April 05, 2014

*RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI BAADA YA ZIARA YA UINGEREZA NA UBELGIJI

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki baada ya kuwasili jana April 4, 2014 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Brussels, Ubelgiji, alikofanya ziara ya kikazi ya siku mbili na kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Afrika na nchi za Jumuiya ya Ulaya. Kabla ya hapo Rais Kikwete alifanya zaiara ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mhe David Camaron. PICHA NA IKULU
April 05, 2014

*RIDHIWANI ALIPORINDIMA PERA

 Mke wa Ridhiwani Kikwete ,Arafa akimuombea kura mumewe kwa wananchi wa kata ya Pera
 Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 Ridhiwani Kikwete akihutbia wakazi wa kata ya Pera kwenye mkutano mkubwa wa hadhara  uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Pera shuleni na kuwahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze kuwa atakuwa Mbunge wa Vitendo zaidi na kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya Jimbo.

JINSI VIONGOZI WA UWT MKOA WA TANGA WALIVYOKUTANA.

April 05, 2014
MWENYEKITI WA UWT MKOA WA TANGA,AISHA KIGODA KUSHOTO AKISALIMIA NA MWEKA HAZINA WA UWT UCHUMI MKOA WA TANGA,AISHA KISOKI MWISHONI MWA WIKI WALIOOKUTANA OFISINI.



BAADA YA KIKAO WAKAPATA VINYWAJI BARIDI NA HAPO WANA FURAHIA JAMBO.

MWEKA HAZINA WA UWT NA UCHUMI MKOA AISHA KISOKY AKIWA KWENYE PICHA YA POZI HIVI KARIBUNI.

April 05, 2014
TAIFA STARS, BURUNDI KUCHEZA APRILI 26
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki na Burundi (Intamba Mu Rugamba) Aprili 26 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa ajili ya mechi hiyo ikiwa na wachezaji waliopatikana katika programu maalumu ya kusaka vipaji.

Baadaye wachezaji wengine wa Taifa Stars ambao wapo nje ya programu ya kusaka vipaji wataungana na wenzao kabla ya kutengeneza kikosi cha mwisho kitakachoivaa Burundi.

Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachezeshwa na waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka nchini Kenya.

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YACHACHAFYA BRAZIL
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia yanayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil baada ya jana kuifunga Indonesia kwa jumla ya mabao 5-3.

Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo unamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2 ndipo ikatumia mikwaju ya penalti kuamua mshindi. Tanzania ilipata penalti tatu dhidi ya moja ya wapinzani wao.

Kwa matokeo hayo, Tanzania sasa itacheza mechi ya nusu fainali leo dhidi ya Marekani ili kupata timu zitakazocheza mechi za fainali na kutafuta mshindi wa tatu. Mechi za fainali na kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho (Aprili 6 mwaka huu).
Timu nyingine zilizoingia nusu fainali na mechi zake zinachezwa leo (Aprili 5 mwaka huu) ni Burundi itakayocheza na Pakistan.

Katika mechi zilizopita, Tanzania ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi, ikaitandika Argentina mabao 3-0 ikailaza Nicaragua mabao 2-0 na ikafungwa na Philippines mabao 2-0.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)