WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

April 14, 2018
Watafiti wa Kodi Barani Afrika wameshauriwa kuimarisha mtandao wao ili kuweza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jitihada zao za kufanya utafiti.


Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John wakati akifunga warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika (ATAF) kwa kushirikiana na Chuo cha Kodi (ITA).


Bw. Michael amesema kwamba watafiti hao wanategemewa sana na mamlaka za mapato wanazoziwakilisha hivyo kuwataka kutumia ujuzi wa utafiti walioupata wakati wa mafunzo hayo ya siku nne kutatua changamoto mbalimbali na kuziongezea uwezo mamlaka za mapato barani Afrika hivyo kupelekea kuongeza makusanyo.


“Nina imani kwamba baada ya mafunzo haya mtaendelea kushirikiana kupitia mtandao wenu ili kwa pamoja mtimize lengo lenu la kutatua changamoto katika utekelezaji wa taratibu, sheria na sera za kodi barani Afrika kupitia utafiti mtakaoufanya”.Aidha amewataka watafiti hao kuzitumia vyema nyenzo za ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa ambazo wamepatiwa wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi huyo wa Rasilimali Watu na Utawala ameipongeza Taasisi ya Kodi Barani Afrika pamoja na Chuo cha Kodi kwa kuandaa na kufanikisha mafunzo hayo ambayo ni muhimu katika utendaji wa usimamizi wa Kodi barani Afrika.


Naye Mkuu wa Chuo cha Kodi Pro. Isaya Jairo ameishukuru ATAF na TRA kwa kukiamini Chuo cha Kodi kuendesha mafunzo kwa watafiti ambao wametoka nchi mbalimbali za Afrika. Ambapo pia amewapongeza washiriki hao kwa kupatiwa nafasi kushiriki mafunzo hayo akisema kwamba ushiriki wao unadhihirisha utayari wa mamlaka za mapato barani Afrika kutatua changamoto zilizopo kwa kuwa na watafiti wenye weledi na ujuzi.


Awali akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa Bw. Alfred Mregi alisema kwamba Usimamizi wa Kodi katika Afrika unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo watafiti wanategemewa kuzitatua ili taasisi zinazosimamia mapato Afrika ziwe rafiki kwa walipakodi na hatimaye kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani.


“Tunawategemea nyinyi kufanya utafiti wa mifumo ya kodi na kutoa suluhisho na mapendekezo kwa watunga sera na wasimamizi wa kodi”, alisema Bw. Mregi.


Warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti Afrika iliwashirikisha watafiti kutoka baadhi ya nchi za Afrika ambao mapendekezo yao ya utafiti yamekidhi vigezo kwa mujibu wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika ambayo inaratibu Mtandao wa Wasimamizi wa Kodi Afrika kwa lengo la kuwajengea uwezo waafrika kufanya utafiti katika usimamizi, sheria na sera za kodi na kuwaunganisha watafiti hao na wanataaluma.


Washiriki wa warsha hii ambayo ni ya Tatu kufanyika, wameishukuru ATAF na Chuo cha Kodi kwa kuendesha mafunzo hayo wakisema kwamba imewapa uelewa zaidi wa kuendelea na utafiti wao.


Mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa kwa lugha tatu: Kireno, Kifaransa na Kiingereza yaliwashirikisha washiriki 24 kutoka, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Niger, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Togo, Benin, Cape Verde, Tunisia, Ivory Coast, Kenya na Tanzania.


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John akimkabidhi mshiriki kutoka Tunisia Bw. Jabali Belhanssen cheti cha ushiriki wa mafunzo ya utafiti ambayo yafanyika jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Afrika (ATAF) na Chuo cha Kodi (IAT). Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi ATAF Bw. Eugenio Bras.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (katikati) akifuatilia matukio wakati wa kufunga na kukabidhi vyeti kwa washiriki wa warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imefanyika jijini Dar es salaam. Wengina kutoka kushoto ni; Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras.

Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) waliosimama wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (aliyekaa katikati) baada ya kufunga mafunzo hayo. Wengine kutoka kulia ni, Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo na Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin

Ecobank Group washirikiana na MTN kuwezesha huduma zaidi za fedha barani Afrika

April 14, 2018


Pichani kuanzia Kushoto kwenda Kulia ni Charles Kie, Mkurugenzi Mtendaji wa, Ecobank Nigeria Ltd; Serigne Dioum, Mtendaji wa MTN’s , Hudma za kifedha kwa njia ya mtandao; Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa, Ecobank Transnational Incorporated (ETI), Rob Shuter, Ofisa Mtendaji mkuu wa MTN na Patrick Akinwuntan, Mtendaji wa Ecobank Transnational Incorporated (ETI)


Na Mwandishi wetu


KAMPUNI ya simu MTN imeingia ubia na moja ya benki inayoongoza barani Afrika ya Ecobank Transnational Incorporated (ETI) kuwezesha wateja wao kufaidika na huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni hayo.

Imeelezwa kuwa MTN ikijivunia idadi kubwa ya wateja wanaotumia huduma zake mbalimbali; mtandao mkubwa wenye uhakika; bidhaa zenye ubunifu na huduma zake za kifedha kwa mtandao imeungana na Ecobank kuwezesha wateja wao kuanzisha kufungua akaunti na kupitisha miamala yao kupitia mtandao wa MTN.

Makampuni hayo mawili maarufu barani Afrika yametiliana saini mkataba wa makubaliano utakaowezesha kushirikiana katika kubuni na kuwezesha huduma za kifedha zenye ubora wa kiwango cha juu kati ya benki hiyo na mtandao wa simu wa MTN.

Miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni kuwezesha miamala mbalimbali kufanyika kwa kutumia simu na akaunti za benki.

Kutumia mitaji iliyopo katika uwekezaji ndani ya Ecobank na MTN kuwezesha miamala ya kimataifa kufanyika kidigitali.

Aidha makubaliano hayo yatachochea ubunifu wa bidhaa mbalimbali katika upande wa hifadhi ya fedha kwa njia ya mtandao na ukopeshaji wake na kutoa nafasi ya malipo kwa njia ya mtandao kwa wateja, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali.

Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank anasema: “ Mabadiliko ya kidigitali katika mifumo ya benki na simu kunatengeneza fursa za namna bora ya kuwezesha kutoa huduma za kifedha. Afrika inalazimika kwenda mbio katika digiti ili kuwezesha fursa zilizopo zitumike kuwatumikia wateja. MTN na Ecobank leo wamechukua hatua kubwa kuwezesha fursa hizo” .

Pia alisema kwamba mkakati wa benk hiyo wa kidigiti kwa muda mrefuj umelenga kuhakikisha nafuu ya uwezeshaji wa miamala katika soko. Akizungumzia ushirikiano huo Ofisa Mtendaji Mkuu na Rais, Rob Shuter alisema: “Ushirikiano kati ya mabenki na watoaji wa huduma za miamala kwa njia ya simu ni muhimu, hivyo uhusiano wetu wa muda mrefu na Ecobank umelenga kuwezesha huduma za fedha kuwafikia wananchi wengi na kwa urahisi zaidi. Tumefurahishwa na maafikiano haya kwani yametupeleka hatua nyingine, kwani ushirikiano wetu utawezesha ubunifu utakaowezesha huduma za fedha kupenya kila mahali katika bara hili.”

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI NAMNA BORA ZAIDI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

April 14, 2018





NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

“Pamoja na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.

Alisema Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.

“Rais wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.

Wakitoa ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.

“Mimi nilikatika mkono wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kazi kwenye Kampuni ya Reli Tanzania, (TRL), na WCF imenilipa fidia ya mkupuo na inaendelea kunilipa pensheni ya kila mwezi, shilingi 170,000/= kwa maisha yangu yote nitakapokuwa hai.” Alisema Bw.Fortunatus Kiwale

Naye Mfanyakazi mwingine wa Kampuni ya Frank Pile International Project Limited ya jijini Dar es Salaam, Bw. Patrick Millinga, yeye alisema Mfuko umemlipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 31.9 baada ya kupoteza jicho lake la kushoto kutokana na kugongwa na kipande cha chuma wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.

Mwingine aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Petronila Mligo, ambaye yeye alifiwa na mumewe katika ajali ya gari wakati akirejea kituo chake cha kazi jijini Mwanza akitokea Dodoma.

“Mfuko umenilipa fidia ya mkupuo kutokana na kifo cha mume wangu, lakini pia ninaendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi mimi na watoto wangu wawili, ambapo kila mtoto analipwa shilingi 175,000/= na mimi ninalipwa shilingi 375,000/=.” Alisema mama huyo mjane ambaye ni mwalimu.

Akiwasilisha mada mbele ya washiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.

Alisema, katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.

“Alisema Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi kifupi.” Alisema.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Eric Shitindi, akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhsuu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (Wanne kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha Mashomba, (Wakwanza kushoto), wakisalimiana na wanufaika wa Fidia kwa Wafanyakazi wa (WCF), Bw. Patrick Millinga, (wakwanza kulia) na Bi. Petronila Mligo, (wapili kushoto), wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma, na kufanyika jengo la LAPF mjini Dodoma. Mkuta huo ulilenga kutoa elimu zaidi na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo. Wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Antony Mavunde, (watatu kulia), Mwakilishi wa ATE, Bw. Almasi Maige, (wapili kushoto) na Katibu Mtendaji wa TCCIA-Dodoma, Bw.Iddi Senga.

Mkutano ukiendelea

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(katikati), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Mashan Mshomba, (kulia), wakimsikiliza Niabu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.


Baadhi ya washiriki

Baadhi ya washiriki

Baadhi ya washiriki
Washiriki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri.


Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati wa mkutano huo wa majadiliano na wadau.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, (kushoto), akiwa na Bw. Mshomba.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Mhe. Waziri Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari.

Mhe. Waziri akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wakati akiwasili ukumbini.


Mnufaika wa Fidia, Bi. Petronila Mligo, akitoa ushuhuda wa faida anayopata kutokana na uwepo wa Mfuko, baada ya kufiwa na mumewe akiwa kwenye safarin ya kikazi.


Bw. Patrick Millinga, naye akitoa ushuhuda kutokana na Fidia aliyopata kutoka WCF baada ya kupoteza jicho lake la kushoto wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.


Mhe. Waziri Mhagama akisalimiana namnufaika mwingine wa Fidia, Bw. Fortunatus Kiwale



Picha ya kwanza ya pamoja.

Picha ya pili ya pamoja.