March 31, 2014

JAPAN YAIPIGA TAFU TANZANIA KATIKA KUINUA KILIMO

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini hati ya makubaliano ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6 unaolenga kukuza sekta ya kilimo uliotolewa   na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. 
March 31, 2014

*HABARI KUTOKA TFF LEO, WANACHAMA WA TFF KUANDALIWA KATIBA MFANO YA MAREKBISHO

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imekutana Machi 30 mwaka huu kujadili utekelezaji wa maagizo ya TFF kwa wanachama wake kurekebisha Katiba zao ili ziendane na Katiba ya TFF pamoja na ile ya FIFA kabla ya Machi 30 mwaka huu.
March 31, 2014

RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA KAMPENI CHALINZE

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Dini kwenye Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange wakati alipopita kuwasalimia na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Jana Machi 30,2014.Picha zote na Othman Michuzi.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Sam wa Ukweli akitoa Burudani kwa wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Shangwe kwa wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange.
Wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM.
March 31, 2014

*BALAA LA MVUA ILIYONYESHA JIJINI DAR JANA

Vijana wakisaidia kulikwamua gari la Polisi, lililokwama katika shimo lililokuwa halionekani kutokana na maji kujaa katika njia nyingi za barabara eneo la Kiwalani jijini Dar es Salaam, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini.
March 31, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

2 (2) 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akitanga Kamati ya Uongozi kutoa ratiba itakayoongoza shughuli za Bunge hilo leo mjini Dodoma
3 (3) 
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Zakia Meghji(kushoto) na Christopher Ole Sendeka(kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya. 
March 31, 2014


JK aitaka halmashauri ya Jiji la Tanga kulipa fidia wananachi. .



NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha inawalipa fidia wananchi waliojenga karibu na eneo la kituo cha mabasi na eneo la kuegeshea malori Kange kwa sababu walipima wenyewe viwanja wakati wakijua kutakuwa na ujenzi huo.

Agizo hilo alilitoa jana wakati alipotembelea stendi hiyo kuweka jiwe la msingi  na kupokea taarifa wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Tanga ambayo aliianza Jumapili wiki hii ya kugadua miradi mbalimbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.


Alisema haiwezekani stendi hiyo kujengwa bila kuwepo kwa eneo mbadala ambalo litaweza kuongezeka wakati matumizi yake yatakapongezeka kutokana na mahitaji ya wakazi wa jiji la Tanga hivyo wanapaswa kufikiria namna ya kufanya ili kuweza kupanua ikiwemo kuwalipa fidia wananchi waliojenga stendi hiyo pembeni yake.

    “Hakikisheni mnafikiria namna ya kuongeza eneo la stendi ili liweza kukidhi mahitaji yatakayotokana na mabasi kuongezeka hivyo halmashauri mnakazi kulipatia ufumbuzi suala hilo kabla ya kukumbana na hali hiyo “Alisema Rais Kikwete.


Aidha aliwataka wasifanye makosa kama waliyoyafanya kwa mara ya kwanza kujenga kwenye eneo hilo kuwa dogo ikiwemo kujenga hapo sasa hakikisheni mipango yenu mengine mnatafuta eneo la kupanua stendi.