MAMIA WAMZIKA KAKA YAKE MUFTI WA TANZANIA,SHEHE SAAD ZUBEIRY ALLY

September 20, 2017
Waomboleaji wakiwemo ndugu,jamaa  na marafiki wakiwa wamebeba jeneza ambalo lina mwili wa  Kaka yake Mufti wa Tanzania,Shekhe Saad Zubeiry Ally ambaye amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakijiandaa kuliingiza kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika jana (Septemba 21) kwenye makaburi ya familia eneo la Kwamndolwa wilayani Korogwe Mkoani Tanga
 Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir katika akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika katika eneo la Kwamndolwa wilayani Korogwe Mkoani Tanga
Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir kulia akiteta jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakati wa maziko ya kaka yake Mufti yaliyofanyika kwenye eneo la Makaburi ya familia eneo la Kwamndolwa wilayani Korogwe kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira,January Makamba wakati wa maziko hayo
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira,January Makamba kulia akiteta jambo na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam walipokutana msibani hapo wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella akiwa na mmoja kati ya waombolezaji katika msiba huo wakielekea makaburini 
Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam kushoto akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku
Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam akiondoka katika eneo la makaburini
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria mazishi hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia,Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Mwanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel wakiwa kwenye eneo la makaburini
Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku wakati wa mazishi hayo jana
 Sehemu ya waombolezaji katika msiba huo
 Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akiwa katika eneo la msiba jana kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia

 Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir akiagana na baadhi ya watu waliohudhuria mazishi ya kaka yake jana
 
 Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi ya kaka yake kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandis Zena Saidi na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katika akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) mbele Marry Chatanda na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi

MBUNGE AZZA HILAL AWAHIMIZA AKINA MAMA KUWEKEZA KATIKA ELIMU BORA KWA WATOTO WA KIKE

September 20, 2017
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) amewataka akina mama kujitahidi kuwekeza katika elimu kwa watoto hususani watoto wa kike na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu bora.
RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA KILOMITA 26 YA KIA-MERERANI MKOA WA MANYARA LEO

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA KILOMITA 26 YA KIA-MERERANI MKOA WA MANYARA LEO

September 20, 2017

m (9)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
m (10)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
m (19)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Simanjiro Mhe. James Ole Milya kwenye sherehe ya kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
m (21)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
m (26)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
m (27)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine akikata utepe  kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
m (32)
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi baada ya kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
Picha na IKULU

WAKULIMA MOSHI VIJIJINI WASEMA N2AFRICA IMEWATOA GIZANI NA KUWAPELEKA KWENYE MWANGA

September 20, 2017
Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde hususani maharagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro wamesifu mbegu bora aina ya Lyamungo 90, Jesca na Uyole Njano zinazotolewa kwa wakulima na Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia Mradi wa N2AFRICA.

Mradi huo unaotekelezwa kwa wakulima 11 katika vijiji sita vya Wilaya hiyo umekuwa na mafanikio makubwa kwao kutokana na mafunzo waliyopatiwa ya kulima kisasa kwa kutumia mbegu kidogo na mavuno makubwa pamoja na kutumia mbolea. 

Wakulima hao wanasema awali kabla ya mradi huo walikuwa wanalima kwa kuchanganya zaidi ya mazao ya aina mbili tofauti katika shamba moja, kutotumia mbolea na kulima pasipo kufuata njia za kitaalamu jambo ambalo liliwapelekea kupata mazao kidogo ambayo hayakuwa na ufanisi mkubwa katika kuimarisha uchumi wao.

Wanasema Kupitia mbinu bora walizojifunza kwa wataalamu kutoka katika Mradi wa N2AFRICA wamebadili mfumo wa maisha kwani kwa sasa wanapata mazao ya kutosha na kuwafanya kuhamia katika kilimo chenya tija kwa ajili ya chakula na biashara.

Janeth Godwin Shao, Achibold Masimba, Mary Mbuya na Fredy Urio wakazi wa kijiji cha Kiruweni , Elizabeth Paschal,na Ester Mbando wakazi wa kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini wanasema kabla ya Mradi wa N2AFRICA walikuwa wanapanda mazao shambani badala ya kupanda mbegu jambo lililofifisha upatikanaji wa mazao mengi.

Waliomba mradi huo kuongeza zaidi ufanisi baada ya kufanikiwa katika kuwanufaisha wakulima kupitia zao la maharagwe sasa waongeze mafunzo kwa wakulima ili kutoa mbegu za mazao mengine kama vile kunde na choroko.

Moja ya malengo muhimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ni kuitoa Tanzania katika kundi la nchi masikini zaidi duniani  na kujenga uwezo zaidi wa kiuchumi kupitia kilimo utakaoifanya iwe miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati kimataifa.

Mtaalamu wa Kilimo katika Kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini Elizabeth Josiah alisema kwa sasa Zao la maharagwe linapendwa na wakulima wengi kwa sababu linachukua muda mfupi kukomaa, halina gharama kubwa katika uzalishaji wake na lina bei nzuri sokoni karibu nyakati zote hata wakati wa mavuno (yaani msimu wake). 

Alisema kuwa Mkulima anaweza kulima maharagwe kwa matumizi ya chakula nyumbani kwake au kwa biashara reja reja au kwa jumla.

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata ya Mwika Kusini Wilfred Ngile alisema Urahisi wa kulima maharage na faida zake lukuki ni kivutio kwa watu wengi sana kwa sasa huku akisema kuwa lakini bila kufuata muongozo wa kitaalam ni ndoto kwa mkulima kupata mavuno anayotarajia.

Alisema mafanikio wanayoyapata wakulima sio ya wataalamu bali ni mafanikio yao wenyewe kutokana na kutumia njia bora kutokana na maelekezo wanayoyapata kutoka kwa wataalamu.

Aidha, aliongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na Mbegu bora zilizofanyiwa tafiti na Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiko (IITA) na kutambulika kisheria ambazo ni pamoja na Uyole Njano, Lyamungu 90, na Jesca.

Naye Afisa Mazao wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini Bi Joyce Kessy alizitaja changamoto zinazowakabili wakulima kuwa ni pamoja na uzalishaji mdogo kwani wanazalisha chini ya tani moja kwa hekta ambapo unachangiwa na sababu za kurudia mbegu, kutotumia mbegu za viwandani, kupanda bila kuacha nafasi, na kupanda zao moja kwa kuchanganya na mazao mengine.

Hata hivyo alisema kuwa mara baada ya Mradi wa N2AFRICA kuanzishwa katika Wilaya ya Moshi Vijijini hamasa imekuwa kubwa kwa wananchi kuhitaji mbegu na mbolea kutoka taasisi ya IIAT hivyo ameiomba taasisi hiyo kuongeza utoaji wa mbegu kwa wakulima wote na kutoa mafunzo.

Alisema kuwa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha  sekta ya kilimo nchini Tanzania jambo ambalo limerahisisha utendaji wa serikali kupitia Wizara ya Kilimo.

Alisema kuwa wakulima wanajifunza zaidi kwa vitendo kuliko nadharia hivyo aliiomba Taasisi hiyo ya IITA kupitia Mradi wa N2AFRICA kuvifikia vijiji vyote na kuwanufaisha wananchi kwa mafunzo ya vitendo zaidi.

Katika awamu ya kwanza ya Mradi huu ilianzishwa mwaka 2009 na kutekelezwa katika nchini DR Congo, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone na Zimbabwe ambapo  Awamu ya pili ilianza Januari 2014 na kufanyika katika nchi tano za Ethiopia, Ghana, Nigeria, Tanzania, na Uganda.

Janeth Godwin mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
Wakulima wa zao la maharagwe walipowapokea wataalamu kutoka IITA katika kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi Vijijini
 Achibold Masimba mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
 Elizabeth Paschal mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
Mtaalamu wa kilimo kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika kusini Elizabeth Josiah akielezea jinsi wakulima wanavyonufaika na kilimo cha maharagwe
Ester Mbando (kulia) Mkulima wa maharagwe Kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa.
Mkulima wa zao la maharagwe  Joseph Towo kutoka Kijiji cha Rauya Kata ya Marangu Mashariki akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
Wanufaika wa mradi wa N2AFRICA wakielezea namna walivyonufaika na kilimo cha maharagwe
Fredy Urio akisimulia changamoto alizokabiliana nazo kabla ya mradi huwa kuwasili kijijini kwao na kuwa na manufaa kwa wakulima
Afisa kilimo Kata ya Mwika kusini Wilfred Ngileakielezea jinsi wakulima walivyonufaika na Mradi wa N2AFRICA katika kata hiyo
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa.
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akielezea jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa. Wengine ni wataalamu kutoka IITA na Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha shamba lake jinsi lilivyostawi kutokana na mafunzo ya kilimo bora kwa kutumia mbegu bora za maharagwe

UBA bank Tanzania yazindua kituo cha huduma kwa wateja cha Masaa 24 Siku 7 za wiki

September 20, 2017
Mkuu wa Kitengo cha Huduma bora za benki ya UBA, Ms Queen Odunga (Kushoto) akizungumzia namna ya Kituo cha huduma kwa Wateja kitakachokuwa kikifanya kazi kwa masaa 24 kila siku katika kuhakikisha kuwa UBA Tanzania inaendelea kutoa huduma bora na zenye kuendana na matakwa ya wateja wa UBA Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika Mapema leo katika ofisi za makao makuu ya benki hio zilizopo barabara ya Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam.Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau.
 Mkuu wa idara ya Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akizungumzia juu ya Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Huduma kwa Wateja cha Benki ya UBA Tanzania Kitakachokuwa kikifanya kazi kwa Masaa 24 kila siku. 
 
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania, Mr Peter Makau akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)mapema leo wakati wa kuzindua kituo cha huduma kwa wateja cha benki ya UBA Tanzania kitakachofanya kazi kwa masaa 24 kila siku.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya UBA Tanzania, Bi Brendansia Kileo akifafanua Juu ya huduma nyingine zinatolewa na benki hiyo huku lengo kubwa likiwa ni kuwafikia wateja wengi zaidi na kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao.
Dar Es Salaam, Benki ya UBA Tanzania leo (Jumatano) imezindua kituo cha Huduma Kwa Wateja Cha Masaa 24 Kila Siku. Kituo hiko kitakuwa kikifanya kazi kwa masaa 24 kila siku huku lengo likiwa ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao na wasio wateja muda wote pale ambapo mteja anahitaji huduma kutoka benki hio.
Kituo hiko cha Huduma kwa Wateja kwa Masaa 24 kitakuwa kikitoa huduma pia kupitia mitandao yao ya Kijamii ya Facebook, Twitter, BBM, E-mail na kupitia simu ya meza. 
Ili mteja aweze kupatiwa huduma anapaswa kuwasiliana nao kwa njia mojawapo kati ya hizi kwa kutumia barua pepe (e-mail: CFC@ubagroup.com, Kupitia mtandao wa twitter Mteja anaweza kuwasiliana nao kupitia https://www.twitter.com/ubacares na kupitia facebook unaweza kuwasiliana nao kwa kutembelea https://www.facebook,com/ubaTanzania na instagram https://www.instagram.com/ubacares
Vilevile mteja anaweza kuwasiliana nao moja kwa moja kupitia namba ya simu ya +255 764 700 782 na kwa wale wanaotumia BBM basi wanapatikana kupitia BBM channel C00211246
Pamoja na kuzindua kituo hiko cha huduma kwa wateja kwa masaa 24 siku 7 za wiki vilevile UBA Tanzania wanatarajia kufungua matawi mapya manne ili kupanua wigo na kuwafikia wateja wengi zaidi na kuwasogezea huduma karibu.

Idara ya hekaheka ya Leo Tena Clouds yafanyika Duka jipya la Tigo Mwanza

September 20, 2017
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds fm, Geah Habib akiendesha kipindi chake ndani ya duka jipya la Tigo mkoani Mwanza hii leo. Hii ni sehemu ya shamrashamra za msimu wa Tigo fiesta 2017.
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds fm, Geah Habib akiendesha kipindi chake ndani ya duka jipya la Tigo mkoani Mwanza hii leo. Hii ni sehemu ya shamrashamra za msimu wa Tigo fiesta 2017.
Wafanyakazi wa Tigo wakiendelea kutoa Huduma 

Msimamizi wa duka la Tigo Barbara ya Nyerere mkoani Mwanza, Neema Mossama akizungumzia jinsi gani wateja wa Tigo wataweza kunufaika na huduma zao ndani ya msimu huu wa Tigo fiesta

KATIBU MTENDAJI BODI YA FILAMU AWATAKA WATANZANIA KUJIANDAA TAMASHA LA JAMAFEST

September 20, 2017
Binagi Media Group
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Bi.Joyce Fisso amewataka watanzania kujiandaa na kutumia vyema fursa ya kuwa wenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika nchini mwaka 2019.

Akizungumza na BMG hii leo, Bi.Fissoo ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST 2017 lililomalizika Kampala nchini Uganda, amesema tamasha hilo linatoa fursa kubwa kwa watanzania kuonyesha ngoma na bidhaa mbalimbali za kiutamaduni na hivyo kukuza soko lao la ndani na nje ya nchi.

Aidha Bi.Fissoo amefurahishwa kwa namna watanzania walivyoshiriki vyema kwenye tamasha la mwaka huu nchini Uganda na kubainisha kwamba walitia fora kwenye maonyesho ya tamasha hilo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kokolo.

Katika kilele cha Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki JAMAFEST mwaka 2017 nchini Uganda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokea bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ishara ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tamasha hilo ambalo kwa mara ya kwanza liliasisiwa nchini Rwanda mwaka 2013.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la JAMAFEST Bi.Joyce Fisso (mwenye bendera) akijiandaa kupongea cheti cha pongezi kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki ya Uganda Mhe.Ali Kivejinja kwenye kilele cha Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki JAMAFEST lililofanyika Kampala nchini Uganda Septemba 14,2017.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Balozi Elibariki Maleko (wa pili kulia) akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo kwenye kilele cha Tamasha la JAMAFEST ambapo Tanzania ilishiriki vyema kwenye tamasha hilo lililofikia tamati Septemba 14,2017 nchini Uganda.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokea bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ishara ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki JAMAFEST mwaka 2019 ambapo kwa mara ya kwanza tamasha hilo liliasisiwa mwaka 2013 nchini Rwanda.