGILI:IMEWEKWA DESEMBA 31.

embeli1 ddb0a
Wananchi mbalimbali wakiwamo wasomi na wabunge, wamelitaka Bunge kuweka wazi majina ya wabunge waliotajwa kuhusika na vitendo vya ujangili wa wanyamapori. (HM)

Wakati akiwasilisha taarifa ya Kamati ndogo ya Uchunguzi ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili, Mwenyekiti wake, James Lembeli alisema baadhi ya wabunge walitajwa kujihusisha na ujangili.
December 31, 2013

TFF KUTOA ELIMU KWA MASHABIKI JUU YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Benki ya CRDB, wamejipanga kutoa elimu kwa mashabiki wa soka nchini juu ya mfumo mpya matumizi ya tiketi za Kielektroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika rasmi katika raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

CRDB ndio wazabuni walioshinda tenda ya kuuza aina hiyo ya tiketi, ambazo mpaka sasa zimeanza kufanyawiwa majaribio ya mauzo katika mechi ya Azam FC, dhidi ya RuvuShooting kwenye Uwanja wa Chamazi wiki iliyopita.
December 31, 2013

Maajabu, jamaa apanda juu ya mnara akishinikiza kuonana na Rais Kikwete


 Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo
December 31, 2013

MISS TANZANIA 2013 KULA MWAKA MPYA 2014 NA YATIMA WA NIRA MBAGALA

Kama tulivyotoa taarifa kwa vyombo vya habari hapo awali   wakati wa Sikukuu ya Noel [Christmass ] Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa, baada ya kujumuika na watoto waishio katika mazingira magumu kule Bigwa Morogoro katika Kituo cha Mgolole,
 
Mrembo huyo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tatu   Clara Bayo, kukabidhi misaada ya kijamii pamoja na kushereheka nao pamoja wakati wa Sikukuu ya Mwaka mpya tarehe 1 Januari 2014, katika kituo kiitwacho Nira Children and Youth Orphans Foundation kilichopo eneo la Mbagala Nzasa A, kwa mzungu kaburi moja, Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke.
 
Miss Tanzania pamoja na warembo wenzake, watakabidhi misaada hiyo ya vyakula, ikiwa ni pamoja na vifaa vya shule, kama vile Madaftari, kalamu,  vitabu n.k.
 
 
Wakati huo huo Mrembo wa Kanda ya Mashariki Diana Laizer, kutoka Mkoa wa Morogoro, nae atakabidhi misaada kama hiyo katika Kituo cha Amani kilichopo Manispaa ya Morogoro, pamaja na kushereheka nao katika Sikukuu hii ya Mwaka mpya 2014.
December 31, 2013

KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA PAMOJA NA NAIBU WAKE LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU
December 31, 2013

SIMBA SC WAKIWA SAFARINI ZANZIBAR KUFUATA 'NDOO' YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

Wachezaji wa Simba SC wakiwa eneo la bandari ndogo, Azam Marine, Dar es Salaam wakielekea kupanda boti asubuhi hii tayari kwa safari ya Zanzibar kwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi, michuano inayoanza kesho visiwani humo.
Kulia Said Ndemla 'Ozil', kushoto Nassor Masoud 'Chollo' na katikati Ramadhani Chombo 'Redondo'. Michuano ya mwaka huu itakwenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Supa staa; Ramadhani Sngano 'Messi' hakuwa na sare ya timu kama wenzake
Nahodha Chollo kushoto akimpa tiketi yake beki Mganda, Joseph Owino. Wengine kulia ni Daktari, Yaasin Gembe na Kocha Msaidizi, Suleiman Matola kushoto
Chollo akimpa tiketi Amri Kiemba
Kulia Redondo, katikati kocha wa makipa Iddi Pazi 'Father' na kushoto mshambuliaji Ali Badru
Kipa Yaw Berko akiikagua tiketi yake baada ya kukabidhiwa na Nahodha Msaidizi, Haruna Shamte kushoto
December 31, 2013
SIMU ZAO HAZIPATIKANI TANGU ASUBUHI
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
RASMI. Yanga SC imejitoa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, kwa sababu timu yao haina benchi la Ufundi, baada ya kufukuzwa kwa Kocha Mkuu, Ernie Brandts.
Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY muda huu kwamba, uongozi umefikia hatua hiyo kwa sababu bado hawajapata benchi jipya la Ufundi.
Kikosi cha Yanga kilichofungwa 3-1 Kombe la Mapinduzi 

Yanga SC ilikuwa imepangwa Kundi C la michuano hiyo inayoanza kesho pamoja na Spice Star, Azam FC na Tusker ya Kenya- maana yake kwa kujitoa kwao, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kitalazimika kupanga upya Ratiba yake au kuiingiza timu nyingine katika nafasi ya mabingwa hao wa Bara.
Mapema jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Mussa Katabaro aliiambia TANGA RAHA kwamba wanachelewa kwenda Zanzibar kwa sababu hawajapata mwaliko na waliwaandikia barua ZFA juu ya hilo, lakini hadi sasa hawajapata majibu.
December 31, 2013

SSRA YAJADILIANA NA JUKWAA LA WAHARIRI KUHUSU MPANGO MKAKATI WA KUPANUA WIGO WA HIFADHI YA JAMII KUPITIA ELIMU KWA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akiwasilisha mada kuhusu hali halisi ya sekta ya hifadhi ya jamii nchini changamoto na mafanikio


Baadhi ya wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakisiliza mada ikiwasilishwa na mkurugenzi mkuu wa SSRA (hayupo pichani)

Mhariri mkuu wa gazeti la Nipashe Bwana Jesse Kwayu akiuliza swali mara baada ya uwasilishwaji mada

Bi.Irene Isaka Mkurugenzi mkuu  wa SSRA akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa Wahariri,kulia kwake Mkuu wa mawasiliano na uhamashishaji wa SSRA  Bi. Sarah Kibonde – Msika

Bi Irene Isaka Mkurugenzi Mkuu wa SSRA akisisitiza juu ya umuhimu wa vyombo vya habari katika kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi,kushoto kwake Bwana Absalom Kibanda ambaye ni mkuu wa Jukwaa la Wahariri nchini na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasilianao na uhamashishaji wa SSRA Bi. Sarah Kibonde –Msika .