UFUNGUZI WA UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO WAFANYIKA ZANZIBAR

September 10, 2017

Na Khadija Khamis –Maelezo

Jamii inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na meno ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya angalau mara mbili kwa mwaka .

Hayo aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .

Alisema afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza meno .Alifahamisha kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .

Aidha alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na vijijini .

“Huu usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.

Alieleza kutoa elimu na uchunguzi wa afya kwa jamii itasaidia kupunguza gharama za matibabu na kuimarisha kinga ya awali na kujiepusha na matumizi ya vyakula ambavyo vinachangia kuleta madhara ikiwemo vyakula vya sukari kuchangia uozeshaji wa meno hasa kwa watoto .

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno ( TBA) Dr Lorna Carneiro alisema mara hii wamepata fursa ya kuja Zanzibar kwa kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ili kujua wale wagonjwa  ambao wanamatatizo na kuwapatia tiba pamoja na kuwapa elimu ya afya .

Alisema Chama hicho kinahimiza umuhimu wa afya bora kwa jamii na kutoa ushauri wa maradhi mbalimbali ikiwemo ukimwi ,saratani ,Kifua kikuu,afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza kwa kuifanya jamii ipate uelewa na kujikinga na maradhi ambayo yanauwezo wa kuepukika .

“Hali ya idadi ya Wagonjwa ni kubwa wakati ya kuwa magonjwa haya yanakingika kwa haraka na kupona lakini kikwazo ni kuwa na uchache wa madaktari ,“alisema Dr Lorna .

Alifahamisha kila ifikapo tarehe 20 machi ya kila mwaka huadhimisha siku ya afya ya kinywa na meno kwa mwaka ujao wanatarajia uzinduzi wa zoezi hilo litafanyika Zanzibar .

Nae Mgonjwa BI Nargisi Uzia ambae alifika kupatiwa huduma ya matibabu katika kituo hicho alisema anaishukuru Serikali kwa kuwaletea wataalamu wa kuchunguza afya zao lakini pia iko haja ya zoezi hilo liwe endelevu kwani matatizo yako mengi yanahitaji uchunguzi.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt,Ismail Amour akitoa Elimu ya kujikinga na maradhi hayo katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.


Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kushoto akifanya mahojiano na Muandishi wa Habari kutoka ITV Farouk Kariym pamoja na muandishi wa Habari Maelezo Zanzibar Khadija Khamis katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.

Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Haspitali ya Arrahma Zanzibar akimfanyia Uchunguzi wa mardhi ya Kinywa na Meno Kauthar Vuai mkaazi wa meli nne, katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

NEW AUDIO : LOD VEE - DELETE MASNITCH ft. PIELINA (Free Download & Listern)

September 10, 2017
YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


IN A SINGLE CLICK
PAKUA NA KUSIKILIZA WIMBO KWA KUFUATA LINK HAPA CHINI:

Image result for DOWNLOAD BUTTON

DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI

September 10, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam
 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu leo Septemba 10, 2017 amefanya kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani ili kuwaeleza dhamira ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kukuza ufanisi na kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo.

Katika kikao hicho wadau wamechangia jumla ya shilingi milioni 3,900,000 ikiwa ni ahadi, Mifuko 100 ya saruji na rasilimali hamasa kwa vijana wa waliohitimu masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali nchini watakaojitolea kufundisha katika shule zenye upungufu wa walimu sayansi katika Wilaya ya Ikungi.

Mhe Mtaturu amewaeleza washiriki wa kikao hicho namna ambavyo Uongozi wa Wilaya umejipanga kwa kuhusisha michango ya wadau na nguvu za wananchi kwa ujumla kwa kuchangia rasilimali fedha ama viwezeshi kama vile saruji, mchanga, kokoto na vitu vifaa vingine vya ujenzi.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Lamada Hotel Jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Mwalimu Athumani Salum ambaye ni Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Mtaturu alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Wilayani Ikungi ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

Mhe Mtaturu aliwaeleza wadau hao wa Mfuko wa elimu kuwa Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu lilitokana na kikao cha wadau wa elimu alichokiitisha mwezi Disemba, 2016 na kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari.

Alisema Kikao hicho kuliadhimiwa maazimio 43 ambayo yalizaa wazo la kuanzisha mfuko wa elimu ambapo wazo hilo lilifikishwa kwenye baraza la madiwani na kupokelewa kwa kauli moja ndipo mwezi Aprili mwaka 2017 baraza liliridhia kuanzishwa mfuko na kuteua wajumbe 15 wa bodi ya mfuko wa elimu wa Wilaya ya Ikungi.

Mhe Mtaturu alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto zote hizo Bodi ilibainisha kuhitajika jumla ya fedha taslimu shilingi bilioni 28.

Hata hivyo Baada ya vikao mbalimbali vya maamuzi Bodi ya mfuko wa elimu imebainisha  mpango mkakati wa miaka mitatu kwa mtazamo wa Shule zenye hali mbaya zaidi hivyo kuandaa makadirio ya gharama za shilingi Bilioni 3.

Mhe Mtaturu alisema kuwa ili kufanikisha mpango huu kwa wakati husika Bodi ilitoa mapendekezo ya wadau watakoombwa kuchangia mfuko ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  kuchangia 3% ya mapato yake ya ndani.

Sambamba na hayo pia alielezea mikakati mbalimbali katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kilimo ambapo alisema wananchi wengi wanafanya kilimo cha kujikimu badala ya kilimo cha biashara hivyo ili kukuza ufanisi wa pato la mkulima Uongozi wa Wilaya ya Ikungi umekusudia kutatoa miche ya mbegu za korosho 500,000 bure kwani ni zao rahisi kulima lisilohitaji uangalizi wa muda mrefu.

Alieza pia namna Wilaya hiyo ilivyojipanga katika sekta ya Afya, Miundombinu, Sekta ya Maji, na kuimarisha hali ya usalama ili wananchi kufanya kazi zao kwa ufasaha pasina wasiwasi wowote.

Kwa upande wa wadau wa elimu Wilaya ya Ikungi walimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kuanzisha mfuko wa elimu wa Wilaya pamoja na kuwashirikisha namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali wilayani humo.

Wamemuhakikishia kuwa watatoa ushirikiano wa hali na mali ili kuinua sekta ya elimu na kuchagiza ufanisi wa kukuza maendeleo katika Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na Mzee Mjengi Gwau wakati wa kikao cha Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani katika, Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017 katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Nkrumah Munjori akichangi  namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salumu M. Chima Akielezea hatua zilizofikiwa na kamati ya Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi na wadau wa mfuko huo waishio Dar es salaam

Tigo Inaungana na Twende App Kuzindua Huduma ya Usafiri

September 10, 2017
 Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) na Mkurugenzi wa Twende App Justin Kashaigili (kulia)  wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma mpya ya simu za mkononi ijulikanayo kama Twende App inayiowawezesha wasari kupata huduma ya haraka na usalama ya usafiri wa umma wa Taxi, pikipiki za bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu kwa kutumia simu za mkononi.


Twende App kuwawezesha wasafiri kupata huduma ya usafiri kupitia simu za mkononi.
Arusha 8 Septembea, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeungana na kampni inayotoa huduma za usafiri Twende App kuzindua huduma mpya itakayowezehsa wasafiri kupata huduma bora, ya haraka na uhakika zaidi kupitia mfumo wa simu za mkononi unaojulikana kama Twende App.

TwendeApp ni mfumo wa kidigitali wa simu za mkononi unaowezesha wasafiri kutafuta na kupata usafiri wa taxi, pikipiki za magurudumu mawili  (bodaboda) na zile za magurudumu matatu  kupitia simu zao za mkononi kwa uhakika zaidi na kwa bei nafuu.

Twende App ambayo, tayari inatumika katika jiji la Dar es salaam, sasa imepanua wigo wake na kufikia miji ya Arusha,  Morogoro, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma Iringa na Mbeya. Kuna mipango ya kusambaza huduma hiyo kwenda Zanzibar, Tanga na Mtwara.

Akizungumza katika uzinduzi wa Wende App jijini Arusha leo, Meneja Uhusiano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Twende App inatumia  teknologia ya GPS kwa kutegemea mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo. Hii inawahakikishia watumiaji huduma ya uhakika, haraka na yenye usalama wa hali ya juu.

‘Kwa sasa magari mengi ya usafiri wa taxi na bodaboda yamepaki kwenye vijiwe wakisubiri wateja. Twende App itawaunganisha madereva na wasafiri kwa muda na sehemu sahihi na inayohitajika. Kwa kupakua mfumio wa Twende App kwenye simu zao za mkononi, wasafiri wataweza kuwasiliana kwa haraka na madereva wa vyombo vya usafiri wa umma ambao wapo karibu zaidi na eneo husika ambapo usafiri wenyewe unahitajika. Hii inaondoa adha ya kutembea kutafuta usafiri na pia inapunguza muda wa kusubiri usafiri kwani mteja anawasiliana kwa haraka na chombo cha usafiri kilichokuwa karibu zaidi naye. Kwa upande wa madereva, Twende App itawaokolea muda, kuwaongezea wateja na kuongeza mapato  kwa kuwa hawahitaji tena kushinda kijiweni wakisubiri wateja,’ alisema.

TAHLISO YAUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA JPM KUPIGANIA NA KUZILINDA RASILIMALI ZA NCHI”

September 10, 2017

Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) limesema linaunga mkono juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya Taifa jambo ambalo litasaidia kuchangia kwa kasi harakati za kimaendeleo.
Hayo yalisemwa  na Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini ambapo alisema tokea Serikali ya awamu ya tano iingie madaraka inakaribia kutimiza miaka miwili lakini ndani ya kipindi hicho watanzania wameona mambo mengi makubwa yakifanywa kwa ajili ya kuipa nchi maendeleo.
Alisema moja kati ya mambo makubwa ni suala la kiongozi huyo kupamaba na vita dhidi ya dawa za kulevya,kuondoa watumishi hewa serikalini pamoja na wenye vyeti feki, Vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi,kufufua shirika letu la Ndege(ATC) kwa kununua ndege ambazo hivi sasa watanzania wanajivunia kuwa ni mali yao.
Mwenyekiti huyo alisema pia mambo mengine ni Ujenzi wa Reli ya kisasa, Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), utoaji wa ajira zaidi ya 50,000 kwa vijana wahitimu, Kuimarisha utumishi wenye nidhamu na uwajibikaji serikalini, Kuinua kwa kasi uchumi wa nchi yetu kimataifa, Kuboresha sekta ya afya pamoja na kupunguza bei za madawa ya binadamu nchini na mengine mengi yaliyoleta maendeleo ya nchi yetu
Alisema pamoja na hayo lakini Rais Magufuli alionyesha ujasiri mkubwa kwa kuzuia mchanga wa madini ya dhahabu (Makinikia) na kuunda tume ili ichunguze namna nchi ilivyokuwa inapoteza mapatoambayo ilionyesha jinsi watu walivyoibiwa mapato ya Taifa kwa kipindi kirefu.
“Lakini hakuishia hapo Juzi Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Madini ya Almas na Tanzanite iliyochunguzwa na kamati mbili zilizoundwa na Mhe. Spika Jobu Ndugai ripoti ambayo imeonyesha jinsi watanzania tulivyoibiwa kwa kipindi kirefu, Mhe. Rais hakusita kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kupelekea Taifa kupoteza mapato”Alisema
Alisema sambamba na hayo suala la ukamataji wa madini ya Almas kwenye uwanja wa Ndege yaliyokua yameripotiwa kuwa na thamani ya 31.4bn tofauti na uhalisia wake ambapo kitaalamu almas ile ina thamani ya 64bn hii ni hatua kubwa sana ya kiukombozi wa nchi yetu ambayo iligeuka kuwa shamba la bibi kila mtu anajifanyia anavyotaka wazungu wanatuibia wanapeleka mali zetu kwao huku wakituachia mashimo makubwa bila kunufaika na rasilimali zetu.
“Kutokana na hayo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwa ameonyesha uzalendo wa hali ya juu bila kumuonea mtu haya bila kujali cheo cha mtu ameonyesha namna anavyokerwa na vitendo viovu dhidi ya rasilimali za Taifa na pia kaonyesha uchungu mkubwa wa kuzijali rasilimali za Taifa letu kwa vitendo huku akituonyesha mfano unaopaswa kuigwa na kila Mtanzania katika vita hii kubwa ya kuzilinda”Alisema na kuongeza kila mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa rasilimali hizo kwenye mahali alipo.
Alisema watanzania wamefika hapa walipo kwa sababu ya baadhi ya watu waliopewa dhamana na serikali katika nyadhifa mbalimbali kukosa maadili ya uongozi kwa makusudi ama kwa bahati mbaya (uzembe) ambao umeligharimu Taifa lna kulisababishia kupoteza fedha nyingi ambazo zingeweza kuisaidia serikali yetu kutuboreshea maisha yetu, upatikanaji wa Maji, ujenzi wa barabara, Utoaji elimu bure hadi Chuo Kikuu, huduma za afya nk.
“Hata hivyo sisi kama TAHLISO Tunawataka ndugu zetu waliopewa dhamana na serikali hii ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa nyadhifa mbalimbali wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili na miiko ya kazi zao”Alisema
Lakini pia wakitangulize uzalendo wa nchi yetu kwa maslahi ya Taifa letu bila kuangalia maslahi yao binafsi huku wakitambua kuwa wamesomeshwa na kodi za wanachi wa Tanzania ili kuwatumikia Watanzania kwa moyo safi na weredi mkubwa.
Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo wa Tahaliso aliwataka vijana kuacha kukata tamaa tusikate tamaa wala kukatishwa tamaa na mtu kwa haya yaliyofanyika huko nyuma badala yake wajipe moyo na kumuunga mkono Rais wa nchi ambaye amejitolea kwa nia dhati kurudishia Tanzania Mpya itakayokuwa na kasi kubwa ya kiuchumi.
“Lakini pamoja na hayo tusiache kumuombea kwa mungu ili aweze kumlinbda na kumpa afya njema katika kipindi chake cha uongozi kutokana na dhamira ya kipekee aliyokuwa nayo kulinda rasilimaliza za nchi “Alisema.

SHAKA AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA NYUMBANI KWAKE MJINI DODOMA

September 10, 2017

Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akizungumza na Kaimu Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka (kushoto) wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma

Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwonyesha kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka kinyango chenye uzito wa tani 1 wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliochorwa na Mwanafinzi wa darasa la saba Mwaka 1982 wakati wa hali ngumu ya uchumi nchini.
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliyochorwa na mjuu wake ikimuonesha yeye na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 Picha ya pamoja Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela na Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha
 Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka  akimuaga  Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela alipomtembelea nyumbani kwake Mtaa wa Kilimani Mjini Dodoma(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

RC MASENZA: MARUFUKU WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI

September 10, 2017
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya ya mufindi wakati wa kutambulisha mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga uliokuwa na lengo la kuonyesha dira ya miaka ya hamsini (50) ya maendeleo ya mji wa Mafinga ambapo inasemeka ni moja kati ya miji inayokuwa kwa kasi .
 hawa ni baadhi ya wadau waliojitokeza katika ukumbu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya mufindi kushuhudia utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka wenyeviti wa vijiji  au wa mitaa kutojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababishwa na viongozi hao.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Masenza alisema kuwa kumekuwa na migogoro ambayo inasababishwa na wenyeviti wa serkali za vijiji au mtaa hivyo ni marufuku viongozi hao kujihusisha na swala hilo.

“Sipendi kusikia mwenyekiti wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji akihusisha kuwa shahidi wa uuzwaji wa ardhi kwa kuwa hilo sio jukumu lao waichie mamlaka ya ardhi kufanya kazi kwa utaalamu wao”alisema Masenza

Aidha Masenza alimtaka wakurugenzi wote wa mkoa wa iringa kuwaambia ukweli viongozi juu ya sheria ya uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro inayosababisha maumivu kwa upande unaonewa na kudhurumiwa haki yao ya msingi na kusababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo.

“Wakurugenzi waambieni vijana wetu waache ujanja ujanja wa kupokea,kuchora,kuonyesha na kuelekeza swala lolote linalohusu uuzwaji wa ardhi ili hii mipango kabambe ya halmashuri ziende vizuri kama serikali inavyopanga”alisema Masenza

Masenza alisema kuwa acheni kufanya kazi kwa ujanja ujanja maana serikali ya uwamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe maguli haitaki wananchi na viongozi kuishi kwa mazoea.

Sixbet Kayombo ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Balali katika halmashauri ya mji wa Mafinga alisema kuwa tamko la mkuu wa mkoa lianukweli ndani yake kwa kuwa kuna wenyeviti wengi wamekuwa wakisababisha migogoro isiyokuwa na maana kwa uroho wa kupokea pesa.

“Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa haiwezekani wananchi kuuza ardhi bila kuwepo ushaidi wa serikali ya mtaa hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa kutafuta njia mbadala ili mwananchi asiwe na ukakasi wowte wakati wa uuzaji wa ardhi yake” alisema Kayombo

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Amani kata ya Upendo Merikioni Ndelwa  alisema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa hasa vijijini kwa kuwa viongozi wengi bado hawana elimu ya mwisho wa madaraka yaho hivyo tunamuomba mkuu wa mkao kutoka elimu wa wenyeviti ili kuepusha migogoro ya ardhi.
Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii

Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii

September 10, 2017

Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.[/caption] Na Mwandishi Wetu, Dodoma MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora inapatikana nchini Tanzania. Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji. Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini. Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo. Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu. Walishauri Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwa sekta ya elimu kama ilivyofanywa kwa sekta ya miundombinu miaka miwili iliyopita, Serikali za mitaa kutunga na kusimamia sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi wanaowanyima watoto haki ya elimu, huku wakiomba fedha za mikopo ya elimu ya juu kutenganishwa na fedha za maendeleo ya wizara ya elimu. Kilio kingine kilichofikishwa katika kamati hiyo ya Bunge ya Huduma za Jamii, ni pamoja na kutaka kuhimarishwa kwa kamati za shule, kuhamashishwa kwa wazazi kuchangia maendeleo ya watoto wao kielimu, kuingiza kipengele cha elimu ya mlipa kodi katika mitaala ya elimu na pia serikali kupunguza vigezo katika upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti eneo hilo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba aliwashukuru wanachama wa TEN/MET kwa kuwa wazalendo kuipigania elimu nchini, hivyo kuwataka watoe muda kwa kamati hiyo ili iweze kuzifanyia kazi hoja hizo kwa maendeleo ya taifa.  
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
 
Afisa Programu toka HakiElimu, Makuba Mwemezi (kushoto) ambaye pia ni mwanachama wa TEN/MET akichangia hoja katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.
 
 Kikao hicho kikiendelea jana mjini Dodoma.