SIMBA YAREJEA KIMATAIFA, YAIGONGA MBAO 2-1 NA KUTWAA KOMBE LA AZAM

May 27, 2017
Na Mahmoud Zubeiry, DODOMA
SIMBA SC imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Katika fainali kali na ya kusisimua ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na mabao matatu yakapatikana katika dakika 30 za nyongeza, Simba mawili, Mbao moja.
Wachezaji Frederick Blagnon raia wa Ivory Coast na Robert Ndaki ambao wote walitokea benchi kipindi cha pili ndiyo waliokwenda kuzifungia mfululizo timu zao.
Wachezaji wa Simba SC wakifurahia na Kombe lao baada ya kukabidhiwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma leo
Mfungaji wa bao la ushindi la Simba, Shiza Kichuya akimtoka beki wa Mbao leo 
Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Frederick Blagnon (katikati) akipambana na wachezaji wa Mbao FC
Beki wa Simba, Mgahan James Kotei aliyeibua Mchezaji Bora wa Mechi akimdhibiti mshambuliaji wa Mbao FC, George Sangija  
Mshambuliaji wa Simba, Mrundi Laudit Mavugo akivuta mguu kufumua shuti dhidi ya wachezaji wa Mbao

Blagnon alianza kuwainua vitini mashabiki wa Simba dakika ya 95 baada ya kumzidi maarifa beki wa Mbao FC kufuatia pasi ndefu ya beki wa kushoto pia, Abdi Banda.
Lakini Ndaki akaisawazishia Mbao dakika ya 109 akitumia makosa ya Banda aliyezubaa akidhani mfungaji kaotea.
Wakati wengi wanaamini mchezo utaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, lakini refa Ahmed Kikumbo akawazawadia Simba penalti baada ya beki mmoja wa Mbao FC kuunawa mpira uliopigwa na Abdi Banda dakika 119.
Wachezaji wa Mbao FC walimzonga refa huyo kabla ya kuamua kutulia na kukubali mchezo uendelee, ndipo winga Shiza Ramadhan Kichuya akaenda kuifungia Simba bao la ushindi na kuamsha shangwe na nderemo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Simba imekata tiketi ya kurejea kwenye michuano ya Afrika baada ya kuikosa kwa miaka minne na mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akaenda kuwakabidhi taji lao Wekundu wa Msimbazi.        
Kilichofuata ni shangwe za wachezaji, viongozi na mashabiki wa Simba kuelekea kwenye mitaa ya mji wa Dodoma, kabla ya kesho asubuhi kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam na Kombe lao.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tahabalala’/Abdi Banda dk51, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Said Ndemla/Frederick Blagnon dk80 na Juma Luizio/Ibrahim Hajib dk60.
Mbao: Benedict Haule, Asante Kwasi, Yussuf Ndikumana, David Mwasa, Salmin Hozza, Boniface Maganga, George Sangija/Dickson Ambundo dk59/Rajesh Kotecha dk104, Jamal Mwambeleko, Pius Buswita, Habib Hajji/Robert Ndaki dk104 na Ibrahim Njohole
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWAPISHA BALOZI, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA MKURUGENZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MEI 27,2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWAPISHA BALOZI, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA MKURUGENZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MEI 27,2017

May 27, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Tixon Tunyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Rajab Omar Luhwazi kuwa Balozi nchini Msumbiji Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Bernard Mtandi Makandi kuwa katibu Tawala Mkoa wa Rukwa  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Clifford Katondo Tandari kuwa katibu Tawala Mkoa wa Rukwa  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha maadili ya utumishi wa umma 

RC MAKONDA AKABIDHIWA MWENGE WA UHURU UKITOKEA MKOANI LINDI

May 27, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.

YANGA YATUA ARUSHA KWA KISHINDO HUKU IKIWA NA KOMBE LAKE

May 27, 2017

Picha na maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha

Kikosi cha Afc Arusha kimejinasibu kuwa kitawafunga mabigwa wa ligi kuu bara msimu uliomalizika  Timu ya  Yanga Afrika,katika mchezo wao wa kirafiki unaotajarajiwa kupichezwa Jumapili hii  May 28 katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa

Akiongea na Tanga Raha Blog Kocha wa kikosi hichi kipya cha timu ya AFC Fikiri Elias  alisema kuwa vijana wake wapo tayari kuwapatia burudani wapenzi wa ke wa soka mkoani hapa huku akiwapa sifa viongozi wa serikali kwa kuwa begakwa bega katika kuhakikisha soka la mkoa wa Arusha linarudi katika ramani yake

Alisema kuwa japo hii ni mechi yao ya kirafiki baina yao na timu ya Yanga lakini watatumia mchezo huu pia kuangalia kikosi bora ambacho kitakaa kambini kwa ajili ya kuandaa timu ya kikosi kitakacho unda AFC mpya itayoshiriki ligi daraja la kwanza .

,, Pamoja ya kuwa timu ya yanga inawachezaji wazoefu wengi na pia ndio wametoka tu kutwaa ubigwa mara ya tatu lakini napenda kusema hivi japo mechi hii ni ya kirafiki lakini nimeaada kikosi kizuri nanauhakika lazima tutaifunga timu hii ili tuweke historia japo ni mechi ya kirafiki ,,alisema Fikiri

Kwa upande wake kocha msaidizi  timu ya  Yanga ambao wameshikilia ubigwa  kwa mara ya tatu mfulukizo ligi kuu bara  Juma Mwambusi alisema kuwa mchezo huu ni muhimu  kwao kwani ni moja  ya program zao katika kujiandaa kuelekea katika michuzano inayowakabili  ikiwemo mashindano ya Sport Pesa

Kikosi hichi cha yanga kipo katika ziara ya kutembeza kombe lake kwa mashabiki wa mikoani ambapo mkoa wa Arusha umekuwa wa kwanza kuona kombe hilo na wakitoka mkoani hapa wanampango wa kulipeleka mkoani Dodoma ,ambapo pia wanajangwan hawa wamekuwa ni timu ya tatu kuoka ligi kuu bara msimu ulioisha kutoa katika aridhi ya jiji la Arusha iliyokuwa na ukame wa timu za ligi kuu mara baada ya timu za Ruvu shooting na Simba  zilizowaikutua hapa katika mtanange wake ulioisha

Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki  mmoja wawaandaaji wa mechi hiyo ambayo katibu wa timu ya AFC  Charles Mwaimu alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika timu zote zipo tayari wanaisubiri tu siku ya mechi ifike.

Aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na pembezoni kujitokeza kwa wingi kuishabikia timuyao ya AFC ikiwa ni ujio mpya wa timu hii mara baada ya kupotea kwa muda ,na aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kuwapa morali wachezaji wao .

Aidha alisema kuwa pia mbali na mechi hii ya yanga kucheza na AFC pia wanampango wa timu hii kwenda mkoani manyara kucheza mechi baada yao na timui ya Merirani.

JUMUIYA YA MADOLA YA WAPIGA MSASA WABUNGE KUTOKA NCHI 16

May 27, 2017
Wajumbe wa Bunge la Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa Mafunzo ya wiki moja yalioandaliwa na Bunge hilo, katika mafunzo hayo Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limewakilishwa na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson na Baraza la Wawakilishi Zanzibar limewakilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said wakishiriki katika masomo ya wiki pamoja huko Afrika Kusini University of Wits ambapo jumla ya Wabunge kutoka nchi 16 kutoka Jumuiya za Madola wameshiriki masomo hayo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwasilisha kazi ya kikundi wakati wa mafunzo hayo ya wiki moja yanayofanyika Nchini Afrika Kusini yalioandaliwa na Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola, akieleza kuhusiana na umuhimu wa kamati za kudumu za mabunge ya Jumuiya Madola kuelekea karne 21. 

Kutoka kushoto ni Mbunge kutoka India Ajay Misra, Naibu Spika Tanzania Dr Tulia Ackson, Seneta kutoka Jamaica Charles Pearnel na Mussa Dlamini Swaziland. Masomo hayo yanafanyika Johanessberg University of Witwatersrand kwa wiki moja na kudhaminiwa na Commonwealth Wealth. 
Wawakilishi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Naibu Spika Dr.Tulia Ackson pamoja Simai Mohammed Said kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa masomomi South Africa University of Witwatersrand wakibadilishana mawazo na Mbunge wa Swaziland Mhe Mussa Dlamini
Naibu wa Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson akisikilizwa kwa umakini na washiriki wenzake. Kutoka kushoto Mhe.Simai Mohammed Said ( Zanzibar ) Pearnel Charles Junior ( Jamaica) Mussa Dlamini ( Swaziland ) na Ajay Misra ( India).
Waheshimiwa Wabunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola wakiwa katika mafunzo  Nchini South Africa. wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini. 
Wajumbe kutoka Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ( Commonwealth Countries) wakitembelea Mahakama ya Katiba ( Constitutional Court ) katika mji wa Johannesburg.
Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo hayo kutoka  kushoto  Mbunge wa Jamaica.Mhe.Heroy Clarke ( MP), Charles Pearnel Seneta pia akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Jamaica, Stewart Michael ( MP) na Victor Wright ( MP ). 
Mjumbe kutoka Jumuiya ya Madola pia akiwa Mwakilishi kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akibadilishana mawazo na Profesa David Everatt ambaye ni Kiongozi wa Skuli ya Utawala katika University of Wits, South Afrika. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Tulia Ackson akitoa nasaha zake za shukrani kwa niaba ya Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola walioshiriki mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa University of Witwaterstrand, Johannesburg South Africa.

WAZIRI MWIJAGE MGENI RASMI UFUNGUZI WA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJINI TANGA KESHO

May 27, 2017
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwa mgeni kwenye maonyesho ya kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga 
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisalimiana na wanawake wajasiriamali wakati akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisalimia na baadhi ya wajasiriamali wakati apokuwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa na Waziri Mwijage
 Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wakiendelea na matayarisho ya  Banda lao ambalo lipo kwenye viwanja Mwahako Jijini Tanga.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Salehe Masoud kushoto akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kukagua na kutembelea kuona maendeleo ya mabanda hii leo
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akisisitiza jambo kwa mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maonyesho hayo,Salehe Masoud wakati alipotembelea kukagua mabanda leo
 Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Salehe Masoud kushoto akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kukagua na kutembelea kuona maendeleo ya mabanda hii leo

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

May 27, 2017
uap1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Tixon Tuyangine Nzunda  kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ikulu jijini Dar es Salaam.
uap3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.
uap5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Benard Mtandi Makali kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
uap6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Clifford Katondo Tandari kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Ikulu jijini Dar es Salaam.
uap7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Ikulu jijini Dar es Salaam.
uap9
Viongozi waliopishwa wakila Kiapo cha Uadilifu –Ikulu jijini Dar es Salaam. wakwanza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Tuyangine Nzunda, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Rajab Omar Luhwavi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Mtandi Makali,  Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clifford Katondo Tandari pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe
uap10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Rajab Omar Luhwavi mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

UCHELEWESHAJI WA PEMBEJEO UMETAJWA KUPOROMOSHA KILIMO CHA PAMBA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA

May 27, 2017


Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza  na waandishi wa habari, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.

MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA

May 27, 2017
Na Leonce Zimbandu

MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha shukurani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani kata ya Majohe, Gabriel Macheho (pichani) baada ya kutambua mchango wake wakuhifadhi na kutunza rasilimali za umma. 

Moja ya rasilimali hizo ni pamoja na kusimamia eneo la umma lisichukuliwe na kumilikiwa na watubinafsi, likiwamo eneo  lamachimboyamchangalililokuwalikimilikiwanaMbezi Tile.
Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu alimkabidhi Macheho cheti hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi ili kutoa motisha kwa wananchi wenye moyo wakutoa utetezi wa mali za umma.

Serikali yaanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja

May 27, 2017
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Richard Kasuga. Picha na Fatma Salum- MAELEZO 



Na Fatma Salum (MAELEZO)

Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System) kutoka nje ya nchi utakaosaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Lazaro Kitandu alisema uamuzi huo wa kuanzisha mfumo mpya umekuja baada ya Serikali kugundua kuwa kwa muda mrefu matumizi ya mbolea hapa nchini si ya kuridhisha kutokana na bei ya mbolea kuwa juu.

“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mbolea imeanzisha mfumo huu baada kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalam waelekezi wa ndani na nje ya nchi na kutumia uzoefu wa taasisi nyingine zinazofanya ununuzi wa bidhaa kwa pamoja” Alisema Kitandu.

Kitandu alieleza kuwa katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA), Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye matumizi ya chini ya mbolea kwa kutumia kilo 19 za virutubisho hivyo kwa hekta katika ngazi ya wakulima wadogo ambapo kiasi hicho hakiendani na malengo ya azimio la Maputo la nchi za SADC linalotaka kufikia angalau kilo 50 kwa hekta moja.

Alisema kuwa kwa msimu wa mwaka 2017/2018 mfumo huo utaanza na aina mbili tu za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na mbolea nyingine zitafuata baadaye kadri itakavyoonekana mfumo huo kuleta manufaa kwa wakulima.

Akifafanua kuhusu faida za mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja, Kitandu alisema utasaidia kuimarisha utaratibu wa usambazaji wa mbolea ambapo wadau wote watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani.

Kwa mujibu wa Kitandu pia mfumo huo utawezesha wafanyabiashara wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.

“Ununuzi wa mbolea kwa pamoja pia utasaidia kudhibiti bei ya mbolea iwapo kutajitokeza ongezeka lisilokuwa na sababu (soko holela) kwa kuwa bei itatangazwa kwa kuzingatia bei halisi ya mbolea, gharama halisi za usafirishaji wa mbolea, tozo mbalimbali na kiwango stahiki cha faida ya mfanya biashara” alibainisha Kitandu.

Serikali kupitia mfumo huu inatarajia matokeo chanya katika kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima hivyo kuongezeka kwa matumizi ya mbolea na uzalishaji wenye tija ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.

BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA NA WASHIRIKA WAKE

May 27, 2017


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula aliyeuongoza Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo ulikuwepo Zanzibar kwa siku Nne kukagua miradi ya Tasaf Awamu ya Tatu. Kati kati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioambatana na washirika wa Maendeleo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar uliofika kukagua miradi ya Tasaf.
Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza na Bibi Azzah Ammin kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji.
Balozi Seif akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga wakishuhudiwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula.


Picha na – OMPR – ZNZ.

Benki ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.

Viongozi wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.