RAIS DKT. SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU NDOGO ZANZIBAR

RAIS DKT. SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU NDOGO ZANZIBAR

July 05, 2024


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Julai, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka pamoja na Viongozi walioapishwa katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Julai, 2024. Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Said Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji, Katibu Mkuu wa Madini Mhandisi Yahya Ismail Samamba pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Yusuph Juma Mwenda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Julai, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Julai, 2024. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhandisi Yahya Ismail Samamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Julai, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan akimuapisha Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Julai, 2024.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO DKT,SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA KONGAMANO LA WANAWAKE ZANZIBAR.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO DKT,SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA KONGAMANO LA WANAWAKE ZANZIBAR.

July 05, 2024



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Baadhi ya Masheikh na Wahadhiri mbalimbali waliohudhuria katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Baadhi ya akina Mama na Waheshimiwa mbalimbali waliohudhuria katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kongamano Sheikh Samir Zulfikar akizungumza katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Muhadhiri Sheikh Muharrami Mziwanda kutoka Dare es Salaam akiwasilisha mada kuhusiana na Mama ni mhimilli Mkuu wa kuwepo Maadili katika Jamii katika katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Muhadhiri Sheikh Othman Maalim kutoka Masjid Nuru Muhamad akiwasilisha mada kuhusiana na Athari ya Fitna katika Jamii katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume akitoa taarifa ya Mwaka Mpya wa Kiislamu katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mwalim Haroun Ali Suleiman akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya wa Kiilamu 1446 katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
……….
Ali Issa- Maelezo Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Tanzania kufuata misingi ya Dini, ili kuepusha mifarakano.

Hayo ameyasema leo katika hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wakati wa Kongamano la Wanawake wa Kiislamu kufuatia maadhimisho ya mwaka mpya wa kiislam 1446 al-Hijra lililoandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar.

Amesema misingi hiyo humuweka mtu katika heshma, uadilifu na Imani ya ucha Mungu itakayompelekea kumuogopa Mwenyezi Mungu kwa kuwa mwema na kuepukana na mifarakano.

“Mtu yoyote Mwenye kufuata dini huwa mstarabu na kuepukana na mifarakano ambayo itampeleka kwenye uasi”alisema Dkt. Samia.

Aidha alisema kuwa wapo baadhi ya watu wanaokiuka misingi ya dini zao na kutamka maneno mabaya na matusi kwa viongozi jambo ambalo halikubaliki kwani huleta uvunjifu wa Amani nchini.

Hata hivyo Rais Samia aliitaka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kusimamia waganga wajadi ili kuweza kuachana na ramli chonganyishi kwani kufanya hivyo kutasababisha maafa kwa jamii .

Nae Sheikhe Othmani Maalimu akitoa mada juu ya athari ya fitna katika jamii alisema wanadamu waepukane na matumizi mabaya ya Ulimi kwani kufanya hivyo husababisha maafa kwa jamii.

Mapema Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema Kongamano la Mwaka Mpya wa Kiislamu limeanzia Pemba kwa shughuli mbali mbali Tarehe 26/6/ 2024 na linatarajiwa kufungwa kesho na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi katika Msikiti wa Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Credit FullshangweBlog
SHILINGI BILIONI 108.43 KUWEZESHA UANZISHAJI, UENDELEZAJI VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI – DKT. BITEKO

SHILINGI BILIONI 108.43 KUWEZESHA UANZISHAJI, UENDELEZAJI VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI – DKT. BITEKO

July 05, 2024








Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imetoa mikopo ya shilingi bilioni 108.43 ili kuwezesha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya uongezaji thamani wa mazao ya kilimo na mifugo nchini.

Hayo yamebainishwa leo Julai 5, 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Kongamano la Wadau na Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (MSMEs) lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited na Kufanyika Jijini Dar es Salaam.

Amesema mikopo hiyo imetolewa hadi kufikia Machi, mwaka huu.

“Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 38. zilitolewa kwa ajili ya uwekezaji na shilingi bilioni 70.427 zilitolewa kwa ajili ya kuendesha. Uwekezaji huo umeendelea kuwahakikishia masoko ya uhakika wakulima, wafugaji na wavuvi nchini,” amesema Dkt. Biteko

Amesema, mwaka 2023/24, Serikali kupitia Mfuko wa Wajasiriamali Wananchi (NEDF) unaotekelezwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) iliweza kutoa jumla ya mikopo 956 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 kwa riba ya asilimia 9. Asilimia 51 ya mikopo hiyo ilitolewa kwa wanawake na asilimia 28 ilitolewa kwa miradi ya vijijini.

Aidha, kupitia programu ya SANVN (SIDO, Azania Bank, NSSF, VETA na NEEC) inayotoa mikopo kwa ajili ya uwezeshaji viwanda kwa wajasiriamali wadogo (Shilingi milioni 8 hadi milioni 50) na wajasiriamali wa kati (Shilingi millioni 50 hadi milioni 500), mikopo 11 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 ilitolewa kwa Wanufaika wa SIDO kupitia Azania Benki na kutengeneza ajira 103 katika mwaka 2023/2024.

Ameeleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na Wajasiriamali wadogo na wa Kati (MSMEs) ili kuboresha, kukuza na kuendeleza biashara zinazochipukia kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.

Aidha, kongamano litaongeza fursa mbalimbali za kuwainua Wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs) ambao wanajadili kuhusu namna ya kuboresha, na kuendeleza ujuzi na hatimaye kukuza biashara ndogo na za kati kama ilivyo katika malengo yetu.

Pia, ameipongeza Mwananchi kwa kuwa na program habari na makala mbalimbali zenye kulenga kuboresha, kuendeleza ujuzi na kukuza biashara ndogo na za kati kama isemavyo,” amesema Dkt. Biteko.

“Tunauona umuhimu wa kampuni zote hizi kwa mchango tunaopata katika kuwezesha kusaidia maendeleo endelevu yenye uwiano katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kutengeneza fursa za uwekezaji, kukuza ajira na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania,” amesema Dkt. Biteko

Dkt. Biteko amesema takwimu zinaonyesha asilimia 90 ya biashara zote Duniani ni ndogo na za Kati (MSMEs) ambazo zinachangia zaidi ya asilimia 50 ya ajira na zinachangia mpaka asilimia 40 ya Pato la Taifa la Uchumi unaokua. Pia takwimu hizo zinaongezeka pale unapohusisha biashara ndogo zisizorasmi.

“Kwa pamoja tushirikishane fursa, na namna ya kushughulikia changamoto, na kupanga mikakati bora kwa maendeleo endelevu ya uchumi wetu,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe amewapongeza Mwananchi Communications Ltd kwa kuandaa kongamano hilo ili kujadili changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo na kutumia fursa zilizopo katika Sekta ya Viwanda hususan katika ukuzaji wa uchumi na kuongeza kuwa Sekta hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa kutoa ajira kwa Watanzania

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu amesema kuwa chombo hicho kina mujibu wa kuchochea maendeleo endelevu nchini kupitia kongamano hilo., muhimu wa kampuni zote hizi kwa mchango tunaopata katika kuwezesha kusaidia maendeleo endelevu yenye uwiano katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kutengeneza fursa za uwekezaji, kukuza ajira na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania,” amesema Dkt. Biteko

Dkt. Biteko amesema takwimu zinaonyesha asilimia 90 ya biashara zote Duniani ni ndogo na za Kati (MSMEs) ambazo zinachangia zaidi ya asilimia 50 ya ajira na zinachangia mpaka asilimia 40 ya Pato la Taifa la Uchumi unaokua. Pia takwimu hizo zinaongezeka pale unapohusisha biashara ndogo zisizorasmi.

“Kwa pamoja tushirikishane fursa, na namna ya kushughulikia changamoto, na kupanga mikakati bora kwa maendeleo endelevu ya uchumi wetu,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe amewapongeza Mwananchi Communications Ltd kwa kuandaa kongamano hilo ili kujadili changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo na kutumia fursa zilizopo katika Sekta ya Viwanda hususan katika ukuzaji wa uchumi na kuongeza kuwa Sekta hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa kutoa ajira kwa Watanzania

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu amesema kuwa chombo hicho kina mujibu wa kuchochea maendeleo endelevu nchini kupitia kongamano hilo.


SEKTA YA MADINI YAJIPAMBANUA KWA WANANCHI

July 05, 2024

 

Imeelezwa kuwa Sekta ya Madini imeanza kujipambanua kipindi cha miaka ya karibuni baada ya kufanyika marekebisho ya Sheria ya Madini mwaka 2017 na kuonyesha kuvutia Watanzania wengi kuliko ilivyokuwa kabla ya kufanyika mabadiliko hayo.

Hayo yameelezwa kwa nyakati tofauti na watu wanaotembelea mabanda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake yaliyopo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. 

Moja kati ya Watu hao, Gregory Kumbuka Mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam amesema kuwa yeye binafsi alidhani kuwa shughuli za Sekta ya Madini zinahusu wawekezaji wa nje kwa kuwa zinahitaji mitaji mikubwa, lakini kupitia vyombo mbalimbali vya habari ameongeza uelewa wake kuhusu sekta ya madini.

Amesema kuwa, mbali na vyombo hivyo vya habari, pia, kupitia maelezo aliyoyapata kwenye mabanda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake, imemsadia kumwongezea uelewa zaidi kuhusu sekta hiyo na kwamba kwa maeneo anapofanyia shughuli zake anafikiria kuwekeza kwenye Madini ya Ujenzi kama mchanga na kokoto.

Kwa upande wake, Salma Fahadi mkazi wa Morogoro Mjini amesema kuwa ameweza kujifunza kuhusu sekta ya madini kupitia vyanzo tofauti ikiwemo vyombo vya habari kwani hapo awali alikuwa hafahamu kuwa mchanga na kokoto ni madini na ili mtu aweze kuchimba kwa tija anahitaji kufuata utaratibu maalum ikiwemo kuomba leseni.

Ameongeza kuwa, kupitia elimu aliyopata pia kupitia wataalam wa Wizara na Taasisi zake waliopo katika Maonesho hayo, anafikiria kutumia fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kupitia vikundi.

Wizara ya Madini na Taasisi zake zinashiriki Maonesho hayo kwa pamoja kwa lengo la kutoa elimu kuhusu Mnyororo mzima wa shughuli za uchimbaji wa madini kwa manufaa ya kiuchumi na maendeleo endelevu kwa ujumla.

KUTANENI KUPANGA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI BAJETI- NAIBU WAZIRI PINDA

July 05, 2024

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Tabora waliokutana kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa bajeti ya 2024/2025 mkoani Tabora tarehe 5 Julai 2024.

Na Munir Shemweta, TABORA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa nchini kuhakikisha wanakutana na kufanya tathmini na kuweka mpango kazi wa utekelezaji Bajeti ya Wizara ya Ardhi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Mhe.Pinda ametoa kauli hiyo tarehe 5 Julai 2024 wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Tabora akiwa njiani kuelekea mkoani Kigoma kikazi.

Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora imeanzisha utaratibu wa kukutana na watumishi wa sekta ya ardhi wa mkoa huo kila baada ya bajeti ya wizara kupitishwa kwa kufanya tathmini na kuweka mpango kazi wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka mpya wa fedha.

Naibu Waziri wa Ardhi amesema, utaratibu unaofanywa na ofisi ya Kamishna wa Ardhi kwa kuwakutanisha watumishi wa sekta hiyo katika mkoa mzima ni mzuri na unapaswa kuigwa na ofisi nyingine za mikoa kwa kuwa unasaidia kujua muelekeo wa wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.

"Huu mfumo mliouanzisha wa kukutana, kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji bajeti kwa mwaka mpya wa fedha ni mzuri na unapaswa kuigwa na ofisi nyingine za makamishna wa ardhi wasaidizi wa mikoa, hiki ni kitu kikubwa katika mpango kazi wenu" alisema Mhe. Pinda.

Amempongeza kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Husein Sadick kwa kazi nzuri na ubunifu wa kukutanisha watumishi wa sekta ya ardhi ambapo ameuelezea utaratibu huo kuwa, pamoja na kujipanga kwa utekelezaji wa bajeti lakini unawezesha kujua namna ya kukabiliana na changamoto za sekta ya ardhi kwenye mkoa kwa mwaka husika.

Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Husein Sadick amesema ofisi yake imewakutanisha watumishi wa sekta ya ardhi katika mkoa huo mbali na mambo mengine kufanya tathmini na kuweka mipango ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/2025.

Katika mwaka wa fedha 2024/2025, vipaumbele vya Wizara ya Ardhi ni kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi mijini na vijijini, kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi, kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika utunzaji wa kumbukumbu, utoaji huduma na upatikanaji taarifa za ardhi, kuhakikisha uwepo wa nyumba bora, ukuaji wa sekta ya milki na maendeleo ya makazi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuimarisha mipaka ya kimataifa.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda yuko njiani kuelekea mkoa wa Kigoma ambapo akiwa mkoani humo mbali na kufanya shughuli za sekta ya ardhi atashiriki ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Husein Sadick akizungumza wakati wa kikao cha kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa bajeti ya 2024/2025 mkoani Tabora tarehe 5 Julai 2024.

Sehemu ya watumishi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Tabora wakiwa katika kikao cha kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa bajeti ya 2024/2025 mkoani Tabora tarehe 5 Julai 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Tabora wakati wa kikao cha kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa bajeti ya 2024/2025 mkoani Tabora tarehe 5 Julai 2024.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)