MKUU WA WILAYA YA MONDULI, NDUGU IDD KIMANTA AWATAKA WANANCHI KUTUMIA HUDUMA ZA KIBENKI

November 01, 2017

Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Idd Kimanta(kushoto) akizungumza na Mameneja wa benki ya NMB mara baada ya kuwasili eneo la Mto wa Mbu kufungua tawi jipya litakalowahudumia wanaochi na taasisi mbalimbali,kutoka kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini,Saria Mlay,Meneja wa tawi la Mto wa Mbu,Happiness Patrick,Meneja wa tawi la Clock Tower,Manyolizu Masanja ,Meneja wa tawi la Business Center,Said Parseko na Meneja wa tawi la Karatu,Elizabeth Chawinga
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Idd Kimanta  akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi la benki ya NMB eneo la Mto wa Mbu ambalo linachangia asilimia 70 ya mapato yote ya wilaya hiyo.
Baadhi ya mameneja waliohudhuria uzinduzi wa tawi la Mto wa Mbu wilayani Monduli.
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Idd Kimanta  akizindua tawi la benki ya NMB eneo la Mto wa Mbu kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini,Saria Mlay na Meneja wa tawi hilo,Happiness Patrick.
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Idd Kimanta  akipata huduma za kibenki kwenye tawi jipya baada ya uzinduzi

SERIKALI YATAIFISHA NG’OMBE 6648 MISENYI KAGERA

November 01, 2017
Waziri Mpina katika Picha akivua samaki aina ya kambale alipotembelea Mradi wa mabwawa ya samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
 Aliyeshika Samakai aina ya Sato ni Waziri Mpina alipotembelea Mradi wa Mabwawa ya Samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misenyi mara baada ya zoezi la kutaifisha ng'ombe.

NA MWANDISHI MAALUM MISENYI
Akiwa katika muendelezo wa ziara zake za operesheni  kamata mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina Ameagiza kukamilisha taratibu za Uhamiaji na Mahakama kupitia mwanasheria mkuu wa Serikali wa Wilaya ya Misenyi Pamoja na Uhamiaji, ili kuweza kupigwa mnada kwa idadi ya ng’ombe 6648 walioingia nchini kinyemela toka nchi jirani ya Uganda na kukamatwa.
Waziri mpina alisema uvamizi wa kundi kubwa kama hilo la wanyama linaweza kusabisha madhara makubwa katika mazingira kama vile mmomonyoko wa ardhi, kuharibifu wa vyanzo vya maji, kumaliza malisho ya mifugo iliyoko nchini, kusababisha migogogoro ya mara kwa mara kwa wakulima na wafugaji na hata kuleta maambukizi ya magonjwa ya wanyama.
“Sisi kama Serikali hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee na mimi kama Waziri Mwenye dhamana nina jukumu la kuhakikisha tunalinda lasimali hii ya malisho” Alisema Mpina.
Mpina alisema suala hili haliingiliani na Ushirika wa Afrika Mashariki kwani Ushirika huo upo kisheria hivyo wavamizi wanaoingiza mifugo kinyemela nchini toka nchi jirani ni wahalifu kama wahalifu wengine.
“Kwa hiyo naangiza ng’ombe hawa 6648 waliokamatwa hatua ziendelee na ambao hawajakamatwa wakamatwe na wataifishwe na Serikali.”Alisisitiza Waziri Mpina.
Kwa upande wa upande wake mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Denis Mwila alisema kuwa zoezi la kutathmini ng’ombe katika wilaya yake bado linaendelea na taratibu za kisheria zinafuatwa.
Alipokuwa Mkoani Kagera Mapema jana Mpina  alitembelea mabwawa ya mradi wa  samaki yaliyopo Wilayani Muleba katika kijiji cha Luhanga na kusema Serikali ina nia ya kukomesha kabisa uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wavuvi haramu kule waliko na  kuwa na nyenzo.
Aidha, akiwa Bukoba Mjini Mpina alitembelea kiwanda cha kuchakata samaki cha Suprime Fish Ltd na kuagiza wamiliki wa viwanda vya samaki nchini kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kufufua viwanda hivyo na kuongeza uzalishaji kwani Serikali imeshaanza kuchukua hatua ya kuhakikisha samaki wanapatikana kwa wingi nchini.

DC WILAYA YA NYANG'WALE ASEMA BILA YA KUWEPO USALAMA WA CHAKULA NCHINI HAKUNA KITAKACHOWEZA KUFANYIKA

November 01, 2017
 Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita
 Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoa wa Geita,  Hamim Buzohera Gwiyama (katikati), akizungumza na watafiti wa kilimo kutoka  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Ukiriguru Mwanza, Ilonga mkoani Morogoro na Waandishi wa Habari kabla ya kukabidhiwa mbegu bora za mahindi na mhogo kwa ajili ya kuzipanda kwenye mashamba darasa katika vijiji vinne wilayani humo leo hii. Kulia ni Diwani wa Kata ya Nyugwa, Ndozi Manual na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Fabian Sospeter ambaye alikabidhiwa mbegu hizo na kuhutubia wananchi kwa niaba ya mkuu huyo wa wilaya.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu katika mashamba darasa uliofanyika Kata ya Nyugwa wilayani humo.
 Diwani wa Kata ya Nyugwa, Ndozi Manual, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Fabian Sospeter, akihutubia wananchi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi, akimkabidhi mbegu ya mhogo aina ya Mkombozi Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Fabian Sospeter kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo.
 Mtaalamu wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, akiwaelekeza wananchi wa Kata ya Nyugwa jinsi ya upandaji wa mbegu ya mhogo aina ya Mkombozi kwenye shamba darasa.

Tunakumbushana #SiUchochezi (Kipindi cha kwanza)

November 01, 2017
Kipindi cha Tunakumbushana #SiUchochezi ni kipindi kipya cha kila wiki kinacholenga kuibua na kuonyesha masuala mbalimbali katika jamii ambapo kitakuwa katika mfumo wa sauti, picha mnato pamoja na picha jongefu (video).

Kipindi hiki kimejikita kukosoa, kuonya na kusifia masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii yakiwemo ya kiutendaji, kisiasa, kiuchumi pamoja na kijamii nchini Tanzania.

Kinaandaliwa na kurushwa na mitandao ya kijamii ya Binagi Media Group (www.bmghabari.com) pamoja na mitandao mingime rafiki kote nchini, lengo likiwa ni kuamsha ari ya kimaendeleo katika jamii.

MPANGO WA UENDESHAJI WA KIJINSIA KWA AJILI YA MWITIKIO WA UKIMWI TANZANIA BARA WATAMBULISHWA RASMI KWA MKOA WA SINGIDA

November 01, 2017
 Mratibu wa Jinsia kutoka TACAIDS Jacob Kayombo na Afisa Jinsia kutoka TACAIDS Judith Luande wakijadili baadhi ya maoni, maswali na mapendekezo ya wajumbe ambao ni timu ya kudhibiti Ukimwi ya Mkoa wa Singida wakati wa Mafunzo juu ya mpango wa uendeshaji wa kijinsia.
Mjumbe wa mafunzo juu ya mpango wa uendeshaji wa kijinsia Afisa wa Serikali za Mitaa Hussein Mwatawala akipitia fomu zitakazotumika katika kukusanya taarifa za masuala ya Kijinsia mkoani Singida.

Serikali kupitia Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeandaa Mpango wa uendeshaji wa Kijinsia kwa ajili ya mwitikio wa Masuala ya Ukimwi ambao umetambulishwa rasmi kwa timu ya Kuthibiti Ukimwi Mkoani Singida.

Mratibu wa Jinsia Kutoka TACAIDS Jacob Kayombo ameongoza mafunzo hayo kwa timu ya kuthibiti Ukimwi Mkoa wa Singida ambapo amewaeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuratibu na kutoa dira katika utekelezaji wa program mbalimbali za Ukimwi kwa ngazi ya Mkoa.

Kayombo amesema Mafunzo hayo yamelenga kuutambulisha mpango huo pamoja na fomu zitakazotumika katika ukusanyaji wa taarifa zihusuzo jinsia na Ukimwi.

“Mafunzo haya tunayotoa yamejikita katika kuufafanua mpango huu utakavyotumika pamoja na namna ambavyo fomu hizi zitatumika kukusanya taarifa za jinsia na Ukimwi kwa Mkoa wa Singida na jinsi ambavyo taarifa hizo zitasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu masuala ya Ukimwi”, amesema Kayombo.

Ameongeza kuwa matarajio yanayotegemewa baada ya mafunzo hayo kutolewa ni kuona masuala yote ya kijinsia yanapewa kipaumbele katika program mbalimbali za Ukimwi.

Kayombo amesisitiza kuwa mpango huu utakuwa ni mwongozo wa wadau wa masuala ya Ukimwi ili waweze kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia usawa wa kijinsia hasa katika kuweka mikakati ya kuthibiti Ukimwi yenye uelekeo wa Usawa wa kijinsia.

MAJABA ALIVYOPOKELEWA KWENYE NYUMBA YAKE BUNJU B JIJINI DAR

November 01, 2017
Nyumba iliyopo Bunju B ilivyokuwa kabla ya makabidhiano jana. Mkurugenzi wa Mkuu wa Global Group, Eric Shigongo (wa kwanza kulia) na George Majaba (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho wakijadiliana jambo kabla ya makabidhiano jana. ... Shigongo akizungumza machache mbela ya nyumba hiyo kabla ya kumkabidhi George Majaba jana. Mara baada ya kukata utepe, Shigongo akifungua nyumba hiyo. Ndani ya nyumba kushoto, George Majaba, Afisa Masoko, Jimmy Haroub, Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo, mke wa Majaba, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho na Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli wakifurahia mandari ya nyumba. George Majaba akiwa na majirani zake wapya wa Bunju B kwenye nyumba yake mpya, hapo walikuwa wakimkaribisha. ...Majaba akizungushwa kuoneshwa mandari ya nje ya nyumba yake mpya. 
Msafara wa magari ukiongozwa na pikipiki zaidi ya tano ulitokea makao makuu ya Global Group Sinza Mori Dar, huku Mshindi wa Shindano la Nyumba Awamu ya Pili, George Majaba akiwa kwenye gari la wazi aina ya BMW huku mke wake akiwa kwenye gari lingine na watoto wao . Msafara ulipita Barabara ya Shekilango, ukaingia Barabara ya Ali Hassani Mwinyi kisha ukaingia New Bagamoyo, njiani kwa kuwa kulikuwa na gari la matangazo, watu walikuwa wamejipanga kumshuhudi Majaba aliyejawa na tabasamu akipita akiwa kwenye gari hilo la wazi.   Msafara ulipofika Tegeta umati ulikuwa mkubwa na wengi waliokuwa wakimuona Majaba walikuwa hawaamini macho yao kwani yeye mshindi alikuwa akiwapungua mkono na msafara ukawa unaenda kwa mwendo wa polepole, hali iliyofanya baadhi ya wananchi kumkaribia mshindi na walisikika wakisema ‘Hongera, Hongera!”   Lakini abiria waliokuwa kwenye mabasi ya daladala nao walionekana wakitoa vichwa vyao madirishani na kumpongeza Majaba ambaye mara zote alikuwa na tabasamu usoni.   Hali ilikua hivyo hivyo msafara ulipofika Boko na baada ya kufika Bunju msafara ulisimama kabla ya kuingia Barabara ya Mabwepande ambapo kwa mwendo mfupi tu msafara uliingia kwenye nyumba mpya ya Majaba.   Mara baada ya kufika, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho alitambulisha kwa wageni na wenyeji waliofika kushuhudia makabidhiano hayo na kisha akampa nafasi Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo kusema machache.   “Kifupi leo tunamkabidhi nyumba yake Bwana Majaba. Ni jambo linalofurahisha kuona yupo hapa na familia yake ya mke na watoto watatu, hivyo bila kupoteza muda karibuni tufungue nyumba,” alisema Shigongo.   Baada ya kusema maneno hayo Shigongo, Majaba na mkewe walishika utepe na Shigongo akaukata kuashirika kuwa sasa wamekabidhiwa nyumba yao.   Baadaye Majaba na watu wengine wakiongozwa na Shigongo waliingia ndani na kuoneshwa kila chumba, baadaye nje na uani ambako kulikuwa na nafasi kubwa na Shigongo alimuambia mke wa Majaba kwamba eneo hilo anaweza kufanyia miradi kama ya kufuga. Wenyeji walimkaribisha Majaba na baadaye wakapiga picha ya pamoja huku wakimpongesha kwa kushinda nyumba hiyo. Shughuli hiyo iliisha saa moja kasoro robo jioni. HABARI NA ELVAN STAMBULI, PICHA MUSSA MATEJA.  

HITILAFU YA MFUMO WA KUPOKELEA GESI KINYEREZI I, TATHIMINI YAONYESHA MATENGENEZO MAKUBWA YANAHITAJIKA, MAFUNDI WAKO KAZINI: TANESCO

November 01, 2017
Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TANESCO


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
TATHMINI iliyofanywa na Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kufuatia mfumo wa kupokea gesi asili kwenye mitambo ya kufua umeme, Kinyerezi I jijini Dar es Salaam kupata hitilafu, imebaini matengeenzo makubwa yanahitajika kufanyika ili kuhakikisha mfumo unarudi katika ubora wake..
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, iliyosambazwa kwa vyombo vya habari leo Novemba 1, 2017, imesema kufuatia mfumo huo kupatwa na hitilafu majira ya mchana Oktoba 32, 2017, hatua ya kwanza iliyochukuliwa na wataalamu wa TANESCO ni kuzima mitambo ili kuruhusu kazi ya usafishaji kuondoa gesi hiyo kufanyika.
”Baada ya usafishaji wa Mitambo kukamilika, matengenezo yalianza usiku wa kuamkia leo Novemba 1, 2017, kwa kutumia wataalamu wa ndani wa Shirika pamoja na Mkandarasi wa kampuni ya JACOBSEN ELEKTRO AS.” Taarifa hiyo ya TANESCO ilisema.
Taarifa hiyo iliendelea kusema, “Kutokana na ukubwa wa matengeenzo na uangalifu wa hali ya juu unaotakiwa katika kazi hii hususan suala la usalama wa mitambo pamoja na watumishi wa Shirika waliopo katika eneo la mitambo, hatua za tahadhari zimechukuliwa.” Taarifa hiyo ilisema.
Aidha taarifa imefafanua kuwa kutokana na Mitambo hiyo kuzimwa ili kuruhusu kazi ya marekebusho ya hitilafu hiyo kukamilika kwa wakati, kutakuwa na upungufu wa umeme katika maeeno mbalimbali ya nchi.
“Uongozi wa Shirika unawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa ujumla kwa maeneo ambayo bado yanakosa huduma ya umeme katika kipindi hiki cha matengenezo hayo na tutaendelea kuwaarifu wananchi jinsi kazi ya matengenezo inavyoendelea hadi kukamilika kwake.” Taarifa hiyo ilisema

MSHINDI WA NYUMBA ATIKISA DAR, MAPOKEZI YAKE SI YA KITOTO

MSHINDI WA NYUMBA ATIKISA DAR, MAPOKEZI YAKE SI YA KITOTO

November 01, 2017
Wafanyakazi wa Global Groups Ltd wakijiandaa kumpokea Mshindi wa Nyumba, George Majaba aliyewasili Dar es Salaam kutoka Dodoma.[/caption] GEORGE Majaba, mshindi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, Jumanne Oktoba 31, 2017 amewasili jijini Dar es Salaam tayari kwa zoezi la kukabidhiwa nyumba yake aliyojishindia baada ya droo kubwa iliyochezwa Septemba 27, mwaka huu.   Majaba akiwasili kwenye ofisi za Global.[/caption] Katika mapokezi hayo yaliyopambwa kwa pikipiki, gari la wazi, muziki na madansa, Majaba aliwasili katika ofisi za Global Group, zilizopo Sinza Mori mishale ya saa tisa na ushee hivi na kupokelewa na wafanyakazi ambao walimpigia makofi ya shangwe na baadaye kumwimbia nyimbo ya kumsifu kwa ushindi.   Majaba akisalimiana na Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Groups Ltd, Eric Shigongo, kushoto ni Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho.[/caption] Mara baada ya kukaribishwa katika ukumbi wa mikutano wa kampuni, Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho alimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji Eric Shigongo ambaye baada ya kumkaribisha Majaba na mkewe, Neema, alimshukuru Mungu kwa ndoto zake kutimia.   Wafanyakazi wa Global wakiwalaki majaba na mkewe baada ya kuwasili ofisini hapo.[/caption] “Siku zote nimekuwa nikiomba Mungu kuwa zawadi hizi tunazotoa, zifike kwa watu wenye uhitaji, tunapotoa zawadi ya nyumba, niliomba iende kwa mtu mwenye uhitaji wa nyumba kweli, kwa sababu tunataka kubadilisha maisha ya watu.   Majaba akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za Global.[/caption] “Niwe mkweli, kama zawadi hii angeipata mtu ambaye tayari ana nyumba tano, nisingefurahi kabisa, lakini kwa mujibu wa makala zako nilizokuwa nasoma, wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga, kwa maana hiyo siku zote ulikuwa ukiomba upate nyumba na leo Mungu amekubariki.  Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho akizungumzia shughuli nzima ya Shinda Nyumba ilivyofanikiwa pamoja na kumpongeza mshindi.[/caption] “Wewe utakuwa balozi mzuri wa Global Group kwa sababu watu wengi wamekuwa wakisema kuna ujanjaujanja katika zawadi, nina uhakika kabla ya leo hakukuwa na mtu yeyote unayemjua hapa, lakini wewe umejikuta ukipata nyumba. Tunakukaribisha sana na asante Mungu kwa ndoto zetu kutimia,” alisema. Eric Shigongo akimpongeza mshindi na kutoa maelezo mafupi kuhusu Shinda Nyumba.
  Baada ya kukaribishwa na kuzungumza machache na wafanyakazi na baadaye kutembezwa katika vitengo mbalimbali vya Global Group, Majaba na familia yake waliondoka kuelekea Bunju B, ambako ndipo ilipo nyumba yake ya kisasa na hivyo kuwa miongoni mwa wamiliki halali wa nyumba za kisasa katika Jiji la Dar es Salaam. Majaba akielezea furaha yake baada ya kushinda nyumba mpya. Mke wa Majaba naye akifunguka. Wakiwa kwenye Ofisi ya Mhariri Mtendaji, Saleh Ally (wa kwanza kulia).

RAIS KARIA AWAPA POLE SILABU

November 01, 2017
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ametuma salamu za pole kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Athuman Kambi kufuatia ajali ya gari iliyopata timu ya Silabu ya Mtwara.
Gari iliyowabeba wachezaji wa Silabu – mabingwa wa Mkoa wa Mtwara ilipata ajali maeneo ya Mchinga mkoani Lindi wakiwa safarini kwenda Pwani kucheza na Kisarawe United katika mchezo wa awali wa kuwania Kombe la Shirikisho la Azam.
Hakuna aliyefariki, lakini majeruhi 12 wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi.
Mchezo huo ulipangwa ufanyike kesho Alhamisi Novemba 2, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi, mkoani Pwani, lakini umeahirishwa hadi hapo utakapotangazwa tarehe mpya.
Rais Karia amesema kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi hao kupona haraka ili kurejea kwenye majukumu yao ya kawaida hususani mpira wa miguu.
“Mungu awafanyie wepesi,” amesema Rais Karia.
Wakati TFF ikiendelea kusubiri taarifa nyingine, taarifa za awali zinasema msafara ulikuwa na wachezaji 18, benchi la ufundi watano na viongozi watatu. Kulikuwa na taratibu za kuhamisha majeruhi katika Hospitali ya Nyangao.

KAMPENI YA WANAWAKE NA ARDHI YAZIDI KUWAFIKIA WATU WENGI ZAIDI

November 01, 2017
Katika kuendelea na kampeni ya Wanawake na Ardhi wadau mbalimbali wamekutana jijini Dar es salaam kujadili juu ya 'Nafasi ya Wanawake katika Michakato ya usimamizi wa ardhi' warsha iliyowahusisha wawakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Mashirika na wawakilishi wa wakulima na wafugaji.
Kwa ujumla warsha hiyo ililenga malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kuelewa michakato ya mabadiliko mbalimbali ya taratibu za usimamizi wa Ardhi(Mfano marejeo ya sera ya Taifa ya ardhi) na athari chanya au hasi kwa wanawake wa Tanzania,kusambaza ujumbe wa kampeni ya wanawake na ardhi kama ulivyokusanywa kutoka kwa wadau ambao ni wakulima wadogo wanawake,wafugaji na mashirika mbalimbali, pia kupata fursa ya kuipatia Serikali maoni ya wanawake katika marejeo ya sera ya ardhi ya Taifa.

 Bi. Wiyagi Kisandu kutoka WLAC akitoa mada juu ya uelewa wa maswala ya kijinsia kwa jamii na wanawake kwa ujumla, ambapo alisema kuwa ni muhimu Serikali na wadau wengine washirikiane kuwapa elemu ya haki miliki ya ardhi ili iwe rahisi hata kipindi cha mchakato wa kushughulikia kupata hati hizo uwe rahisi.
 Bi. Naomi Shardrack Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam akielezea kuhusu dhana ya kuwawezesha wanawake kumiliki rasilimali ardhi, pia alielezea utafiti wa maswala ya umiliki wa ardhi uliofanywa na shirika la Oxfam na namna mifumo dume inavyo wakandamiza wanawake katika kumiliki Ardhi.
 Bw. Stephano Mpangala kutoka RUDI akielezea kisa mkasa kilichohusu mzee Kuzenza Magoso(80) ambaye alikuwa na wake sita(6), kwa kutambua umuhimu wa hati milki ya ardhi aliwapatia  wake zake wote hati za kumiliki ardhi ili kuondoa migogoro ambayo ingeweza kujitokeza mbeleni.
Bi.Elisa Simioni   Aliyewahi kushiriki shindano la Mama wa chakula linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la  Oxfam Tanzania akieleza kisa mkasa cha  namna akina amama  walivyoweza kushiriki kikamilifu katika kupigania na kurejesha msitu  kijijini kwao ambao ulivamiwa na kutumika vibaya
 Bw. Adam Ole Mwarabu akielezea zaidi juu ya Kisa mkasa alichozungumzia Bi. Elisa Simion kuhusu uharibifu wa misitu na kusisitiza kuwa licha ya akina mama hao kupigania msitu isiharibiwe, lakini pia akina mama takribani 100 walikwenda kulala katika msitu huo kwa lengo la kuonesha kuwa hawakufurahishwa na uharibifu huo, na mpaka sasa hakuna tena wavamizi katika eneo hilo.
 Bi. Rehema Abdallah mhamasishaji wa umiliki wa ardhi kwa wanawake, alisema kuwa wao wapo tayari katika kushiriki kuchangia gharama za mchakato wa kuhakikisha wanapata hati miliki za ardhi kwa kuwa ni kitu cha muhimu.
 Mh. Yannick Ndoinyo  Diwani wa kata ya Ololosokwani- Longido akielezea namna wakina mama walivyopewa nafasi kubwa katika kumiliki ardhi.
 Dr. Adam Nyaruhume Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro, alieleza kuwa ni muhimu kuwajulisha na kuwaelimisha wanakijiji hasa kuhusiana na maswala ya mipango na matumizi ya ardhi pamoja na umilikishwaji wa ardhi, pia aliwapongeza Asasi ya RUDI kwa kufanya vizuri katika mipango na matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali wanayoyashughulikia.
 Bw. Joseph Rutaizibwa, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi akitoa ushauri kuwa Baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi kiuchumi lishirikishwe katika michakato hii muhimu inayohusu maswala ya ardhi.
 Bi. Eva Mageni akielezea changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo wanawake hasa katika umilikishwaji wa ardhi.
 Bi. Rosada Msoma Afisa Maliasili Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,alisema kuwa Wizara inatoa ushirikiano wa karibu kwa wananchi katika kuhakikisha kuna utunzaji bora wa maliasilizetu.
 Wawakilishi mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi,Wizara ya Kilimo,Wizara ya Mifugo, Wawakilishi wa wakulima na wafugaji, Asasi za Kiraia za Nchini pamoja na za kimataifa,na wadau wengine wakiwa katika makundi mbalimbali kujadili mipango mikakati ya kuendeleza haki za wanawake katika rasilimali ardhi nchini
 Bi. Anne Manangwa Mtafiti kutoka TNRF akitoa mapendekezo kwa niaba ya Asasi za Kiraia ambapo kati ya mambo waliyo omba yafanyiwe kazi katika kampeni  ya wanawake na ardhi ni pamoja na, Elimu itolewe kwa njia ya vyombo vya habari juu ya kumiliki ardhi, haki za wanawake katika kumiliki ardhi pamoja na ushirikishwaji wa wanawake katika kuandaa Sera,uandaaji wa mikakati pamoja na kutunga Sheria.
 Bi. Marcelina Kibena Mwakilishi kutoka MVIWATA, wao katika kikundi chao walitoa maoni kuhusu kutambua makundi mbalimbali kupitia elimu itasaidia kuondoa mfumo dume,kuhamasisha wanawake katika kushika nyadhifa mbalimbali za maamuzi, vyombo vya habari kuandaa programu mbalimbali za uelewa kuhusu kumiliki ardhi na mgawanyo wa rasilimali kuanzia ngazi ya kijiji.
Wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Care International,WLAC,PINGOs,UCRT,FFH,LANDESA,PWC,NES
na ILRI pamoja na waendeshaji wa kampeni hiyo Shirika 
la Kimataifa la Oxfam Tanzania pamoja na TALA wakiwa katika warsha hiyo .