ZAIDI YA TRILIONI 2 KUFANYA MAGEUZI SEKTA YA MIFUGO

October 26, 2022

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (kulia) akiangalia mashine ya kukamulia maziwa mara baada ya kufika kwenye banda la Kampuni ya pembejeo za Mifugo ya "Afrifarm" leo (26.10.2022) ikiwa ni muda mfupi kabla ya kufungua kongamano la Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) linalofanyika jijini Arusha

3

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (kushoto) akielezea umuhimu wa hereni za kielektroniki alipofika kwenye banda la Kampuni ya pembejeo za Mifugo ya "Afrifarm" muda mfupi kabla ya kufungua kongamano la Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) leo (26.10.2022) jijini Arusha. Kulia ni Afisa Mauzo wa kampuni hiyo Bw. Emanuel Senge.
Meneja Masoko wa kampuni ya Maziwa ya Asas kwa upande wa kanda ya Kaskazini Bw.Tumainieli Joakim (kulia) akimkabidhi zawadi ya Maziwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ( Mifugo) Dkt. Charles Mhina leo (26.10.2022) ikiwa ni muda mfupi kabla hajazindua kongamano la Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) linalofanyika jijini Arusha. Katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Jonas Kizima

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (wa kwanza kushoto) na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) wakifuatilia uwasilishwaji wa maandiko ya wanataaluma mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kongamano la chama hicho linalofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 26-28, 2022




Dkt. Kizima abainisha namna TSAP inavyo wainua wataalam mbalimbali wa sekta za Mifugo na Uvuvi

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza zoezi la utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa miaka 5 wa Sekta ya Mifugo ambao unatarajia kutumia zaidi ya shilingi Trilioni 2 mpaka kukamilika kwake.

Hayo yamesemwa leo (26.10.2022) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa upande wa Sekta ya Mifugo Dkt. Charles Mhina katika hotuba yake ya Ufunguzi wa kongamano la Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) uliofanyika kwenye Ukumbi wa “Olasit Garden” jijini Arusha.

Dkt. Mhina ametumia jukwaa hilo kuwasisitiza wataalam waliopo kwenye chama hicho kuendelea kufanya tafiti zenye tija na zinazolenga kuboresha ufugaji na maisha ya wafugaji kwa ujumla ili kuirahisishia Serikali katika utekelezaji wa Mpango huo.

“Mpango huu unalenga kuboresha sekta ya Mifugo kwa ujumla kuanzia katika eneo la uzalishaji wa mifugo hasa katika eneo la uhimilishaji na matumizi ya madume bora ya mbegu, uzalishaji wa malisho kupitia mashamba darasa ambayo tunaenda kuyaanzisha kwenye Halmashauri takribani 100 ili wafugaji wetu waweze kujifunza namna ya kulima mbegu na malisho yenyewe kuanzia kupanda hadi kuyavuna na lengo letu ni kuhakikisha mbegu hizo zinapatikana kwenye maduka mbalimbali ya pembejeo hivyo ninaamini kupitia maandiko yenu kama wanataaluma tutaendelea kupata suluhu ya namna ya kufanikisha hayo ” Amesisitiza Dkt. Mhina.

Dkt. Mhina ameongeza kuwa eneo jingine ambalo Mpango huo utaliangazia ni lile la afya ya Mifugo ambapo Wizara yake imeendelea kuongeza dawa za kuogeshea mifugo na chanjo za magonjwa mbalimbali yanayoikabili mifugo hapa nchini.

“Lakini pia kupitia mpango huo tunaendelea kuboresha huduma za ugani, tafiti na uanagenzi ambapo tumeanzisha Vituo atamizi 8 vinavyolenga kuwasaidia vijana waliopo mtaani wenye taaluma ya ufugaji kujifunza kwa vitendo namna ya kufanya unenepeshaji wa Mifugo ambapo tunawapatia mifugo ya kunenepesha, tunawafundisha namna ya kunenepesha na wakimaliza mafunzo tunawagawia ng’ombe hao kama mtaji wa kuanzia huko waendako na kwa mwaka huu tumeanza na vijana 240” Amebainisha Dkt. Mhina.

Katika hatua nyingine Dkt. Mhina amewapongeza wataalam wanaounda Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) kwa kuandaa maandiko ya tafiti zao na kuziwasilisha ili zijadiliwe kabla ya kuchapishwa kwa matumizi ya sekta ya Ufugaji ambapo amebainisha kuwa utekelezaji wake utakuwa na tija kwa mfugaji mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Jonas Kizima amesema kuwa lengo la kufanyika kwa kongamano hilo kila mwaka ni kujadili na kuchambua mada za kisayansi zinazoonesha matokeo ya utafiti ili matokeo hayo yapelekwe kwa wadau mbalimbali wa sekta za mifugo na Uvuvi.

“Uchambuzi wa mada hizo ukishakamilika utatupa picha ya aina ya teknolojia zinazopaswa kutumika ili kuongeza tija katika sekta za Mifugo na Uvuvi na matokeo hayo tutayaweka kwenye chapisho kwa ajili ya kutumiwa na wadau wa sekta hizo” Ameongeza Dkt. Kizima.

Dkt. Kizima amesema kuwa machapisho yote ya kisayansi yanayopitishwa kupitia kongamano hilo la wataalam huwekwa kwenye majarida ya kisayansi yanayopatikana mitandaoni ambayo pia huweza kumsaidia mtaaluma husika kupanda cheo kwenye ajira yake na kumruhusu kuyawasilisha katika majukwaa mbalimbali ya wanataaluma.

Kongamano hilo la 49 la wanataaluma litafanyika kwa muda wa siku 3 kuanzia Oktoba 26-28 ambapo mwaka huu linaambatana na dhima isemayo “kuenzi matokeo ya teknolojia na ubunifu ili kuongeza chachu katika maendeleo ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi.


BALOZI ADADI AWATAKA WANAFUNZI WA SHULE YA MUHEZA MUSLIM KUSOMA KWA BIDII

October 26, 2022
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akizungumza wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muheza Muslimu
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne  wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne  wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab  katikati akiwa na wadau wa maendeleo na wajumbe wa bodi ya shule ya Sekondari Muheza Muslim wakati wa maafali hayo


Na Oscar Assenga,MUHEZA

KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi katika shule ya Sekondari Muheza Muslim kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili wataalamu mbalimbali waweze kupatikana kupitia huko.


Balozi Adadi aliysema hayo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Muheza ambapo alisema lazima wanapokuwa shuleni waweze kujiandaa na  kuzingatia nidhamu ,malengo na kusoma vizuri ili baadae waje kufanikiwa kupitia elimu.

Alisema kwamba  mitihani inahitaji maandalizi mazuri ili waweze kufanya vema hivyo hawana budi kuhakikisha wanajiandaa ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao.

Katika Mahafali hayo Balozi Adadi aliendesha Harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule hiyo ambapo huku akihaidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanapata mafanikio.

Kamishna huyo aliuomba uingozi wa shule kwamba hiyo maabara utakapo kamilika ipewe jina la Bahoza Laboratory ili kuwaenzi kwa juhudi kubwa ambazo wamezifanya kufanikisha maabara hiyo.

Hata hiyo Balozi Adadi alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imefanya mambo makubwa na kuleta maendeleo huku akieleza fedha ambazo zinakuja zinatokana na kurudisha mahusiano ya na mataifa mengine ambayo yalikatika na ameyarudisha kwa kasi kubwa.

Alisema kutokana na kurejesha mahusiano hayo yamewasaidia kupata fedha nyingi za kujenga shule, maabara,barabara na kila Jimbo kuhakikisha maendeleo yanapatikana  ule ufufuaji wa mahusiano na  mataifa mengine.

Katika hatua nyengine Balozi Adadi aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kuhakikisha wana buni  mbinu zinazoweza kudhibiti vitendo vya rushwa ya ngono nchini.

Balozi Adadi alisema kwamba vitendo vya rushwa ya ngono vimekuwepo na  Takukuru wamepewa jukumu la kudhibiti  vitendo hivyo ni wakati sahihi kuhakikisha wanakuja na mwarobaini wake.

Alisema kwamba wao wanapaswa kuona namna nzuri ya kubuni mbinu ambazo zinaweza kupelekea 
 kudhibiti badala ya kusubiri matukio yanatokea ndio waweze kuanza kupambana nayo.

" Haya mambo yapo kwa sababu kwenye vyuo hivyo ni jinsi ya vyombo vilivyo kabidhiwa kufanya kazi hiyo wanafanya nini ili kuweza kuondokana na tatizo hilo"Alisema Balozi Adadi.

Aidha alisema kwamba wanataka wanaofanya vitendo hivyo wakamatwe ili iweze kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hiyo kuweza kubadilika hivyo suala hili lina umuhimu wake  hasa chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia.



JIJI LA TANGA LAWAITA WAWEKEZAJI

October 26, 2022
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusu fursa za uwekezaji katika Jiji hilo na namna walivyojipanga kupokea wawekezaji ambao watafika.

 


Na Oscar Assenga,TANGA.


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imewaita wawekezaji  kutoka ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo kutokana na uwepo wa  maeneo yanayotosha kwa ajili ya viwanda hasa sekta mbalimbali ikiwemo  ya Madini.

Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu fursa za uwekezaji katika Jiji hilo na namna walivyojipanga kupokea wawekezaji ambao watafika.

Aliyataja maeneo ambayo yanafaa kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya Madini katika Jiji hilo yapo katika eneo Maere,Chumvini,Kisosora,Ndaoya,Machui,Tongoni, Chongoleani,Mwarongo.

Dkt Sipora alisema katika maeneo hayo yana hekta 212 na yanafaa kwa ajili ya maeneo ya viwanda vya saruji,chokaa,chumvi pamoja na rangi kwamba sababu chumvi inayozalishwa inatumika uzalishaji bidhaa mbalimbali hivyo wanatangaza na kualika wawezekezaji wafika kwa ajili ya viwanda.

"Katika maeneo ya madini tunawaalika  wawekezaji wakubwa na wadogo  wa Madini na chumvi hivi sasa uzalishaji ni mdogo sana unakuta wazalishaji wadogo wadogo wanazalisha kama tani 6000 hazitoshi hivyo tunawaalika kuja kuwekeza na tumehaidi hakutakuwa na urasimu wa kupata maeneo hayo ambayo tayari yameshapimwa"Alisema Dkt Sipora.


Alisema pia katika maeneo hayo yanayofaa kwa ajili ya sekta ya uvuvi yaani uchumi wa bluu kutokana na uwepo wa bahari hivyo kuna fursa ya kufanya uvuvi na kuwaalika wawekezaji wanaoweza kuja kuingia meli kubwa na boti kwa ajili ya kufanya uvuvi.


"Lakini pia unenepeshaji wa magongoo bahari,kilimo cha mwani hao wote tunawaita lakini pia ufungaji wa samaki kwenye vizimba na uvuvi wa kutumia vyombo vya kisasa" Alisema


Alisema wameamua kuwaita wawekezaji hao kwa ajili ya shughuli za uwekezaji na viwanda ambavyo ni muhimu sana huku akieleza Rais Samia Suluhu ametangza ameifungua nchini na kuiunganisha nchi na masoko nje ya nchi hivyo kilichobakia ni wana Tanga waongeza uzalishaji ku
uza nje ya nchi na zile zilizopo kwenye bara la Afrika


"Tunapokuwa na viwanda inasaidia kuchukua nguvu kazi ya vijana ,twaliopo baada ya kilimo wanakuwa hawana cha kufanya kwa hiyo wote watapata ajira kwenye viwanda ambavyo vitaongeza thamani na muda wa kuishi kwa bidhaa husika kwa mfano unaposafirisha machungwa yanaweza kuozea njiani lakini wanapounguza gharama za kusafirisha na kukuta nafasi kubwa inchukuliwa kwenye gari na bidhaa nyengine zinaharibikia njiani hivyo kupunguza upotevu wa mazao na kuongeza thamani ya mazao" Alisema Mkurugenzi huyo.


Aidha aliwataka wawekezaji ambao wanakwenda kuwekeza Visiwani Zanzibar kupitia uchumi wa bluu waona namna ya kugawana na wengi wake Jijini Tanga ambako mako kuna fursa ya uwekezaji huo ambao ni muhimu kwa maendeleo.


Mwisho