March 08, 2014

WAFANYAKAZI WANAWAKE KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAUNGANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA UWANJA WA MWEMBE YANGA

 Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiungana na wanawake wenzao kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika maandamano yaliyokuwa yakielekea katika Uwanja wa Mwembe Yanga Mapema leo Katika Kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani ambapo wafanyakazi wanawake wa PPF nao waliweza kujumuika na wanawake wenzao katika kusherehekea Siku hiyo

KUTOKA KWENYE BUNGE LA KATIBA NI RAHA TU JANA

March 08, 2014
Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.Pandu Amir Kificho akiwa amesimama kutoa muongozo wakati wa kikao kilichofanyika jioni ya leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Job Ndugai akibadilishana mawazo na Mhe.Samweli Sitta. 
March 08, 2014

MJUMBE WA KAMATI KUU YA (CCM) JERRY SILAA AMPIGIA DEBE GODFREY MGIMWA KUCHUKUA JIMBO LA KALENGA

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kulia akiteta jambo na Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kata ya Mgama halmashauri  ya Iringa vijijini mkoani Iringa, Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila na wana Kalenga kwa ujumla wake kumchagua Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha  na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dr. William Mgimwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA) 2 
March 08, 2014

WAFUASI WANAODAIWA KUWA WA CHADEMA WAMSHAMBULIA DEREVA WA MWIGULU NCHEMBA

DEREVA wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Mohamed Kunambi, ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wanaodhaniwakuwa wafuasi wa chama cha CHADEMA.

Tukio hilo liletokea usiku wa kumkia leo eneo la Ifunda jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini mkoa wa Iringa.

Mbali na dereva huyo diwani wa kata ya Ifunda, Eliya Mngwila, naye amejeruhiwa na watu hao waliposhambulia gari alilopanda.

March 08, 2014

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI, JOHN MINJA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUFUNGA RASMI MAFUNZO KOZI NAMBA 08 YA MWAKA 2014 KWA MAAFISA MAGEREZA NCHINI MSUMBIJI

1  
Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(kulia vazi jeupe) akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa Magereza Wahitimu wa taaluma ya Uaskari Magereza Nchini Msumbiji katika Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zilizofanyika Machi 07, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza kilichopo Maputo, Msumbiji ambapo Nchi mbalimbali za Afrika zilialikwa zikiwemo Afrika Kusini, Zambia, Namibia, Zimbabwe, Swaziland pamoja na Tanzania. Jumla ya Wahitimu Maafisa 430 wamehitimu vyema mafunzo hayo ya Uaskari wa Magereza.
March 08, 2014

MAMA PINDA ATAKA WAZAZI WAJALI ELIMU YA WATOTO WAO BILA KUWABAGUA

IMG_0136 
MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amewataka wazazi hapa nchini watoe kipaumbele kwenye suala la elimu kwa vijana bila ubaguzi wa kijinsia.
Ametoa wito huo leo mchana (Jumamosi, Machi 8, 2014) wakati akifungua Kongamano la Wanawake wa Afrika ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
March 08, 2014

Dkt Fenella aadhimisha siku ya wanawake dunia kwa kushiriki bonanza la mpira kikapu!!

DUCE 1  
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wanawake mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Mpira wa Kikapu lililoandandiliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya DUCE. Kushoto ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi chuoni hapo Dkt. Constansia Rugumamu na kuli ni Kamishina wa wanawake TBF Bi. Angella Grolia Bondo.DUCE 2 Kamishina wa wanawake TBF Bi. Angella Grolia Bondo akitoa maelezo kuhusu Bonanza la Mpira wa Kikapu lwaliloandaa kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake dunia,Mwenye koti jeupe ni jijini Dar es Salaam katika viwanja vya DUCE. Kushoto ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi chuoni hapo Dkt. Constansia Rugumamu na kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo.
March 08, 2014

*KAMPENI ZA CCM ZATINGA KIJIJIJINI KWA MGOMBEA WA CHADEMA LEO

 Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji cha Wangama jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM, kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa CCM jimboni humo, leo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wapo wanachama wengine 50 alioambatana nao kutoka Chadema. Kijiji hicho cha Wangama ndiko anakotoka mgombea wa Chadema katika uchaguzi huo, Grace Tendega.
 Mwanamke, mkazi wa Kijiji cha Wangama akimpongeza Fred Mgata baada ya uamizi wake wa kuhamia CCM kutoka Chadema.
 Mgombea wa CCM jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akimshukuru Mwenyekiti wa Chadema Kijiji cha Wangama baada ya kutangaza kuhamia CCM leo.
 Wananchi wsa Kijiji cha Wangama wakiishangilia CCM kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho leo.