KILUVYA, MBAO FC, MJI NJOMBE, MJI MKUU ZAPANDA FDL

March 11, 2015

Timu za Kiluvya United ya Pwani, Mbao FC ya jijini Mwanza, Mji Njombe kutoka mkoa mpya wa Njombe na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma zimepanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuongoza katika misimamo ya makundi yao ya Ligi Daraja la Pili (SDL).

Kwa kuzingatia Kanuni ya 5 (8) ya Ligi Daraja 9SDL Toleo la 2014, hatua ya pili Ligi Daraja la Pili kutafuta Bingwa na sasa timu hizo zitacheza kusaka Bingwa wa ligi Daraja la Pili.

Mji Njombe itacheza na timu ya Kiluvya United tarehe 14 Machi mwaka huu katika uwanja wa Amani Makambako, na mchezo wa marudiano kufanyika tarehe 18 Machi, 2015 katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Nayo Mbao FC ya Mwanza watawakaribisha timu ya Mji Mkuu FC mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na mechi ya marudiano itachezwa Machi 18, 2015 katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Fainali inatarajiwa kufanyika Machi 22 mwaka huu jijin Dar es salaam (uwanja wa mchezo utatangazwa baadae) kwa kuzikutanisha timu zilizopata pointi nyingi katika michezo hiyo miwili ya awali.

   
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE MKOA WA TANGA(TWMO) WAIPIGA TAFU HALMASHAURI UJENZI WA MAABARA

March 11, 2015
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdula Lutavi akipokea mabati zaidi ya 20 kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Tanga(TWMO) Bertha Mwambela ikiwa ni
juhudi ya chama hicho kuunga mkono agizo la Rais Kikwete kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule mbalimbali wilayani ya Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdula Lutavi kushoto akimkabidhi mabati 20 yalitotolewa na chama cha Waandishi wanawake Mkoa wa Tanga(TWMO) kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule mbalimbali jijini Tanga.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE MKOA WA TANGA(TWMO)BERTHA MWAMBELA AKIZUNGUMZA NENO BAADA YA KUKABIDHI VIFAA HIVYO KWA MKUU WA WILAYA YA TANGA.
WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI MJUMBE WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE MKOA WA TANGA (TWMO) AKITOA NENO BAADA YA KUKABIHDI MABATI HAYO
WAKINA MAMA WAKIFUATILIA MAADHIMISHO
WAKINA MAMA WA MSANJA WAKIWAJIBIKA.

TTCL ilivyoshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

TTCL ilivyoshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

March 11, 2015

TTCL na Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani TTCL na Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, mawaziri na viongozi wa mkoa wa Morogoro wakipokea maandamano ya akina mama katika viwanja vya Jamhuri mkoani Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, mawaziri na viongozi wa mkoa wa Morogoro wakipokea maandamano ya akina mama katika viwanja vya Jamhuri mkoani Morogoro.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya akina mama baada ya kutembelea banda la TTCL kwenye maadhimisho hayo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya akina mama baada ya kutembelea banda la TTCL kwenye maadhimisho hayo.Picha ya pamoja ya baadhi ya akina mama na viongozi wa mkoa waliohudhuria katika siku yao muhimu. Picha ya pamoja ya baadhi ya akina mama na viongozi wa mkoa waliohudhuria katika siku yao muhimu.Akina mama kutoka TTCL wakiwa na bango lao lililobeba ujumbe wa maadhimisho ya siku wa wanawake duniani mwaka huu.  Akina mama kutoka TTCL wakiwa na bango lao lililobeba ujumbe wa maadhimisho ya siku wa wanawake duniani mwaka huu.
Akina mama kutoka TTCL wakiwa na bango lao lililobeba ujumbe wa maadhimisho ya siku wa wanawake duniani mwaka huu.  Akina mama kutoka TTCL wakiwa na bango lao lililobeba ujumbe wa maadhimisho ya siku wa wanawake duniani mwaka huu.kina mama kutoka TTCL wakiwa na bango lao lililobeba ujumbe wa maadhimisho ya siku wa wanawake duniani mwaka huu.  kina mama kutoka TTCL wakiwa na bango lao lililobeba ujumbe wa maadhimisho ya siku wa wanawake duniani mwaka huu.

MADRID YAFUZU ROBO FAINALI KIMTINDO, YACHAPWA BAO 4-3 NA SCHALKE NYUMBANI

March 11, 2015



Real Madrid wamefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini "kimkanda mkanda" baada ya kuchapwa mabao 4-3 na wageni wake Schalke 04.



Madrid imefungwa nyumbani baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini nchini Ujerumani hivyo kufanya ifuzu kwa jumla ya mabao 5-4.

Mashabiki wake, waliwazomea wachezaji hao wakati wakiboronga na kufungwa na Madrid walifanikiwa kusawazisha mara tatu, lakini wakashindwa kufanya hivyo mara ya nne.

Mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao mawili, lakini akashindwa kuonyesha cheche kabisa.

Mashabiki walionyesha kutofurahia uchezaji wa timu hiyo ambao ndiyo mabingwa watetezi kufuzu kwa hofu.



MAFUNZO YATOLEWA NA BOT KWA MAOFISA WA BENKI NCHINI JINSI YA KUTATUA MIGOGORO YA KIBENKI

March 11, 2015

Senior Marketing AccessBank Mr Muganyizi Bisheko akiwa na Naibu Gavana wa BOT Lila Mkila.



 Mkurugenzi wa Kampuni ya Jayax Development and Training, Jemima Njeri akiongea katika mkutano ulioandaliwa na benki Kuu kujadili na kutatua Migogoro ya kibenki jijini Dar es Salaam 
Mameneja kutoka benki mbali mbali waliohudhuria semina hiyo, wa pili kutoka kushoto ni Senior Marketing AccessBank Mr Muganyizi Bisheko wakati wa mkutano ulioandaliwa na benki Kuu kujadili na kutatua Migogolo ya kibenki jijini Dar es Salaam 
 Naibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT, Lila Mkila (kulia) akisalimiana na Senior Marketing AccessBank Mr Muganyizi Bisheko wakati wa mkutano ulioandaliwa na benki Kuu kujadili na kutatua Migogolo ya kibenki jijini Dar es Salaam.
ZITTO KABWE ALIVYOVULIWA UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI

ZITTO KABWE ALIVYOVULIWA UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI

March 11, 2015
Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe 
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo.
Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari.
Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani.
MAMA MARIA NYERERE AKANUSHA UVUMI ULIOENEA JANA KUWA AMEFARIKI DUNIA

MAMA MARIA NYERERE AKANUSHA UVUMI ULIOENEA JANA KUWA AMEFARIKI DUNIA

March 11, 2015

unnamed (69)
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo amezungumza na waandishi wa habari,nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam juu ya uvumi ulioenea nchini kuwa amefariki Dunia.
Mama Maria amewathibitishia watanzania kuwa bado yu hai na mwenye nguvu hivyo wasiwe na hofu nae.
Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.
Amesema alipopokea taarifa hizo wala hakushtushwa badala yake alifanya sara kwani uvumi huo wawezekana inatokana na vuguvugu la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, pia utandawazi uliopo wa sayansi na teknolojia wa karne ya 21.
“jana nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto wangu, wake wa watoto zangu, pamoja na familia,walikuwa wakinisalimia, wengine waliposikia sauti yangu walikata simu” alisema Mama Maria.
Mama Maria alisema taarifa hizi za kuzushiwa kifo si mara ya kwanza kwani hata miaka ya nyuma akiwa na hayati baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere walipokea taarifa nyingi za uvumi wa kifo.
Mjane wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam leo,juu ya uvumi wa kufariki Dunia ulioenea jana kupitia simu na mitandao ya kijamii.
KINANA AMALIZA ZIARA YAKE BAHI MKOANI DODOMA, KESHO KUENDELEA WILAYANI CHEMBA

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE BAHI MKOANI DODOMA, KESHO KUENDELEA WILAYANI CHEMBA

March 11, 2015


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba mtaro pamoja na viongozi wa mkoa wa Dodoma  kwa ajili ya kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Kata ya Mundemu kijiji cha Nguji katika wilaya ya Bahi wakati alipotembelea mradi huo na kukagua shughuli za ujenzi wa tanki la maji na usambazaji wa mfumo wa mabomba akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma, Kinana yuko Katika ziara ya mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 akiongozana na msemaji wa chama hicho Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika mkoa wa Domoma.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BAHI-DODOMA) 2 
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa, Mh. Badwel Mbunge wa jimbo la Bahi na Luteni Mstaafu Chiku Galawa Mkuu wa mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nguji. 6 
Moja ya nyumba za walimu zinazojengwa katika kijiji cha Kongogo kata ya Babayu ambayo katibu mkuu aliikagua na kushiriki katika ujenzi wake. 11 
Mbunge wa jimbo la Bahi Mh. Badwel akizungumza na wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza katika kijiji cha Kongogo. 13 
Nape Nnauye naye akiendesha moja ya matrekta mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Chonde. 18 
Nape Nnauye akiwasili katika eneo la mkutano katika kijiji cha Chonde.

MKUU WA WILAYA KINONDONI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA PALESTINA KUANGALIA UTENDAJI WAKE

March 11, 2015

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dkt. Benedicto Luoga iliyopo Sinza jijini Dar es Salaama mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. Pembeni ni Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Waandishi wa Habari walioambatana na Mkuu wa Wilaya wakifuatilia.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dkt. Benedicto Luoga akitoa maelezo machache.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akipewa maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa maabara Dokta  Mniko Kimori.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na akinamama waliopo katika wodi ya uzazi wakieleza uhaba wa majengo kusababaisha msongamano.
Akipokelewa na Mkunga…
Akiongea na wagonjwa…
Akionyeshwa X-Ray na mmoja ya wagonjwa…
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dkt. Benedicto Luoga iliyopo Sinza jijini Dar es Salaama akisoma taarifa ya hospitali mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea akina mama aliyowakuta wakipata huduma katika hospitali ya Mwananyamara mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonyani (kulia).
Akinamama wakifurahia kuongea na mkuu wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea  mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonyani (kulia) akimuongoza Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.  
Wananchi walifika kupata huduma katika hospitali ya Mwananyamala wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (hayupo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akisalimiana na mmoja ya madokta wa hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea akina mama aliyowakuta wakipata huduma katika hospitali ya Mwananyamara mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akionyeshwa jinsi X-Ray inavyofanya kazi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akipata maelezo mara baada ya kuingia chumba cha maabara ya hospitali ya Mwananyamala mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonyani akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Madokta wa hospitali ya Mwananyamala wakishauriana jambo.